Friday, April 1, 2011
MKE WA 20 PERCENT AMJERUHI MTOTO WAKE MKONO AKISHANGILIA USHINDI WA MUMEWE
Ushindi alioupata msanii kutoka pande za Kimazinchana, wilayani Kisarawe mkoani Pwani, Hamis Abbas Kinzasa ‘20%’ (pichani) wa kupata tuzo tano za Kili hivi karibuni, ulizua balaa baada ya mtoto wake kujeruhiwa mkono na mama yake wakati akishangilia.
Chanzo chetu makini kilitutonya kuwa, siku ya tukio baada ya mwanamke huyo kusikia mumewe kafunika mbaya, alinyanyuka kwa lengo la kushangilia lakini aliporudi kukaa alimkalia mwanae aitwaye Faraja (2) na kumuumiza mkono.
“Yaani furaha ghafla iligeuka kilio kwani mtoto huyo aliumia sana, usafiri ulitafutwa haraka na walimkimbiza katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam kwa matibabu,”alisema mtoa habari wetu.
Akizungumza na mwandishi wetu 20% alikiri mwanae kupatwa na ajali hiyo lakini akaeleza kuwa, baada ya matibabu hali yake inaendelea vizuri.
“Ni kweli mwanangu aliumia wakati mama yake akishangilia ushindi wangu, hata hivyo alipelekwa hospitalini na nashukuru anaendelea vizuri,” alisema 20%.
Wakati huo huo, msanii wa filamu aliyeshirikishwa kwenye video ya Wimbo wa Tamaa Mbaya wa 20%, Zuena Mohammed ‘Shilole’ alijikuta akipagawa baada mshkaji huyo kuzoa tuzo kibao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment