Friday, December 2, 2011

Lowassa amtisha Kikwete kujiokoa

Edward Lowassa na Frederick Sumaye
Edward Lowassa na Frederick Sumaye
Vita ya ufisadi yageuzwa vita ya urais
Mchezo mchafu wahusisha familia
Mukama: Hakuna fisadi atakayepona

WAKATI Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akimgeuzia kibao Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, imebainika kwamba watuhumiwa wa ufisadi walitumia nguvu kubwa kujilinda zikihusisha mchezo mchafu ulioratibiwa na familia ya mmoja wa watuhumiwa anayepaswa kujivua gamba, Raia Mwema, imeelezwa.
Lowassa, ambaye amekuwa akijinadi kwamba Kikwete ni rafiki yake ambaye “hawajakutana barabarani”, alisimama ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichomalizika, wiki iliyopita,  mjini Dodoma, na kumshambulia Rais Kikwete waziwazi, na  kuaminisha umma kwamba kashfa zote zinazoelekezwa kwake Kikwete anazifahamu.
Lowassa azungumza NEC
Akiwa mmoja wa viongozi ambaye muda wake wa kujiuzulu kwa ‘hiari’ umekwisha, Lowassa alizungumza katika NEC na kulalamika kwamba anaonewa na si kweli yeye ni fisadi;  huku akielekeza moja kwa moja mashambulizi kwa Kikwete kwa hasira.
Imeelezwa kwamba mashambulizi ya Lowassa kwa Kikwete, yalilenga kumtisha na kupotosha umma kuhusu dhana nzima ya ufisadi, hasa pale alipokumbushia mchakato wa kutafuta mgombea urais wa CCM mwaka 2005, ambako ilielezwa kwamba Mwenyekiti mstaafu Benjamin Mkapa ndiye aliyeokoa jahazi.
“Lowassa kumdhalilisha Rais mbele ya wajumbe wa NEC ni kosa linalohalalisha kuchukuliwa hatua, lakini pia wizi hauwezi kuhalalishwa kwa kumsema hakimu. Kikwete pale alikuwa hakimu, sasa unasema hakimu naye si msafi ili akusamehe ama akuhukumu?” alihoji mjumbe mmoja wa NEC ambaye yuko serikalini.
Mjumbe huyo amesema ukimya wa Kikwete unaweza kuwa na tafsiri nyingi, lakini kubwa ni ama amemuogopa Lowassa ama anajiandaa kuchukua hatua madhubuti kwa kutumia ushahidi uliokusanywa na vyombo vyake.
Simu zapigwa Lowassa akizungumza
Hata hivyo, taarifa za kiuchunguzi kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinabainisha kuwa wakati wote ambao Lowassa alikuwa akizungumza, kulikuwa na simu zilizokuwa zimepigwa kwa watu maalumu nje ya kikao hicho ambazo watu hao walikuwa wakimsikiliza moja kwa moja kutoka kikaoni.
Baada ya Lowassa kumaliza kuzungumza, inaelezwa kuwa simu hizo ziliendelea ‘kubaki hewani’ na alipoanza kuzungumza Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, naye alikuwa akisikika moja kwa moja kutoka kwenye kikao hicho cha NEC. Sumaye alikuwa ameketi jirani na Lowassa ndani ya kikao hicho cha NEC kilichoketi Novemba 23 na 24, 2011.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa maelezo ya Sumaye yalipindishwa na waandishi wa habari maalumu waliopata taarifa kutoka kwa mtu maalumu aliyekuwa akisikiliza kikao cha NEC kupitia simu na ikaripotiwa kuwa “Sumaye amemtetea Lowassa.”
Watu waliokaribu na Sumaye wanaeleza kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani hadi sasa hakufurahishwa na upotoshaji huo uliofanywa dhidi yake.
Sitta anyimwa nafasi kumjibu Lowassa
Katika kile kinachoonyesha kushindwa kuvumilia kauli za Lowassa kuhusu kashfa ya Richmond ndani ya NEC, aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, aliomba nafasi ya kuzungumza akionekana kutaka kufichua zaidi yaliyofichwa kuhusu uhusika wa Lowassa na kashfa ya Richmond.
Hata hivyo, Sitta hakupewa nafasi hiyo na Kikwete ambaye alikuwa akiendesha kikao hicho na hivyo maelezo ya Lowassa kwamba hahusiki yakabaki salama. Inaelezwa kuwa ni Mkapa aliyemshawishi Kikwete kutowapa nafasi wengine kuzungumza baada ya Lowassa na Sumaye kuzungumza.
Wengine ambao kutokana na uamuzi huo walikosa nafasi ya kuzungumza ni pamoja na Kingunge Ngombale Mwiru, anayetajwa kuwa mtetezi mkubwa wa Lowassa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja
Katika kikao hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, alielezwa kusimama baada ya Lowassa, kuonyesha hasira zake kwa Mwenyekiti Kikwete na wajumbe wa Sekretarieti, kuhusiana na kuyumba kwao katika kufanya maamuzi ya utekelezaji wa uvuaji gamba na kuruhusu mjadala wa hoja iliyokwisha kufanyiwa maamuzi na NEC.
Ni katika kikao hicho ambacho Sumaye anaelezwa kutaka ufafanuzi kuhusu kauli za wajumbe wa Sekretarieti, akiwamo Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, na Naibu Katibu Mkuu, John Chiligati ambao walizunguka nchi nzima kuelezea dhana ya uvuaji gamba kwa kuwataja majina baadhi.
“Sumaye alikua mkali kwa kuigeuzia kibao meza kuu kutokana na kuonyesha ugeugeu baada ya kumruhusu Lowassa. Alisema kama Nape na Chiligati walikosea, basi, wachukuliwe hatua na kama waliyosema ni maamuzi ya NEC, basi, yatekelezwe badala ya kuyumba. Kauli yake ilipotoshwa sana na nyie waandishi kwa maslahi yenu,” anasema mjumbe mmoja wa NEC.
Viongozi wengine wastaafu ambao wameelezwa kuonyesha mshangao mkubwa wa hali ya mambo ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye amenukuliwa wiki hii na mmoja wa watu walio karibu naye akiwashangaa Lowassa na wenzake kushangilia ushindi, akisema, “huu ni ujinga kwa mtu kusema haya maazimio ya NEC yememsafisha Lowassa”.
Hata hivyo, Mkapa anatajwa kuwa miongoni mwa wastaafu ambao wameonyesha kutopendelea dhana na uvuaji gamba, kwa maelezo kwamba ikitekelezwa kwa dhati, itawamaliza wanasiasa wengi akiwamo yeye binafsi ambaye amekuwa akiandamwa na tuhuma kadhaa za ufisadi, zinazohusishwa na uanzishaji wa kampuni ya ANBEM Limited, akiwa madarakani. Mkapa na mkewe Anna wameifilisi kampuni hiyo kwa hiari.
Makongoro Nyerere afichua msimamo
Taarifa za kina zinaeleza kuwa Makongoro Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa, ambaye pia kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM, mkoani Mara, hakuwa akificha fikra zake kabla na wakati wote wa vikao vya NEC.
Makongoro anatajwa kueleza bayana kuwa kama akipewa nafasi ya kuzungumza ndani ya NEC na hasa kwa kuzingatia kuwa uamuzi wa kuvua gamba umeyumba, basi, angetamka: “Natoka mimi na kama mkiamua kuwatoa baadaye, nitarudi”;  akiwa na maana ya kujiondoa kwenye wadhifa wake hadi wahusika wa ufisadi watakapong’olewa na yeye atakuwa tayari kurudi.
Makongoro ndiye katika kikao cha NEC kilichotangaza kujivua gamba alitoa mashambulizi makali dhidi ya wahusika ambao ni Edward Lowassa, Andrew Chenge na aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi, ambaye alijiuzulu ndani ya muda wake wa hiari kama walivyopewa na CCM.
Makongoro kwenye kikao hicho cha NEC alinukuliwa akimwambia Kikwete kwamba japo yeye ni Mwenyekiti wa Taifa, yeye (Makongoro) naye ni Mwenyekiti wa Mara na kwamba NEC ndio waajiri wa Mwenyekiti Taifa.
“Akasema anapokaa Mwenyekiti wa Taifa ni mahala patakatifu na kwa ajili hiyo pasingeweza kusogelewa na shetani, hata kama siku moja Mungu alipata kukutana na shetani barabani.
Uvuaji gamba kwa lazima wasubiriwa
Msingi wa dhana ya kujivua gamba umejengwa katika azimio la NEC iliyofanyika Aprili 10 na 11, 2011, kwa lengo la kukipa chama hicho sura ya mageuzi na taswira mpya.
Azimio hilo la NEC linasema: “Viongozi wanaotuhumiwa na ufisadi watafakari, wajipime na kuchukua hatua wao wenyewe kwa maslahi ya chama, wasipofanya hivyo chama kiwawajibishe bila kuchelewa.”
Taarifa zilizotolewa mara baada ya kikao cha NEC, wiki iliyopita, zinaeleza kuwa kazi ya kuwandoa wahusika sasa ipo chini ya Kamati Kuu, kupitia Kamati ya Maadili.
Kauli ya Kikwete kuhusu Lowassa
Kwenye kikao hiki cha NEC, Lowassa ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu kwa kashfa ya zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond, alijitetea.
Utetezi wa Lowassa ni pamoja na kujieleza kuwa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond kwa kumpigia simu Rais Kikwete.
Ni kutokana na utetezi huo wa Lowassa na wajumbe wengine kutaka kumjibu papo hapo, taarifa zinaeleza kuwa Rais Kikwete alisikika akisema usiwe na haraka tutawaita kwenye Kamati ya Maadili ya chama chetu tukiwa na vielelezo vyote ili mtoe utetezi wenu. Tukishachukua hatua tutawaelezeni wajumbe wa NEC nyeupe na nyeusi. Safari hii tunataka “Natural Justice” ichukue nafasi yake.
Mchezo mchafu UVCCM Dodoma
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, wabunge zaidi ya wanne akiwamo Saidi Mtanda wa Mchinga, mkoani Lindi na Dk. Hamis Kingwangala wa Nzega, mkoani Tabora, ni miongoni mwa waliokuwa tayari kufichua mchezo mchafu wa matumizi ya mamilioni ya fedha kuhonga baadhi ya vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM.
Wakati mchezo huo unafanyika wabunge hao na wenzao walikuwapo Dodoma ambako kabla ya vikao vya CCM walikuwa wakishiriki shughuli za Bunge.
Inaelezwa ya kuwa hata hivyo, licha ya kuwa tayari wabunge hao walishindwa kupewa nafasi ya kufichua siri hiyo mbele ya NEC-CCM, inayotajwa kuhusisha familia ya kigogo huyo kupitia kwa mtoto wake mmoja.
Mtoto huyo ambaye kwa sasa jina lake tunalihifadhi kutokana na kushindwa kumpata kwenye simu yake ya mkononi, anatajwa kuwa mmoja wa walipaji posho kwa vijana wa CCM inayofikia hadi Sh milioni moja kwa mjumbe mmoja, fedha ambazo zinatajwa kutoka katika familia yake na watu wengine wasiojulikana.
Mtoto huyo pia anadaiwa kuwa kambi moja na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha, James ole Millya, katika vurugu za mara kwa mara zilizokuwa zikiibuka UVCCM-Arusha ambazo hata hivyo, zilisuluhuhishwa na Steven Wassira, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika, alikuwa Nape Nnauye (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) aliyemtaka Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete kumpa mwongozo kuhusu kundi la vijana wa CCM kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania waliosafirishwa, kulipwa posho nono na gharama za malazi, wako Dodoma kwa shughuli gani na kwa sababu gani.
Nape anatajwa kueleza bayana kwamba ushahidi wa vijana hao kuwapo Dodoma kwa kuitwa na kundi la mafisadi upo, ushahidi ambao hata Kikwete anatajwa kuutambua na baada ya Nape kuhoji hivyo, Kikwete alimhoji Beno Malisa; fedha hizo  wamezipata wapi.
Beno, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM anatajwa pia kushambuliwa na mawaziri, William Lukuvi na Steven Wassira ambao hata hivyo walikuwa wakitoa lugha zenye mwelekeo wa kumuonya na si kutaka ashughulikiwe kwa mujibu wa kanuni za UVCCM au chama hicho.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya Malisa kupigwa mashambulizi ndani ya siku ya kwanza ya vikao hivyo, alifikisha taarifa hizo kwa wenzake waliosafirishwa “kwa kazi maalumu” Dodoma na baadhi yao walitishika na kuanza kufunga safari ya kurudi mikoa walikotoka.
“Vijana hawa walisafirishwa kuletwa hapa kwa kazi kubwa mbili. Kwanza kuna maneno waliambiwa uongozi wa UVCCM unavunjwa, lakini pili kuna hofu kwamba wale viongozi mafisadi watang’olewa katika kikao hicho cha NEC.
“Kwa hiyo walikuja kutibua masuala hayo mawili kwa vitisho kwamba kama ingekuwa hivyo wangehamia Chadema, lakini baada ya Rais Kikwete kusema kwenye kikao wasitutishe, waende hata kesho baadhi ya vijana waliogopa wakakimbia wengine usiku kurudi walikotoka,” anaeleza mtoa habari wetu.
Katika mchakato huo wa mawasiliano, gazeti hili limeshuhudia ujumbe wa simu ya mkononi kutoka kwa mmoja wa viongozi wa vijana katika moja ya mikoa ya Kanda ya Juu Kusini, ambaye pia ni mwalimu katika moja ya vyuo vikuu nchini.
Kiongozi huyo ndiye aliyekuwa akisambaza ujumbe wa kuita vijana wafuasi wa viongozi wanaopaswa kujiuzulu ili wakusanyike Dodoma ambapo kwa mikoa ya mbali kama Kigoma, Raia Mwema imeelezwa kuwa tiketi za ndege kwa vijana waliokuwa tayari kuelekea Dodoma zilikuwa zikipatikana kwa masharti tu, ukifika Dodoma uungane na kundi hilo.
Taarifa zinabainisha kuwa bajeti ya mamilioni ya fedha ilitengwa na kutumika katika kugharimia vijana hao kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mpango huo pia ulikuwa ukiratibiwa na kijana mwingine ambaye ni mtumishi katika moja ya kampuni za aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi.
Hujuma zilianza mapema
Taarifa za kiuchunguzi zinaelekeza kuwa mpango wa kuhakikisha mchakato wa kujivua gamba unahitimishwa kwenye kikao cha NEC uliandaliwa na kundi la watuhumiwa wa ufisadi, ukiratibiwa na mmoja wa wajumbe wa Sekretariati ya CCM (jina linahifadhiwa).
Kigogo huyo ndani ya sekretariati ndiye aliyepewa jukumu la kuandaa waraka maalumu kuhusu hali ya kisiasa ambamo ndimo masuala ya kujivua gamba na mengine yanapaswa kuhusishwa.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka kitengo cha maadili, jukumu la kuandaa waraka huo lililikuwa la kitengo hicho lakini baadaye lilikasimiwa na mjumbe huyo wa sekretariati, ambaye anadaiwa kufanya ‘uchakachuaji’ ili kupenyeza matakwa ya mtandao wa kifisadi.
Hata hivyo, taarifa za kina zinabainisha kuwa waraka huo ulikataliwa mara kadhaa na Kikwete ambaye alikuwa anaukataa kupitia kwa Katibu Mkuu, Wilson Mukama.
Kutokana na kiongozi huyo kijana wa sekretariati kusumbuliwa kila mara kwa kurudishwa akatengeneze vizuri waraka huo; huku akishindwa kujua yalikuwa ni maagizo ya Kikwete na si Mukama, kuna wakati anatajwa kutishia kujiuzulu kutokana na kusumbuliwa akiamini ulikuwa ni usumbufu unaosababishwa na Mukama pekee.
Taarifa zinabainisha kuwa ingawa hatimaye alifuta maelezo yenye kuhujumu mpango wa kujivua gamba ndani ya waraka huo kama walivyotaka watuhumiwa wa ufisadi, lakini alikuwa akichomekea mawazo hayo wakati alipokuwa akifanya uwasilishaji kwenye vikao husika, vikiwamo vya Kamati ya Maadili iliyoketi kabla ya Kamati Kuu.
Mikakati ya kubadili upepo
Kumekua na juhudi kubwa za kubadili vita ya ufisadi kwa kuiwekea kinga ya kuwa chanzo chake ni vita ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, ukihusisha watu wanaotajwa kuwania kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Juhudi hizo zinazoendeshwa kwa gharama kubwa, zinalenga kuwasafishia njia watuhumiwa wa ufisadi ili kuweza kuingia katika mbio za urais na hatimaye kuingia madarakani baada ya Kikwete kwa gharama zozote zile.
Madai hayo yameanza kwa kujaribu kuuaminisha umma kwamba chimbuko la hali mbaya ya kisiasa ndani ya CCM ni wanamtandao walioshiriki kumpitisha mgombea Jakaya Kikwete mwaka 2005.
Katika kuuaminisha umma, watuhumiwa wa ufisadi wamefanikiwa kuwaaminisha watu kwamba tuhuma dhidi yao ni za kupikwa na kwamba baada ya kumpitisha Kikwete na baada ya kuwa na hakika ya ushindi dhidi ya Upinzani, wanamtandao mmoja mmoja walianza kujitathimini juu ya uwezekano wa wao wenyewe kuwania urais baada ya Kikwete.
Vinara wa kundi hilo walikuwa Edward Lowassa, Samuel Sitta, Rostam Aziz, Getrude Mongella, Zakia Meghji, Abdulrahman Kinana, Bernard Membe, Juma Jamaldin Akukweti (sasa marehemu), Kingunge Ngombale Mwiru, Philip Marmo, Emmanuel Nchimbi, Ali Karavina, Juma Mwapachu, Henry Shekifu, Ponsian Nyami, Makongoro Mahanga, Nazir Karamagi, Stephen Wassira na Sophia Simba.
Sasa maelezo ya watuhumiwa yanaanza kulikumbushia kundi hilo kwa kudai kwamba, kundi hilo lilikuwa pia likijipanga kwa ajili ya nafasi karibu zote za uongozi wa juu wa serikali na mihimili mingine baada ya uchaguzi wa mwaka 2005.
Pamoja na kuwa sababu hasa ya minyukano ndani ya CCM inapotoshwa, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma ya kuwa “hali ya siasa ndani ya chama ni shwari lakini si shwari sana”.
Kwa mujibu wa  Mukama, makundi kinzani yameshamri ndani ya chama hicho na sasa yanapangana safu za uongozi kwa kutumia fedha jambo ambalo alisema ni kansa ambayo inakitafuna chama hicho polepole.
Alisema kwa ajili hiyo chama kilikuwa kimeamua katika kikao cha NEC kutafuta dawa ya tatizo hilo na kwa kuanzia tuhuma zote za viongozi wote zitashughulikiwa kwa ngazi mbalimbali chini ya kamati za maadili husika na ambao tuhuma zao zitathibiti watachukuliwa hatua bila kuchelewa.
Akinukuu waraka wa NEC, Mukama alisema: “Kwa kutambua kuwa suala la ufisadi limekuwa mzigo mkubwa sana kwa Chama cha Mapinduzi licha ya juhudi kubwa ambazo Serikali ya CCM imezifanya katika kupambana na tatizo hilo, NEC iliamua kuwa viongozi wa CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari, wajipime na kuchukua hatua wenyewe kwa maslahi ya Chama. Wasipofanya hivyo Chama kiwawajibishe bila kuchelewa.
“Ni dhahiri kuwa azimio hili lililenga viongozi wote wa Chama, katika ngazi zote cha chama chetu, kuanzia ngazi ya Taifa hadi Tawi. Ni dhahiri pia azimio hilo lilikusudiwa liwe sehemu ya utamaduni wa kusimamia maadili ya viongozi na wanachama  wa chama chetu, yaani kwamba viongozi au wanachama, wanavunja maadili watachukuliwa hatua zinazostahili bia kuchelewa.
“Hali ilivyo hadi sasa, takriban miezi saba baada ya azimio hilo kupitishwa hatujapata mwitiko wa kuridhisha kutoka kwa viongozi wa ngazi yoyote ambao ni walengwa wa azimio hilo. Bila shaka wakati sasa umefika kwa chama kutekeleza ile sehemu ya pili ya azimio husika kwa kuwawajibisha wahusika. Lakini utekelezaji wake utafanyika vipi ili haki ionekane inatendeka? Jibu ni kwamba utekelezaji huo hauna budi ufanyike kwa kufuata utaratibu uliowekwa na kanuni za CCM za uongozi na maadili.”
Aliongeza Mukama: “NEC imeagiza kupitia Kamati za Usalama na Maadili zianze mara moja  mchakato wa kutekeleza azimio hilo kwa mujibu wa kanuni na taratibu na vilevile  kwamba zoezi hilo  lifanyike bila kuchelewa.”
Kauli hiyo ya NEC ilikuja siku moja baada ya mmoja wa watu ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa ufusadi Lowassa kuzungumza mkutanoni akisema alikuwa ametuhumiwa sana kwa kuitwa fisadi ili hali yeye si fisadi na kwamba alijiuzulu katika kashfa ya Richmond kulinda heshima ya CCM na serikali yake.
Aidha ilikuja baada ya NEC kutangaza ya kuwa ilikuwa imemvua madaraka Katibu wa  CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kirumbe Ng’enda, ambaye alikuwa anatuhumiwa kuvuruga zoezi la kura za maoni katika chaguzi za wabunge na madiwani mkoani kiasi cha kuwashusha baadhi ya wagombea waliopata kura nyingi. Uamuzi huo umeelezwa kuwa ni, “kuchukulia hatua dagaa na kuacha mapapa.”
Wakati tukienda mitamboni, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amekutana na waandishi wa habari na kusema hakuna aliyesafishwa katika vikao vya chama hicho mjini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mukama amesema baadhi ya vyombo vya habari vimepotosha maamuzi ya vikao vya juu vya CCM kwamba vimesafisha watuhumiwa wa ufisadi, wakati kinachoendelea ni mchakato wa kuwachukulia hatua.
Mukama amesema kwa sasa Kamati ya Maadili na Usalama Taifa, imepewa nguvu zaidi na kuwa Tume ambayo itakuwa na uwezo wa kuwachukulia watu hatua moja kwa moja bila kusubiri vikao vya juu.
Akirejea maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) na hotuba ya Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete, Mukama alisema Kamati ya Maadili na Usalama itawaita watuhumiwa na kuwataka wajitetee kabla ya kufanya uamuzi.
Alisema kamati hiyo inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, ikiwa na wajumbe wengine wakiwamo wawili kutoka Zanzibar na wawili kutoka Bara na yeye akiwa mjumbe mpya aliyeingizwa katikia utaratibu mpya.
“Mhusika ataitwa na kuhojiwa, badala ya kumhoji kwenye NEC ambayo ina watu wengi ambao mtu asiye na kosa anaweza kuhukumiwa kwa hisia za kisiasa ama mhalifu anaweza kupona kwa hisia.
“Kuhusu maadili tumekubaliana kutokuwa na ajizi katika kupambana na rushwa, viongozi wajitafakari na kujiwabisha wenyewe, wasipofanya hivyo chama hakitasita kuchukua hatua. Katika kufanikisha hilo, tumemua kuiongezea nguvu kamati ya maadili na kuibadilisha na kuwa tume kamili yenye watu 14 kutoka 12 na kuipa mamlaka ya kuamua bila kusubiri vikao,” alisema Mukama.
Alisema mabadiliko hayo yanalenga katika ngazi zote pamoja na kuwa Tume ya Maadili na Usalama itakuwa moja tu kitaifa na katika ngazi ya mikoa na wilaya zitaendelea kuwa Kamati ya Maadili na Usalama ambazo nazo zitakuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi moja kwa moja.
Mukama alisema CCM haikukurupuka katika uamuzi wake wa kufanya mageuzi na kujisafisha, na kwamba kila jambo litafanyika kwa umakini wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na utafiti uliofanyika ndani na nje ya nchi.

Walimu watangaza mgomo nchi nzima


Raymond Kaminyoge
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimetangaza mgomo wa walimu nchi nzima kuanzia Januari mwakani ikiwa ni hatua ya  kuishinikiza Serikali iwalipe walimu deni la malimbikizo ya stahili zao mbalimbali, linalofikia Sh49.6 bilioni.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuanza kuwalipa walimu fedha hizo tangu Novemba mwaka huu.  Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na wandishi wa habari kuwa Serikali iliahidi kuwalipa walimu Novemba hadi Desemba mwaka huu ili kumaliza deni hilo. 

“Natangaza kuwa shule zitakapofunguliwa mwezi Januari 2012, sisi walimu tutaendelea kuwa likizo mpaka kero zetu zitakapotatuliwa,” alisema Mukoba.  Alisema tangu Juni mwaka huu, CWT na Serikali wamekuwa na vikao kadhaa kuhusu madai hayo na ikafikia uamuzi wa kuwalipa walimu katika kipindi cha miezi miwili  ambayo ni Novemba na Desemba mwaka huu.

“Kumbe Serikali haikuwa na nia ya kweli kutaka kutulipa, waliona tunaweza kugoma katika kipindi cha mitihani ya taifa wakatudanganya,” alisema.  Alisema kwa kuwa Serikali haina nia ya dhati katika kulipa madai hayo, wameamua kufikia uamuzi wa kutoendelea kufundisha.

Mukoba alisema wakati mishahara na  posho za wabunge zikizidi kuongezeka, walimu wanashindwa kulipwa madai yao ya msingi.  “Tunawaomba wazazi watuunge mkono katika mgomo huu ili watoto wenu wapate elimu sahihi,” alisema Mukoba.  Kwa mujibu wa Mukoba, madai hayo yanayowahusu zaidi ya walimu 3,000 ni ya kuanzia mwaka 2008.

Alisema kero nyingine inayowafanya walimu wagome ni waraka kandamizi uliotolewa na Serikali mwaka 2007 unaowashusha vyeo walimu wanaojiendeleza kielimu.  “Serikali ilikubali kuufuta waraka huo baada ya kuridhika kwamba ulikuwa unawakandamiza walimu, lakini hadi sasa unaendelea kutumika, haujafutwa,” alisema.   Mukoba alisema waraka huo umelenga kuwakatisha tamaa walimu ili wasijiendeleze kielimu.

Aidha, Mukoba alisema walimu wanakaa kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo ingawa wanastahili kulingana na sifa zao.   “Walimu tumekosa nini, kwa nini kilio chetu hakisikiki na Serikali? Iweje tunadanganywa kila siku? Sasa ni lazima tuchukue hatua,” alisema Mukoba.  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawamba hakupatikana jana kuzungumzia tishio hilo la mgomo baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana kabisa. 

Waziri mkuu wa Zimbabwe 'afuta' ndoa


Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amesema uhusiano wake na mfanyabishara Locadia Tembo umefikia tamati, siku chache baada ya kutoa mahari.
Bw Tsvangirai alisema uhusiano wao "umeharibiwa na hautengenezeki" baada ya "kutekwa" na wapinzani wa kisiasa.
Wawakilishi wake walitoa mahari ya maelfu ya madola na ng'ombe katika sherehe zilizofanyika Novemba 18.
Bw Tsvangirai yuko kwenye serikali ya muungano na mpinzani wake, Rais Robert Mugabe.
Katika taarifa iliyotolewa, Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka, 59, alisema anatia shaka kama uhusiano wake utakuwa na "umoja thabit" na Bi Tembo mwenye umri wa miaka 39, mfanyabiashara na dada wa mbunge mmoja kutoka chama cha Bw Mugabe Zanu-PF.
"'Ndoa hii' imegubikwa na mambo mengine na kuna mkono wa kisiasa ambao sasa unaushughulisha mchakato huu," alisema kwenye taarifa hiyo.
Mke wa kwanza wa Bw Tsvangirai, Susan, alikufa kwenye ajali ya gari siku chache baada ya kuwa waziri mkuu.

'Njama nzito'

Bw Tsvangirai alikana taarifa za vyombo vya habari kuwa alikuwepo kwenye sherehe za kimila Novemba 18.
Alisema, alikuwepo ofisini mwake na kutuma ujumbe kwenye familia ya Bi Tembo "kuuweka rasmi" uhusiano huo.
Bw Tsvangirai aliongeza, "Nimekuwa mtazamaji katika uhusiano huu na mambo yanaenda haraka sana, kwenye kamera bila mimi kufahamu."
"Hii imenifanya niamini kuna njama nzito linalolikumba suala hili iliyoshusha imani yangu kwenye uhsiano huu."
Bw Tsvangirai alisema ameiarifu familia ya Bi Tembo juu ya kuvunja uhusiano huo.
"Sifa zimeharibiwa na uaminifu baina ya pande zote mbili zimepotea," alisema.
"Uhusiano huu umeharibiwa kiasi ambacho hauwezi kutengamaa na umefikia kiwango ambacho ndoa haiwezi hata kufikirika."
Shaka baina ya chama cha Bw Tsvangirai cha Movement for Democratic Change (MDC) na Zanu-PF imekuwa ikiongezeka kabla ya uchaguzi, unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Siri zafichuka ufisadi wa rada


SERIKALI YADAIWA KUZUIA UCHUNGUZI WA VIGOGO
Mwandishi Wetu
KASHFA nyingine imeikumba Serikali ya Tanzania, kufuatia tuhuma kwamba ina mkakati maalumu kuzuia watuhumiwa wa ufisadi wa rada kufikishwa mahakamani.Taarifa za mtandao wa Wikileaks ambao umekuwa ukifichua siri za kidiplomasia na ufisadi duniani, umeibua tuhuma hizo mpya kwa Serikali na kwamba hicho ndicho kikwazo cha watuhumiwa husika kutofikishwa mahakamani.Taarifa ya mtandao huo uliyosambazwa jana imeeleza kuwa mpango huo, ndio ulioathiri jitihada za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Clare Shot kuzuia Tanzania kuuziwa rada hiyo.


Kwa mujibu wa mtandao huo, juhudi za Shot zilijumuisha kuinyima Tanzania misaada inayofikia Paundi 35 Milioni kutokana na kununua rada hiyo kwa bei ya kuruka.

"Pamoja na shinikizo hilo, juhudi za Shot zilishindwa kabisa kuzuia ununuzi wa rada hiyo ambayo thamani yake ilikuwa Paundi 28 Milioni kutoka kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza," ulisema mtandao huo na kuendelea:

"Suala hilio si jipya. Gazeti la The Guardian la Uingereza liliwahi kutoa ripoti yake ya uchunguzi wake kuhusu uuzwaji wa rada hiyo ambao ulimsababishia pia Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Tony Blair kuamuru kikosi chake cha kuchunguza makosa makubwa (SFO) kuingilia kati na kuchunguza namna BAE ilivyohusika."

Ilichobaini Wikileaks ni kwamba viongozi wa Serikali ya Tanzania ilikuwa ikifanya juhudi za kuficha kasoro zote zilizokuwa katika mpango wa ununuzi wa rada hiyo.

Hata kwa upande wake, mtu mahususi aliyetakiwa kushughulikia kashfa hiyo kwa kufanya uchunguzi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru), Dk Edward Hoseah alinukuliwa akimweleza Afisa wa Ubalozi wa Marekani nchini kwamba aliwahi kutishiwa kuuawa mara kadhaa na kukumbushwa kwa ujumbe wa maneno kila siku.

Mara kadhaa, kutokana na kashfa hiyo ya rushwa, Serikali ya Uingereza na ya Tanzania ziliingia katika mvutano.

BAE Systems ni kampuni kubwa ya uuzaji wa vifaa vya ulinzi ambayo iwapo ingefungiwa kufanya biashara yake kungekuwa na athari kubwa kwa Uingereza.

Suala la uchunguzi wa aina yoyote ambao ungemweka matatani Rais wa zamani, Benjamin Mkapa na washirika wake wa karibu (kwa mujibu wa Wikileaks) lilikuwa ni gumu kuweza kufanyika.

Ulisema baada ya kumalizika kwa kipindi cha ukimya bila kushughulikiwa kwa kashfa hiyo, suala la kutafuta ufumbuzi lilionekana kuwa muhimu kwa nchi zote mbili, lakini kasoro kubwa ni pale kila aliyehusika katika kashfa hiyo ya BAE nchini Uingereza na Tanzania kukwepa kuchunguzwa.

Hata hivyo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Tonny Blair alifanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba SFO wanafanya uchunguzi na kama ikiwezekana BAE ifungiwe kufanya kazi katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Kwa upande wake, Tanzania ilikuwa ikilaumiwa kwa kufanya juhudi za kutetea ununuzi huo na hata kumtisha Mkurugenzi wa Takukuru kumtaka aachane na suala hilo.

Dk Hosseah
Jana Dk Hosea hakupatikana kuzungumzia taarifa hiyo, lakini akizungumzia tuhuma za kufichua siri ya Rais Kikwete kupitia mtandao huo Desemba 20 mwaka jana, alikiri kupata vitisho vinavyohatarisha maisha yake kutokana na mapambano yake dhidi ya rushwa.

Dk Hoseah alisema hayo alipotakiwa kuzungumzia madai ya mtandao huo wa Wikileaks kuhusu kauli yake na Afisa wa Ubalozi wa Marekani kwamba kiongozi huyo wa nchi, asingependa vigogo Serikalini kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Mtandao huo pia ulidai kuwa mkuu huyo wa Takukuru ameshindwa kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika na kashfa ya rada kwa sababu anahofia usalama wake.

Mbali na hofu hiyo, mtandao huo ulieleza kuwa Dk Hoseah alipewa maelekezo maalumu na Rais Kikwete kutoshughulikia kesi za rushwa zinazowahusu vigogo katika Serikali yake na hasa marais waliomtangulia.

The Guardian lilitoa taarifa hiyo likiunukuu mtandao wa habari wa WikiLeaks uliojizolea umaarufu duniani kwa kutoa habari za kiuchunguzi hasa baada ya mwasisi wake, Julian Paul Assange, kutiwa matatani
Akijibu hoja hizo mwaka jana, Dk Hoseah alisema ni kawaida kwake kukutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kila mwaka na kujadiliana nao mambo mengi kuhusu Tanzania, lakini hakumbuki kuzungumza naye mambo hayo.

Alisema mabalozi ni wadau wakubwa katika bajeti ya Tanzania na hivyo huwa wanakutana kila mwaka kujadili mambo mbalimbali ya kuhusu kusaidia bajeti ya Serikali.

“Mimi huwa nakutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kwa sababu wao ni wadau katika mradi wa ‘government budget support’ (Mpango wa kusaidia bajeti ya Serikali), hivyo hilo sio tatizo,” alisema Dk Hoseah.

“Msimamo wangu ni kwamba mapambao dhidi ya ufisadi ni endelevu hadi hapo tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili,” alisema Dk Hosea na kukiri:

“Vitisho vipo vingi tu, kutoka kwa watu wanaotuhumiwa, lakini si hata ninyi waandishi mnamwagiwa ‘tindikali’ katika mapambano yenu, hivyo hivyo hata mimi napata vitisho.”

Alisisitiza kuwa pamoja na vitisho hivyo, hawezi kurudi nyuma katika mapambano ya rushwa na ufisadi.

“I’m a Tanzanian, I will die in Tanzania, it is my country’ (mimi ni Mtanzania, nitakufa Tanzania, ni nchi yangu), siwezi kuhama nchi kwa vitisho vya watu wachache wanaotuhumiwa kwa ufisadi na rushwa,” alisisitiza Dk Hoseah.

“Hilo la kwamba nafikiria kuhama nchi wametia chumvi si unajua magazeti? Sijafikiria kuhama nchi licha ya vitisho, mimi naona ni changamoto na jambo la kawaida katika mapambano,” aliongeza Dk Hoseah.

Kuhusu Rais Kikwete kukwamisha mapambano ya ufisadi kama alivyonukuliwa na gazeti hilo la The Guardian, Dk Hoseah alipiga chenga kulijibu badala yake akaeleza:

“Ili umpeleke mtu mahakamani si lazima umtuhumu na kumfanyia uchunguzi? Lakini pia lazima tujenge utamaduni wa kuwaheshimu viongozi wetu.”

Siku hiyo, Takukuru ilituma taarifa iliyoeleza kuwa Dk Hoseah alishangazwa na Ofisa wa Ubalozi wa Marekani kumnukuu vibaya huku akisema hajui ana lengo gani.

Katika taarifa hiyo, Dk Hoseah alikiri kukutana na ofisa huyo wa Ubalozi wa Marekani ofisini kwake Julai mwaka 2007, lakini akasema ripoti ya mazungumzo yao aliyoipeleka nchini kwake imechakachuliwa.

“Kwa mfano haikutokea katika mazungumzo yetu kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete hakutaka kuruhusu sheria kuchukua mkondo wake, kuwashitaki vigogo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi kama ilivyodaiwa na Ubalozi wa Marekani,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na idara ya mahusiano ya Takukuru.

“Nilichosema ni kwamba Rais hayuko tayari kuruhusu kushitakiwa kwa vigogo wa Serikali au mtu mwengine yeyote kwa tuhuma za uvumi au kwa ushahidi dhaifu, kwa sababu kufanya hivyo, Serikali itakuwa hatarini kwa kulipa gharama kubwa ya fidia ikiwa mtuhumiwa huyo atashinda kesi mahakamani,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza.

Kuhusu hofu ya maisha yangu, nakumbuka niliulizwa na Ubalozi wa Marekani kwamba je, naogopea maisha yangu au la, nikiwa Mkuu wa Takukuru? Na jibu langu lilikuwa rahisi kwamba ‘bila ya shaka’ unapopambana na wakubwa na matajiri kama hao wanaotuhumiwa unapaswa kuwa makini na maisha yako.

Lakini hata siku moja sikusema kwamba napanga kuhama nchi kwa sababu maisha yangu yapo hatarini. Ni mshangao kuona kwa mara nyengine ofisa wa Ubalozi wa Marekani ananinukuu mimi vibaya au nje ya mada na sielewi kabisa lengo lao lilikuwa nini.”

Alsema rekodi yake, akiwa Mkuu wa Takukuru iko wazi kabisa wakati wowote anapokuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa yeyote wa ufisadi hawaogopi lolote isipokuwa ni kumburuza mahakamani bila ya kujali cheo chake.

Bunge la Uingereza
Taarifa ya mtandao huo imekuja siku moja tangu Bunge la Uingereza liitake Serikali ya Tanzania kuwafikisha mahakamani watu wote walioshiriki mchakato wa ununuzi wa rada na kuingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya fedha.

Kupitia kamati yake ya Maendeleo ya Kimataifa, Bunge hilo lilisema lingependa kuona watu wote walioshiriki kwenye mchakato wa ununuzi wa rada hiyo, wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi.

Taarifa ya kamati hiyo iliyonukuliwa juzi na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), ilieleza kuwa wajumbe wake ambao ni wabunge kutoka vyama mbalimbali, watatoa ushirikiano wa dhati kwa Tanzania iwapo itaamua kuwashtaki watuhumiwa hao nchini Tanzania au Uingereza.

Wito huo wa wabunge wa Uingereza umekuja wakati tayari Kampuni ya BAE System, iliyoiuzia Tanzania rada hiyo, ikikubali kuwa kulikuwa na kasoro katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo na hivyo kuirudishia Tanzania Dola za Marekani 46 milioni kama fidia. 

Girl, 15, talks about pregnancy and marriage on Facebook

A 15-year-old girl has allegedly bragged about being pregnant and getting married on social networking site Facebook.
A contributor to citizen journalism website said the 15-year-old girl has been posting status updates on Facebook about her pregnancy.
The contributor, who went by the name of "Hello There" said there wasn't a need for the 15-year-old girl to brag about being pregnant.
"Firstly, she does not think that it's disgraceful. Secondly she is just a minor, and is she proving that she had sexual intercourse with a guy at age 15?
"Well I don't really assume she starting have sexual activities at age 15, maybe younger than that, what has become of Singaporean teenage girls? Being boastful about their indecent acts?" the contributor said.
In Singapore, it is against the law for anyone to have sex with those under the age of 16. If a girl under the age of 14 is involved, the crime is treated as statutory rape.
The contributor also criticised the girl's friends and parents for encouraging her to take care of the baby and herself.
"Teenagers and her friends are encouraging her to take care of the baby herself and her husband. I don't think that this good, what she really needs is a wake-up call to stop being so childish and mature up."
"What are parents thinking nowadays? Allowing their daughter marry at age 15? The law should step in for this," she said.

Thursday, December 1, 2011

Woman given 'chipmunk' cheeks by fake butt-boosting doctor


Another victim of the 'doctor' who injected cement into the buttocks of a Florida woman has come forward, revealing a horrifically disfigured face with chipmunk-like hard lumps in her cheeks.

Rajee Narinesingh, 48, told the press that Oneal Ron Morris, 30, had identified herself as a doctor and had injected a toxic mixture of cement and tyre sealant into her face, CBS Miami News reported.
Ms Narinesingh, who similar to Morris, was born a man but identifies as a woman, also suffers from a misshapen chin and bloated upper lip after the backroom beauty treatment went wrong.
She told reporters that she had heard of Morris by word of mouth in the transgender community.
She said as a transgender person, she was desperate to want to match her outside with her inside identity, and was willing to take the risk to undergo an illegal procedure for a low price.
Ms Narinesingh said she did not have enough money to pay a proper certified plastic surgeon to aesthetically enhance her face.
Morris was arrested earlier this month for injecting the same toxic cocktail of chemicals into a woman who wanted a bigger bottom, including cement, tyre sealant, superglue and mineral oil, then sealing the incision with superglue.

"Wolf dad" says hitting his kids got them into top college

BEIJING - The list of rules in Xiao Baiyou's house is endless: No Coca Cola while surfing the Internet, no air conditioner even in the summer, no pocket money, and definitely no socializing or extra curricular activities.
His four children are not even allowed to open his refrigerator without getting permission.
The punishment for rule-breaking is more often than not a whack with a rattan cane.
"A father is like a general, and there are rules to abide by and punishment to shoulder if they are broken," said the 47-year-old.
"Nowadays Chinese parents are too soft; they have abandoned the traditional Chinese way of good parenting."
Xiao, who was nicknamed "Wolf Dad" in a recently published memoir, even credits his stern parenting style for the fact that three of his offspring now attend Peking University, one of China's most prestigious educational institutions.
According to Xiao's philosophy, children under 18 are like animals and cannot distinguish right from wrong.
"Only through brutal means can they be taught," he said when China Daily caught up with him at one of his Beijing homes this week.
He said his eldest son, Xiao Yao, 21, received most of the canings that were dished out - and each time his three sisters were told to stand and watch.
"The eldest should take the lead," he added in his usual booming voice.

Mahakama yawaachia huru Muro, wenzake


MAHAKAMA jijini Dar es Salaam, imewaachia huru aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro na wenzake Edmund Kapama na Deogratius Mgasa, baada ya kuonekana kuwa hawana hatia katika mashtaka matatu yaliyokuwa yakiwakabili, likiwamo la kuomba rushwa ya Sh 10 milioni. 
Katika kesi hiyo ilikuwa inadaiwa kuwa Januari 29 mwaka jana, Muro na wenzake walitenda  makosa ya  kula njama, kushawishi kupewa rushwa ya Sh 10 milioni kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage na kujitambulisha kuwa ni maofisa wa Takukuru.

Hukumu iliyowaachia huyu washtakiwa hao, ilisomwa jana saa 3:15 asubuhi na Hakimu Mkazi Frank Moshi  wa Mahakama ya Kisutu.

Hakimu huyo alisema mahakama imewaachia huru washtakiwa  baada ya upande wa mashtaka, kushindwa kuyathibitisha makosa pasipo kuacha shaka.  Katika shtaka la kula njama, Hakimu Moshi alisema  baada ya mahakama kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka, iliwaona washtakiwa  kuwa wana kesi ya kujibu na kuwataka kuwasilisha utetezi wao . 
Alisema hata hivyo baada ya kupitia ushahidi na utetezi uliotolewa na washtakiwa pamoja na ule wa shahidi wao mmoja (dereva wa Muro) katika shtaka la kula njama, mahakama imewaachia huru washtakiwa wote.

 ”Mahakama imewaachia huru washtakiwa katika shtaka la kula njama kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa  kuithibitishia mahakama kama kweli washtakiwa walikutana na Wage na kufanya mawasiliano kupitia simu ya mkonon,” alisema hakimu Moshi.  Alisema mahakama imeona kuwa ushahidi wa nakala za picha za CCTV za hoteli ya Sea Cliff, zilizowasilishwa  na upande wa mashtaka zikionyesha watu watatu, sura zao zilikuwa hazionekani, jambo linalofanya ushahidi huo kuwa na upungufu.

Hakimu huyo alisema ili  watu waweze kutenda kosa la kula njama lazima wawe wanafahamika na kwamba  hakuna ushahidi mwingine wowote  unaonyesha kuwa kweli washtakiwa hao walitenda kosa hilo.   Alisema upande wa mashtaka ulishindwa hata kumuita dereva wa Wage  ili aweze kuthibitisha kama kweli Wage na Muro waliwahi kuwa na mawasiliano au  kukutana katika Mgahawa wa Calfonia .

Alisema upande wa mashtaka pia ulishindwa hata kwenda kwenye makampuni ya simu ili kupata nakala za ujumbe mfupi wa simu (sms) waliokuwa wakitumiana Wage na Muro.

Alisema kitendo hicho kinaifanya mahakama isiamini kama kulikuwa na kosa la kula njama.  “Pamoja na kutokuwepo  kwa ushahidi wa mawasiliano pia upande wa mashtaka ulitakiwa upeleke mahakamani hati ya gwaride la utambuzi  ili kuithibitishia mahakama kama washtakiwa waliwahi kutambuliwa lakini hilo haliufanyika,”alisema hakimu Moshi.
Katika shtaka la kuomba rushwa, hakimu Moshi alisema  mahakama haijaonyeshwa  ushahidi  wa kuthibitisha kuwa washtakiwa walipokea rushwa ya Sh 1 milioni  kutoka kwa Wage  kama kitangulizi  cha rushwa waliyoiitaji ya Sh10 milioni.

Alisema mahakama ilitegemea kuwa kungekuwa na ushahidi wa mawasiliano au wa kuona ili kuonyesha uhalisia na kwamba eneo la Hoteli ya Sea Cliff,.

Aliongeza kuwa washtakiwa  Kapama na Mgasa walikamatwa katika maeneo tofauti tofauti, jambo liliosababisha mahakama kuwaachia huru hasa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka hilo.  Kuhusu shtaka  la kujitambulisha kuwa ni maofisa wa Takukuru, linalokuwa likiwakabili Kapama na Mgasa, Hakimu Moshi alisema kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na vielelezo, hakuna ushahidi ulioonyesha kuwa Wage aliwatambua washtakiwa hao katika gwaride la utambuzi. 
Alisema   vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani na upande wa mashtaka vinaonyesha kuwa mshtakiwa Mgasa alikiri kujitambulisha kuwa ni wafanyakazi wa TBC wakati katika maelezo ya mashahidi, inadaiwa kuwa walijitambulisha kuwa ni maofisa wa Takukuru.

Alisema kwa msingi huo mahakama inawaachia huru washtakiwa hao kuwa shtaka hilo linajikanganya.
“Washtakiwa wote wameachiwa huru  hata hivyo mahakama hii inazingatia kuwa kuna vielelezo kama risiti, pingu na bastola ambavyo havikuwa na mgogoro  hivyo virejeshwe kwa Muro. Na  kwa Yule  ambaye hajaridhika, haki ya kukata rufaa iko wazi,” alisema hakimu Moshi.

Muro alipanda kizimbani Agosti 18 mwaka huu ambapo alijitetea na kuiomba mahakama  imuone kuwa hana hatia, akidai kuwa kesi inayomkabili ni ya kubambikiziwa na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi.

Kesi hiyo ilipata hakimu mpya Frank Moshi Mei 2 mwaka huu  baada ya  Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe  kuhamishiwa katika Mahakama Kuu.Machi 8 mwaka huu hakimu huyo aliwaona washtakiwa hao kuwa wana kesi ya kujibu.Kwa kipindi chote hicho cha kusikilizwa kwa kesi hiyo washtakiwa wote walikuwa nje kwa dhamana kwa mujibu wa sheria.
Yaliyojiri katika kesi
Muro aingia matatani Dar
Januari 31 mwaka jana, siku kadhaa baada ya Muro kutoa habari zilizoanika rushwa zinazofanywa na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, mwandishi huyo aliingia matatani kwa kukamatwa aidaiwa  kuomba na kupokea rushwa.

Baada ya kukamatwa alishikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Muro, ambaye aliwahi kushinda tuzo ya Mwanahabari Bora wa mwaka 2009 kufuatia habari yake ya rushwa inayofanywa na askari wa usalama barabarani, alikumbwa na mkasa huo saa 6:00 jijini Dar es Salaam.

Alikamatwa wakati akiwa katika Hoteli ya Sea Cliff.
Taarifa za awali zilisema Muro alikamatwa baada ya kuwekewa mtego na polisi kufuatia taarifa zilizokuwa zimetolewa na  mfanyabiashara mmoja, ambaye jina halijawekwa bayana kuwa mwandishi huyo alikuwa anadai rushwa ya Sh10 milioni.

Apekuliwa, akutwa na Pingu
Baada ya kukamatwa, polisi walilipekuwa gari la alilokuwa akilitumia na kukuta pingu pamoja na bastola.Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova, alisema baada ya kulifanyia upekuzi gari la Muro, polisi walikuta pingu na bastola na baadaye walimwamuru mwandishi huyo awapelekee stakabadhi zinazoonyesha kuwa alinunua pingu hizo kwa njia halali.


Muro apandishwa kizimbani
Februari 5 mwaka jana Muro alipandishwa kizimbani akishtakiwa kwa mashtaka ya kula njama na kuomba rushwa ya Sh10 milioni.

Alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Alipandishwa kizimbani akiwa na wenzake wawili  waliokuwa wakidaiwa uwa alishirikiana nao katika kutenda kosa hilo. Watu hao walisomewa mashtaka matatu.Washtakiwa walifikishwa mahakamani wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamevalia nguo za kiraia.

Kesi yaanza kusikilizwa
Kesi dhidi ya Muro na wenzake wawili ilianza kusikilizwa Juni 24 mwaka jana katika hatua ya awali.Hatua hiyo ilikuja baada ya  kukamilika kwa upelelezi wa kesi uliokuwa umekwama kwa muda mrefu.

Wakili wa Serikali, Martha Misonge, alisema mbele ya Hakimu Gabriel Milumbe siku hiyo,  ilikuwa ni ya  kusomewa washtaiwa maelezo ya awali.Hata hivyo  aliomba  wasomewe siku iliyofuatia kwa sababu upande wa mashtaka haukuwa tayari.

Katika hatua hiyo washtakiwa walitakiwa kueleza mambo wanayokubaliana nayo na yale wasiyokubaliana nayo.

Muro alidai kusomea jeshi Marekani, Afrika Kusini
Juni 16 mwaka jana, upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa  Muro alijinadi kuwa ni askari wa JWTZ mwenye cheo cha Kapteni  ambaye alipata mafunzo yake katika nchi za  Marekani, Uingereza na Afrika Kusini.

Maelezo hayo yalitolewa na wakili wa serikali, Boniface Stanslau mbele ya Hakimu Gabriel Mirumbe.
Ilidaiwa kuwa Muro alimweleza Michael Karoli aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuwa  kwa  mafunzo hayo alikuwa na uwezo wa kumweka chini ya ulinzi na kwamba alimuonyesha pingu na bastola kama vifaa vyake vya kazi.

Korti yaelezwa njama za kumkandamiza Muro
 Agosti 24 mwaka jana, mshtakiwa Deogratias Mgasa alidai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Mkumbo na wenzake walimlazimisha  aandike maelezo ya kumkandamiza Muro na kwamba kama angekataa wangembambikia kesi ya mauaji.

Mgasa aliyasema hayo  wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi, Gabriel Mirumbe.

Akitoa ushahidi wake,Mgasa alidai kuwa Februari 3 mwaka jana, alikubali kuandika maelezo yanayomkandamiza Muro, baada ya kulazimishwa na Mkumbo ambao walimwambia kuwa asipofanya hivyo watampa kesi nyingine ikiwamo ya mauaji.

Mahakama yapokea mkanda wa video

Novemba 13 mwaka jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, ilipokea nakala za picha zilizotolewa katika mtandao wa CCTV Camera ya Hoteli ya Sea Cliff, kama moja ya  vielelezo vya ushahidi  katika  kesi ya Muro na wenzake wawili.

Nakala hizo za picha , zinawaonyesha washtakiwa Muro , Deogratias Mgasa na aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage Karoli, ambaye inadaiwa walimuomba rushwa,wakiwa katika eneo la Hoteli ya Sea Cliff.


Shahidi adai Muro alinunua pingu duka la JWTZ

Januria 25 mwaka huu,  shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, Inspekta wa Polisi Anthony Mwita (45), aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa Muro aliwahi kumkabidhi stakabadhi ya pingu aliyoinunua katika duka la JWTZ, Upanga, jijini Dar es Salaam.

Mwita alitoa madai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe alipokuwa akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo.

Pingu za Muro zawasilishwa kortini   
 Siku ya Januari 26 mwaka huu, pingu alizokutwa nazo Muro ziliwasilishwa katika Mahakamani ya Kisutu kama sehemu ya ushahidi.Ilidaiwa kuwa pingu hizo zilikutwa ndani ya gari la Muro wakati akikaguliwa na Inspekta wa Polisi.

Madai hayo yalitolewa na Mrakibu  Mwandamizi wa Polisi, Duwan Nyanda (49), mbele ya Hakimu Mkazi Mirumbe, wakati akitoa ushahidi wake.


“Wage aliniambia kuwa pingu hizi zilitumiwa  na Muro kumfunga  wakati anamtishia na kumuomba rushwa,”alidai shahidi huyo wa sita wa upande wa mashtaka.

Muro na wenzake wana kesi ya kujibu
Machi 8 mwaka huu, Muro na wenzake walipatikana na kesi ya kujibu katika  mashtaka matatu yaliyokuwa yakiwakabili likiwamo la kuomba rushwa ya Sh 10 milioni kutoka kwa Kalori.

Mashtaka mengine ni ya kula njama  na kujitambulisha kuwa ni maofisa wa serikali.

Uamuzi huo, ulitolewa na Hakimu Mkazi Mirumbe baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Boniface Stanslaus kufunga ushahidi wa upande wa mashtaka.


Muro amlipua Masha
Agosti 18 mwaka huu, Muro aieleza mahakama kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alimtambia kuwa hatochomoka katika sakata hilo.

Muro alieleza hayo alipoanza kujitetea kwa mara ya kwanza dhidi ya tuhuma ziizokua zikimkabili.

Katika utetezi wake uliodumu kwa saa tatu akiongozwa na mawakili wake, Majura Magafu na Richard Rweyongeza, Muro alidai kwamba Masha  alisema mwisho wa kesi hiyo unampeleka (Muro) kaburini.

Chadema: Rais ametuuza


YASUSIA MCHAKATO WA KATIBA ALIOSAINI JK, CUF NAO WAALIKWA IKULU
Patricia Kimelemeta
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011, kimekiuka makubaliano yao, hivyo kimeamua kususia mchakato mzima wa kuratibu maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya kwa kutumia sheria hiyo.Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa hatua hiyo imefikiwa ili kuonyesha kutoridhishwa na namna kiongozi huyo wa nchi, alivyowachezea akili. 
"Kitendo cha Rais Kikwete kuusaini muswada huo bila ya kuupitia ni kinyume na makubaliano, jambo ambalo linatufanya tususie mchakato mzima wa kuuratibu maoni ya kwa ajili ya Katiba Mpya kupitia sheria ailiyoisaini,"alisema Mnyika na kuendelea:
“Tumeamua kujitoa kwenye mchakato mzima wa kuratibu Marekebisho ya Muswada wa Sheria ya Katiba kutokana na Rais kukiuka makubaliano yetu Ikulu yaliyomtaka aupitie kwanza kabla ya kuusaini.”  Mnyika aliendelea kueleza kuwa Chadema iliwasilisha waraka wa mapendekezo sita kwa Rais ikiwa ni pamoja na kumtaka asiusaini muswada huo kutokana na wananchi kutoshirikishwa ipasavyo kwenye mchakato wa ukusanyaji wa maoni.

 Alisema mapendekezo mengine ni uundaji wa tume huru, upatikanaji wa uwakilishi kutoka pande zote mbili za Muungano; Zanzibar na Bara ili kutoa fursa ya kupata maoni yao katika marekebisho hayo.  "Suala la tatu ni uundaji wa Bunge la Katiba na kupunguza mamlaka ya Rais na jambo la nne ni nafasi ya Zanzibar katika Muungano pamoja na mfumo mzima wa uwakilishi wa pamoja katika muundo wa Bunge la Katiba."
Mnyika alisema kutokana na hali hiyo iliyojitokeza ya Rais kutowasikiliza, watawasilisha waraka huo waliompa, kwa wananchi ili nao wausome na kutoa maoni yao.

Alisema katika kutekeleza mkakati huo, hawatafanya maandamano yeyote, isipokuwa watatoa elimu sahihi kwa wananchi juu ya Katiba wanayopaswa kuwa nayo.

 “Nia yetu ni mzuri, lengo ni kuboresha upatikanaji wa Katiba iwe bora na itakayoweza kutoa nafasi ya ushiriki wa pande zote. Lakini kinachofanyika sasa ni kinyume. Tumeamua kuwarudishia wananchi wenyewe ili waweze kuamua kama tumekosea au la,”alieleza.  Tamko hilo la Chadema limekuja siku moja baada ya Rais Kikwete kutia saini muswada huo hivyo kuufanya kuwa sheria.

  Rais Kikwete alitia saini muswada huo ikiwa ni siku moja baada ya yeye na viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kukubaliana kwamba ipo haja ya kuendelea kuuboresha muswada ili ukidhi mahitaji ya kuaminiana na muafaka wa kitaifa.  Pia, walikubaliana yawepo mawasiliano na mashauriano ya mara kwa mara kati ya Serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo kwa lengo la kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa Katiba Mpya.

CUF nao wakubaliwa kukutana JK

 Katika hatua nyingine, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeomba kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili kujadili Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya Mwaka 2011, iliyotiwa saini juzi na mkuu huyo wa nchi.  Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa baada ya kupata ombi hilo, Rais Kikwete alikubali kukutana nao.

"Ofisi ya Rais, Ikulu, imepokea barua kutoka CUF kikiomba kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete," ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:  " Rais amekubali ombi hilo la CUF na ameelekeza maandalizi ya mkutano huo yafanyike mara moja." 

Wasomi, wanaharakati wapinga 
Wakati huo huo, wasomi, wanaharakati na wanasiasa wametoa maoni tofauti kuhusu hatua ya Rais Kikwete kusaini sheria hiyo, huku Jukwaa la Katiba likieleza kuwa litafanya maandamano nchi nzima, kupinga hatua hiyo.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba aliliambia Mwananchi jana kuwa hatua hiyo ya Rais, ni sawa na ‘maombolezo kwa taifa’.“Wananchi hawana uwezo wa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais, uwezo wao ni kufanya maandamano ya amani yasiyo na ukomo nchi nzima,”alisema Kibamba anayeongoza Jukwaa hilo lenye Asasi za Kiraia zaidi ya 180.

“Serikali hii siyo sikivu, inaandaa Katiba kwa maslahi yake. Sisi  tunatoa juma moja kwa polisi kukubali madai yetu ya kufanya maandamano vinginevyo uvumilivu basi,”alisema Kibamba.

Alisema kitendo cha Rais Kikwete kusaini muswada huo muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Chadema ni dharau kwa chama hicho na wananchi.

Bana asema Rais ametimiza wajibu

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk Benson Bana alisema Rais ametimiza wajibu wake katika kusaini muswada huo kuwa sheria. Alisema kabla ya wananchi kuanza kulaumu, wanatakiwa kusubiri kwanza Rais aunde tume hiyo ndipo watoe maoni yao.

“ Duniani kote Katiba haiwezi kutosheleza mahitaji ya kila mtu, ni lazima pande fulani zitailalamikia hata kama itakuwa inafaa kwa asilimia kubwa,”alisema Dk Bana.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema chama hicho kinasubiri kuiona Tume ya Katiba itakayoundwa na Rais.  “Tunaunga mkono Rais kusaini muswada huo, tunachosubiri ni kuiona tume hiyo ikikusanya maoni ya wananchi, wakichakachua maoni ndipo tutakapoingilia kati,”alisema Mtatiro. 

Monday, November 28, 2011

Msichana ajinyonga akibisha kupika chakula

MWANAFUNZI wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Mbezi Juu, Kinondoni mkoani Dar es Salaam, amejinyonga kwa kutumia kitenge baada ya kubishana na kaka yake kuhusu nani apike chakula cha mchana.

Mwanafunzi huyo wa kike mwenye amri wa miaka 11 (jina limehifadhiwa), alikutwa amejinyonga chumbani kwake juzi akiwa amejitundika kwa kutumia kitenge kilichofungwa katika nondo ya dirisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema jana kuwa msichana huyo kabla ya kuchukua uamuzi huo, alibishana na kaka yake mwenye umri wa miaka 12 (jina limehifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo.

Alisema inavyoonekana, msichana huyo alichukua uamuzi huo baada ya kugombana kuhusu nani apike chakula cha mchana kwa kuwa baada ya ugomvi, aliingia ndani ya chumba chake
na ndipo baadaye mwili wake ukakutwa ukining’inia.

Katika tukio lingine, mfanyabiashara Ahmed Mguni (27), mkazi wa Mbagala Charambe amekutwa juzi amekufa na mwili wake umelala kitandani bila jeraha lolote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema sababu ya kifo chake haijafahamika na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi huku mwili wake ukiwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema Polisi inamtafuta dereva
na gari lililomgonga fundi ujenzi aliyetambuliwa kwa jina moja la James (35) na kufa papo hapo.

Shilogile alisema fundi huyo aliyekuwa akitembea kwa miguu aligongwa na gari juzi asubuhi
katika eneo la Mvuti kwenye barabara ya kwenda Msongola.