SAKATA la samaki wanaodaiwa kuwa na sumu kutoka Japan walioingizwa nchini, limefikishwa bungeni na wabunge wameitaka Serikali ifafanue ukweli wa jambo hilo ikiwa ni pamoja na kueleza ni namna gani waliingizwa.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kambi ya Upinzani pamoja na wabunge waliochangia jana bungeni kwa nyakati tofauti, walieleza kushitushwa na taarifa hizo na wakataka Serikali itoe tamko bungeni.
“Kuna taarifa kwamba samaki wenye sumu wameingizwa nchini, pamoja na uzito wa jambo hili, Serikali haijatoa tamko. Kwa mamlaka niliyo nayo, naitaka Serikali itoe tamko ieleze ukweli wa suala hili na hatua zinazochukuliwa,” alisema Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba (CCM) kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati, Profesa David Mwakyusa.
Mbunge huyo alikuwa akisoma taarifa ya Kamati ya Bunge kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Makadirio ya Matumizi ya mwaka 2011/12.
Kambi ya upinzani kupitia kwa Msemaji wake Mkuu kwa Wizara ya Maendeleo na Mifugo, Silvester Kasulumbayi, ikitumia taarifa za vyombo vya habari vya Julai 26, ilihoji ni namna gani kampuni ya Alphakrust Limited ya Dar es Salaam, iliruhusiwa kuingiza samaki hao.
“Kama TDFA ndiyo waliotoa kibali cha kuingizwa kwa samaki hao baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha kuwa hawana madhara, ni nani na wa mamlaka gani aliyegundua kuwa wana madhara? Ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya maofisa waliohusika kutoa kibali husika?” alihoji Kasulumbayi.
Wabunge hao wa upinzani walihoji sababu ya Tanzania yenye maziwa na bahari kuagiza samaki kutoka nje ya nchi. “Kwa rasilimali hii yote tuliyopewa na Mwenyezi Mungu iliyojaa samaki wengi wa kila aina, kama Taifa tuna haja kweli ya kuagiza samaki kutoka nje ya nchi?
“Kwa nini fedha zetu za kigeni zisitumike kununua mahitaji mengine ambayo hayapatikani nchini?” aliendelea kuhoji.
Naye Amir Mhando, anaripoti kwamba Mbunge wa Nyamagana Ezekia Wenje na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, wote wa Chadema jana ‘walichafua hewa’ kwa muda kwenye ukumbi wa Bunge kutokana na hoja zao tofauti.
Hatua hiyo ilisababisha Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Dole, Sylivester Mabumba (CCM), kumtoa nje ya ukumbi Wenje na pia kumtaka Lissu athibitishe kauli yake, kwamba Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa, amesema uongo bungeni.
Zogo lilianza muda mfupi baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu saa nne asubuhi, wakati Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), aliposimama na kuomba kutoa taarifa kuhusu tukio lililotokea mapema wakati wa kipindi cha maswali na majibu likimhusisha Lissu.
Machali alisema isingekuwa busara kwa Lissu kuambiwa apeleke uthibitisho wake kwa Mwenyekiti kuhusu kauli kwamba Naibu Waziri kasema uongo.
Alisema badala yake Lissu alitakiwa afanye hivyo saa tano asubuhi, wakati muda huo ilikuwa saa nne, huku shughuli zikiendelea, hivyo angepewa nafasi mpaka saa saba mchana wakati shughuli za Bunge zinapokuwa zimesitishwa kwa muda.
Lakini akizungumzia jambo hilo, Mwenyekiti Mabumba alisema kwa vile Lissu wakati anatoa kauli hiyo alisema ana ushahidi ambao angeweza kuuwasilisha hata wakati anazungumza, hilo si tatizo na kuongeza kuwa wakati anatoa kauli yake pia alishaanza kugusia uthibitisho wake.
Kutokana na majibizano hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisimama na kusema hakuna haja ya wabunge kuvimbiana na kwa vile Lissu aliahidi mwenyewe apeleke na kama ataona muda hautoshi amwambie Mwenyekiti amwongeze muda.
Baada ya kauli ya Lukuvi, Wenje alisimama na kuomba Mwongozo wa Mwenyekiti, lakini hakuruhusiwa na kusikika akiita mara kadhaa: “Mwenyekiti hoja ya dharura… hoja ya dharura Mheshimiwa Mwenyekiti ”.
Mwenyekiti alijibu kuwa hakuna haja ya hoja ya dharura, kwani hoja hiyo inawasilishwa kama kuna vita na nchi sasa haina vita, hivyo kumtaka Katibu aendelee na ratiba nyingine, ambayo ilikuwa ni hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Lakini Wenje aliendelea kumwita Mwenyekiti na kutaka Mwongozo, huku Mwenyekiti naye akimtaka akae chini, lakini waliendelea kubishana kwa dakika kadhaa na Mwenyekiti kutishia kumtoa nje ya kikao.
Hata hivyo bado Wenje hakutii agizo la Mwenyekiti, ndipo alipoagiza askari wamtoe ukumbini na hatua hiyo kutekelezwa mara moja, huku baadhi ya wabunge wakilalamika chini chini hasa wa upinzani, wakati wa CCM wakipiga meza zao kuunga mkono.
Akizungumza nje, Wenje alisema Mwenyekiti hakumtendea haki kwani hoja yake ya dharura aliyokuwa anataka izungumzwe ni kuhusu taarifa ya kuingizwa nchini kwa samaki wenye sumu kutoka Japan.
Alisema taarifa alizonazo ni kuwa kuna tani 1,600 za samaki hao mitaani hazijakamatwa na Polisi na wananchi wanawatumia na hali hiyo ni hatari na jambo linalohitaji udharura.
Showing posts with label samaki. Show all posts
Showing posts with label samaki. Show all posts
Thursday, July 28, 2011
Tuesday, July 26, 2011
Kilo 1000 za samaki wa sumu zasambazwa Dar, Morogoro
![]() Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa samaki hao ni sehemu ya kilo 124,992 zilizoingizwa nchini kutoka Japan. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tayari Serikali imeanza msako mkali kuwatafuta samaki hao, lakini ikaonyesha wasiwasi kwamba juhudi hizo huenda zisizae matunda kwa kuwa sehemu ya shehena hiyo imeshaingia sokoni. Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa samaki hao tayari wameingizwa katika masoko ya Dar es Salaam na Morogoro. “Wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Idara za Afya za Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro na Jeshi la Polisi, ili samaki waliobaki wapatikane,” alisema Nyoni. Nyoni aliutahadharisha umma kuwa athari za sumu inayohofiwa kuwapo kwenye samaki hao ni ya mionzi ya nyuklia ambayo kimsingi hujitokeza taratibu katika mwili wa binadamu.“Samaki wenye uzito wa tani 1.319 wanafuatiliwa na kumbukumbu zinaonesha kuwa wamesambazwa kupitia soko la Feri, Dar es Salaam, Morogoro Mjini na Kilombero,”alisema Katika kuhaha ili kuokoa maisha ya Watanzania, Nyoni anasema: “Wizara inaviomba vyombo vya habari, viiarifu na kuielimisha jamii juu ya kuwepo kwa samaki hao wanaochunguzwa kwa kuhisiwa kuwa na madhara.” Pamoja na juhudi hizo, alifafanua “kazi hii ya ufuatiliaji na uchunguzi, inaendelea usiku na mchana hadi samaki hao watakapopatikana.” Samaki hao wametoka wapi? Nyoni alisema samaki hao aina ya “Mackerel” waliingizwa nchini na kampuni ya Alphakrust Ltd ya Dar es Salaam kutoka kampuni ya Kaneyama Corporation ya Chiba, Japan. “Samaki hao walisafirishwa kupitia Bandari ya Yokohama, Japan na kuingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Nyoni akidai kuwa taarifa zinaonyesha waliingizwa baada ya kukidhi masharti ya kisheria na taratibu zilizowekwa “Kwa mujibu wa nyaraka za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mzigo huo ulifika Bandari ya Dar es Salaam tarehe 18 Julai, 2011,” alisema Nyoni na kuongeza: “Wizara ilipata taarifa siku ya Jumamosi kwamba samaki hao wanahisiwa kuchafuliwa na mionzi ya nyuklia iliyotokea huko Japan, mwezi Machi, 2011.” Nyoni alisema hadi kufikia juzi asubuhi, kiasi cha samaki wenye uzito wa tani 123.673, kati ya tani 124.992 walioingizwa nchini, walipatikana na kuzuiliwa katika maghala ya kampuni ya Alphakrust Ltd.Kufuatia taarifa hiyo, Nyoni alisema wizara yake iliiagiza TFDA kuchukua hatua za haraka za kuzuia usambazaji wa samaki hao hadi uchunguzi utakapokamilika. Alisema samaki hao walisindikwa tangu Desemba mwaka jana na muda wake wa mwisho kutumika ni Juni, 2012.Alisema samaki hao waliruhusiwa kuingizwa nchini kwa kibali cha TFDA namba TFDA11/F/IPER/0896, cha Julai 11 2011. Wauzaji wanasemaje? Baadhi ya wauzaji wa samaki wa Soko Kuu la Feri, walisema hatua ya Serikali ya kusitisha usambazaji wa samaki hao, imechelewa kwani tayari sehemu kubwa ya mzigo ilishauzwa. “Hawa Kamongo ni Samaki adimu sana, Ijumaa tulipopata taarifa kuwa mzigo umeshuka, haraka tulifika kule Jet ambapo ndiyo kuna hilo ghala la Wajapani kwa ajili ya kununua,” alisema Juma Rashid kuongeza: “Tulifika pale na watu wa vipimo wakaingia na DFP yao (namba za ushajili za gari), wakafungua kontena wakapima halafu wakatuambia mzigo uko safi. Tukachukua kila mtu kwa kiasi alichotaka, mpaka Jumapili wanakuja kukamata mimi nilishamaliza mzigo wangu wa boksi tano wote.” Kwa mujibu wa wachuzi hao, boksi moja la samaki hao ambalo lina uzito wa kilo15, linauzwa Sh51,000 kwa bei ya jumla.Juma Amiri (45), alisema shughuli ya kukamata samaki hao ikifanyika Jumapili, alikuwa amebaki na boksi moja tu.Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Samaki sokoni hapo, Abdala Mjanga, alisema hana taarifa rasmi za suala hilo, lakini alishuhudia kamata kamata hiyo iliyokuwa ikiendeshwa sokoni hapo. Kauli ya TFDA Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Hiiti Silo alisema taarifa hiyo ya wizara ni msimamo wa Serikali na idara zake zote ikiwamo TFDA "...Lakini TFDA tunafanya uchunguzi kwa kasi ili tuimalize kazi hiyo mapema kuokoa maisha ya watu," alisema. |
Subscribe to:
Posts (Atom)