Thursday, September 6, 2012

Wachimba migodi waliosalia waachiliwa


Wachimba migodi 106 waliosalia kuzuiliwa na polisi nchini Afrika Kusini wameachiliwa baada ya kesi tatanishi dhidi yao kutupiliwa mbali kufuatia shinikizo za umma.
Wachimba migodi hao wanatarajiwa kurejea katika mgodi wa Marikana ambako polisi waliwapiga risasi na kuwaua wenzano 34 waliokuwa wanagoma mwezi jana.
Chama kimoja cha wafanyakazi kiimekataa kutia saini mktaba wa amani na serikali pamoja na wamiliki wa mgodi huo, Lonmin,wakisisitiza kuwa wataendelea kugoma hadi matakwa yao yatakapotimizwa.
Mgomo huo uliitishwa na chama cha wafanyakazi wa migodini na wale wa ujenzi. wadadisi wansema kuwa hatua ya chama hicho kukataa kutia saini mktaba huo, heunda isiathiri kivyovyote mgogoro unaoendelea
Chama cha wafanyakazi cha NUM ambacho kina uhusiano na chama tawala, ANC, kilitia saini mkataba huo ulioafikiwa kwa usaidizi wa viongozi wa makanisa.
Hapo awali, mwanaharakati wa kisiasa nchini Afrika Kusini, Julius Malema, alitoa wito wa wachimba migodi kuendelea na mgomo wao hadi matakwa yao yatakapotimizwa na waajiri wao.
Tamko la Malema linakuja wakati mgogoro wa mishahara kati ya wachimba migodi wa Marikana na waajiri wao ukitokota.
Bwana Malema hata hivyo anasema kuwa tamko lake sio uchochezi wa ghasia.
Takriban wachimba migodi, 34 waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi tarehe kumi na sita mwezi Agosti.
Wachimba migodi zaidi walioshtakiwa kwa madai ya kusababisha mauaji hayo, wanatarajiwa kuachiliwa baadaye leo.
Vyama kadhaa vya wafanyakazi, vimetia saini makubaliano yatakayowafanya kurejea kazini, kulingana na wamiliki wa migodi hiyo.
Bwana Malema anatarajiwa kuzuru mgodi wa Marikana hii leo, siku moja baada ya wachimba migodi 3,000 kuandamana kuunga mkono wachimba migodi wenzao
Aidha Malema, ambaye alikuwa kiongozi wa chama cha ANC tawi la vijana, alifukuzwa chamani baada ya kuonekana kutofautiana kwa sera na Rais Jacob Zuma.
Bwana Malema awali aliwataka wachimba migodi hao kuendelea kutatiza shughuli za migodi.
Aliambia BBC kuwa '' Watu wametafsiri visivyo wito wangu kwa wachimba migodi kutatiza kabisa shughuli za migodi. Nilicho maanisha ni kwamba waendelee kugoma. Sipendekezi, ghasia wala vurugu wala sitoi wito wa mauaji. Wafanyakazi hawapaswi kukubali kunyanyaswa. Hatutaki dhulma tena, ila ikiwa tu serikali itakubali kuwalipa pesa za kutosha ''
Malema alisema muwa waekezaji wa kigeni wameiba kila kitu nchini Afrika Kusini na akasema kuwa wako tayari kufanya kila hali kurejeshewa kila kilicho chao.
Alisema jibu lililosalia kwa matatizo ya migodini ni kutaifisha migodi.
Siku ya Jumatano, wachimba migodi wa Marikana, walifanya maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mauaji ya wafanyakazi wenzao kuzua hisia kali.
Wachimba migodi hao wanaolipwa kati ya dola miatatu na mianne wanataka nyongeza ya hadi dola miasaba au mianane kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment