MWANAMKE mkazi wa Ronsoti mjini Tarime mkoani Mara, Debora James (30), anatuhumiwa kumuua mwenzake, Teresia Nago, kwa kumchoma kisu katika mauaji yanayohusisha kugombea mwanamume.
Kwa mujibu wa Polisi, Teresia aliuawa jana saa 4.30 asubuhi Bomani mjini Tarime, baada ya kuchomwa visu viwili tumboni na kifuani na mgomvi wake huyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rorya/Tarime, Sebastian Zakaria, alisema Debora alikuwa akituhumiwa kuwa na uhusiano na mume wa Teresia, John Nago ambaye ni mtumishi wa Idara ya Ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Kaimu Kamanda alisema, wanawake hao wawili walikuwa na ugomvi wa muda mrefu na vurugu wakigombea mwanamume huyo.
Alisema, jana Teresia na Debora walikwenda kusuluhishwa na mzee wa Kanisa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja eneo la Bomani.
Lakini wakiwa Bomani, kulitokea vurugu na Debora ambaye alikuwa na kisu alimshambulia Teresia kwa kumchoma kisu kifuani karibu na moyo na tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo, baada ya kutokwa damu nyingi naye akajichoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake kwa lengo la kujimaliza.
Kamanda Zakaria alisema Debora amelazwa katika hospitali ya wilaya mjini hapa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kujijeruhi.
Showing posts with label tarime. Show all posts
Showing posts with label tarime. Show all posts
Wednesday, June 29, 2011
Friday, May 27, 2011
CUF yamtaka Nahodha ajiuzuru
*Yalaani, yasema huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu
BARAZA Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) limemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani kuwajibika kutokana na mauaji yaliyotokea wilayani Tarime lakini pia kufanyika kwa uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo.
Hatua hiyo ilifikiwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyoazimiwa na kikao cha baraza hilo.
Alisema kuwa baraza hilo linalaani vitendo vya ukiukaji na uvunjaji wa haki za binadamu hususan mauaji ya raia yanayofanywa na Jeshi la Polisi ambayo yamekuwa yakiripotiwa kila mara.
"Inatuumiza sana kwa kuwa inaonekana jambo hili ni la kawaida kwa sababu watendaji wake hawachukuliwi hatua yoyote," alisema.
Prof. Lipumba alisema kuwa baraza hilo pia linamtaka Rais Jakaya Kikwete kutambua kuwa jukumu la kuleta maendeleo ya Watanzania ni la watu wote hivyo serikali yake isisite kutumia sera mbadala za CUF kwa maendeleo ya taifa.
Alisema serikali kupitia wizara ya Fedha na Uchumi na Wizara ya Nishati na Madini inatakiwa kuchukua hatua za kuhakikisha nchi na wananchi wake wananufaika na rasilimali za madini zilizopo hapa nchini hususani madini ya dhahabu ambayo bei yake katika soko la dunia imepanda.
"Dhahabu inayouzwa nje ni dola bilioni 1.5 kwa mwaka sawa na asilimia 40 ya bidhaa za Tanzania zinazouzwa nje ya nchi," alisema.
Alisisitiza kuwa baraza hilo linataka kuona utajiri wa nchi unawanufaisha wananchi na kuisaidia nchi kujikomboa kutoka katika dimbwi la umasikini na kuacha kutegemea misaada kutoka nje ambayo imeifanya nchi kuwa tegemezi kwa miaka mingi.
Aliongeza kuwa baraza hilo linamtaka Waziri wa Nishati na Madini Bw.William Ngeleja kujiuzulu kwa kuwa ameshindwa kutumia vyanzo vya umeme vilivyopo nchini ili kukabiliana na tatizo sugu la nishati linaloikumba nchi yetu kwa sasa.
Alisema nchi imejaliwa vyanzo vingi ya umeme na maeneo mengi ya maporomoko ya maji, makaa ya mawe, madini na hata umeme wa jua ambao hauna gharama kubwa ya kufua.
"Ni miaka 50 tangu tupate uhuru hatuna sababu yoyote ya kutokuwa na umeme wa uhakika, ni ufisadi tu ambao umekithiri katika serikali yetu," alisema.
Alisisitiza kuwa serikali ni lazima itambue kuwa hali ya kutokuwa na umeme wa uhakika imezorotesha uzalishaji viwanda,biashara,huduma katika hospitali na shule hivyo kusababisha uchumi wa nchi kuzorota.
Aliitaka serikali kuzingatia mapendekezo na hoja zinazotolewa na kamati ya Nishati na Madini ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zinazolenga kupata ufumbuzi wa matatizo ya umeme.
Pia alisema baraza hilo linaitaka serikali kuwa makini katika suala zima la utunzaji na uhifadhi wa silaha nzito za kivita zenye madhara makubwa na kutaka zihifadhiwe mbali na makazi ya watu ili matukio ya milipuko ya mabomu ambayo yameshatokea mara mbili yasijirudie tena.
Thursday, May 26, 2011
Lissu na wenzake marufuku Nyamongo
| Maiti wazikwa, wananchi wataka kurejesha majeneza polisi |
MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, na wenzake saba ambao juzi walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kusomewa mashtaka matatu ya kuingia eneo la hospitali bila kibali, kufanya mkutano na kuzuia watu kufanya kazi, wamepata dhamana lakini wamezuiwa kutembelea maeneo ya Nyamongo hadi kesi inayowakabili itakapokwisha. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Yusto Roboroga alitoa uamuzi huo akisema ni kwa mujibu wa kifungu cha Sheria Namba 148 cha Makosa ya Jinai, kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambacho kinatoa haki kwa watuhumiwa kupata dhamana. Alitoa uamuzi huo baada ya kupitia pingamizi lililowekwa na upande wa mashtaka kutaka wasipewe dhamana. Hata hivyo, alisema: “Washtakiwa wanazuiwa kutembelea maeneo ya Nyamongo mpaka kesi hiyo itakapokuwa imekwisha." Hakimu huyo alisema kwa kuwa washtakiwa hao ni viongozi wakubwa wa chama walizuiwa ili kupunguza shinikizo la wanachama kutokana na tukio lililojitokeza, lakini kwa kuwa mazishi yameshafanyika, alisema wanaweza kudhaminiwa kama watakidhi masharti. Hakimu Ruboroga alitaja masharti ya dhamana hiyo kuwa ni kusaini mkataba wa dhamana wa Sh5 milioni kwa wadhamini wawili wanaoaminika. Kwa wasio wakazi wa Tarime, alisema watatakiwa kupeleka mahakamani hati za mali isiyohamishika. Washtakiwa wote walikidhi masharti na kuachiwa kwa dhamana hadi Juni 26, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Juzi, Lissu na wenzake, Waitara Mwita Mwikwabe, Stanslaus Nyembea, Anderson Deogratias Chacha, Andrew Andalu Nyandu, Mwita Marwa Maswi, Bashiri Abdalllah Selemani na Ibrahimu Juma Kimu walifikishwa mbele ya mahakama hiyo na kusomewa mashtaka hayo matatu na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Casmir Kiria ambaye alisema, waliyatenda Mei 23, majira ya saa nne usiku. Wote walikana mashtaka hayo. Wakati huo huo maiti wote waliokuwa wametelekezwa barabarani wamezikwa na ndugu zao huku baadhi ya familia zikikataa kuwazika kwa majeneza ya polisi na kutumia yale yaliyokuwa yameandaliwa huku wengine wakipanga kuyarudisha kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime, Constantine Massawe. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kewanja, Om’tima Tanzania alisema kuwa mmoja wa marehemu hao, Chacha Ngoka alizikwa na jamii. Hata hivyo, alisema polisi waliweka mwili wake ndani ya jeneza bila kuweka sanda hali ambayo iliwalazimu kumweka ndani ya jeneza lao na kumvika sanda. Hilo lilifanyika pia katika eneo la Nyakunguru alikozikwa marehemu Emmanuel Magige. Katika Kijiji cha Bonchugu, Serengeti, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Mwikwabe Makena alidai kwamba walilazimika kuzika mwili wa marehemu Chawali Bhoke uliotelekezwa na polisi. Alidai kwamba kabla ya kuutelekeza, walifyatua mabomu ya machozi na risasi hewani baada ya wananchi waliokuwa wamebeba pinde, mishale, mikuki na mapanga kujaribu kuzuia gari la polisi. Alisema walilazimika kuzika bila kuwapo kwa ndugu wa marehemu waliokuwa wameachwa Tarime.Hata hivyo, Kamanda Massawe na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz hakuwa tayari kuzungumzia madai hayo. |
Wednesday, May 25, 2011
Polisi 'wapora' maiti mochwari
*Tundu Lisu akamatwa, afikishwa kortini Tarime
JESHI la Polisi limewakamata na kuwafikisha mahakamani Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na maofisa wengine wa chama hicho baada ya kudaiwa kufanya mkusanyiko usio halali na kuzuia watu kuzika ndugu zao.
Sambamba na hatua hiyo jeshi hilo limedaiwa kuingia mochwari ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime na kuchukua kwa nguvu maiti nne za watu waliouawa na polisi hivi karibuni na kwenda kuzitelekeza maeneo mbalimbali ili kuzuia mkusanyiko wa kuaga maiti hizo kwa pamoja, kwa kile wanachoeleza ni kuzuia uvunjifu wa amani.
Bw. Lisu na wenzake wanadaiwa kukutwa katika Hosptali ya Wilaya ya mjini hapo wakilinda miili hiyo baada ya kusikia tetesi kuwa polisi walikuwa na mpango wa kuichukua na kuisafirisha kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Bw. Casmil Kria alisema watuhumiwa wanakabiliwa na mashtaka matatu, yaliyosomwa mbele ya Hakimu wa Wilaya, Bw. Yusto Ruboroga.
Mashtaka hayo ni kuingia eneo la hospitali bila kibali, kufanya mkusanyiko usio halali na kuzuia watu kuchukua miili ya ndugu zao.
Watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kukutwa eneo hilo saa 4:00 usiku baada ya kusomewa mashtaka na kuyakana, walirudishwa rumande kwa 'sababu za kiusalama', na kesho watafikishwa tena mahakamani kwa ajili ya kupewa dhamana, endapo miili ya waliouawa itakuwa imeshazikwa.
Walioshtakiwa ni Mbunge wa Singida Magharibi, Bw. Tundu Lissu (43), Bw. Mwita Mwikwabe (36), Bw. Stancelaus Nyembea (33), Anderson Deogratias (35), Bw. Andrew Andaru (63), Bw. Mwita Marwa (48) Bw. Bashiri Abdallah Seremani (35) pamoja na Ibrahimu Juma Kimi (27) ambaye ni dereva wa Bw. Lissu.
Wakati huo huo, waandishi wanne wa habari pamoja na Mbunge Viti Maalumu, Bi. Ester Matiko (CHADEMA) nao walishikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kidogo cha Nyamwaga na baadaye kuachiwa huru baada ya mahojiano.
Wandishi hao ni Bi. Beldina Nyakeke wa The Citizen, Anna Mroso (Nipashe), Bw. Anthony Mayunga (Mwananchi) pamoja na Mabere Makubi wa Chanel Ten ambao walikuwa kwenye msafara wa Bi. Matiko.
Waandishi wengine wa habari waliofika katika mahakama ya wilaya kufuatilia tukio hilo walizuiliwa kuingia na kutishiwa kupigwa
risasi na ofisa mmoja wa polisi.
Ofisa huyo ambaye hakufahamika jina aliwatimua waandishi hao, huku akiomba bunduki kutoka kwa askari mwenzake na kuiandaa mithili ya kupambana na adui.
“Toka! Toka! Naombeni bunduki yangu hapa naona nyinyi hamjui kufanya kazi, hatukuja kufanya mchezo hapa waondoe na wale watu upesi mahali hapa wasongee mbali huko hatutaki mtu hapa!” alisema.
Askari hao wakiwa wameziba njia huku ofisa huyo akiendelea kuelekeza bunduki yake kwa raia waliokuwa eneo hilo.

Wednesday, May 18, 2011
Polisi waua watano
POLISI wameua watu watano na kujeruhi wengine kadhaa katika mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold, Tarime mkoani Mara.
Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi zilisema tukio hilo lilitokea jana alfajiri katika eneo la Nyabirama.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Constantine Massawe, alisema askari walilazimika kutumia risasi za moto baada ya kutumia mabomu ya machozi bila mafanikio kutawanya kundi la watu waliojaribu kuingia kwa jinai na kupora mawe yenye dhahabu mgodini.
“Askari walilazimika kutumia risasi kukabiliana na watu wanaokadiriwa kuwa kati ya 800 na 1,000 waliokuwa wamevamia mgodi huo ili kuokota mawe yenye dhahabu,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamanda Massawe, watu watatu walikufa katika eneo la tukio na wengine wawili walifia katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime. Majina yao hayakufahamika mara moja.
Hata hivyo, Kamanda huyo alitaja baadhi ya majina ya majeruhi waliolazwa hospitalini hapo kuwa ni Francis Emmanuel (20) mkazi wa kijiji cha Kewanja, Chacha Mwasi (23) mkazi wa kijiji cha Bisarwi wilayani Tarime na Mwikwabe Marwa (30) mkazi wa Mugumu wilayani Serengeti.
Alidai kwamba polisi wawili waliofika eneo la tukio walijeruhiwa kwa mawe yaliyokuwa yakirushwa kwa kombeo.
Akizungumzia tukio hilo kwa simu kutoka Dar es Salaam, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM), alilaani mauaji hayo na kuahidi kuchukua hatua.
Alilaani matumizi ya nguvu kubwa yaliyofanywa na polisi kukabiliana na wananchi waliojaribu kuvamia mgodi.
“Ninalaani sana kitendo cha askari kutumia nguvu kubwa ya kuua na kujeruhi wananchi kwa tuhuma za kuvamia mgodi. Nitachukua hatua kali dhidi ya wote waliohusika katika tukio hilo la kusikitisha,” alisema Nyangwine bila kutaja aina hiyo ya nguvu alizoahidi.
Kamanda Massawe alisema ofisi yake inakusudia kuitisha mkutano maalumu wa viongozi wa mgodi wa dhahabu wa North Mara na wakazi wa vijiji vilivyo jirani kutafuta ufumbuzi thabiti wa matukio ya uvamizi na mauaji ambayo yamekuwa yakitokea mgodi hapo.
Alitoa wito kwa wananchi kuepuka vitendo vya uvamizi na uporaji mali katika mgodi huo kwa vile unamilikiwa kihalali na kampuni ya African Barrick Gold.
Wimbi la matukio ya uvamizi, uporaji mawe yenye dhahabu na mauaji ya watu katika mgodi wa dhahabu wa North Mara limeendelea kuwepo, huku baadhi ya askari, walinzi na wafanyakazi wa mgodi huo wakituhumiwa kupokea rushwa ya fedha na kuruhusu watu kuingia kuokota mawe yenye dhahabu.
Labels:
African Barrick Gold,
Kamanda,
mwema,
North Mara,
polisi,
tarime,
waua
Subscribe to:
Posts (Atom)