Tuesday, June 14, 2011

Majambazi wavamia hospitali ya Muhimbili, wapora mamilioni ya fedha

RPC Suleiman Kova 
Kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni Majambazi wakiwa na Pikipiki wamevamia na kupora Mamilion ya fedha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam. Tukio hilo la ujambazi limefanyika leo asubuhi ambapo inadaiwa kuwa askari Juma Magungu, wa Kampuni ya Full Time Security aliyekuwa analinda katika Idara ya Uhasibu amepigwa risasi Kifuani na majambazi hao na kusababisha kifo chake. 
 
Afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Ndugu Aminiel Aligeisha alisema kuwa tukio hilo limetokea leo saa mbili asubuhi ambapo wahasibu wawili wa Hospitali hiyo walikuwa katika zoezi la kuzipeleka fedha Idara kuu ya Uhasibu wakiwa na gari ndipo kundi hilo la Majambazi likatokea na kuwavamia. 
 
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano huyo, gari hilo lenye namba za usajili SU-36713 aina ya Nisani ikiwa na watumishi Wanne wa Idara ya Uhasibu walivamiwa na kundi hilo la watuhumiwa wa ujambazi wakiwa na Bastola moja.  Zaidi ya shilingi Miloni13 zinadaiwa kuibiwa.

MWANAFUNZI WA SHULE YA LIVINGSTONE NJOMBE ATEKWA ACHINJWA

 
WATU wasiofahamika wamevamia shule ya kimataifa ya Livingston ya wilayani Njombe mkoani Iringa na kumteka mwanafunzi mmoja wa kike katika shue hiyo na kumchinja kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.
Imedaiwa kuwa watu hao ambao idadi yao haijafahamika walivamia shule hiyo majira ya saa 10 alfajiri ya kuamkia juzi na kuingia katika bweni la wasichana na kufanikiwa kumteka mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Doris Lutego (12) ambaye ni mkazi wa mtaa wa shule ya Uhuru mjini Makambako wilaya ya Njombe.

Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa kwa kuwa si msemaji wa juu wa tukio hilo alisema kuwa mwanafunzi huyo alitekwa usiku wa kuamkia jumapili na kuwa pamoja na jitihada za kumtafuta zilizofanywa na wananchi na viongozi wa shule hiyo jitihada zilishindikana .

“Baada ya taarifa ya kuvamiwa kwa shule hiyo na kutekwa mwanafunzi huyo wananchi tuliendesha msako mkali wa kuwasaka wavamizi hao ila hatukufanikiwa hadi leo asubuhi baada ya wakazi wa eneo la kitongoji cha Kambarage Njombe kufanikiwa kukuta mfuko wa Salfeti ambao ulikuwa na mwili wa mtoto huyo. Mfuko huo ulikutwa nyuma ya nyumba ya balozi wa kitongoji hicho na baada ya kutafuta zaidi ndipo kichwa chake kilikutwa karibu na nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho huku kikiwa kimehifadhiwa katika mfuko wa madaftari ya mwanafunzi huyo.
 
Hata hivyo alisema kuwa mbali ya kufanikiwa kukuta mwili wa mwanafunzi huyo ila bado hawajafanikiwa kuwakamata wahusika wa mauwaji hayo ya kinyama . Alisema kuwa mauwaji hayo yamewaweka katika maswali zaidi wakazi wa mji wa Njombe na wilaya nzima kwani inaonyesha wazi wauwaji hao wamefanya hivyo kama sehemu ya kulipiza kisasi katika familia ya mtoto huyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarit Mangalla amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai kuwa mtoto huyo alikuwa akisoma darasa la tano katika shule hiyo .

Kamanda Mangalla alisema
kuwa taarifa zilizofika polisi mapema jana zillikuwa ni za kutekwa kwa mtoto huyo na kukutwa kwa baadhi ya meno yake na damu katika kitanda chake na kuwa bado jeshi la polisi linafanya uchunguzi zaidi na kuwasaka wahusika wa tukio hilo.

Askofu Mdegela awasamehe waliohusika kumzushia kashfa


Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Dk. Owdenbug Mdegela, amesema anawasamehe wote waliohusika katika kumzushia tuhuma ambazo zimethibitika kuwa za uongo.
Ametoa kauli hiyo baada ya Halmashauri Kuu ya Dayosisi hiyo na jopo la wachungaji wa kanisa hilo kumsafisha.

Taarifa ya askofu Mdegela aliyoitoa kwa waumini wa kanisa hilo jana inaeleza kuwa tuhuma hizo zilizochapishwa na kusambazwa kwa makusudi na watu aliowaita ‘waumini wasio raia’ zina lengo la kulivuruga kanisa na kuichafua dayosisi hiyo mbele ya jamii na waumini.

Mdegela alitoa tamko hilo jana kwa waumini wa KKKT Dayosisi ya Iringa ambao walihudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa kuu la Cathedral.
“Natangaza rasmi uamuzi wangu wa kuwasamehe baadhi ya viongozi wakiwemo maaskofu na wachungaji wenzangu waliotumika kuasisi mpango huo wenye lengo la kulivuruga kanisa, dayosisi pamoja na kunichonganisha na waumini pasipo kutathmini madhara ya matamko yasiyolenga kuwajenga waumini wao kiroho,” alisema Mdegela.

Alisema wiki iliyopita kanisa liliitisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi na wachungaji wote na kujadili kilichojitokeza baada ya maaskofu watatu kufika katika dayosisi hiyo kwa nia ya kuchunguza habari ambazo wanadai zinasikika mara kwa mara.

Alisema kuwa Halmashauri Kuu na wachungaji hao walikaa Juni 8, mwaka huu ili kuangalia mfululizo wa matukio hayo na baadaye kuyapuuza.

Polisi yapiga wanafunzi mabomu



Jeshi la Polisi limetumia mabomu kuwatawanya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom). Milio ya mabomu ilisikika katika eneo la Bunge mjini Dodoma, baada ya polisi kuwatawanya wanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Jamii cha Udom, kuandamana hadi bungeni wakitaka kumuona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, kushinikiza kulipwa posho za mafunzo kwa vitendo.

Mapema asubuhi, wanafunzi hao walikusanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini hapo na ilipofika saa 4.00 asubuhi walianza kuandamana hadi bungeni wakishinikiza kumuona Pinda na Kawambwa. Hata hivyo, jitihada zao zilishindikana baada ya polisi kuwaamuru kuondoka katika eneo hilo na walipokaidi amri hiyo ndipo walipopigwa kwa mabomu ya machozi yaliyofanya wanafunzi hao kukimbia ovyo.

Katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma hususan bungeni kulikuwa na ulinzi mkali wa askari wa Kikosi cha Kuzuia Fujo (FFU), waliokuwa wamebeba bunduki na mabomu ya kurusha kwa mkono.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Sanaa ya Lugha na Sayansi za Jamii, Mwakabinga Philipo, alisema wameamua kuandamana kutokana na kutotekelezewa madai yao ambayo ni kupatiwa fedha za mafunzo kwa vitendo ambazo wamekuwa wakiahidiwa, lakini hawapatiwi.

Alisema Seneti ya Udom Juni 8, mwaka huu ilitoa taarifa kuwa tatizo la madai ya fedha za mafunzo kwa vitendo halitatokea tena. Alifafanua kuwa licha ya ahadi hiyo, wanashangazwa kuona mpaka sasa haitekelezeki ndio maana waliamua kwenda bungeni kuonana na viongozi hao.

Mwakabinga alisema kutokana na ahadi zilizotolewa na viongozi hao ndio maana waliamua kwenda kuonana na Pinda na Kawambwa ili kupata ufumbuzi wa fedha hizo. Baada ya kutawanywa na polisi, ilipofika majira ya saa 6:00 mchana, wanafunzi hao walikusanyika tena katika viwanja vya Nyerere wakidai kuwa Waziri Kawambwa angekwenda kuzungumza nao.

Baada ya wanafunzi hao kukusanyika, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, James Msekela, alifika katika eneo hilo kwa lengo la kuwatuliza, lakini jitihada zake ziligonga mwamba baada ya kumzomea na kumwambia “hatukutaki wewe, tunamtaka Waziri.” Baada ya Dk. Msekela kuzomewa, askari wa FFU walianza kuwatawanya wanafunzi hao na kukimbizana nao katika mitaa mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata baadhi yao.

Mahakama yaamuru Askofu Mokiwa, Hotay wakamatwe



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imeagiza kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa na Askofu mpya wa Kanisa hilo aliyewekwa wakfu juzi, Stanley Hotay.Askofu Mokiwa, alimweka wakfu Hotay Jumapili, siku mbili tangu Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa maagizo ya kusitishwa kwa shughuli hiyo.

Kitendo hicho cha Askofu Mokiwa kuendelea na mchakato wa kumweka wakfu Askofu Hotay pamoja na amri ya Mahakama kutaka shughuli hiyo isitishwe, kimeelezwa kuwa ni dharau kwa mahakama.

Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu huyo zilifanyika juzi Makao Makuu ya Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na zilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Claudio Bitegeko na maofisa kadhaa kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Uamuzi wa kukamatwa kwa maaskofu hao, ulitolewa jana na Jaji Kakusulo Sambo baada ya wakili wa mashtaka, Meinrad D’souza kuwasilisha maombi maalumu ya kutaka Mahakama Kuu itoe adhabu kwa Dk Mokiwa na Hotay kwa kukaidi amri ya Mahakama.

Akitoa uamuzi ambao ulichukua takriban saa moja, Jaji Sambo alisema haihitaji elimu ya chuo kikuu chochote kuona kuwa walichokifanya Maaskofu hao wa Anglikana ni dharau kwa amri halali ya Mahakama.

Alisema kitendo walichokifanya ni kudharau Mahakama tena Mahakama Kuu na kwamba kama hatua kali zisipochukuliwa, nchi haitatawalika katika misingi ya sheria.

“Nchi hii inaongozwa kwa misingi ya sheria  na Rais Jakaya Kikwete amekuwa akieleza kuwa kila mtu anapaswa kuheshimu utawala wa sheria. Inasikitisha kama viongozi wa dini wanakiuka sheria, tukiendelea hivi itakuwa tabu sana,” alisema Jaji Sambo.

Alisema mtu yeyote anayeishi Tanzania ni lazima atii na kuheshimu sheria zilizopo hata kama ni raia wa nchi nyingine.Jaji Sambo alisema wasomi wa sheria wanatambua kuwa, Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kifungu cha 37(2) kinaeleza namna ya kuwashughulikia watu wanaokiuka amri ya Mahakama.

Alisema Askofu Mokiwa ameeleza katika tamko lililowasilishwa Mahakamani jana kuwa alimweka wakfu Askofu Hotay kama Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, lakini hatua hii imekuja kabla ya Mahakama haijatoa uamuzi kwa shauri lililokuwa limefikishwa Mahakamani.

“Hii ni sawa sawa na mwenendo mzima wa kesi unakuwa hauna maana tena, kwani tayari Askofu anayelalamikiwa ameapishwa na taratibu za kumpata Askofu ni zilezile ambazo zimelalamikiwa, hivyo kutokana na hali hii, nimeridhika kuwa amri halali imekiukwa,” alisema Jaji Sambo.

Jaji Sambo alisema katika mazingira hayo, ni wazi kuwa kuna namna ya kuwashughulikia wanaokiuka amri halali ya Mahakama.

Alisema Sura 11 ya Kanuni ya Adhabu Cap 16 ya mwaka 2002, inaeleza kuwa ni makosa kuingilia chombo cha utoaji haki na imeeleza ni nini kinaweza kufanyika kwa atakayekiuka.

Jaji huyo alisema Kifungu cha 114 (i) C na K cha CPA, kinafafanua kosa la kuingilia mwenendo wa kesi Mahakamani na katika kifungu hichohicho, kipengele cha tatu kinaipa Mahakama mamlaka ya kumwadhibu mtu anayevunja sheria hiyo.

"Mtu yeyote ambaye anasababisha kuingiliwa kesi au kuvuruga mwenendo wa kesi yupo hatiani,” alisema Jaji Sambo na kuongeza kuwa kifungu cha 124 CPA kinafafanua kuwa mtu anayevunja maagizo ya Mahakama achukuliwe hatua.“Kwa mazingira haya uamuzi mdogo ambao ulipaswa kutolewa leo sitautoa hadi hapo nitakapopanga tena na wahusika watajulishwa.”

"Hivyo katika uamuzi huu wa sasa, naagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dk Valentine Mokiwa na mlalamikiwa wa pili, Stanley Hotay na taratibu za kujibu kosa hilo la jinai zianze."


Awali, Wakili D’souza alisema kitendo cha Askofu Mokiwa kumweka wakfu Hotay kimeingilia uhuru wa Mahakama na kimeshusha heshima ya Mahakama Kuu, kwani ilitoa agizo la kusitishwa shughuli zozote za kuapishwa kwa kiongozi hiyo.

Hata hivyo, Mawakili wa Utetezi, Joseph Thadayo na Issa Mavura waliomba Mahakama kutokubali maombi ya kuchukuliwa hatua Askofu Mokiwa na Askofu Hotay kwa maelezo kuwa hawakuingilia mwenendo wa kesi hiyo.

Thadayo alimkabidhi Jaji Sambo tamko la Askofu Mokiwa ambalo linaeleza kilichotokea kuwa Hotay amesimikwa kama Askofu wa Anglikana Tanzania na siyo Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.Mara baada ya uamuzi huo, Wakili Thadayo alisema hawana la kufanya zaidi ya kutekeleza maagizo hayo.

“Tutashauriana cha kufanya lakini kwa sasa ndiyo hivyo imeamriwa,” alisema Thadayo.

Spika: Tutamfukuza Zitto


  •  Wanaharakati nao watakaposho za wabunge zifutwe




VITA ya kufutwa posho za wabunge na watumishi wengine wa umma, imechukua sura mpya, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kusema kwamba Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe anaweza kufukuzwa ubunge kwa kutosaini karatasi za mahudhurio.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge baada ya kuahirisha mkutano wa asubuhi, Makinda alisema Zitto anaweza kukumbwa na adhabu hiyo iwapo hatasaini karatasi za mahudhurio ambazo ndizo zinazothibitsha uwepo wa mbunge katika mikutano na vikao vyake.

"Kwa mujibu wa kanuni zetu, asipohudhuria mara tatu anakabiliwa na adhabu tena ya kufukuzwa bunge, hizo ndivyo kanuni zinavyosema." Hata hivyo, Zitto amepuuza kauli hiyo ya Spika akisema kwamba kama ni kwa ajili ya kukataa posho, yuko tayari kufukuzwa bungeni.

"Nitafanya hivyo tuone. Kanuni inasema mikutano mitatu mfululizo na siyo vikao vitatu mfululizo. Nitatumia uzoefu wangu wa siasa za wanafunzi kukwepa mtego wake. Lakini kama anadhani ni sawa kunifukuza ubunge kwa kukataa posho, nipo tayari," alisema Zitto.

Kauli ya Makinda inafuatia msimamo wa Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), kukataa posho za vikao na kwamba kwa kuwa kinachohalalisha yeye kulipwa posho ni karatasi za mahudhurio basi hatasaini karatasi hizo. Zitto alisema juzi mjini Dodoma kuwa, tangu Juni 10, mwaka huu alijibu barua ya Spika akikataa "kushinikizwa kuchukua posho za vikao" na kwamba hatua atakayoichukua ni kutosaini karatasi za mahudhurio katika vikao vyote.

Mahudhurio hayo ndiyo hulalalisha mbunge kupewa posho hizo.
"Kuanzia kikao cha juzi cha Tume ya Mipango, sikusaini na mkitaka nendeni mkaangalie ile orodha na kesho ndani ya Bunge sitasaini ili kuondoa uhalali wa kupewa posho hizo.

Sasa hapo tutaona watanilazimisha kwa njia gani," alisema Zitto. Lakini jana, Makinda alisema mujibu wa sheria malipo yote lazima yapelekwe kwa mbunge mwenyewe na kwamba ofisi yake haitafanya vinginevyo kwa wabunge ambao wamekataa posho hizo. Kanuni 143 (1) ya Bunge inabainisha kuwa kuhudhuria vikao ndiyo wajibu wa kwanza wa kila mbunge na kwamba asipohudhuria mikutano mitatu ya Bunge bila ruhusa ya Spika atapoteza ubunge wake.

Kwa maana hiyo, Zitto anaweza kufukuzwa Bunge ikiwa hatasaini mahudhurio ya vikao vyote vya Mkutano wa Bunge la Bajeti, vikao vya mkutano ujao ambao kwa kawaida huwa wa Oktoba na mkutano wa kwanza wa mwaka 2012.

"Mbunge yeyote atakayeshindwa kuhudhuria Mikutano ya Bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya Spika iliyotolewa kwa maandishi, atapoteza ubunge wake kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1) (c) ya Katiba na Spika ataiarifu Tume ya Uchaguzi," inaeleza kanuni hiyo namba 143 (2) ambayo iko chini ya sehemu ya 10 ya Kanuni za Bunge toleo la mwaka 2007.

Kadhalika, Kanuni hiyo ya 143 (3) inakwenda mbali zaidi na kusema kuwa mbunge asipohudhuria nusu ya vikao vya mkutano mmoja bila sababu ya msingi atapewa onyo.

Fasili za kanuni hizo zinamtaka mbunge asiyehudhuria vikao vya Bunge au vile vya Kamati za Bunge kupata kibali cha Spika katika Ofisi za Bunge hilo zilizopo Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma. Hata hivyo, kanuni hizo haziweki utaratibu wa kudhibiti mahudhurio ya wabunge na jukumu hilo ni kama limeachwa kwa Spika ambaye kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) amepewa uwanda mpana wa kuamua mambo mengine ambayo hayakutajwa moja kwa moja na kanuni hizo.

Kauli ya Serikali Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema jana kuwa wabunge wanaokataa posho ni wanafiki wanaotafuta umaarufu kwa umma."Mtu huwezi kusema kwamba eti posho hutaki halafu unasema zipelekwe Kigoma, kama suala ni kukataa posho ili kupunguza matumizi ya Serikali basi unazikataa kabisa," alisema Mkulo katika viwanja vya Bunge.

Tayari Mkulo alikuwa amesema kuwa ikiwa wapinzani watabeba ajenda hiyo, atawaandalia fomu kwa wale wasiotaka posho ili wakajaze na fedha hizo zipelekwe kwa wahitaji wa misaada mbalimbali.

Awali, Zitto alitaka fedha zake za posho zipelekwe katika taasisi ya Kigoma Development Inititive (KDI) lakini Juni 10 mwaka huu, Spika Makinda alimwandikia barua kimweleza kuwa ofisi yake haiko tayari kufanya hivyo na kusisitiza kwamba fedha hizo za posho zitaendelea kuwekwa katika akaunti yake benki.

Wanaharakati nao watakaposho za wabunge zifutwe

WANAHARAKATI wa taasisi mbalimbali nchini wameunga mkono uamuzi wa Chadema wa kukataa posho.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wanaharakati hao kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na ule wa Jumuiko la Wadau wa Maendeleo (Ado), wametaka posho hizo zifutwe ili fedha zipelekwe katika shughuli nyingine za maendeleoMkurugenzi Mtendaji wa Ado, Ntamilyango Buberwa alisema taasisi yake imepanga kuzunguka nchi nzima kutafuta watu milioni moja wanaounga mkono hoja hiyo ili walipeleke suala hilo kwa Rais Jakaya Kikwete.
"Baada ya kuwapata watu hao, tutawataka wasaini fomu maalumu ambayo tutaipeleka wa Rais Jakaya Kikwete kuelezea kutoridhishwa kwetu na jambo hilo. Ado itafanya na kumaliza kampeni hiyo kabla ya kusomwa kwa Bajeti ya Wizara ya Fedha.”

Alisema ni vyema wabunge wenye nia njema na taifa na ambao wamelenga kweli kuwawakilisha wananchi, wakaunga mkono hoja ya kufutwa posho hizo. Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya alisema siyo haki kwa serikali kuendelea kuongeza posho kwa wabunge na maofisa wa ngazi za juu serikalini na kwamba suala hilo linapaswa kuzingatia hali halisi ya nchi na watu wake ambao alisema wengi wao ni maskini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mallya alisema kumekuwa na kasumba kwa serikali kuwalipa posho kubwa maofisa wa ngazi za juu na wabunge na kuwasahau wafanya kazi wa kiwango cha chini bila kuangalia hali halisi ya maisha.

“Nchi nyingine zinaongeza  kiwango cha mshahara kwa kuangalia hali ya maisha yanavyokwenda, hapa kwetu ni tofauti, ukisafiri posho kwa mfanyakazi wa juu ni kubwa kuliko ya yule wa ngazi ya chini, posho inapaswa kuwa na uwiano sawa na si kuleta tofauti baina ya mtu na mtu.”

Alikosoa  kitendo cha serikali kusamahe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa baadhi ya watumishi wa serikali na wafanya kazi wa taasisi zinazopata ruzuku kutoka serikalini akidai mpango huo utawanufaisha vigogo na si wale wa ngazi za chini.

Thursday, June 9, 2011

Bajeti ya Fedha


WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, amesema matatizo yanayowakabili wananchi katika kukabiliana na ugumu wa maisha na umuhimu wa kukuza uchumi, ndiyo misingi ya vipaumbele vya bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2011/12.

Alisema lengo ni kuwezesha shughuli za uchumi na maendeleo ya jamii kufanyika kwa wakati wote, kuimarisha miundombinu ya maji, reli, bandari na kudhibiti mfumko wa bei uliosababishwa na kuongezeka kwa bei za vyakula, mafuta, umeme na gharama za uzalishaji.

Waziri Mkulo aliyasema hayo jana katika hotuba yake kuhusu hali ya uchumi kwa mwaka 2010/11 na malengo ya uchumi kipindi cha muda wa kati, mwaka 2011/12 na 2015/16.

Alisema vipaumbele vingine katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha, ni kuongeza upatikanaji chakula kwa kuhimiza kilimo, hasa cha umwagiliaji na kuimarisha hifadhi ya chakula, ili kujikinga na tatizo la uhaba wa chakula.

Hali kadhalika, kuongeza fursa za ajira na kuwanufaisha wananchi walio wengi hasa vijana ambao ni kundi kubwa kwenye soko la ajira.

Kauli hiyo ya waziri Mkulo imekuja huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa wananchi, kuhusu hali ngumu inayowakabili wengi wao na kuitaka serikali kuhakikisha bajeti ya mwaka ujao inawaondelea hali hiyo.
Katika malalamiko yao, wananchi wamediriki kusema hali ngumu ya maisha inayowakabili, inapingana na ahadi ya serikali kwamba ingefanya jitihada kuhakikisha maisha ya Watanzania yanakuwa bora.
Katika hotuba yake, Mkullo alikiri umaskini miongoni mwa wananchi haujapungua kwa kiwango kikubwa hasa kwenye kaya zinazotegemea zaidi shughuli za kilimo.

‘’Pia, ingawa uchumi ulikuwa unaongezeka, ukuaji huo ulikuwa chini ya kiwango kinachohitajika kufikia shabaha na malengo ya dira,’’ alisema waziri Mkulo na kuongeza:
“Vyanzo vya ukuaji uchumi havikuwagusa watu wengi, hususan maskini wa vijijini maeneo ya pembezoni.’’
Alisema licha ya mambo mengine, hali hiyo imechangiwa na tatizo la kushindwa kutumia kikamilifu fursa za rasilimali nyingi za asili na jiografia ya Tanzania kupakana na bahari, katika kuinua uchumi.
‘‘Tunahitaji kuboresha miundombinu hususan ya usafirishaji, ili tuweze kutumia kikamilifu fursa ya kupakana na bahari kuweza kuwa kitovu cha biashara cha kuhudumia nchi za maziwa makuu na zisizopakana na bahari,’’ alisema.

Kuhusu deni la taifa, Mkullo alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, lilifikia dola 11,380.2 milioni za Marekani na kwamba, liliongezeka kwa dola 654.28 milioni ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2009.

Mkullo alisema ongezeko hilo lilitokana na mikopo mipya ya ndani na nje yenye masharti nafuu kugharimia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa mujibu wa Mkullo, malipo ya deni la taifa kipindi cha robo tatu cha mwaka kilichoishia Machi mwaka huu, yalikuwa Sh803.64 bilioni.‘’Malipo ya deni la nje kwa kipindi hicho yalikuwa Sh73.66 bilioni,’’ alisema.

Wednesday, June 8, 2011

NATO: Time to plan for post-Gadhafi Libya

(CNN) -- It is time to start planning for what to do in Libya after leader Moammar Gadhafi's departure "because Gadhafi's reign of terror is coming to an end," NATO Secretary General Anders Fogh Rasmussen said Wednesday.

Rasmussen, talking with reporters in Brussels, insisted that NATO bombing had saved lives in Libya.
Pressed by reporters on why airstrikes will be able to dislodge Gadhafi when "the history of the last 30 years" shows that air attacks alone do not win wars, Rasmussen offered no clear answer, saying only, "We have no intentions to put troops on the ground."

He said the alliance had agreed to extend its military mission for another 90 days past the end of June and had the resources it needed to keep up the campaign for that long.

But he refused to predict how long it would take, saying: "We will keep up the pressure for as long as it takes to bring this crisis to an early conclusion."
Gadhafi vowed Tuesday that "we will not surrender," even as NATO airstrikes bombarded his compound in Tripoli.
"I am now speaking as planes and bombs fall around me," Gadhafi said in a live audio broadcast on state television. "But my soul is in God's hand. We will not think about death or life. We will think about the call of duty."

At least three explosions rocked Tripoli late Tuesday night; it was not immediately clear what they hit.
Earlier in the day, NATO targeted a military base and Gadhafi's compound, state television reported. A spokesman for the Libyan government said that at least 31 people were killed, including a number of civilians, and dozens more were wounded after 60 missiles struck the capital city.

Rasmussen reiterated Wednesday that the alliance was doing all it could to avoid civilian casualties.
The Gadhafi compound was under "intensive continuous bombardment," according to state TV, which reported buildings and infrastructure were destroyed.

The blasts Tuesday, and others Monday that Libyan officials said hit state television buildings, elicited heated responses from the government spokesman.
"We believe NATO understands that its military campaign is failing miserably," said spokesman Musa Ibrahim. "No one has the right to shape Libya's future except for Libyans."
Ibrahim said Tuesday's morning blasts hit the popular guard compound and revolution compound, which are military barracks near Gadhafi's Bab al-Aziziya compound.

The spokesman said the attack on the television network killed two people and wounded 16.
NATO disputed the account.

"We did not target or hit the Libyan broadcast facilities. What we did target was the military intelligence headquarters in downtown Tripoli," the alliance said. "The story coming from Libyan officials that we targeted and hit the state broadcaster's building is bogus."
The back and forth between Libyan officials and NATO continues a public relations war between the two sides. Libyan officials have continually charged that NATO airstrikes have damaged civilian facilities and killed hundreds of civilians.

This week, the Libyan government said it had evidence that alliance airstrikes were harming civilians.
Officials took journalists to Tajura, a city east of Tripoli, to show them a small crater that held what appeared to be the remains of a rocket.

The reporters were also taken to nearby homes that the government said had been damaged by airstrikes.
NATO said it had been active in the area hitting military sites but could not say whether the attacks had caused the damage in the residential area.

Reporters were also taken to a nearby hospital to see Nasib, a comatose baby who was a victim of the airstrikes, the government said.

A woman, who the government said was Nasib's mother, cried over the child's listless body.
Journalists were not allowed to talk to the woman or to the doctors. But one doctor quietly slipped a note to one of the journalists that said the girl was injured in a car accident, not a bomb attack.

British Foreign Secretary William Hague, speaking Tuesday to British lawmakers, said the European Union has added six additional ports controlled by pro-Gadhafi forces to its sanctions list in an effort to starve Gadhafi's troops of military supplies.

He said the United Kingdom intends to push for additional sanctions against Gadhafi's regime.
"Any political settlement in Libya requires an end to violence and Gadhafi's departure," Hague said.

LEO NI BAJETI

Mawaziri wapigia debe bajeti 

MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa. Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta.

Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha.

Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo.

Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, bajeti ya serikali imekuwa ikisomwa siku za Alhamisi ya wiki ya kwanza ya Juni, lakini mwaka huu imebadilika ikielezwa kwamba hiyo ni kutokana na siku hiyo kuangukia siku ya Uhuru wa Uganda.

Akizungumza bungeni jana asubuhi, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema bajeti hiyo itatanguliwa na hotuba ya hali ya uchumi itakayosomwa pia na Waziri Mkulo. Alisema hotuba hiyo itasomwa asubuhi, wakati ile ya bajeti itasomwa jioni.

Baadhi ya mawaziri akiwamo Mkulo wameifagilia bajeti hiyo huku Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) likitoa mapendekezo na matumaini yake.

CTI: Tunataka bajeti ya uchumi wa viwanda

Shirikisho hilo limesema kuwa linaisubiri kwa hamu bajeti hiyo likitaka iwe ya kukuza uchumi na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji. Kauli ya CTI huku likilalamikia kupanda kwa gharama za uzalishaji zilizotokana na mgawo wa umeme wa Tanesco.

Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, Christine Kilindu alisema jana kwamba serikali inapaswa kutoa bajeti ambayo pia itaondoa kodi zinazoumiza uzalishaji mkubwa. Alisema kodi kubwa zisizo za msingi zinachangia kupanda kwa gharama za uzalishaji ambao mwishowe husababisha kupanda kwa gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida. 

"Tunataka bajeti ambayo itaondoa kodi zinazokwamisha uzalishaji mkubwa na ukuaji uchumi, tunataka bajeti itakayopunguza makali ya maisha kwa mwananchi kwa kumwezesha kupata bidhaa kwa urahisi," alisema Kilindu.

Alisema bajeti hiyo inapaswa pia kuweka mazingira mazuri na yanavyovutia kibiashara ili kuifanya Tanzania kuwa kituo muhimu cha uwekezaji. Alisema kwamba anategemea kuona umeme ukiwekewa mazingira ya kukuza uchumi na uwekezaji nchini, akisema bila kufanya hivyo hakuna kitu kitakachofanyika.

"Bila umeme hakuna kitu chochote, serikali inapaswa kuongeza nguvu na msukumo kuona umeme siyo tu unamulika maisha ya watu kwa kutoa mwanga, bali iwe ni nguvu ya kusukuma ukuaji wa uchumi wa nchi."

Mawaziri wapigia debe bajeti

Katika kujiwekea mazingira mazuri na kuzuia kubanwa na wabunge, baadhi ya mawaziri wamepigia debe bajeti za wizara zao huku Mkulo, akiahidi kuwa malimbikizo ya vyombo vya usalama yatalipwa mwezi huu.

Mara kwa mara baadhi ya wabunge wamekuwa wakitishia kukwamisha baadhi ya bajeti za wizara, kutokana na kukosa majibu ya msingi kwa mambo mbalimbali ya msingi. Jana asubuhi baadhi ya mawaziri walipokuwa wakijibu maswali bungeni walisisitiza kuwa mambo mengi waliyokuwa wakiulizwa yamezingatiwa katika bajeti.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Hamis Kagasheki, akijibu swali kuhusu malipo ya malimbikizo ya posho za polisi ikiwamo za wakati wa uhamisho, alisema wizara yake imeandaa mwongozo wa kisera wa namna ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.Alisema katika mwongozo huo ambao tayari ulikubaliwa na Wizara ya Fedha na Uchumi, wizara yake imejipangia utaratibu wa kutatua kero hiyo kuanzia kwenye bajeti ya mwaka huu.

Balozi Kagasheki alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Mohammed Sanya, ambaye alitaka kujua mkakati huo ukoje kutokana na tatizo hilo kuwa ni la muda mrefu. Baada ya majibu hayo, Waziri Mkulo alisimama na kukuongeza kuwa siyo malimbikizo ya polisi pekee, bali ya vyombo vyote vya usalama na kwamba serikali imejipanga kuhakikisha yanalipwa kabla ya mwezi huu kumalizika.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe naye alipigia debe bajeti ya wizara yake ambayo tayari ilisifiwa na Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kutokana na kugusa kila eneo huku ikitajwa kuandaliwa kwa weledi wa hali ya juu.

Akijibu maswali likiwamo lililohusu ujenzi wa Barabara ya Babati, Dareda hadi Minjingu na kuhusu kero za barabara katika Jimbo la Ludewa linaloongozwa na Profesa Raphael Mwalyosi, Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa wizara yake ni sikivu na mambo mengi yatazingatiwa ndani ya bajeti.

Alisema wizara iko makini na Bajeti ya Ujenzi imezingatia mambo mengi ya msingi huku akitupa kete ya kuomba uungwaji mkono kwa wabunge ili waipitishe.

Tuesday, June 7, 2011

5 FACTS IN THE WORLD.... Joke

FACT 1: You cannot touch all your teeth with your tongue!!!


FACT 2: After reading the first fact, all fools will try it


FACT 3: Fact 1 is false, ha ha ha



FACT 4: Now you are laughing because you are one of the fools


FACT 5: You are going to forward this now because you don't want to be the only fool