Wednesday, April 4, 2012
Mengi yaibuka ushindi wa Chadema Arumeru
SIOI SUMARI ALITOSWA NA VIGOGO WA CCM MKOA, WILAYA, WAFUASI 61 WA CHADEMA WATIWA MBARONI, WADAIWA KUVUNJA KIOO GARI LA KAMANDA WA POLISI
Waandishi wetu, Arumeru, Dar
MAMBO mengi zaidi yamezidi kuibuka kuhusu uchaguzi wa Arumeru Mashariki uliomalizika juzi, baada ya taarifa kusema kuwa aliyekuwa mgombea CCM, Sioi Sumari alitelekezwa na viongozi wa chama hicho Wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha wanaodaiwa hakuwa chaguo lao wakati wa kura za maoni.
Wakati Sioi akidaiwa kutelekezwa, shamrashamra za Chadema kusherehekea ushindi wa mgombea wao, Joshua Nassari juzi ziliingia dosari baada ya wafuasi wake 61 kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuvunja kioo cha gari la Mkuu wa Operesheji wa jeshi hilo, Isaya Mngulu.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini, mmoja wa wajumbe wa timu ya kampeni za Sioi anayetoka wilayani Arumeru alisema mfano dhahiri wa kutengwa kwa mgombea huyo ni siku ya kupigakura ambako hakuna kiongozi yeyote aliyehangaika kuzunguka vituoni kukagua.
Alisema hali ilikuwa mbaya zaidi ilipofika wakati wa kukusanya masanduku ya kura na matokeo kutoka vituoni kabla majumuisho yaliyofanyika katika ofisi ya mji mdogo wa USA-River, ambako hakukuwa na kiongozi yeyote aliyejitokeza kusimamia wala kushuhudia majumuisho hayo.
“Huwezi kuamini kuwa hakukuwa na kiongozi wala mwakilishi yeyote wa CCM kwenye chumba cha majumuisho ya kura hadi ilipofika Saa 7:00 usiku, ndipo mgombea mwenyewe alipoamua kwenda kushuhudia na kusimamia kura zake,” alisema mjumbe huyo ambaye ni kiongozi wa ngazi ya mkoa.
Mwandishi wa habari hizi aliyekesha kwenye kituo hicho cha majumuisho alimshuhudia Sioi akifika eneo hilo akiwa ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM), Benno Malisa pamoja na makada wengine watatu ambao hata hivyo, waliondoka baada ya dakika 40 na kumwacha mgombea huyo peke yake.
Sioi aliyekuwa akiwania kurithi kiti cha ubunge kilichokuwa kikishikiliwa na marehemu baba yake, Jeremia Sumari, alibaki ukumbini hapo akiwa ameketi viti vya nyuma hadi alipoondoka ukumbini Saa 10:30 alfajiri, huku mwenzake, Joshua Nassari wa Chadema waliyekuwa wakichuana vikali akiwa ameketi mbele akiwa amezungukwa na kundi kubwa la viongozi wa kitaifa na mawakala wake.
Nje ya ukumbi wa majumuisho, pia walikuwepo viongozi kadhaa wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe waliokuwa wameweka kambi hapo na kukesha hadi matokeo yalipotangazwa kesho yake Saa 12:30 asubuhi.
Mbali ya Mbowe, baadhi ya viongozi wengine wa Chadema walikuwapo ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mbunge wa Mbozi Mashariki, David Silinde na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche.
Licha ya kususwa na kutelekezwa kwenye mchakato wa majumuisho ya kura, inadaiwa kuwa Sioi pia hakupewa fedha za kutosha na chama chake kwa ajili ya kampeni kwani hadi zinamalizika, CCM ilikuwa imetoa milioni 60 pekee tofauti na ilivyofanya kwa wagombea wengine kwenye chaguzi ndogo ambako chama hicho hubeba gharama zote.
“Mpaka usiku wa kuamkia Ijumaa, chama kilikuwa kimetoa milioni 60 pekee kwa kampeni nzima, fedha ambazo hazikutosha hata kulipa mawakala 327 na wale wa akiba ambao kila mmoja tulipanga alipwe Sh30,000. Yaani kama vile chama kilijitenga na kampeni za Sioi,” alisema na kulalamika kiongozi mwingine aliyeongoza kampeni za mgombea huyo.
Kiongozi huyo ambaye kama mwenzake alizungumza kwa sharti la kutotajwa akiogopa ‘kushughulikiwa’ alisema gharama za kampeni za mgombea huyo wa CCM zilikuwa zaidi Sh200 milioni ambazo zilitokana na michango binafsi za wanafamilia na marafiki.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alipoulizwa kuhusu madai hayo, alikataa kusema lolote akisisitiza kwamba hayo ni mambo ya ndani ya chama yanayostahili kuzungumzwa na kujadiliwa ndani ya vikao.
“Hao waliokuletea taarifa hizo siyo tu kwamba wanakwenda kinyume cha katiba na kanuni za CCM, bali pia wanatoa siri za ndani nje ya chama. Sisi tunatarajia kukutana kufanya tathmini ya uchaguzi huo na yale yanayostahili kuwekwa hadharani tutawaeleza na yanayofaa kufanyiwa kazi ndani ya chama pia tutafanya hivyo kwa maslahi na maendeleo ya chama chetu,” alisema Chatanda.
Sioi akubali yaishe
Kwa upande wake, Sioi jana alitangaza kuyakubali matokeo hayo na kuahidi kumpa ushirikiano wa dhati mbunge mteule atakapomhitaji.
Sumari alishindwa kwenye uchaguzi wa ubunge baada ya kupata kura 26,757 ambazo ni sawa na asilimia 44.56 huku Nassari akipata kura 33,972 sawa na asilimia 54.91.
Sioi ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kukipongeza Chadema kwa kuibuka kidedea katika uchaguzi huo huku akikitaka kihakikishe kinatimiza ahadi kilizozitoa kwa wakazi wa jimbo hilo.
Sioi alisema kwamba amekubaliana na matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo,Trasias Kagenzi juzi alfajiri. Alisema ameridhishwa na matokeo hayo na kamwe hatarajii kwenda mahakanani kuyapinga.
Sioi aliwaomba wakazi wa Arumeru Mashariki kumpa ushirikiano wa kutosha mbunge mteule wa jimbo hilo huku akisisitiza ya kwamba hata yeye yuko tayari kufanya hivyo.
Pia alimtaka Nassari kutimiza ahadi zote alizokuwa akizitoa kwa wakazi wa jimbo hio wakati wa kampeni hasa za maji, elimu na miundombinu.
Shamrashamra
Wakati hali ndani ya CCM ikiwa hivyo, vijana 53 wa Chadema walikamatwa na kuachiwa huru baadaye na polisi juzi usiku wakati wakisherehekea ushindi wa Nassari.
Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chadema, John Mrema alisema vijana hao, wameachiwa kwa dhamana kutokana na maombi ya mbunge huyo mteule kwa polisi.
“Kama ambavyo mbunge aliahidi kuwa asingeweza kuendelea na sherehe za ushindi bila vijana walioshikwa, tunafuraha kuwaeleza kuwa vijana 53 wameachiwa bado vijana saba ndiyo tunawashughulikia,” alisema Mrema.
Vijana hao, walikamatwa na polisi katika operesheni kubwa iliyofanyika juzi usiku ikihusisha matumizi ya mabomu baada ya vijana hao kuandamana bila utaratibu na pia kudaiwa kuvunja vioo vya magari.
Polisi limeeleza kuwa vijana hao walikamatwa kwa kosa la kuvunja vioo vya magari likiwemo la Mngulu aliyekuwa mkuu wa operesheni wa polisi katika uchaguzi huo.
Tendwa asifu
Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, John Tendwa amesifia ukomavu wa kisiasa uliojitokeza katika chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zilizofanyika Aprili Mosi, mwaka huu jlicha ya kujitokeza kwa upungufu mwingi.
“Ukomavu wa kidemokrasia umejitokeza japo mapungufu ni mengi sana yaliyojitokeza pamoja na kuwapo kwa tume ambayo ilijaribu lakini hawakusitisha, sikuweza kuingilia maamuzi yale, kama kutoleana maneno machafu na kejeli ni jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa, uvumilivu wa kisiasa unahitajika,’’ alisema Tendwa.
Alikipongeza CCM kwa kuonyesha ukomavu wake wa kisiasa na Chadema kwa kushinda jimbo hilo na kuvitaka kwa vyama vyote vya siasa nchini kutekeleza kanuni na taratibu zote wakati wa uchaguzi ili kuboresha demokrasia ya nchi.
Monday, April 2, 2012
CCM hali mbaya Arumeru
CHADEMA YAFANYA VIZURI KATA 11KATI YA 17, YASHINDA PIA UDIWANI MWANZA. SONGEA,MBEYA,CUF YAPETA TANGA
Waandishi Wetu
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeongoza kwenye kura za awali kwa mgombea wake, Joshua Nassari kupata kura nyingi katika kata 11 kati ya Kata 17 za Jimbo la Arumeru Mashariki.
Dakika chache kabla ya kutangaza matokeo hayo, baadhi ya wafuasi wa CCM waliokuwa wamefurika katika Ofisi za Mji Mdogo wa Usa River na baadhi ya polisi, walikuwa wameondoka eneo hilo, wakiwaacha wapambe wachache wa mgombea wao, Sioi akiwamo, Beno Malisa.
Huu ni uchaguzi wa kwanza mdogo kwa Chadema kushinda katika jimbo lililokuwa likishikiliwa na CCM na uchaguzi wa pili kwa chama hicho cha upinzani, kushinda katika uchaguzi mdogo baada ya ule uliofanyika katika Jimbo la Tarime, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe.
Katika matokeo hayo yanayokusanywa na kujumlishwa katika ofisi za mji mdogo wa USA River, CCM, imefanya vema katika kata tatu ambako mgombea wake, Sioi Sumari amepata kura nyingi ikilinganishwa na Nassari.
Takwimu zinaonyesha kuwa Chadema wanaongoza katika kata za Akheri ambako ni nyumbani Kwa Sioi, Poli, USA-River, Mbuguni, Seela, Sing'isi, Nkoarua, Maji ya Chai, Kikwe, Maroroni, Nkoaranga, King'ori na Songoro ambako ni nyumbani Kwa Nassari. Jimbo la Arumeru Mashariki lina kata 17.
Mgombea wa CCM Sioi ameongoza katika kata za Makiba, Leguruki na Mkoandrua hadi saa 7:15 usiku jana ambapo msimamizi wa uchaguzi, Trasias Kagenzi alikuwa akisubiri masanduku ya kura kutoka kata mbili.
Kata ambazo masanduku na matokeo yake yalichelewa kutokana na umbali wa maeneo hayo ni Kikatiti na Ngarenanyuki.
Mbali na Chadema kuongoza Arumeru chama hicho pia kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Mwanza.
CUF imeambulia kiti kimoja cha udiwani Tanga na CCM Dar es Salaam.
Katika tukio lingine, wakala wa Chadema katika chumba Cha kujumlisha kura, Godbless Lema, jana alilazimika kutumia nguvu dhidi ya msimamizi msaidizi wa kata ya Maroroni ambaye jina lake halikupatikana mara moja baada ya kumtuhumu kutaka kubadili tarakimu za matokeo kwenye fomu rasmi zilizowasilishwa.
"Yule msimamizi alikuwa akitaka kuchezea tarakimu katika fomu za matokeo kutoka kwenye kata yake bila kujua kama nilikuwa namfuatilia," alisema Lema.
Waandishi Wetu
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeongoza kwenye kura za awali kwa mgombea wake, Joshua Nassari kupata kura nyingi katika kata 11 kati ya Kata 17 za Jimbo la Arumeru Mashariki.
Dakika chache kabla ya kutangaza matokeo hayo, baadhi ya wafuasi wa CCM waliokuwa wamefurika katika Ofisi za Mji Mdogo wa Usa River na baadhi ya polisi, walikuwa wameondoka eneo hilo, wakiwaacha wapambe wachache wa mgombea wao, Sioi akiwamo, Beno Malisa.
Huu ni uchaguzi wa kwanza mdogo kwa Chadema kushinda katika jimbo lililokuwa likishikiliwa na CCM na uchaguzi wa pili kwa chama hicho cha upinzani, kushinda katika uchaguzi mdogo baada ya ule uliofanyika katika Jimbo la Tarime, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe.
Katika matokeo hayo yanayokusanywa na kujumlishwa katika ofisi za mji mdogo wa USA River, CCM, imefanya vema katika kata tatu ambako mgombea wake, Sioi Sumari amepata kura nyingi ikilinganishwa na Nassari.
Takwimu zinaonyesha kuwa Chadema wanaongoza katika kata za Akheri ambako ni nyumbani Kwa Sioi, Poli, USA-River, Mbuguni, Seela, Sing'isi, Nkoarua, Maji ya Chai, Kikwe, Maroroni, Nkoaranga, King'ori na Songoro ambako ni nyumbani Kwa Nassari. Jimbo la Arumeru Mashariki lina kata 17.
Mgombea wa CCM Sioi ameongoza katika kata za Makiba, Leguruki na Mkoandrua hadi saa 7:15 usiku jana ambapo msimamizi wa uchaguzi, Trasias Kagenzi alikuwa akisubiri masanduku ya kura kutoka kata mbili.
Kata ambazo masanduku na matokeo yake yalichelewa kutokana na umbali wa maeneo hayo ni Kikatiti na Ngarenanyuki.
Mbali na Chadema kuongoza Arumeru chama hicho pia kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Mwanza.
CUF imeambulia kiti kimoja cha udiwani Tanga na CCM Dar es Salaam.
Katika tukio lingine, wakala wa Chadema katika chumba Cha kujumlisha kura, Godbless Lema, jana alilazimika kutumia nguvu dhidi ya msimamizi msaidizi wa kata ya Maroroni ambaye jina lake halikupatikana mara moja baada ya kumtuhumu kutaka kubadili tarakimu za matokeo kwenye fomu rasmi zilizowasilishwa.
"Yule msimamizi alikuwa akitaka kuchezea tarakimu katika fomu za matokeo kutoka kwenye kata yake bila kujua kama nilikuwa namfuatilia," alisema Lema.
Kisa na Mkasa na Salim Kikeke
Ajali mkono
Mkono ulikatika kabisa (sio huu)
Bwana mmoja nchini Uingereza aliukata mkono wake kwa bahati mbaya kwa kutumia msumeno wa umeme wakati akikata kuni.
Baada ya kuukata mkono wake, bwana huyo Stuart Frain alishika kipande kilicho katika na kwenda kuomba msaada. Gazeti la Manchester Evening News limesema bwana huyo wa Rochdale, kaskazini magharibi mwa England aliukata mkono wake wa kushoto chini kidogo mwa kiwiko chake.Mkono wake ukiwa unaninginia akikimbilia katika barabara kuu, na kuweza kusaidiwa na wapita njia. Mara moja bwana huyo alikimbizwa hospitali, na mkono wake huo kuwekwa katika barafu ili usiharibike.
Hata hivyo mtandao wa courier mail.com haukusema iwapo ataweza kuutumia tena mkono wake huo.
Bwana huyo aliliambia gazeti la Manchester kuwa alikuwa katika bustani yake akikata kuni, na mashine hiyo kumzidi nguvu na kuukata mkono.
"Nilipofika hospitali madaktari waliniambia ningechelewa dakika moja tu, basi ningekufa" amekaririwa akisema.
Ajikata mguu asiende kazini
Uvivu mwingine hauna maana
Shirika la habari la Reuters limesema bwana huyo baada ya kukaa muda mrefu bila ajira, alipata mwaliko wa kwenda katika ofisi ya ajira ili apatiwe kazi.
Saa kadhaa kabla ya kwenda katika ofisi hizo ili apimwe afya yake na kupatiwa ajira, bwana huyo mwenye umri wa miaka hamsini na sita, alichukua msumeno wa umeme na kuukata mguu wake wa kulia.
Shirika la utangazaji la ORF la Austria limesema bwana huyo aliukata mguu wake juu ya kiwiko.
Taarifa zinasema, huku akitokwa na damu nyingi, alichukua kipande cha mkuu wake na kukitupia jikoni - ndani ya oven-- yaani jiko la kuokea. Baada ya hapo alijikokota na kwenda kupiga simu hospitali akiomba msaada.
Shirika la utangazaji la ORF limesema jitihada za madaktari kujaribu kuunga kipande cha mguu wake kimeshindika.
Aita polisi kwa upweke
Polisi watakiwa kumpa 'kampani'
Bwana huyo alikuwa akipiga simu polisi na kuripoti mambo ya uongo ili akamatwe na kupelekwa gerezani.
Gazeti la Chongqing Evening News limesema bwana huyo aitwaye Chen mwenye umri wa miaka arobaini na tisa, alikuwa akipiga simu polisi na kudai kuwa kuna watu wanataka kumuua, au kwamba anaomba msaada kwa kuwa anakaribia kufa kutokana na maradhi mabaya. Taarifa zinasema kila mara polisi wakienda katika eneo la tukio wanamkuta akiwa amelewa chakari, na hakuna tatizo lolote.
"Chen hakuwa akisema kwa nini anatupigia simu, alikuwa akituomba tu tumpeleke jela" amesema polisi ambaye mara kadhaa alikwenda kwa bwana Chen. Polisi wanaamini kuwa kufuatia kupewa talaka na mkewe, bwana Chen alikuwa mpweke na alikuwa akitaka tu kujumuika na watu.
Chafya yatengua shingo
Taratibu unapopiga chafya
Mwanamama huyo Monique Jeffrey alitengua mifupa miwili ya shingo yake wiki mbili zilizopita, baada ya kupiga chafya huku akiwa amekaa kitandani kwake.
"Nilihisi kuna tatizo tu, nikasikia maumivu makali" amekaririwa akisema mama huyo mwenye umri wa miaka ishirini na nane. Mtandao wa Top news.com umesema mwanamama huyo mwenye mtoto mdogo mwenye umri wa miezi kumi, hakuweza hata kujisogeza baada ya tukio hilo. Kwa bahati nzuri, alikuwa na simu yake karibu, na kwa taabu kabisa akafanikiwa kumuandikia mumewe ujumbe mfupi wa maandishi - text messege.
Alipelekwa hospitali na kuambiwa kuwa labda ni misuli tu imekaza na kuambiwa afanye mazoezi. Hata hivyo hali ilibadilika saa chache baadaye ambapo alianza kuhisi ganzi kwenye mkono wake wa kushoto. Mara moja alipelekwa katika kitengo maalum ambapo waligundua mifupa miwili kwenye uti wa mgongo ulikuwa imetenguka.
Kuku na Taka
Kuku kila nyumba
Maafisa wa kijiji cha Pince, kilichopo kaskazini magharibi mwa Ufaransa wamesema kuku hao watakuwa na uwezo wa kula kilo mia moja na hamsini ya taka hizo kwa mwaka.
Taarifa zinasema, inadhaniwa kuwa mbali na kusaidia kupunguza taka kijijini hapo, mpango huo pia utasaidia familia hizo kupata mayai, na hivyo kusaidia kuichumi. Maafisa wa kijiji wamesema familia ambazo zingependa kujiunga na mradi huo zitapatiwa kuku hao mwezi Septemba mwaka huu.
"Watu walidhani ni utani tulipoanza" amesema meya wa Pince, Lydie Pasteu, akizungumza na kituo cha TV cha France 3. Takriban familia kumi na tano hadi ishirini zimeonesha nia ya kujiunga na mpango huo.
Bikra atafuta mume
Masharti magumu?
Mtandao wa rednet.cn umeripoti kuwa mwanamama huyo mwenye umri wa miaka thelathini na nane aliandika tangazo hilo kwenye wavuti uitwao Sina Weibo. Mwanadada huyo anayejulikana kwa jina la Tu, aliandika vigezo anavyovitaka ambavyo mume huyo awe navyo.
Amesema lazima awe mwanachama wa chama kinachotawala nchini China, au awe mfanyakazi wa serikali. Aidha amesema iwapo mchumba atapatikana, hakutakuwa na tendo la ndoa kabla ya ndoa, na vile vile hakuta kuwa na tendo hilo pia hadi miaka mitatu ya baada ya harusi.
Ujumbe huo wa Dada Tu, umezua sokomoko na kusomwa na zaidi ya watu elfu kumi katika kipindi cha saa moja tu. Baadhi ya wachangiaji wa sakata hilo wamesema kwa vigezo hivyo kamwe hatopata mchumba.
Kwa mujibu wa Mwanamama Tu ambaye anatokea jimbo la Hubei, amesema hana muda tena wa kusubiri mchumba kwa njia za kawaida na ndio maana ametoa tangazo hilo kwenye mtandao.
Na kwa taarifa yako...... Huwezi kukoroma na kuota ndoto kwa wakati mmoja..
Tukutane wiki ijayo.... Panapo Majaaliwa
World's strongest girl weighs only 40kg, but can lift up to 350kg
| Varya Akulova, 22, has been dubbed 'The Strongest Girl in the World' for her amazing display of strength. Weighing only 40kg, the girl from Ukraine is capable of lifting up to 350kg. This youngster has tremendous will-power, translucent body and thread-like tendons. In an email to citizen journalism website Stomp, netizcen MuscleMan said: "It's amazing what this tiny girl can do. If you look at her, she doesn't even look that muscular. "Her dad had wanted a strong boy when her mother was pregnant, and when Varya was born, he thought his hopes were dashed. "What a lucky surprise for him!" | ||||
Subscribe to:
Posts (Atom)

