Tuesday, January 3, 2012

Youssou N'dour atangaza kuwania urais


Mwanamuziki mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N'dour, ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.
Youssou N'dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia ni balozi wa shirika la umoja wa matataifa kuhusu maswala ya watoto (UNICEF).
Mwandishi wa BBC mjini Dakar, Thomas Fessy, anasema hatua ya bwana Youssou N'dour kutangaza kuwa atawania kiti cha urais, haijawashangaza wengi. Hii ni kufuatia tangazo alilotoa mwisho wa mwaka uliopita kuwa atajitosa katika ulingo wa kisiasa.
Katika hotuba iliyopeperushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki huyo amesema atapunguza matuzi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Senegal.

''kuwa rais ni kazi sio taaluma''

Youssou N'dour anakubali kuwa yeye sio msomi lakini anaelezea wadhifa wa rais kama ''kazi na sio taaluma''.
Youssou N'dour alikuwa rafiki wa karibu wa rais Abdoulaye Wade, lakini baada ya Wade kutangaza nia ya kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu, aligeuka na kuwa mpinzani wake mkuu.
Lakini haitakuwa kazi rahisi kwa Bw. Youssou Ndour kuwabadili maelfu ya wafuasi wake wa muziki kumpigia kura.
Aidha, Youssou N'dour amewahi kuwashutumu viongozi wa nchi za Afrika kuhusu jinsi walivyoshughulikia janga la njaa nchini Somalia.

Bunge halijamalizana na Luhanjo, Jairo


Fredy Azzah
LICHA ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo kung’atuka kwenye nafasi zao, Bunge limesema linasubiri ripoti ya utekelezaji wa maagizo yake juu ya kuwajibishwa kwao.
Msimamo huo wa Bunge umekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Balozi Ombeni Sefue kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Eliakim Maswi, ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Jairo, kushika nafasi hiyo rasmi. Luhanjo alistaafu kwa mujibu wa sheria Desemba 31 mwaka jana.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema juzi kwamba pamoja na hatua hiyo ya Serikali, bado Bunge linasubiri utekelezaji wa maazimio yake ambayo yanapaswa kuwasilishwa bungeni na Serikali katika Mkutano wake wa mwezi ujao.
“Kamati teule ilisoma ripoti yake bungeni na Serikali ikaomba ipewe muda wa kutekeleza maazimio ya Bunge. Tunasubiri katika Bunge la Februari pamoja na mambo mengine, Serikali isome utekelezaji wake juu ya maazimio ya Bunge,” alisema Ndugai.
Hii si mara ya kwanza kwa Serikali kupiga danadana maazimio ya Bunge. Wakati wa sakata la Richmond, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu wa Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi, walishindwa kuwajibishwa kama Bunge lilivyoazimia hadi walipostaafu.
Pia hadi sasa, Serikali haijatekeleza azimio la Bunge kuhusu Richmond lililotaka mamlaka ya juu kumwajibisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah.
Alipoulizwa Ndugai endapo kustaafu kwa Luhanjo na kuondoka kwa Jairo katika nafasi zao kama hakutaathiri utekelezaji wa maazimio ya Bunge kama ilivyokuwa kwa Richmond, alijibu: “Sitaki kuzungumza chochote juu ya hilo, lakini siku zote mtu muungwana huwa anakuwa na subira. Tusubiri muda tuliopeana na Serikali uishe na sasa hata hayo maswali nitaweza kuyajibu.”
Lissu: Tunasubiri ripoti
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu, alisema kambi hiyo haitafumbia macho hali yoyote itakayoonyesha nia ya kutaka kutoyatekeleza maazimio ya Bunge.“Tunasubiri wailete hiyo ripoti yao bungeni, wakija na maelezo ya ubabaishaji sisi kambi ya upinzani tutapambana nao,” alisema.
Alisema Serikali inafanya siasa katika jambo hili na inataka kuwaamisha wananchi kwamba viongozi hao wameondoka kwenye nyadhifa zao katika utaratibu wa kawaida.“Ukweli ni kuwa hawa watu wameondoka katika nafasi zao kwa aibu wakiwa na kashfa ripoti ya Bunge inaonyesha wazi hilo,” alisema Lisu.
Hata hivyo, wiki iliyopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe alisema Serikali itawasilisha utekelezaji wa maazimio ya Bunge katika Mkutano wa Februari kama ilivyoahidi.

Sakata lilivyokuwa
Novemba 19, mwaka jana Kamati Teule ya Bunge, ilipendekeza Serikali imchukulie hatua za kinidhamu Jairo kwa matumizi mabaya ya madaraka, kukusanya na kutumia fedha za Serikali kinyume cha sheria.
Kamati hiyo, iliundwa na Bunge kwa ajili ya kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini, kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti ya 2011/12, bungeni.
Pamoja na Jairo pia Kamati ilipendekeza Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na watumishi wote wa wizara hiyo, waliotajwa kwenye taarifa hiyo, nao wawajibishwe na hasa Ngeleja, kwa kuwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Baraza la Mawaziri, ndiye Msimamizi Mkuu wa Wizara.
Kwa upande wa Luhanjo, Kamati hiyo ilielezea kusikitishwa kwake na kitendo chake cha kutoa kwenye vyombo vya habari taarifa za kumsafisha Jairo kabla ya kuifikisha kwanza ripoti yake bungeni, kwa kuwa huko ndiko hoja ilikoanzia.
Ilisema Katibu Mkuu Kiongozi aliamua kwa makusudi kumsafisha Jairo kwa kuficha ukweli na kutangaza kuwa hakuwa na kosa la kinidhamu, kitendo ambacho kimeupotosha umma.
Kamati hiyo iliundwa baada ya Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), kuibua hoja kwamba Jairo alichangisha takriban Sh bilioni moja kutoka taasisi zilizo chini ya wizara yake kwa ajili ya bajeti bungeni huku akiwa na ushahidi wa barua.

Magufuli atakiwa kuomba radhi


WABUNGE wa Mkoa wa Dar es Salaam wamemjia juu Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa
kupandisha nauli ya kivuko cha mv Magogoni na kumtaka awaombe radhi wakazi wa Kigamboni kwa kauli aliyoitoa kwao.

Wakizungumza jana katika ofisi ya Mbunge wa Ilala iliyoko Boma, Dar es Salaam, wabunge hao walisema kitendo cha Magufuli kutangaza ongezeko la nauli ya kivuko hicho kwa asilimia 100
bila kushirikisha wananchi, hakina tofauti na udikteta.

Katibu wa Umoja wa Wabunge wa Dar es Salaam, John Mnyika wa Ubungo – Chadema, alisema uamuzi wa wizara hiyo kupandisha nauli hiyo, umepokewa kwa mshituko na wabunge na wananchi wa Dar es Salaam na hivyo waliitaka Serikali kutathimini upya uamuzi huo.

Alisema jambo lolote linalotakiwa kufanywa na Serikali wananchi wanapaswa kufahamishwa, na si Wizara ikurupuke na kupandisha nauli bila wananchi kutaarifiwa, suala alilodai kuwa ni ubabe kufikia uamuzi.

“Anachokifanya Magufuli ni ukiukaji wa misingi ya utawala bora, yeye akiwa kiongozi wa wizara kwanza alipaswa kushirikisha wananchi katika kutoa uamuzi wa jambo hilo ili nao watoe mchango wao wa mawazo,” alisema Mnyika.

Alisema hata kama kiongozi huyo anajitetea kuwa wizara ilitoa tangazo katika Gazeti la Serikali, kuhusu kupandishwa kwa nauli hiyo, wananchi wengi hawapati fursa ya kuliona wala kulisoma gazeti hilo, jambo alilosema kuwa lisingeweza kufikia wote.

Alisema kilichopaswa kufanywa na wizara, ni kuangalia kwanza namna ambavyo wangeweza kudhibiti mapato kutokana na ufujaji uliopo katika kivuko hicho, badala ya kukimbilia kupandisha bei.

Mnyika alikwenda mbali na kudai kuwa kauli ya Magufuli kuwataka wakazi wa Kigamboni
kupiga mbizi ili kuvuka eneo la bahari, kuwa ni sawa na matusi, hivyo anapaswa kuhakikisha kuwa anawaomba radhi wananchi hao kwa madai kuwa amewadhalilisha.

Alisema kiongozi anayepewa dhamana kwa ajili ya wananchi, anapaswa kulinda maslahi ya wananchi wake.

Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile (CCM), mbali na kudai kushangazwa kauli hiyo ya
Magufuli, alisema hana tatizo na nauli kupanda, isipokuwa mfumo uliotumika kufikia hatua hiyo.

Alisema inashangaza kuona wananchi wanazidi kuongezewa mzigo wa nauli hizo, wakati tayari
mzigo wa kupanda kwa gharama za maisha unawakabili na kudidimiza Taifa kiuchumi.

Kwa pamoja, wabunge hao waliitaka Serikali kushughulikia upungufu uliojitokeza na kama hilo
litashindikana, watapambana na wizara hiyo katika mkutano ujao wa Bunge Dodoma.

Wabunge wengine waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa Umoja huo, Abbas Mtemvu
(Temeke), Mussa Azzan Zungu (Ilala) na wa viti maalumu, Mariamu Kisanji, Zarina Madabida na Philipa Mtulano.

Wabunge ambao hawakuhudhuria ni Makongoro Mahanga (Segerea), Eugen Mwaiposa
(Ukonga) na Halima Mdee (Kawe), Iddi Azzan (Kinondoni).

Juzi Dk Magufuli aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam, kuwa Serikali imeamua kupandisha nauli hiyo kutoka kati ya Sh 50 na Sh 100 hadi Sh 200 kwa safari moja ya kivuko hicho, kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu.

Alisema nauli iliyokuwapo ni ya tangu mwaka 1997 huku nauli za vivuko vingine zaidi ya 30 nchini imekuwa ikipanda mara kwa mara.

Magufuli alisema kivuko cha Magogoni kimekuwa kikitoza nauli za chini ikilinganishwa na cha Chato kinachotoza Sh 300, Pangani Sh Sh 200, Kisorya Sh 300, Lugolola Sh 500, Nyakarilo Sh 300, Chato-Bukombo Sh 2,000, Kirambo Sh 500 na Utete Sh 300; huku wanafunzi wakisafiri bure.

Sambamba na upandishaji nauli kwa watu, pia nauli ya magari imepanda ambapo madogo yanatozwa Sh 800 na Sh 1,500, pick-up Sh 1,000 na Sh 2,000 na yale yenye uzito wa kuanzia tani tatu na nusu Sh 5,000 hadi Sh 7,500.

Juhudi za Magufuli kupatikana azungumzie msimamo huo wa wabunge wenzake, zilishindikana
jana baada ya kufuatwa ofisini kwake na waandishi kuambiwa yuko mkutanoni na hata simu yake haikuwa inapatikana.

Flooding in southern Thailand traps tourists

Some Singaporeans and Malaysians who were in the Thai city of Hat Yai over the new year were stranded in their hotel rooms by flood waters that hit the city over the weekend.
Flooding in southern Thailand traps tourists

SINGAPORE - Some Singaporeans who were in the Thai city of Hat Yai over the new year were stranded in their hotels by flood waters that hit the city over the weekend.

Bangkok Post reported that tourists from Malaysia and Singapore were trapped because their tour buses that ply the Singapore-Hat Yai route could not use the road to Sadao, at the border with Malaysia.
Nine tour buses were believed to be affected, disrupting travel for hundreds of passengers.

One passenger said that the water level of the flood was about two feet high.
Those who managed to get out before the floods worsened had their journey home delayed as bus operators waited for the water to subside before travelling back to Singapore.

Wawili wafa maji sikukuu ya mwaka mpya

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime na kusema kuwa watu hao wamekufa maji baada ya kupigwa na wimbi zito na hadi sasa miili hiyo bado haijaonekana.

Aliwataja kuwa ni Emmanuel Mwanyika (23), mkazi wa Kibada ambaye alikufa fukwe iliyopo eneo la Sunrise Beach Kigamboni kwa kupigwa na wimbi zito kuzama na kunywa maji mengi akiwa na wenzake

Wa pili ni Asha Ibrahim (14), mkazi wa Kibugumo, ambaye alizama wakati akiogelea na wenzake katika eneo la Zabada Beach Kigamboni.

Kamanda Misime amesema miili hiyo bado haijapatikana na juhudi za kuisaka bado zinaendelea

Monday, January 2, 2012

JK aonywa


ASEMA ATAUNDA TUME YA KATIBA NDANI YA MIEZI MITATU
Elias Msuya
SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete imeonywa kwamba kama haitakuwa makini kusimamia vyema mchakato wa kuunda Katiba mpya na kudhibiti mfumuko wa bei katika mwaka huu wa 2012, nchi itayumba.Watu mbalimbali wakimo wasomi na viongozi wa dini, wameuelezea mwaka uliopita wa 2011 kuwa  ulijaa matatizo makubwa kisiasa na  kiuchumi na kwamba hali hiyo  ikiendelea mwaka huu, italeta maisha magumu zaidi kwa wananchi na hata  kuiyumbisha nchi.
Mwaka jana Watanzania walishuhudia matukio makubwa ya kisiasa likiwemo lile la kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya huku wabunge wakilumbana kwa hoja motomoto ndani ya Bunge na kwa upande wa pili , vyama vya siasa vikigubikwa na migogoro.Mwaka jana pia Watanzania wameshuhudia mdororo mkubwa wa uchumi huku mfumuko wa bei ukipanda katika miezi ya mwisho na kufikia asilimia 19, hali inayochangia kuongezeka kwa umasikini.Akizungumzia matukio ya kisiasa, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema kuwa mwaka 2011 umekwisha vibaya kutokana na kile alichokiita, mchakato wa katiba kupoteza mwelekeo.
“Ndani ya mwaka 2011, tulitarajia kuwa na mwanzo mzuri wa kupata Katiba mpya hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza azma hiyo na tulianza mchakato vizuri, lakini mwaka umeisha, tumepoteza kila kitu na hii ni hatari,” alisema Bashiru na kuongeza; “Watu walijitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kwenye midahalo, lakini Bunge limefanya haraka bila hata kuwashirikisha wananchi”.
Hata hivyo, Bashiru alisema bado hatujachelewa na kumshauri Rais Kikwete kutoendelea na mchakato hata kama amesha saini sheria  hiyo ya kuanzisha mchakato  wa Katiba. “Bado hatujachelewa, Rais asianze mchakato, asiteue Tume ya Katiba. Ajue kwamba amechaguliwa na wananchi, hata wabunge wamechaguliwa na wananchi, Tume ya Bunge ya Mambo ya Katiba irudi kwa wananchi kuwauliza wanataka nini,” alisema Bashiru.
Akizungumzia matukio ya kisiasa ya Afrika kwa mwaka 2011, Bashiru alisema vita ya kumwondoa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddaf imetoa somo kwa nchi za Afrika kwamba hazina uwezo wa kulinda rasilimali zake.
“Tukio la kuondolewa madarakani kwa Kanali Gaddaf  limetoa fundisho kwa nchi za Afrika kwamba hazina uwezo wa kulinda rasilimali zake. Nadhani kuna haja ya kuanza kuangalia upya misimamo ya kina Nyerere na Nkrumah,” alisema. Akizungumzia suala la kushuka kwa uchumi hasa kutokana na kuongezeka kwa mfumuko wa bei hadi kufikia asilimia 19 kutoka asilimia tano aliyoikuta Rais Kikwete,alipoingia madarakani mwaka 2005,  Bashiru alisema linatokana na kuukumbatia mfumo wa ubepari na siasa uchwara.
“Mfumuko wa bei umeongezeka na bado utaongezeka kwa sababu, tulidanganywa kukumbatia mfumo wa ubepari wa soko huria na siasa uchwara za kubinafsisha kila kitu tukakubali,” alisema Bashiru na kuongeza;“Miaka 26 tangu alipoondoka Mwalimu Julius Nyerere, tumekuwa na siasa uchwara, tunasubiri kila kitu kifanywe na watu wa nje, unategemea nini?” alihoji na kuongeza" Tukoelekea ni kubaya. Akitoa mtazamo wake kwa mwaka mpya wa 2012, Bashiru alipendekeza kuwepo mjadala wa kitaifa wa kubadilisha mfumo wa maisha kutoka katika ubepari uchwara uliopo ili kuwa na mustakabali wa kitaifa, badala ya kuongozwa na matukio.
“Nchi nyingine ipo mijadala rasmi ya mataifa yao. Lakini sisi hapa tunaongozwa na matukio, mara kujivua gamba, mara maandamano Arusha, mara uchaguzi Igunga, hadi mwaka unaisha hakuna tulichofanya zaidi ya kujadili matukio,” alisema Bashiru.
Twalibu
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora wa Afrika (APRM), Rehema Twalibu, alisema japo mwaka uliopita ulikuwa na mwamko mkubwa kutoka kwa wananchi, bado jitihada kubwa zinahitajika katika kuwashirikisha katika mijadala ya kitaifa. “Mwaka huu (2011) umekuwa na mwamko mkubwa kwa wananchi ambapo uelewa wa mambo ya siasa umeongezeka.
Hata hivyo, jitihada zaidi zinahitajika katika kuwashirikisha,” alisema Rehema. Akizungumzia Katiba mpya alisema japo Sheria ya imeshasainiwa na rais, bado wananchi wanahitaji kushirikishwa zaidi kuchangia maoni yao. Kuhusu uchumi, alisema kumekuwa na hali ngumu ya uchumi inayosababishwa na matumizi mabaya ya rasilimali zilizopo.“Bado hatujaweza kutumia rasilimali zetu ipasavyo. Tunazo rasilimali nyingi ambazo kama zitatumika vizuri, hatutakuwa na umasikini huu tulionao,” alisema Rehema.
Askofu Mokiwa
Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Dk Valentino Mokiwa aligusia matukio ya kijamii yaliyovuma mwaka 2011 hususan mafuriko yaliyolikumba jiji la Dar es Salaam Desemba mwaka jana. Alisema tukio hilo ni fundisho kwa taifa kutunza mazingira ili kukabiliana na tishio la mabadiliko ya tabia nchi,“Tusiitazame mvua hii kishetani, bali tumtazame Mungu aliyetupa mvua hiyo. Hicho ni kiashiria cha mabadiliko ya tabia nchi. Watu hawayatendei heshima mazingira na bado wanakimbilia kuishi bondeni, hili liwe fundisho kwa mwaka mpya” alisema Dk Mokiwa.
Katika tukio hilo, aliinyooshea kidole serikali akisema kuwa imezembea katika kuwatahadharisha wananchi wanaojenga mabondeni, “Kuna matatizo ya urasimu na uzembe katika idara za mipango miji zinazohusika na ugawaji wa radhi, ndiyo zinasababisha yote hjaya,” alisema.Akitathmini hali ya uchumi nchini, Dk Mokiwa alisema kuwa mwaka uliopita ulitawaliwa na ongezeko la mfumuko wa bei, pengo kubwa  kati ya walionacho na wasionacho na gharama za maisha kupanda.
“Hii ni changamoto kwa wachumi wetu, nchi yetu bado ni changa kiuchumi na bado nchi zilizoendelea zinaifanya kuwa jalala la bidhaa zao. Lazima tuwe na mikakati ya kuzalisha bidhaa zetu wenyewe. Tusiogope hata kuwakaribisha wawekezaji wenye uwezo kuja kuwekeza ili kuleta maendeleo,” alishauri.Kuhusu mwenendo wa Bunge kwa mwaka uliopita, alisema kuwa Bunge lilionyesha mifano mibaya kwa jamii kwakuwa na majibizano yasiyokuwa na sababu.
“Bunge lilionyesha picha ya mbaya, kulikuwa na majibizano yasiyo na msingi. Wabunge wajue kwamba bungeni ni mahali patakatifu, siyo mahali pa vurugu. Mikutano ya Bunge ichagie kuimarisha uchumi na maisha ya wananchi, lazima wabunge wawe makini wanapowawakilisha wananchi,” alisema Dk Mokiwa.
Sheikh Mattaka
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini, Sheikh Khamis Mattaka, alisema kuwa hali ya uchumi imekuwa mbaya kwasababu ya serikali kushindwa kutambua vipaumbele vya kiuchumi, “Uendeshaji wa serikali siyo mzuri, kuna kitu kinaitwa ‘Opportunity cost’, yaani kama unamahitaji mawili kwa wakati mmoja, kwa mfano unataka kununua soda Sh 500 na daftari sh 500, kipi bora? Leo serikali inapoona kuna mahitaji ya ‘ambulance’(gari la kubeba wagonjwa),  inakimbilia kununua magari ya kifahari.
Ndiyo maana kila mara taarifa za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaonyesha ubadhirifu,” alisema Sheikh Mattaka.Kuhusu suala la Katiba, alitetea sheria ya Katiba iliyosainiwa na Rais Kikwete  akisema kuwa wanaoipinga hawaiamini serikali, “Hatuwezi kujenga kama hatuaminiani, hawa wasomi na wanasiasa wanaoipinga sheria hiyo hawaiamini serikali. Mbona sheria nyingi tu zimetungwa hivyo hivyo?” alisema Mattaka.
JK Salamu za mwaka mpya
Katika salamu zake za mwaka mpya kwa taifa jana, Rais Kikwete alisema Tume ya Katiba itakuwa imekamilika ndani ya robo ya kwanza ya mwaka huu na itaanza kazi yake katika robo ya pili au ya tatu ya mwaka huu.

"Ni matarajio yangu kuwa ndani ya robo ya kwanza ya mwaka ujao uundaji wa Tume ya Katiba utakuwa umekamilika.  Katika robo ya pili au ya tatu ya mwaka 2012, Tume hiyo itaanza kazi yake ya kukusanya maoni," alisema.

 Aliwataka Watanzania wajiandae kushiriki kutoa maoni yao kwa Tume ya Katiba na kuwaonya kujiepusha kuzuia watu kutoa maoni yoa kwa uhuru hasa wale wenye manoni tofuati na serikali.

"Iwe ni mwiko kwa mtu yoyote au kikundi chochote kumzuia mtu au watu wowote kutumia haki yao hiyo.  Iwe ni mwiko pia kwa mtu, watu au taasisi yoyote kujaribu kuhodhi mijadala hiyo.  Ni vyema tukajua kuwa tunatengeneza Katiba ya watu wote na kwa maslahi yetu sote," alionya Rais Kikwete.

 Alisisitiza kwamba serikali yake haina nia ya kutengenezi katiba ya watu fulani wateule au kikundi fulani cha kisiasa au kijamii kwa maslahi yao na kusisitiza watu waachwe watoe maoni yao kwa uhuru.

Kuhusu malimbikizo ya posho za watumishi wa umma, Rais Kikwete alisema anashangaa kuona bado kuna watumishi wanaendelea kuidai serikali wakati alizuia watu kuhamishwa bila ya kulipwa posho zao.

"Bado ningependa kujua imekuwaje tena kuwe na malimbikizo makubwa kiasi hiki.  Mambo haya tulikwishaelewana kuhusu namna ya kuepuka malimbikizo.  Kulikoni?   Je, lini tabia hii ya kulimbikiza madeni itakoma?   Nataka majibu toka kwa wahusika," alihoji.

Kuhusu sensa, Rais Kikwete alisema maandalizi ya kufanyika kwa sensa hiyo Agosti mwaka huu yanaendelea vizuri na kwamba maelekezo yatandelewa kutolewa na wajibu wa kila mwananchi.

"Ninawaomba Watanzania wenzangu msikilize maelezo na maelekezo hayo.  Pia naomba nyote muhifadhi na kuikumbuka tarehe hiyo ili siku hiyo mtu asikose kuhesabiwa. Mwisho, naomba kila mmoja wetu awepo kuhesabiwa siku hiyo,"alisema

Magufuli achafua hali ya hewa Dar


BAADA YA KUWAAMBIA WAKAZI KIGAMBONI WAKISHINDWA KULIPA NAULI MPYA ZA VIVUKO WAPIGE MBIZI
Ramadhan Semtawa
WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli amechafua hali ya hewa na kuingia kwenye mgogoro na wakazi wa Kigamboni, Dar es Salaam baada ya kuwaeleza kuwa ni lazima walipe nauli mpya za vivuko vya Mv Kigamboni na Alina na kama watashindwa, wapige mbizi baharini kuvuka.

Kauli hiyo ya Dk Magufuli imekuja siku mbili baada ya wizara hiyo kutangaza viwango vipya vya nauli mnamo Desemba 29, mwaka jana ambavyo vimepanda kwa asilimia 100 na vilianza kutumika jana Januari Mosi nchi nzima.

Baada ya kutangazwa kwa viwango hivyo vipya vya nauli, wakazi wengi wa Kigamboni walipinga kutokana na kile wanachosema hawakushirikishwa na ndipo jana asubuhi, Dk Magufuli alipoamua kufanya ziara ya ghafla katika vivuko hivyo na kusisitiza kwamba viwango hivyo lazima vilipwe.

Katika ziara hiyo, vyanzo vya kuaminika vilisema Dk  Magufuli alipofika eneo hilo la Kivukoni, alitoa msimamo huo na ndipo wananchi waliokuwa wakimsikiliza walipoanza kumzomea na kukatisha hotuba yake mara kwa mara.

Vyanzo hivyo viliongeza kwamba, kitendo hicho cha zomeazomea, kilimkera Dk Magufuli ambaye pamoja na mambo mengine, alisisitiza nauli hizo lazima zilipwe na mtu asiyetaka ni vyema akapiga mbizi kwa kuogelea kutoka Kigamboni hadi ng'ambo ya pili au apite Kongowe kuingia katika katikati ya jiji.

Msemaji: Waziri amechukizwa
Akizungumzia tukio hilo, Msemaji Mkuu wa wizara hiyo, Martin Ntemo alisema Waziri Magufuli hakufurahishwa na kitendo cha baadhi ya watu kumzomea wakati alipokuwa akizungumza... “Amechukizwa na baadhi ya watu kuzomea wakati alipokuwa akizungumza. Alichokuwa akisisitiza ni kwamba nauli mpya lazima ilipwe lakini wapo waliokuwa hawataki kuelewa wakawa wanapinga.”

Alisema kuna watu walikuwa wamepangwa kufanya mgomo kupinga nauli mpya kitendo ambacho pia kilimkera waziri alipokuwa kwenye ziara hiyo.

Magufuli na waandishi

Baada ya kuzomewa Kigamboni, Dk Magufuli alifanya mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kwamba, “Kuanzia Januari, Mosi, mwaka huu Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), imeongeza viwango vya nauli katika vivuko vyote vya Serikali nchini.”

Alisema kwa muda wa miaka 14 iliyopita Kivuko cha Kigamboni kimekuwa kikitoza nauli ya Sh100 kwa mtu mmoja, wakati vivuko vingine vyote nchini, vimepandisha nauli zaidi ya mara mbili tangu mwaka 1997 kuendana na gharama za uendeshaji.

“'Kwa mfano, Kivuko cha Pangani ambako umbali wa uvushaji hauzidi ule wa Magogoni kilikuwa kinatoza Sh 200 na hali ya uchumi kwa wananchi ni ya chini kuliko Dar es Salaam. Kivuko cha Kilombero kilikuwa kikitoza Sh200 ikilinganishwa na Sh100 zilizokuwa zikitozwa hapa Magogoni.”

Dk Magufuli alitaja sababu zilizochangia kupandisha nauli hizo kwamba ni pamoja na ongezeko la mishahara ya watumishi serikalini kwa zaidi ya asilimia 100, ongezeko alilosema la zaidi ya asilimia 400 la bei ya mafuta ya dizeli na mafuta ya kulainishia mitambo ambayo hutumika kuendeshea vivuko hivyo.

Alitaja sababu nyingine kwamba ni pamoja na: “Ongezeko la bei za vipuri na kodi zake linalowiana na kushuka kwa thamani ya shilingi na ongezeko la bei kwa jumla.”

Alisema upandishaji wa nauli hizo ulifanywa kwa kuzingatia taratibu za kisheria na hatimaye kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali toleo Na. 367 la Novemba 4, mwaka jana kwa mujibu wa sheria za uendeshaji wa vivuko vya Serikali.

“Sura 173 Kifungu cha 11(b), mwenye mamlaka ya kupanga nauli za vivuko vya Serikali ni Waziri mwenye dhamana na vivuko vya Serikali. Hata hivyo, kabla ya kufikia uamuzi huu, kumekuwa na jitihada za aina mbalimbali katika kuimarisha mapato ya vivuko. Machi, 2009, Wakala wa Ufundi na Umeme wakishirikiana na
Jeshi la Polisi pamoja na Askari kutoka Kikosi cha Wanamaji waliendesha zoezi la kudhibiti mapato ya Kivuko.”

Alisema hilo liliwahi kufanywa na na Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart mnamo Aprili 17 hadi 20, mwaka jana kwa makubaliano na Temesa. “Zoezi hilo liliendeshwa tena Septemba 16 hadi 20, 2010 na
Wizara kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi.”

Alisema Julai, 2011, Temesa iliamua kubadili wakata tiketi na kuajiri wengine akisisitiza kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kupambana na matukio ya watumishi wasio waaminifu. Hatua nyingine ni ile ya Temesa  kuondoa askari wa kuajiriwa na badala yake kuingia mikataba na kampuni za ulinzi.

“Kwa sasa katika Kivuko cha Magogoni, Kampuni ya ulinzi ya Suma JKT ndiyo inayotumika kufanya kazi hiyo,” alisema.

Alisema juhudi hizo zimesaidia kuongeza mapato kwa siku kutoka Sh5.5 milioni mwaka 2009 hadi Sh9 milioni kwa sasa katika Kivuko cha Magogoni na kusisitiza kwamba wizara itaendeleza hatua hizi kwa lengo la kubana uvujaji wa mapato na matumizi yasiyo ya lazima kwa vivuko vyote.

Magufuli alisema kwa utaratibu, watumiaji wote wa huduma za vivuko wanatakiwa walipie huduma hiyo na kuongeza: “Tunaomba utaratibu huu uzingatiwe isipokuwa kwa wanafunzi waliovaa sare za shule. Tunasisitiza watumiaji wa vivuko waheshimu sheria na taratibu zote za vivuko kwa ajili ya usalama wao na ufanisi wa huduma.”


Mbunge achukizwa

Kwa upande wake Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile alikiri kusikia maneno ya Magufuli ambayo hayakuwafurahisha wapiga kura wake na kuahidi kuendelea kufuatilia kujua undani hasa wa kauli hizo.

Dk Ndugulile alifafanua kwamba baada ya tangazo hilo la ongezeko la nauli, aliwasiliana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki na taarifa alizonazo ni kwamba nauli hizo zimesitishwa.

Alifafanua kwamba baada ya kuwasiliana na waziri mkuu, jibu alilopata jana saa 1: 00 usiku ni kwamba mpango huo wa kupandisha nauli umesitishwa hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.

Dk Ndugulile alisema sababu zilizomfanya yeye na wananchi kupinga nyongeza hiyo ya nauli ni Serikali kushindwa kueleza wazi vigezo vilivyotumika na kushindwa kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika. Alitoa mfano wa Bajaji ambao alisema ni usafiri wa wanyonge uliokuwa ukitozwa Sh300 lakini kwa viwango hivyo vipya, itavushwa kwa Sh1,300 huku baiskeli ya miguu mitatu inayotumiwa na wanyonge pia kuchukulia bidhaa kutoka Kariakoo ikiongezewa nauli kutoka Sh200 hadi Sh1,800 na gari ndogo sasa zinatakiwa kulipa Sh1,500 badala ya Sh800.

“Sasa angalia hivyo vigezo, utaona mwananchi wa kawaida amezidi kuumizwa. Leo hii tayari bei za bidhaa zinazoletwa Kigamboni kutoka sokoni kama Kariakoo kwa kutumia maguta zimepanda. Mtu mwenye gari anapadishiwa bei chini ya mwenye guta, vigezo gani hivi? Baada ya kuona hivyo, niliwasiliana na Waziri Mkuu Ijumaa (Desemba 30, mwaka jana) na jana Mkuu wa Mkoa akanipa jibu kwamba Waziri Mkuu kasema nauli hizo zisipandishwe kwanza. Kwa hiyo mimi na wananchi wangu tunajua hivyo,” alisema na kuongeza:

“Hili ni jambo la ajabu sana. Yaani Waziri Mkuu anasema hivi halafu waziri wake anafanya vingine! Uko wapi sasa utendaji kazi wa pamoja wa Serikali?”


Baadhi ya wananchi wamelaani kauli hiyo za Dk Magufuli wakisema haikupaswa kutolewa na waziri ambaye ana dhamana ya kuhakikisha matatizo ya wananchi yanatatuliwa. Mmoja wa wakazi wa Kigamboni aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Bwamkuu alisema: “Waziri anatoa kauli za kejeli namna hii! Ametusikitisha sana na kwa kweli tunamuomba Rais Jakaya Kikwete amchukulie hatua za kinidhamu.”

Pia wananchi hao wamemshutumu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Dk Hurbet Mrango na Temesa kwa kushindwa kuwashirikisha na pia kumshauri vibaya waziri katika jambo hilo.

"Katibu Mkuu ndiye mtendaji na Temesa wao ndiyo wakala lakini hawakumwambia kwamba wananchi hawakujua na hata mbunge wetu. Kwa hiyo hawa ni sehemu ya tatizo na hii si mara ya kwanza.”

Hamad kufukuzwa CUF

Hamad kufukuzwa CUF


Na Saed Kubenea - Imechapwa 28 December 2011

ALIYEJIAPIZA kumng’oa Maalim Seif Shariff Hamad ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), sasa kufukuzwa uanachama, imefahamika.
Hamad Rashid Mohammed, mbunge wa Wawi, kisiwani Pemba, ndiye amekuwa akisema anataka kuchukua nafasi ya katibu mkuu wa CUF kwa madai kwamba Maalim Seif ameshindwa uongozi, amedhoofisha chama na hana fikra mpya.
Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, taratibu za kumchukulia hatua Hamad pamoja na wenzake wanaopanga kumuengua Maalim Seif tayari zimeanza.
Hamad na wenzake wanaweza kuwa wameshafukuzwa kwenye chama hicho kabla ya 5 Februari mwaka kesho.
Habari zinasema maandalizi ya vikao vya kumfukuza Hamad na wenzake yalitarajiwa kuanza jana Jumanne (27 Desemba 2011), ambapo Hamad alitakiwa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Nidhamu na Maadili.
Hamad na wenzake wanasema tangu Maalim Seif ateuliwe kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), chama kimedhoofika hasa Tanzania Bara ambako kwa sasa CUF “kinaonekana kama tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM).”
Mawasiliano kati ya viongozi wakuu wa chama hicho ambayo yametawanywa jijini Dar es Salaam kwa wiki mbili sasa yanasema, Hamad hawezi kusalimika.
Mawasiliano hayo kati ya Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho taifa, katibu mkuu Maalim Seif, Julius Mtatiro, naibu katibu mkuu Tanzania Bara na Khamisi Khassani, mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CUF, yanaonyesha Hamad atafukuzwa wakati wowote kuanzia sasa na 5 Februari 2012.
Mbali na Hamad wengine wanaotajwa kuchukuliwa hatua au kufukuzwa, ni pamoja na mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, Khassani Doyo na mbunge wa zamani wa Micheweni, Pemba, Shoka Khamisi Juma.
Kwa mujibu wa mawasiliano hayo, tayari Maalim Seif ameagiza kuitwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya chama wale anaowaita, “Hamad na genge lake” ili wahojiwe.
Anasema mara baada ya kazi ya kuwahoji kukamilika, kamati ya maadili iwasilishe taarifa yake kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji Taifa (KUT) kinachotarajiwa kufanyika wakati wowote mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya kuchukua hatua.
Akiandika kwa njia ya imeili kwa Profesa Lipumba, 14 Desemba 2011, saa 10:04 asubuhi, Maalim Seif anasema, “Tayari nimeshauriana na Makamu (Makamu mwenyekiti wa CUF, Khamis Machano Alli) na tumeona kuna haja ya jamaa yako (Hamad Rashid) na genge lake kuitwa katika kamati ya nidhamu na maadili kuhojiwa.”
Maalim anasema tayari ushahidi wa kutosha umekusanywa na idara ya usalama dhidi ya Hamad, Doyo na Shoka na kwamba sharti Hamad afukuzwe ndani ya chama hicho.
Anasema, “KUT ichukue uamuzi mgumu wa kuwasimamisha uongozi vinara wao na wengine kupewa karipio,” anaeleza Maalim katika mawasiliano yake hayo na Profesa Lipumba.
Anasema, “KUT ifikishe taarifa yake katika kikao cha Februari 2012 mbele ya Baraza Kuu Taifa (BKUT) kwa uamuzi.” Anasema iwapo itaonekana kuna haja ya kuitishwa kwa mkutano wa dharula wa baraza kuu basi hilo lifanyike haraka iwezekanavyo.
Akisisitiza umuhimu wa Hamad Rashid na wenzake kufukuzwa ndani ya chama hicho, Maalim anasema amekubaliana na ushauri wa Profesa Lipumba wa kuwadhibiti kinidhamu viongozi hao.
Anasema wanachama walio wengi wa chama hicho “wanatudadisi kwa nini hatuchukui hatua?” Anasema, “Sasa ni kumuacha jamaa yako aendelee kufanya kazi aliyopewa na rafiki yake ya kukivuruga chama au chama kimvuruge yeye!”
Hata hivyo, Maalim Seif hajaeleza katika mawasiliano hayo, huyo anayeitwa “rafiki” wa Hamad Rashid aliyempa kazi ya kuivuruga CUF ni nani.
Bali MwanaHALISI limeona nyaraka iliyoandaliwa na idara ya usalama ya chama hicho, pamoja na baadhi ya mawasiliano kati ya Profesa Lipumba, Maalim Seif, Ismail Jussa, Juluis Mtatiro na Khamis Khassani, zikitaja waziri mkuu Mizengo Pinda na mahali pengine mbunge wa Monduli Edward Lowassa, kuwa ndiyo wanaompa nguvu Hamad kuvuruga CUF.
Akionekana kukerwa na tabia hiyo, Maalim anasema, “…leo jamaa yako (Hamad Rashid) kafikia hadi kukodi wahuni na wavuta bangi wanaokadiriwa kufikia 150 kuwahujumu BGs (kikosi cha ulinzi cha CUF)!”
Anasema, “Ikihitajika hata kikao cha dharura cha BKUT kiitishwe. Sisi tunahisi chama ki-act decisively, hasa dhidi ya jamaa yako. Yeye muono wetu tumfukuze kwenye chama na akiamua kwenda mahakamani na mahakama kutoa maamuzi ya kumpendelea yeye, mwache awe mbunge wa mahakama kama ilivyokuwa kwa akina Asha Ngede na Naila Majid Jidawi.”
“Ikishajulikana kuwa si mwanachama tena,” anasema Maalim, “atakuwa hana mashiko! Muache aende CCM (Chama Cha Mapinduzi) au CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo) akawe mgombea mwenza!”
Awali akiandika kwa Profesa Lipumba, Maalim Seif anasema, “Nimefurahi kwa mahojiano yako na DW (kituo cha redio na Tv cha Ujerumani cha Deutsche Welle) kuwa ukatibu mkuu hautafutwi kwa mbinu za kimafia.
Anasema tayari Mtatiro ametahadharisha jeshi la polisi mkoani Tabora juu ya Hamad Rashid na wenzake. Maalim anasema Mtatiro ameeleza mkuu wa polisi wa mkoa wa Tabora (RPC) na mkuu wa polisi wa wilaya ya Urambo kuwa wanaokwenda mkoani mwao kufanya mikutano ya hadhara ndio waliosababisha fujo jijini Dar es Salaam.
Barua ya Mtatiro ya 15 Desemba 2011 kwenda kwa mkuu wa polisi wa mkoa wa Tabora, inatuhumu viongozi wawili waandamizi wa chama hicho, Khassani Doyo na Amir Kirungi, kuzunguka wilaya zote nchini bila kuzijulisha mamlaka za chama zilizowekwa kikatiba na kuhamasisha wanachama wake wakihame chama chao.
Hata hivyo, mpango wa Maalim Seif kutaka kufukuza wenzake kwenye chama unapingwa na mjumbe wa baraza hilo, Abubakari Rakesh. Katika mawasiliano yake na Profesa Lipumba, 14 Novemba 2011, Rakesh anasema ni bora Profesa Lipumba kuingilia kati mgogoro kati ya Hamad Rashid na Maalim Seif kuliko kuendekeza utamaduni wa kufukuzana.
Anasema, “…mimi ni kijana wa chama hiki wa muda mrefu…Maalim Seif ni katibu wangu mkuu na Hamad Rashid ni kiongozi wa chama ninayemheshimu sana...nakushauri uingilie kati mgogoro huu ili viongozi hawa waondoe tofauti zao, vinginevyo chama kinaelekea kubaya.”
Rakesh alikuwa anamweleza Profesa Lipumba jinsi anavyosakamwa kutokana na mchango wake alioutoa kwenye mkutano wa baraza kuu uliofanyika kwenye hotel ya Lamada, ambapo pamoja na mambo mengine, aliungana na baadhi ya wajumbe waliokuwa wamemtuhumu Maalim Seif kushindwa kutenda kazi zake Tanzania Bara.
Awali Mtatiro akiandika kwa Profesa Lipumba anasema, Doyo na Kirungi wameelekea mkoani Tabora kwa ziara ya kila wilaya; msisitizo wao uko kwenye jimbo la Urambo Magharibi ambako Kirungi aligombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na 2010.
Anasema, “Wanakwenda huko kufanya kampeni ya wazi ya mikutano ya hadhara na vikao vya ndani kwa lengo kubwa la kutoa notisi ya siku 30 kwa katibu mkuu (Maalim Seif) na mwenyekiti (Profesa Lipumba) wajiuzulu, vinginevyo ngome ya chama yote ihamie CHADEMA.”
Mtatiro anasema, “Tuhuma zao ni kuwa mwenyekiti, japokuwa anatokea Tabora, ameshindwa kabisa kukijenga chama na kuwa amepoteza mwelekeo na eti hata katika uchaguzi wa Igunga mwenzie Mbowe (Freeman Mbowe, mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA) alipigana wiki kadhaa, lakini mwenyekiti wetu amekimbilia nje ya nchi.”
Pili, Mtatiro anasema, Doyo na Kirungi wanadai kuwa katibu mkuu amepoteza mwelekeo na anaua chama Bara, kwa hivyo lazima waondolewe kwa notisi.”
Katika mawasiliano mengine, Maalim anamtuhumu mbunge wa Lindi Mjini (CUF), Salum Barwani kutaka kuhujumu ziara yake mkoani Lindi. Anasema Baruani alishawishi baadhi ya watu wasijitokeze kwenye mapokezi yake kwenye uwanja wa ndege wa Lindi.
Anasema, “Nasikia alipingwa vikali na mkutano ulifanikiwa sana. Bila kumtaja, wakati najibu risala yao niliwaeleza kuwa hakuna mgogoro katika chama, isipokuwa kuna mtu na wenziwe wanachochea ionekane kuna mgogoro, na nikaeleza yaliyotokea….”
Iwapo Hamad atafukuzwa CUF, atakuwa mbunge wa pili wa upinzani kuachia ubunge ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja tangu kumalizika uchaguzi mkuu. Mwingine aliyefukuzwa uwanachama, ni mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR- Mageuzi, David Kafulila.
Kwa upande wake, Habibu Mnyaa, mbunge wa Mkanyageni, Pemba anamtuhumu Jussa kwa hatua yake ya kutoshiriki vikao vya Maalim Seif kisiwani Pemba.
Akiandika kwa Profesa Lipumba, Mnyaa anasema kikao hicho kilifanyika kwa usalama na amani na wajumbe walitoa michango yao kwa uwazi na kwa nia ya kujenga chama.
Hata hivyo, Mnyaa anasema, pamoja na kwamba makamu mwenyekiti wa chama chake alihudhuria mikutano iliyoitishwa na Maalim Seif, lakini Jussa hakuhudhuria mkutano hata mmoja ingawa alikuwa kisiwani Pemba wakati huo. Hakueleza sababu.
Lakini taarifa zinasema, baadhi ya viongozi wa CUF wanamtuhumu Jussa kumpotosha Maalim Seif kwa maslahi yake binafsi na kukivuruga chama cho kwa maslahi ya CCM.
Wanatoa mfano wa uchaguzi mkuu uliopita, ambapo Jussa alishindwa kukusanya kura kwenye baadhi ya majimbo na kisha kumshinikiza Maalim Seif kukubali matokeo ya urais hata kabla karatasi za kura hazijapatikana.
Mbunge wa Ole, Rajab Mohamed ambaye katika toleo lililopita alitajwa kama mmoja wa wanaomuunga mkono Hamad, amesema “hahusiki kwa namna yoyote na mpango huo.”
Ameliambia gazeti hili kwa njia ya simu juzi kuwa hawezi kushiriki na hajapata kushiriki kikao chochote chenye lengo la kuchafua chama. “Mimi ni mbunge mpya jimboni, ninaheshimu viongozi wangu ngazi zote hivyo siwezi kushiriki vikao haramu,” alisema.
Idara ya usalama ya CUF ndiyo iliyosambaza taarifa za kuwamo Rajabu kwenye mpango wa kumng’oa Maalim Seif.

Tanzania yatukanwa na kudhalilishwa


Huku akitumia, mtindo wa dharau na kebehi kubwa, Ehud Barak, ametolea mfano wa nchi zisizo na maana kuwa ni Tanzania, Mouritania na Tripolitania.
Wakati huo huo msimamizi wa ubalozi mdogo wa Tanzania nchini Israel, Bwana Altzanzy Noraal, kwa niaba ya serikali makini ya Tanzania, amepeleka barua rasmi ya malalamiko dhidi ya kebehi za Ehud Barak. Katika nakala za barua hiyo ambayo NIFAHAMISHE imebahatika kuona nakala yake, Mheshimiwa Altzanzy Noraal ameitaka serikali ya Israel ilaani vikali kauli za waziri Ehud.
Akiendelea kutoa malalamiko yake, Noraal, alimfafanulia waziri wa mambo ya nje wa Israel kuwa, Ehud ameamua kuidhalilisha Tanzania kwa kuifagilia Ulaya kiasi cha kuifanananisha Tanzania na nchi isiyokuwepo duniani, akimaanisha ile Tripolitania.
Noraal aliwahabarisha Waisrael kuwa Tanzania ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika Mashariki ikiwa na idadi ya watu kama milioni 46. Huku akiikumbusha Israel uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Israel kiuchumi na kiusalama. “Tanzania ni nchi muhimu sana wala haipaswi kupuuzwa” amesema Bw. Noraal. “Nitafurahi sana nitakapotembelea Tanzania nikiwa na mwakilishi wa Israel ili aone uzuri wa Tanzania nchi yenye eneo kubwa na mazingira halisia na watu wanaopenda amani” amesisitiza kwa kuwakejeli kisiasa kwa namna wanavyopenda vita na Warabu kila kukicha.

Tanesco ina mzigo wa gharama -JK

RAIS Jakaya Kikwete amesema Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linakabiliwa na mzigo mzito wa gharama za uzalishaji uliosababishwa na uzalishaji wa umeme kupitia mitambo ya mafuta.

Kutokana na gharama hizo, Rais Kikwete amesema juzi katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa
Taifa, kuwa shirika hilo limelazimika kupeleka maombi ya kuongezabei ya umeme kwa asilimia zaidi ya 100 kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

“Kwa sababu ya kutumia mafuta, umeme huu ni ghali na umekuwa mzigo mkubwa wa gharama kwa Tanesco. Kutokana na sababu hizo, Tanesco wamepeleka maombi Ewura ya kutaka kuongeza bei ya umeme,” alisema Rais.

Rais Kikwete alisema kwa muda mrefu shirika hilo limekuwa likijiendesha kwa kutegemea zaidi umeme wa mvua na hivyo kukabiliwa na wakati mgumu wakati wa ukame huku kukiwa na upungufu wa gesi na hivyo kulazimisha mitambo ya kampuni za kufua umeme kutumia mafuta.

“Lakini, kwa sababu ya kutumia mafuta, umeme huu ni ghali na umekuwa mzigo mkubwa wa
gharama kwa Tanesco. Kutokana na sababu hizo, Tanesco wamepeleka maombi Ewura ya kutaka kuongeza bei ya umeme,” alisema Rais Kikwete.

Historia ya gharama za Tanesco
Akifafanua historia ya gharama hizo, Rais Kikwete alikumbushia ukame ulioikumba nchi mwaka 2006 ambao alisema ulisababisha kupungua sana kwa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.

Kutokana na upungufu wa maji, Rais alikumbusha kuwa taifa liliingia katika tatizo kubwa la upungufu wa umeme na ili kukabiliana na tatizo hilo, Tanesco ikalazimika kuingia mikataba na kampuni za kuzalisha umeme kwa malipo.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kwa kuwa gesi inayozalishwa hivi sasa kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kufulia umeme iliyopo Ubungo haitoshelezi mahitaji ya taifa,
kampuni hizo zililazimika kutumia mitambo inayotumia mafuta.

Alisema kampuni hizo zilipata mitambo inayozalisha umeme kwa kutumia mafuta na tayari inazalisha umeme ndiyo maana mgawo sasa haupo lakini akatahadharisha kuwa umeme huo gharama yake ni kubwa na ndio iliyosababisha mzigo wa gharama kwa Tanesco.

Hali hiyo ilisababisha mwishoni mwa mwaka jana Tanesco kuomba kupandisha bei za umeme kwa wastani kutoka Sh 141 ya sasa kwa uniti hadi Sh 359 ifikapo Januari mwaka huu ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 155.

Tatizo la umeme kuwa historia
“Nilisema kuwa tutaanza juhudi za kuendeleza vyanzo vingine vya nishati hasa gesi asilia na makaa ya mawe mpaka tufikie mahali ambapo hata kama maji hayatoshi katika mabwawa ya vituo vya umeme, nchi haitakosa umeme,” alisema Rais Kikwete.

Alisema Serikali itaendelea kutekeleza uamuzi huo kwa busara na kwamba hadi sasa Serikali kupitia Tanesco imeshaongeza megawati 245 za umeme unatokana na gesi asilia.

Aidha alisema maombi ya Serikali kwa Serikali ya China ya kupata mkopo wa kujenga bomba la
kusafirisha gesi kutoka Mtwara na mtambo wa kuchakata gesi inayotoka Songo Songo tayari yamekubaliwa.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, baada ya kukubaliwa kwa maombi hayo, kwa sasa utekelezaji wake unatarajiwa kuchukua miezi 18 na gesi itakayoletwa inaweza kuzalisha mpaka Megawati 3,000 za umeme.

“Baada ya hapo kasi ya kuongeza umeme itakuwa kubwa zaidi na tatizo la upungufu wa umeme linaweza kuwa historia,” alisisitiza.