WATU wasiofahamika wamevamia shule ya kimataifa ya Livingston ya wilayani Njombe mkoani Iringa na kumteka mwanafunzi mmoja wa kike katika shue hiyo na kumchinja kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.
Imedaiwa kuwa watu hao ambao idadi yao haijafahamika walivamia shule hiyo majira ya saa 10 alfajiri ya kuamkia juzi na kuingia katika bweni la wasichana na kufanikiwa kumteka mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Doris Lutego (12) ambaye ni mkazi wa mtaa wa shule ya Uhuru mjini Makambako wilaya ya Njombe.
Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa kwa kuwa si msemaji wa juu wa tukio hilo alisema kuwa mwanafunzi huyo alitekwa usiku wa kuamkia jumapili na kuwa pamoja na jitihada za kumtafuta zilizofanywa na wananchi na viongozi wa shule hiyo jitihada zilishindikana .
“Baada ya taarifa ya kuvamiwa kwa shule hiyo na kutekwa mwanafunzi huyo wananchi tuliendesha msako mkali wa kuwasaka wavamizi hao ila hatukufanikiwa hadi leo asubuhi baada ya wakazi wa eneo la kitongoji cha Kambarage Njombe kufanikiwa kukuta mfuko wa Salfeti ambao ulikuwa na mwili wa mtoto huyo. Mfuko huo ulikutwa nyuma ya nyumba ya balozi wa kitongoji hicho na baada ya kutafuta zaidi ndipo kichwa chake kilikutwa karibu na nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho huku kikiwa kimehifadhiwa katika mfuko wa madaftari ya mwanafunzi huyo.
Hata hivyo alisema kuwa mbali ya kufanikiwa kukuta mwili wa mwanafunzi huyo ila bado hawajafanikiwa kuwakamata wahusika wa mauwaji hayo ya kinyama . Alisema kuwa mauwaji hayo yamewaweka katika maswali zaidi wakazi wa mji wa Njombe na wilaya nzima kwani inaonyesha wazi wauwaji hao wamefanya hivyo kama sehemu ya kulipiza kisasi katika familia ya mtoto huyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarit Mangalla amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai kuwa mtoto huyo alikuwa akisoma darasa la tano katika shule hiyo .
Kamanda Mangalla alisema kuwa taarifa zilizofika polisi mapema jana zillikuwa ni za kutekwa kwa mtoto huyo na kukutwa kwa baadhi ya meno yake na damu katika kitanda chake na kuwa bado jeshi la polisi linafanya uchunguzi zaidi na kuwasaka wahusika wa tukio hilo.
Kamanda Mangalla alisema kuwa taarifa zilizofika polisi mapema jana zillikuwa ni za kutekwa kwa mtoto huyo na kukutwa kwa baadhi ya meno yake na damu katika kitanda chake na kuwa bado jeshi la polisi linafanya uchunguzi zaidi na kuwasaka wahusika wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment