Wednesday, February 23, 2011

Wasanii wa kike hutembea na producers

Kumekuwa na fununu kwamba ili msanii wa kike apangwe kucheza filamu au kutoa kazi yake toka studio hana budi kutembea na producer, yani kutoa rushwa ya ngono. Je kuna ukweli wowote kuhusu suala hili? Wanaharakati mmefatilia na kuona kama kuna udhalilishaji wa namna hii? Naomba mchango wenu wadau.

Kwa nini makundi ya wasanii huvunjika?

Tanzania kuna makundi mengi sana ya wasanii, hasa wa filamu, muziki wa kizazi kipya, na ngoma. Makundi haya huwa na malengo ya kuendeleza vipaji vyao na kujipatia ajira. Utakuta kundi limetoa filamu au album yao na kuanza kupata mafanikio. La kushangaza ni pale ambapo baada ya muda mfupi tu wanaanza malumbano, ugomvi na hatimaye kundi kuvunjika. Napenda kufahamu kama kuna mtu ameona au imetokea kwenye kundi lake atuambie sababu ilikuwa nini, na wengine wachangie nini kifanyike ili mambo hayo yasijirudie na hatimaye tuendeleze sanaa na ajira nchini.