Wednesday, December 21, 2011

Viongozi dhalimu komeni

Na editor
 
Maoni ya Mhariri
TAARIFA za viongozi wa serikali ya wilaya ya Meatu “kufungia wananchi” ili wasitoe malalamiko yao kwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kapteni George Mkuchika zinasikitisha sana.
Kwa kuamini kwamba siri waliyoitunza haitafichuka kwa namna yoyote ile, viongozi hao chini ya Mkuu wa Wilaya yao wakajikuta wanaadhirika. Wananchi walivujisha “siri” hiyo kwa waandishi wa habari ambao walimsimulia waziri kama anafahamu suala hilo.
Zaidi ya askari polisi 30 waliobeba silaha za moto pamoja na mabomu ya kutolea machozi, walizingira kijiji cha Mwangudo kabla ya kuwasili kwa Waziri Mkuchika, na kuwaweka mahabusu kwa saa kadhaa kwa madai kuwa kulipangwa njama za kuvuruga ziara ya waziri huyo.
Siri ikafichuka kwamba polisi waliwataka wananchi hao wema wasieleze kile walichotendewa wakati wa operesheni ya serikali kuhamisha kwa nguvu wakazi katika maeneo yanayodaiwa kuwa ni ya hifadhi ya taifa. Wananchi walitoa siri hiyo kwa waandishi wa habari na kumweleza Waziri Mkuchika.
Tangu mwanzo kulikuwa na mipango ya kuzuia uhuru wa wananchi kujieleza. Hizo ni hatua za kidikteta na zisizofikirika za kuficha ukweli wa mambo.
Kwa jinsi viongozi walivyokuwa mahayawani, baada ya kuwafungia katika mahabusu wananchi wenye akili zao na familia zao, viongozi hao wakapanga wananchi waliowashurutisha maelezo ya kuyatoa mbele ya Waziri Mkuchika. Maelezo ya kupanga yaliashiria kuwa eneo hilo hakuna tatizo lolote na kwamba operesheni hamisha wakazi iliendeshwa vizuri.
Huu ni uhuni usio na sababu kwa viongozi wanaojiheshimu na kutambua wajibu wao. Sasa zimefichuliwa taarifa kwamba wakati wa operesheni hiyo, nyumba za wananchi zilichomwa moto, vyakula vyao vikateketea pamoja na mali nyingine mbalimbali.
Kitendo kilichofanywa na viongozi wa wilaya ya Meatu ni kibaya na kinachohitaji uchunguzi makini. Wananchi wamekuwa wakilalamikia vitendo vya kinyama wanavyotendewa na operesheni mbalimbali za serikali, kumbe bado kuna viongozi wanadhani wanayo haki ya kudhalilisha raia kwa visingizio visivyo mashiko.
Mpaka sasa serikali haijalipa fidia wananchi wa Mbarali na maeneo mengine waliodhalilishwa kwa kufukuzwa na mifugo yao hadi ikaporwa na mingine kufa njiani kwa njaa. Vivyo hivyo kwa wananchi wa Kimasai wa maeneo ya Loliondo waliochomewa makazi yao na polisi wa serikali. Udhalilishaji wa namna hiyo umefanywa pia Kilosa na miezi miwili iliyopita kijijini Njedengwa, mkoani Dodoma ambako polisi wa serikali walisimamia uvunjaji wa nyumba za raia bila ya uhalali wowote wa kisheria.
Ni wapi serikali inajificha na kujivuna kuwa inaongoza kwa misingi ya utawala bora na kuzingatia sheria? Wakati tunataka uchunguzi ufanywe katika tukio la Mwangudo, wilayani Meatu, tunataka pia viongozi wa serikali, wa ngazi yoyote ile, wakome kudhalilisha raia. Tunajua hatuna polisi wala waendesha mashitaka wala mahsakama au gereza la kushughulikia viongozi madhalimu kama hawa, lakini tunaahidi kuwafichua kadiri tunavyopata taarifa ili waone aibu machoni kwa wananchi. Huenda hiyo itakuwa dawa yao baada ya kuridhika kwamba serikali ngazi za juu haiguswi na udhalimu wa viongozi wake.

Polisi wanaua, viongozi washerehekea

Na Paschally Mayega

SIMANZI. Festo Andrea na mdogo wake Sumbuko wa kijiji cha Rungwempya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, mchana wa saa nane, walifanyiwa unyama.
Polisi wanane, wenye wajibu wa kulinda usalama, amani na haki za kuishi za vijana hao, waliwafungulia kutoka chumba walichokuwa wamefungiwa. Kilichofuata ni mateso yasiyomithilika.
Polisi hao waliwavua nguo zote vijana wale, wakaanza kuwapa kipigo kwa kutumia vitako vya bunduki, chupa za bia, na mbaya zaidi, wakawaingiza vijiti kwenye sehemu zao za haja kubwa hadharani, huku wananchi wakishuhudia pamoja na baba yao mzazi.
Polisi walipojiridhisha kwa unyama huo, waliwalaza ndani ya gari kifudifudi kisha wakawakandamiza kwa magunia manne ya mkaa juu ya migongo yao na kuondoka nao kuelekea Kasulu mjini.
Habari kama hizi za kuumiza, kuhuzunisha, kusikitisha na kufedhehesha sana zilisikika sana enzi za utawala wa Makaburu, Afrika Kusini.
Huko polisi walikuwa wakiwatesa, waliwaua kinyama watu weusi hasa wapigania uhuru ili wasitishe harakati za kusaka uhuru. Kwa kweli, tulishasahau habari hizi tangu siasa za ubaguzi wa rangi zilipokoma mwaka 1994 na shujaa Nelson Mandela kuwa rais wa kwanza mweusi.
Miaka 17 baadaye, polisi wa Tanzania wanatukumbusha unyama ule. Maskini, Festo Andrea alipoteza maisha kutokana na mateso hayo ya polisi huku mdogo wake, Sumbuko akivunda gerezani.
Daktari Said aliyechunguza mwili wa marehemu alisema Festo alikufa kutokana na kipigo kilichosababisha kupasuka bandama, michubuko usoni iliyosababisha kuvuja damu nyingi na jeraha kubwa sehemu ya kichwani. Hii inathibitisha jinsi marehemu Festo alivyouawa kinyama na polisi wa serikali.
Keshokutwa Watanganyika  wanaombwa kujitokeza kwa wingi kwenye kilele cha sherehe za Tanganyika au Tanzania Bara kutimiza miaka 50 ya kuwa huru.
Ni uhuru upi unaoweza kusherehekewa katika hali ya kinyama kama hii? Uongozi unaoheshimu maadili ungejiuzulu kutokana na makosa yaliyofanywa na watendaji walio chini yao.
Huko Rungwempya walienda kwa amri yao wenyewe? Hakuna kiongozi ambaye ameonyesha kuguswa na tukio la kusikitisha kama hili. Kuwaambia watu hawa hawa washerekee kwa sababu wamekuwa huru kwa miaka 50 sasa ni zaidi ya kuwatukana.
Waachieni viongozi wenu washerehekee uhuru wao na ninyi endeleeni na kuhangaika kwenu! Wote kuanzia Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD) mpaka Waziri wa Mambo ya Ndani wote bado wapo ofisini kama vile hakuna tukio kubwa la kusikitisha lililotokea katika nchi!
Waziri mwenye dhamana, hata kauli tu ya mdomoni kulaani kitendo hiki hatoi? Bora kuku kuuawa kwake huchinjwa mara moja yakaisha. Hateswi kama hivi.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Rungwempya, Mosi Kilenge ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amenukuliwa akisema amesikitishwa na kifo hicho.
“Festo alikuwa mchapakazi, hakuwa mlevi, hakuwa jambazi,” anasema Mzee Samba, baba mzazi wa Festo.
“Kitendo cha polisi kuwaingiza vijiti sehemu zao za haja kubwa watoto wangu wakiwa uchi wa mnyama na mimi nikishuhudia, kwa macho yangu, inanisikitisha sana. Tangu nizaliwe sijawahi kuona polisi wakifanya unyama wa aina hii. Naiomba serikali imwachie mtoto wangu Sumbuko anayeendelea kuteseka gerezani bila kosa lolote ili arudi alione kaburi la kaka yake kabla majani hayajaota.”
Keshokutwa wakati viongozi watakapokuwa katika majukwaa wakitazama magwaride na mbwembwe nyingi, ninyi pazeni sauti zenu, muwalilie huruma, wawaonyeshe uhuru wenu!
Hivi watu wangapi wanateseka magerezani kwa kesi za kubambikiwa na polisi? Wangapi wamekufa wakiwa wanaisadia polisi?
Unyama huu wa polisi, unakumbusha tukio la mwaka 2006 ambapo polisi wa serikali waliwateka vijana wanne wafanyabiashara ya madini wa Mahenge na dereva teksi mmoja eneo la Sinza, Dar es Salaam, wakawapeleka katika msitu wa Pande na kuwamiminia risasi visogoni bila hatia yoyote. Damu hii kwa hakika haitapotea bure!
Mahakama ilipopewa jukumu kuwatendea haki vijana wale, ikawaachia huru polisi wote waliohusika kuteka, kuwapeleka msitu wa Pande, kufyatua risasi, kurejesha maiti mochwari ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Eti ikadai si wauaji na wala hawakula njama za kuua; vijana wale walisifia wenyewe.
Yako wapi masikio ya serikali ya watu? Mtu atakuwa na furaha gani ya kufanya sherehe wakati vilio vya watu vimetamalaki nchi nzima?
Viongozi wetu wako radhi kutumia mabilion ya shilingi kufurahisha nafsi zao na familia zao kwa halaiki ya siku moja ya watoto wadogo huku madege ya kivita yakipita angani kwa sekunde chache, lakini hawajali maisha ya watu wao yanayopotea hospitalini kwa kukosekana dawa!
Wala viongozi hawa hawajali elimu duni inayotolewa kwa watoto wetu, wakiwa katika mavumbi kwa kukosa madawati na mahali pengine hakuna majengo. Bila kujali vijana wetu wanaonyanyasika kwa mikopo ya elimu ya juu.
Wafanyakazi wa chini wamepigika. Vijana hawana ajira nao hawaijui kesho yao. Wamachinga wanapigwa na kunyang’anywa hata kile kidogo walichonacho. Fahari ya fala isiwavunje moyo kwakuwa sasa Mungu amesikia kilio chenu!
Ole wao watu hao waliowafikisha hapo! Siku itafika jua litakapozuiwa kutoka mpaka nchi itakaporudishwa kwa Wananchi!
Nawahurumia trafiki wa Mbagala Rangitatu kwenye msongamano mkubwa wa magari. Mvua yao, jua kali lao. Nao wanashinda wakitafuna mavumbi ya barabara inayojengwa. Polisi wema wapo wengi lakini wanyama wachache wanalichafua jeshi zima.
Zamani siku kama ya keshokutwa tungeimba kwa furaha, uhuru na kazi, uhuru na umoja, uhuru na maendeleo! Leo kazi, umoja na maendeleo viko wapi? Vimekwenda. Tumebaki kulia na maisha magumu, dhuluma na uporwaji wa maliasili zetu na wageni kwa msaada wa viongozi wetu.
Tumekuwa kama watoto wa marehemu. Tunalia ngoa ganjoni tutasikiwa na nani? Basi na tuitazame milima, msaada wetu utatoka wapi?

CUF na kiherehere cha ikulu



Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 07 December 2011

NIMEJITOSA kujadili hatua ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kujipeleka ikulu kuonana na Rais Jakaya Kikwete. Kwangu mimi hatua ile ya CUF naiona kama ni kujikanyaga.
Naomba nithibitishe kwa nukuu zifuatazo kutoka kwenye kumbukumbu za bunge (Hansard) za wabunge wa chama hicho, wakati wa kujadili Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 bungeni.
Kwanza, Mhe. Khalifa Suleimani Khalifa (Gando - Pemba):
Mheshimiwa spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii ya pili katika jambo hili muhimu kwa mustakabali wa taifa letu. Mimi kama mbunge niliyekuja bungeni hapa kupitia Chama cha CUF leo ni miongoni mwa siku ambayo nimefurahi sana.
Nimefurahi kwa sababu chama changu kimekuwa mstari wa mbele kuiomba serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa nchi hii kuandaa mazingira ya kupatikana katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Makofi).
Mheshimiwa Spika, sisi tulifanya hivyo kwa madhumni ya kuwasaidia Watanzania. Chinua Achebe anasema; “he who paves the way to the great paves the way to his own greatness.” Tulifanya vile ili heshima hii ikipatikana inarudi kwetu wenyewe. Huo ulikuwa utangulizi (Makofi).
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana umefanya juhudi kubwa kwa niaba ya bunge hili kuhakikisha kuwa muswada huu unapata nafasi inayostahili ya kujadiliwa. Lazima tukubali ulipokuja mara ya kwanza ulikuwa na matatizo mengi lakini kwa juhudi zako umelisaidia bunge letu kuweza kuwa katika mazingira mazuri ya kuujadili (Makofi).
Pili, napenda nishukuru hatua zote zilizochukuliwa na upande wa pili wa Muungano kwa ushirikiano na viongozi wa Zanzibar katika kufanikisha muswada huu. Ushirikiano umekuwa zaidi ya asilimia 95 hiyo ni +A. Sasa unapofikia hapo binadamu lazima uone kuwa wenzako wamefanya juhudi (Makofi).
Pili, Mhe. Hamad Rashid Mohammed (Wawi- Pemba):
Mheshimiwa Spika, sisi katika Chama cha Wananchi (CUF), Naibu Katibu Mkuu wetu, Ndugu Mtatiro (Julius Mtatiro) alifanya maandamano kupeleka rasimu ya katiba katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), tukidai mabadiliko ya katiba; ni sisi tuliofanya hili, mbona wao hawakufanya? (Hapa alikuwa anazungumzia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Hatukuwaona wakifanya hilo, tumeandamana kwa hili kwa kudai katiba, leo Rais (Rais Jakaya Kikwete) ambaye ana mamlaka kabisa kwa mujibu wa katiba yetu, angesema anaunda tume bila ya kuja bungeni na tume ikasimama na ikafanya kazi bila ya kutushauri.
Lakini amefanya busara ametuletea muswada huu ili tuujadili na tuupitishe hapa, lakini watu wanakataa wanasema kuna udikteta. Udikteta gani zaidi ya kwamba madaraka aliyonayo akayakasimu mwenyewe, akayaleta kwenye bunge (Makofi).
Mheshimiwa Spika, tunataka nini? Eti leo tukatembee nchi nzima kwa kupeleka tena muswada huu, tunachotaka kupeleka kule ni fujo, sisi tunakataa, sisi tunakataa kupeleka fujo!
Kama ni mawazo yametoka na yametoka kikamilifu. Wakati tunaingia kwenye kamati wenzetu walikuwa hawaji kwenye kamati, mimi nikakaa nao, nikawaambia kama tuna mawazo kwanini tusije kwenye kamati tukazungumza? Leteni mawazo yenu tuyachambue yenye maana tutayakubali, ndiyo baadaye wakaanza kushiriki.
Mheshimiwa Spika, mimi ningeomba sana ndugu zangu, the Nation has to remain as a Nation, hatuwezi kuwa na taifa lenye vipande vipande na mawazo potofu, tubaki na taifa na taifa litapatikana kama mchakato huu wa katiba tutakwenda nao kwa salama na amani, kwa utulivu kwa kuaminiana na kwa busara na kuheshimiana.
Hiyo process (utaratibu) ndiyo itatusaidia kupata taifa lililotimia na ndiyo lengo la rais kwamba sasa jamani baada ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara, baada ya miaka 46  ya Mapinduzi hebu tukae tujitazame upya chombo ambacho tunakitumia kuendesha nchi kiweje?
Hayo ndiyo madhumuni makubwa. Sasa mimi nafikiri busara ikitaka kutumika turudi tukae kitako.
Tatu, Mhe. Habibu Mnyaa (Mkanyageni, Pemba):
Mheshimiwa spika, …leo nina furaha kusema kwamba marekebisho haya ya serikali ambayo wameleta haya, schedule of amendment, yamechukua asilimia kubwa ya haya ambayo chama changu walitaka yawemo (Makofi).
Kwa nukuu hizo za bunge, ni ukweli uliyowazi kwamba viongozi na wabunge wa CUF walikubaliana na sheria iliyopitishwa kwa asilimia miamoja. Hili linathibitishwa na nukuu yao iliyosema, “Tulikubaliana kabla ya kuja hapa kupitisha muswada huu kwa kuwa ni mzuri na unakidhi mahitaji ya taifa.”
Hizo ndizo kauli kuu za wabumnge wa CUF. Sasa kama walikuwa wanakubaliana na sheria iliyopitishwa, kipi kiliwasukuma kwenda kwa Rais Kikwete? Kama walikuwa na hoja tofauti na ile waliojadili bungeni, mbona mpaka sasa, hawajatoa waraka walioupeleka ikulu kwenye majadiliano yao na serikali?
Aidha, aliyeweka msingi wa mjadala wa CUF kwenye muswada bungeni, ni Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakary. Ni yeye ambaye ni mwandishi wa sheria na mwanasheria mkuu wa zamani wa Zanzibar, aliyenukuliwa akisema yote ambayo chama hicho kimekuwa kikiyapigania kwa miaka yote tokea kuwepo kwake, yamezingatiwa katika sheria hiyo.
Sasa kama yote ambayo CUF imeyapigania yametekelezwa kikamilifu, safari ya ikulu ililenga nini kama siyo kumchosha kiongozi wa nchi?
Au ni kweli kwamba CUF wamekwenda ikulu baada ya kuona wenzao CHADEMA wamekutana na rais? Uthibitisho ni kauli ya Celina Kombani, waziri wa sheria.
Alisema, “Mheshimiwa spika, kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kumshukuru mheshimiwa Aboubakar Khamis Bakar, waziri wa katiba na sheria wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa ushauri wake na ushirikiano alionipa katika kipindi cha kuandaa muswada huu.”
Kwenda kwao kukutana na rais kunaweza kutafsiriwa kuwa ni mojawapo ya njia ya kutaka kuwaonyesha wananchi kuwa CUF ya sasa imekuwa chama cha kukurupuka bila ya kupanga hoja zake.
Ukipitia sheria iliyopitishwa na serikali na kupigiwa vigelele na wabunge wa CUF, utabaini kuwa bado kuna mapungufu mengi ya kimsingi hasa kwenye kifungu cha 9(2) ambacho hakitambui kuwepo kwa serikali tatu kama ulivyo msimamo wa CUF kwa miaka yote tangu kuanzishwa kwake.
Badala yake, sheria inaeleza, “Mfumo wa Muungano utaendelea kama ulivyo,” jambo ambalo litaendelea kuinyima nafasi Zanzibar katika jumuiya za kimataifa kama vile, umoja wa mataifa (UN), umoja wa Afrika (AU), umoja wa nchi za Kiislamu (OIC) na nyinginezo likiwamo shirika la soka la kimataifa (FIFA).
Sasa katika mazingira hayo, nani anaweza kusema hatua ya CUF kushiriki mjadala bungeni na kisha kwenda kumuona Rais Kikwete ilikuwa ni mujarabu? Bila shaka hakuna.
Ndiyo maana hata viongozi wenyewe wa CUF wanashindwa kueleza kilichowasukuma kwenda ikulu.

Waziri kumkimbia Lowassa CCM

Na Alfred Lucas

WAZIRI mmoja mwandamizi ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete, yuko mbioni kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM), imefahamika.
MwanaHALISI limeelezwa kuwa hatua ya kigogo huyo kutaka kuondoka CCM, inatokana na “kukasirishwa na hatua ya rais Kikwete kushindwa kufukuza mafisadi” ndani ya chama chake.
Mtoa taarifa wa gazeti hili ambaye amezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini amesema, waziri huyo tayari ameanza mazungumzo na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanayolenga kutafuta njia ya kujiunga na chama hicho.
Kwa sasa, gazeti hili linahifadhi jina la waziri mhusika na kiongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA anayesimamia mazungumzo hayo.
Taarifa zinasema waziri anayedaiwa kutaka kuondoka CCM, anaungwa mkono na baadhi ya viongozi wenzake waandamizi wakiwamo wabunge, viongozi wastaafu na wale waliopo madarakani.
Kuibuka kwa taarifa hizi mpya, kumekuja wiki tatu baada ya chama hicho kushindwa kutekeleza mradi wa “kujivua gamba” uliolenga kuwafukuza wanaowaita watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini, ambao wamechangia kukiporomosha chama mbele ya jamii.
Kulingana na taarifa hizo, waziri huyo na kundi lake wamekatishwa tamaa na hali inayoendelea ndani ya CCM na hasa pale chama hicho kilipoamua kurejesha kwenye ngazi ya chini suala la watuhumiwa ufisadi.
“Hapa haifai kudanganyana. Ngoma imekuwa nzito kwa rais na mwenyekiti wetu. Nguvu aliyokuwa nayo awali imeanza kupotea hasa baada ya wajumbe wa kamati kuu kugoma kufukuzwa kwa Lowassa (Edward Lowassa) na wenzake ambao ndio walionadiwa kwa miezi saba kutakiwa kuondoka,” kimeeleza chanzo chetu cha habari.
Mpango uliopo ni kujipanga ikiwemo kuimarisha upinzani ili kuja kuikabili vilivyo CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Unajua, sisi wengine hatuko tayari kuongozwa na Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015. Hatutaki yeye ashike bendera halafu sisi tunamfuata nyuma. Ndio maana tunaondoka mapema ili kukabiliana naye kutokea upinzani,” ameeleza.
Anasema, “Kwa hali ya sasa ya uongozi dhaifu kwenye serikali na chama, hatuamini kama chama chetu kinaweza kumfukuza tena Lowassa. Kuna kila dalili kuwa badala ya kufukuzwa, sasa anatengenezewa njia.”
Tangu kumalizika mikutano ya CCM iliyofanyika Dodoma, wiki tatu zilizopita, mgawanyiko mkubwa na ulio wazi umezidi kuonekana kati ya makundi mawili hasimu ndani ya chama hicho – kundi la watuhumiwa wa ufisadi na wale wanaojiita wapinga ufisadi.
Aidha, tangu kumalizika vikao hivyo, vita vya makundi yanayowania urais vimezidi kushika kasi; baadhi ya viongozi “wakiweka kambi” makanisani kuusaka urais.
Wanaotajwa hadharani kusaka urais, ni pamoja na Lowassa, Samwel Sitta, waziri wa Afrika Mashariki, na Benard Membe, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
Hata hivyo, Sitta na Lowassa ndiyo wanaonekana zaidi kutumia makanisa kujijenga kisiasa na wakati mwingine wakipigana vijembe.
Jumapili iliyopita, Sitta aliongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu jijini Arusha, ambako alimtuhumu Lowassa kutumia makanisa kujisafisha.
Akiongea kwa tahadhari, Sitta alisema, “Wananchi mnawatambua viongozi wenu ambao ni waadilifu na pia mnawatambua wale wengine, ambao wanatumia makanisa kujisafisha.”
Sitta alionya waamini wa kanisa hilo kujihadhari na dhambi ya unafiki na kile alichoita, “kusengenyana.”
Sitta hakumtaja Lowassa kwa jina.
Kuhusishwa kwa Lowassa kwenye kauli yake, kunatokana na pale aliposema, “Sitarajii kulitumia kanisa kujisafisha kwa kuwa mimi si mchafu kama wale wengine wanaokuja huku kujisafisha.”
Alisema ingawa anayo mengi ya kusema, lakini hapo si mahali pake. Alisema, “Wananchi mnatujua hata tukisemaje.”
Katika harambee hiyo, waziri Sitta na familia yake walitoa mchango wa Sh. 2 milioni.
Wengine waliochangia, ni waziri mkuu, Mizengo Pinda, aliyetoa kitita cha Sh. 5 milioni, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, aliyetoa Sh. 10 milioni, waziri mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye aliyetoa Sh. 1 milioni na naibu waziri wa viwanda na biashara, Lazaro Nyalandu aliyetoa Sh. 1 milioni.
Nyalandu anayedaiwa kuwa katika moja ya kambi inayowania urais huku yeye akiahidiwa uwaziri mkuu, alitajwa kwenye mkutano huo wa kidini na Sitta, kama kijana mahiri na mchapakazi shupavu.
Kabla ya kuhudhuria hafla hiyo, Nyarandu alihudhuria harambee nyingine katika Kanisa la St. James, ambako Waziri Membe alikuwa mgeni rasmi.
Wakati Sitta akijitokeza kwenye makanisa na kusema hayo, Lowassa tayari ametua kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Amani, mjini Singida, Kanisa Katoliki Parokia ya Nyakato, jijini Mwanza na Kanisa la Anglikana Segerea, jijini Dar es Salaam.
Akiwa Singida, mwanasiasa huyo alichangia Sh. 10 milioni, jijini Mwanza, Sh. 11 milioni na Segerea Sh. 20 milioni.
Akizungumza wakati wa Harambee hiyo iliyofanyika jijini Mwanza, Lowassa alikemea “kulala” kwa serikali akionya tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, ni miongoni mwa mambo yanayoweza kulilipua taifa.
Akirudia kauli yake kuhusu ajira, Lowassa alijifananisha na Yohana Mbatizaji.
Alisema, “Ninapozungumzia hili (uhaba wa ajira) siyo nia yangu kumlenga mtu. Mimi ni Yohana Mbatizaji, hii ni sauti inayolia nyikani.”
Hatua ya Lowassa kuhaha kujisafisha hadi kufikia hatua ya kumchafua Rais Kikwete kuwa anahusika na mkataba tata wa Richmond na hatua ya rais kunyamazia tuhuma hizo, ndiko kunaelezwa na wachambuzi wa mambo kuliko wakatisha tamaa wale wote waliokuwa mstari wa mbele kutaka kiongozi huyo afukuzwe kwenye chama.

CUF sasa yameguka

Na Mwandishi wetu 

SEIF Shariff Hamad, katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), yuko hatarini kung’olewa kwenye uongozi wa juu wa chama hicho, MwanaHALISI limeelezwa.
Taarifa zinasema mkakati wa kumng’oa kiongozi huyo maarufu kwa jina la “Maalim Seif,” unasukwa kwa ustadi mkubwa na unaweza kutekelezwa wakati wowote kuanzia sasa.
Viongozi 19 waandamizi ndani ya CUF, wakiongozwa na mbunge wa Wawi, kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohammed, wametajwa kuwa vinara wa mkakati unaoweza kumwangamiza Maalim Seif kisiasa.
Mtoa taarifa anasema Hamad Rashid ndiye anataka nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho maarufu zaidi visiwani Unguja na Pemba.
Uamuzi wa Hamad na wenzake kutaka kumg’oa Maalim Seif kwenye uongozi, unatokana na kile wanachoita, “Kutoridhishwa na hatua yake ya kukabidhi chama kwa Ismail Jussa Ladhu,” naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar.
Jussa anadaiwa kukitumia chama cha CUF “kwa maslahi binafsi.”
Alipoulizwa Hamad Rashid juu ya taarifa ya kutaka kumng’oa Maalim Seif kwenye nafasi yake alisema, “Ni kweli, nimemwandikia barua mwenyekiti wangu, Profesa Ibrahim Lipumba. Nimemueleza mengi kuhusu chama chetu.”
Hamad amesema hadi juzi Jumatatu, Profesa Lipumba alikuwa hajajibu barua yake hiyo.
Alipoulizwa iwapo ni kweli kwamba anakusudia kunyakua ukatibu mkuu, Hamad alisema, “Ndiyo. Mimi ni mwana-CUF na nina sifa za kushika wadhifa huo.”
Alisema, “Nataka kugombea nafasi hii ili kuondokana na utamaduni wa kuufanya ukatibu mkuu kama utume kwenye chama chetu. Ifike wakati ukatibu mkuu uwe utumishi, badala ya kuwa utume ndani ya chama.”
Kauli ya Hamad inaendana na madai ya baadhi ya vijana na viongozi wengine, kwa zaidi ya miezi sita sasa, kuwa Maalim Seif amekaa sana kwenye nafasi hiyo “kama kiongozi wa kiroho.”
Kwa upande wake, Jussa aliliambia gazeti hili, “Hatufanyi kazi kupitia magazetini.”
Jussa alikuwa ameulizwa kuhusu mwenendo wake ambao inadaiwa umefanya baadhi ya waasisi na viongozi wengine wa chama kuamua kupambana na Maalim Seif.
Akionesha kuongea kwa tahadhari, Jussa ambaye pia ni mwakilishi wa Mji Mkongwe, Unguja alisema, “Tunawashangaa sana watu wanaotumia magazeti. Kama kuna tofauti tutakwenda kuzimalizia kwenye vikao.”
Kwa mujibu wa mawasiliano miongoni mwa viongozi, ambayo gazeti hili limenasa, kuenguliwa kwa Maalim Seif “kunalenga kunusuru CUF na kukiwezesha chama hicho kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Visiwani.”
Mawasiliano muhimu juu ya mkakati huo ni miongoni mwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba, naibu katibu mkuu wa CUF – Tanzania Bara, Julius Mtatiro, Hamad Rashid, Jussa Ladhu na Jubeir Shamte, mwanachama wa chama hicho anayeishi Dubai.
“Jussa ndiye anavuruga CUF. Hili tumelifahamu muda mrefu, lakini tumeshindwa kulieleza kutokana na kulindwa na Maalim Seif. Hivyo, ili kukinusuru chama chetu, tumeamua kumuondoa Maalim ili kumdhibiti Jussa,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa CUF kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Anatoa mfano wa matokeo ya uchaguzi mkuu visiwani, ambapo inadaiwa kuwa chama hicho “kimeshindwa” hadi sasa, kukusanya baadhi ya fomu za matokeo ya uchaguzi kwenye majimbo matano ya Unguja.
Amesema, “Huyu bwana ndiye alikuwa msaidizi maalum wa katibu mkuu. Katika uchaguzi ule, CUF ilishindwa kukusanya matokeo ya uchaguzi katika majimbo matano ya Unguja, huku Jussa akiharakisha kushawishi Maalim akubali kushika nafasi ya pili katika serikali. Haya mambo hayakufanyika kwa bahati mbaya.”
Haijafahamika iwapo matokeo hayo yalitumika kusaidia CCM “kushinda.”
Kuibuka kwa taarifa za kumwengua Maalim Seif kumekuja mwaka mmoja baada ya gazeti hili kuripoti kuwapo kwa mawasiliano ya shaka kati ya Jussa Ladhu na January Makamba (Mbunge wa Bumbuli – CCM).
Katika mawasiliano maalum, Makamba anadaiwa kumwandikia i-meili Jussa na kusema, “Utakumbuka yale makubaliano yetu; imekuwaje mwafaka wa kutoenda personal (kushambulia mtu binafsi)?
Naye Jussa akijibu Makamba alisema, “January, maelewano yetu yako palepale. Kosa lilikuwa langu kumsubiri (Lipumba) hadi tuonane uso kwa uso ili nimpe briefing (taarifa). Bahati leo amekuja Zanzibar na tumeelewana…”
Hatua ya Makamba kulalamikia Jussa ilitokana na taarifa zilizochapishwa na gazeti la Tanzania Daima zikimkalili Profesa Lipumba akimtuhumu Rais Jakaya Kikwete, mkewe Salma na mwanae Ridhiwani kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.
Katika barua pepe iliyotumwa na Hamad Rashid kwa Profesa Lipumba na kunakiriwa kwa Shamte, tarehe 12 Novemba 2011, mbunge huyo wa Wawi anaeleza dhamira yake ya kumng’oa Maalim Seif kwenye wadhifa wa ukatibu mkuu kwenye uchaguzi mkuu wa chama mwaka kesho.
Hamad ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa upinzani bungeni anasema, “…Kwa kuzingatia nililokuandikia, naomba kukuarifu rasmi kuwa Mwenyezi Mungu akinijalia uhai na uzima; natia nia ya kugombea ukatibu mkuu wa chama wakati wa uchaguzi ndani ya chama utakapowadia.”
Awali akiandika kwa Profesa Lipumba, Hamad anamtaka arejee kikao chao chini ya uenyekiti wake (Lipumba) kilichofanyika Zanzibar, Masons Hotel, baina ya (Hamad Rashid), Makamo Mwenyekiti (Khamis Machano Alli) na katibu mkuu na makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar (Maalim Seif).
Kikao kilizungumzia, pamoja na mambo mengine, sababu “zilizonifanya kuandika kijitabu nilichokiita ‘Yaliyojiri’ baada ya kubaini njama zilizopangwa za kutaka kuniua kisiasa.”
Hamad Rashid anasema katika mazungumzo hayo, wote wanne walikubaliana kwenda kwa wanachama wa CUF kuwaambia kuwa wamemaliza tofauti zao; (na kwamba) wamekubaliana pia kuitishwa kwa mkutano wa pamoja utakaowashirikisha wabunge, wawakilishi na viongozi wa juu wa chama hicho.
Hata hivyo, Hamad Rashid anasema hakuna hata moja lililotekelezwa miongoni mwa waliyokubaliana. Anasema alikuwa anamwandikia  kumtaarifu juu ya vitendo vinavyofanywa na katibu mkuu na wasaidizi wake, vya kumtangaza yeye na wanachama wenzake 18 kuwa ni waasi ndani ya chama.
Hamad Rashid anasema kuwa ameambiwa kwamba kugombea ukatibu mkuu “…kwa chama chetu ni utume…na eti Mhe. Salum Khalfan Barwany (Mbunge wa Lindi Mjini,) anataka kugombea uenyekiti ambao nao pia ni utume ndani ya chama chetu.”
Katika kudhihirisha kupamba moto kwa mgogoro hatari ndani ya CUF, Hamad Rashid anasema baada ya Maalim Seif kukutana na wenyeviti na makatibu wa wilaya mjini Wete, kisiwani Pemba siku ya Baraza la Eid El Hajj, maagizo yalitolewa kuandaa vikao vya Kamati ya Utendaji  na mikutano mikuu ya Wilaya ili kuwajulisha viongozi hao juu ya uasi uliomo ndani ya chama.
Anasema baadhi ya viongozi hasa wabunge na wajumbe wa baraza kuu la uongozi la taifa waliotoa hoja ya udhaifu wa utendaji, matumizi mabaya ya fedha na kudhoofika kwa chama hasa Tanzania Bara, kwenye kikao halali cha baraza kuu, walituhumiwa kuwa ni vibaraka wake.
MwanaHALISI limeelezwa kuwa mgogoro huo umezidi kupamba moto baada ya CUF kufanya vibaya kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Igunga.
Waraka wa Hamad Rashid unadai, “Pamoja na chama kutumia zaidi ya Sh. 300 milioni kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga, baadhi ya wajumbe wa baraza kuu waliochangia ajenda ya hali ya kisiasa, ‘wote waliitwa vibaraka wangu,’ na kwamba eti mimi ‘napewa pesa na Mhe. Pinda kuiua CUF.”
Wanaotajwa kuwa vibaraka wa Hamad Rashid, ni pamoja na mbunge wa Gando, kisiwani Pemba, Khalifa Suleiman Khalifa, mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa, mbunge wa Mtambile, Masoud Abdulla Salim, mbunge wa Chambani, Salim Hemed na mbunge wa Lindi Mjini, Barwany.
Wengine wanaotajwa kuwa vibaraka wa Hamad na hivyo kupachikwa tuhuma za uasi ndani ya chama, ni wajumbe wa baraza kuu, Hassan Doyo, Masoud Kirungi, Rakesh na Masoud Abdallah Masoud, mbunge wa zamani wa Micheweni kisiwani Pemba.
Gazeti hili lilipomuuliza Hamad Rashid kwa njia ya simu, kwa nini mpango wake wa kutaka kugombea ukatibu mkuu uhusishwe na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alijibu haraka, “Akutukanaye hakuchagulii tusi. Sijatumwa na Pinda kuvuruga chama na wala situmiki bali naeleza ukweli wa yaliyomo ndani ya CUF.”
Profesa Lipumba akimuandikia Maalim Seif kuhusu madai ya Hamad, Jumatatu ya 14 Novemba 2011, saa 12 asubuhi anasema, “…Nimepata barua pepe toka kwa Jubeir Shamte. Sidhani kama nimekutana naye. Hamad Rashid alimpelekea nakala ya barua aliyoniletea. Sijamjibu Hamad wala sijui la kumjibu. Lakini suala linakuzwa. Mwenyekiti.”
Waraka wa Lipumba uliotumwa kwa Maalim Seif ulinukuliwa kwa Jussa na Mtatiro.
Hatua ya Profesa Lipumba kumuandikia Maalim Seif ilifuatia Shamte kumtaka kiongozi huyo wa CUF kuchukua hatua “kukinusuru chama.”
Akiandika kwa uchungu, siku hiyohiyo ya 14 Novemba 2011, Shamte anasema, “…  Natumai hali yako nzuri na nimearifiwa kuwa uko USA kwa muda wa miezi sita… Nimesikitishwa sana na hali inayoendelea kwenye chama chetu. Japokuwa mie niko mbali (Dubai), lakini naona huzuni kubwa kuona mambo haya ambayo yanaweza kutuweka pabaya kama hayajatuweka bado.”
Anasema, “Sisi tuliochangia kwa hali na mali kuanzisha chama hiki… hatutafurahi kuona mbuyu unaanguka. Tutakuwa na fakhari kuona mti unazaa matunda na watu wanafaidika…”
Awali Hamad akiandika kwa Profesa Lipumba kwa njia ya kulalama anasema, “…Tarehe 10 Novemba 2011, kamati tendaji ya wilaya Chake Chake ilikutana bila mimi kujulishwa jinsi ya kutekeleza maagizo ya katibu mkuu, ambapo pamoja na mambo mengine, yanataka kufukuzwa kutoka ndani ya chama viongozi 19 kwa madai ya uasi ndani ya chama.”
Hamad Rashid anaeleza katika andishi lake kwa Profesa Lipumba, “Pamoja na mvutano mkali uliotokea katika kikao hicho, hasa  kutoka  kwa wajumbe wa jimbo langu la Wawi ambao wanaelewa kiini na ukweli wa mipango ya Jussa na wenzake; wakipewa nguvu na  katibu mkuu, lakini viongozi wa wilaya wameamua kuitisha mkutano mkuu wa wilaya 14 Novemba 2011 ili kutimiza agizo” hilo.
Katika barua yake kwa Profesa Lipumba anasema “…nataka kukuthibitishia kuwa mpango huu ulioandaliwa kijasusi, kuzidi kukiua chama chetu unavyoendelea; Jussa ambaye kinyume cha katiba ya CUF amepewa wadhifa wa katibu wa kamati ya ulinzi na usalama, leo 12 Novemba 2011 kwa kutumia viongozi wa Blue Guard (kikosi cha ulinzi cha chama), ameitisha kikao cha Blue Guard na kuwapa kazi ya kuzunguka nchi nzima, kuchafua majina yetu na kupandikiza maneno ya uwongo.”
Mwanasiasa huyo ambaye amewahi kuwekwa kizuizini Zanzibar kwa miaka mitatu kwa madai ya kutaka kuipindua serikali ya Dk. Salmin Amour, analalamika kuwa “…fedha za walipa kodi na michango ya wabunge na wawakilishi inatumika kuua chama badala ya kukiendeleza.”
Akiandika kwa uchungu Hamad Rashid anasema, “Chama kinatumia fedha zote hizi ili kufanikisha mradi binafsi na kwa maslahi binafsi.”
Anasema chama chake kimeshindwa kupeleka ruzuku wilayani, hasa Tanzania Bara kwa zaidi ya miezi sita sasa; wajumbe wakihoji wanaitwa wasaliti wa chama.
“Mhe. Mwenyekiti, nakuandika taarifa hii fupi kwa madhumuni ya kukupa fursa, angalau ya kupata muhtasari wa yanayojiri huku katika chama unachokiongoza; wala si kwa madumuni ya kuomba shufaa, kwani haya nilikwishayaeleza katika kijitabu changu cha ‘Yaliojiri,’ ambacho uliniomba nisiendelee kukisambaza, lakini huenda nikavisambaza zaidi ili Watanzania waujue upande wa pili wa shilingi,” anaeleza Hamad Rashid.
Kuhusu Maalim Seif kung’atuliwa, Hamad anasema, “…hakuna asiyejua na kutambua mchango wa Maalim Seif katika mustakbali wa kisiasa Zanzibar na Tanzania kwa jumla. Ametoa mchango mkubwa wa kuhakiksha nchi inabaki katika amani, ameshirikiana na viongozi wenzake katika kuanzisha chama na akakisimamia hasa Zanzibar ambako leo tuko katika serikali ya umoja wa kitaifa.”
Anasema mchango wa Maalim Seif hauwezi kupita hivihivi. Anaeleza, “Nidhahiri Maalim anafaa kuheshimiwa na kuenziwa, ili mradi mwenyewe aamue kupewa heshima hiyo, kama ambavyo aliamua rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Andishi la Hamad Rashid juu ya Maalim Seif linafanana na kauli iliyotolewa na Doyo kwenye mazungumzo yake kwa njia ya simu na mmoja wa washirika wake.
Katika mazungumzo hayo, Hassan Doyo anasema wakati wa Maalim Seif kung’atuka kwenye chama umefika. Anataja sababu kadhaa ikiwamo kutingwa na shughuli za umakamu wa rais. Vilevile anaunga mkono mpango wa Hamad Rashid kugombea nafasi ya katibu mkuu.
Anasema, “Tunataka mabadiliko makubwa ya uongozi. Tunataka katibu mkuu apumzike. Umakamu umemzidi mpaka chama hakitaki. Hana ziara popote, yeye ni umakamu na ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za chama.”
Anasema, “Kwa hiyo, tunafanya harakati za mabadiliko ya uongozi kwa kuanzia na yeye. Tunataka abaki kwenye umakamu ili tupate katibu mkuu atakayekuwa katibu mtendaji.”
Kuhusu Lipumba, Doyo anasema, bado anaweza kuendelea kubaki kukiongoza chama hicho kutokana na umri wake kuwa mdogo na kwa elimu yake pana; akiongeza kuwa huyo hajawahi kufanya mabaya kwa chama chake.
Anasema, “Lakini katibu mkuu tunataka aondoke, siyo kwa sababu amekifanyia chama mabaya, hapana. Bali, muda wake wa kufanya shughuli za kisiasa ni mdogo; ” jambo ambalo anasema linakifanya chama hicho kuonekana kama hakina katibu mkuu.
Doyo anasema, “Leo nani utamueleza CUF akakuelewa? Mara tunaitwa CCM B… Badala ya watu kufanya kazi za kisiasa wilayani, wanaishia kuitisha “press” (mikutano ya waandishi wa habari) Dar es Salaam. Hizi ndizo harakati ambazo tunazungumza na wala siyo mbaya.”
“…hayo mabadiliko yanayotajwa ni ya kweli. Na sisi tunayaongoza bila woga kwa sababu ni sehemu ya demokrasia. Naamini katika ninachokifanya na Hamad Rashid ametangaza kugombea nafasi ya katibu mkuu; nami namuunga mkono,” anaeleza Doyo.
Mwanasiasa huyo machachari anasema, muda si mrefu watasambaza alioita “washikadau” nchi mzima ili kufanya mikutano ya kuelemisha wanachama na wananchi kwa jumla juu ya umuhimu wa kufanyika mabadiliko.
Anasema, “Tutakwenda nchi mzima kusambaza jambo hilo. Kwanza, katibu mkuu wetu hatutaki atukanwe. Pili, hatutaki akashifiwe na hatutaki adhalilishwe. Ila tunataka kuwaambia wanachama wa CUF kuwa tunataka mabadiliko. Miaka ya katibu mkuu ni mingi; amekitumikia chama kwa zaidi ya miaka 20, lakini chama kinarudi nyuma. Tunataka mawazo mengine ya kuweza kusogeza chama chetu mbele.”
Doyo anasema, hiyo ndiyo ajenda ambayo wanakwenda nayo kwa wananchi. Gazeti hili halikufanikiwa kumpata kueleza mipango ya kumwengua Maalim Seif imefikia hatua gani.
Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, hakupatika kujibu iwapo anajua kinachotendeka ndani ya chama chake na hatua ambazo anachukua kukiokoa kisigawanyike kati ya Pemba na Unguja. Imeelezwa yuko nchini Marekani kikazi kwa miezi sita.
Gazeti lilituma ujumbe kupitia i-meili uliotaka kufahamu kwa nini hakutuma majibu ya barua ya Hamad kwake mwenyewe. Hadi  tunakwenda mtamboni juzi Jumatatu, Profesa Lipumba alikuwa hajajibu ujumbe huo.
Naye, makamu wake wa CUF, Machano Khamis Ali hakupatikana. Imeelezwa yuko nje ya nchi kikazi. Haikuweza kufahamika yuko nchi gani na amekwenda kwa kazi gani.
Lakini Julius Mtatiro, alipoulizwa alisema, “Binafsi sielewi. Nimeona tu kwenye vyombo vya habari, Mhe. Hamad Rashid wakim-quote (wakimnukuu) juu ya mvutano ndani ya CUF. Tatizo ni nini; sielewe kinachoendelea…”
Alisema, “…ninavyofahamu mimi ni kwamba kuna vikao vya kamati tendaji, baraza kuu na mkutano mkuu wa chama. Masuala yote yanajadiliwa kwenye vikao na niseme ukweli tu kwamba; si vema masuala yetu yakaendeshwa kwa njia ya magazeti. Inaleta picha mbaya mbele ya jamii.”
Alipoelezwa gazeti halikuletewa habari na Hamad bali limepata mawasiliano kati ya Lipumba, Jussa na yeye; Mtatiro alisema, “Sawa. Lakini si vizuri mambo ya siasa yakaendeshwa na magazeti.”
Wengine wanaodaiwa kuwa ni watu wa Hamad Rashid, ni Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi kwenye serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Masoud, Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakari Khamis Bakari na aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho, Nassoro Seif Amour.
Msemaji wa chama hicho, Salim Bimani amesema, “Sisi tunapokea taarifa kwenye vikao na kufanya kazi kwa maagizo ya vikao. Tuna ngazi za kuzungumza mambo yetu.” Alisema vikao hivyo vinatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Foreigners flock to China for job opportunities


By Yu Ran
SHANGHAI - Shanghai has China's second-largest population of foreigners and overseas Chinese, and 27.3 per cent of them have come to the city purely for jobs, according to a report released on Monday by the municipal statistics bureau.

A total of 104,300 residents, more than 50 per cent of the city's foreigners and overseas Chinese - people from Hong Kong, Macau and Taiwan - came to the city primarily for long-term work or short-term business in 2010, said the report, which is based on the sixth national census conducted in November 2010.
This is the first time foreigners and overseas Chinese were counted in the census.
"Shanghai has seen a rapidly increasing flow of foreigners coming for jobs over the past three to five years, and the trend continues and is expected to grow significantly in the near future, given the booming local economy," said Sun Haode, director of the labour and employment centre for foreigners under the labour and social security bureau in Shanghai.
Sun said that he and his team are working to help local enterprises recruit foreigners, sign work agreements and apply for work permits for them.
According to the report, foreigners in Shanghai stay on average for 21 months, with people from South Korea, Malaysia, Singapore, the United Kingdom, France, Germany and Canada staying the longest.

Real tears in North Korea over Kim's death: Witnesses


In tightly controlled North Korea where the ruling Kim family is a centerpiece of everyday life, it is no surprise to find people shedding tears over the passing of a dictator, but what may surprise is that some of the tears shed are spontaneous.
North Korea, an impoverished state of 25 million people, stages annual mass gymnastic events featuring tens of thousands of people. Some who were there at the time Kim Jong-il's death was announced Monday said that while grieving was coordinated, there were also individual outbursts.
"It is as if your father had died. They cried themselves blind," said Kim Dong-soo, a South Korean worker at a kitchen utensil maker at a joint South-North venture in the Kaesong Industrial Complex in North Korea.
"Today is also full of tears. They can't even speak a word," he said as he crossed back into South Korea.
At Beijing Airport, grim-faced North Koreans, some carrying white chrysanthemums - a flower of mourning - and foreigners told of a nation grieving deeply over the death of their 69-year-old "Dear Leader."
One Chinese man arriving in Beijing, who declined to be named, said he was at a village for a farming project about 100 km (62 miles) outside Pyongyang when loudspeakers called people for a special announcement at noon Monday.
"Every village has speakers like that, and everyone was very orderly as they gathered around them," said the man, who would not give his name. "Everyone started crying very loudly."
Kim Jong-il's bier was placed in the mausoleum Tuesday where the embalmed body of founding father Kim Il-sung is displayed in a glass sarcophagus.
Britain's top diplomatic official presently in Pyongyang, Barnaby Jones, the British Embassy's first secretary, told a press conference in Seoul by telephone that the situation in the North Korean capital was subdued and calm.
"In most places across the city, you are not seeing crowds, but large groups," he said.
At the time of the death of Kim Il-sung, the founding father of North Korea, tens of thousands of people wept openly in the streets in an outpouring of grief.
A Chinese student arriving from Pyongyang said she also witnessed scenes of a grieving populace like those seen on state-run television.
"You could see they were real tears," said Wang Haoyan, who attends Kim Il-sung University.
"People greatly respected Kim Jong-il, and would stand straight at attention when applauding him."

Mvua ya radi yaua watano


MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana mkoani Dar es Salaam ikiambatana na radi,
imesababisha maafa ya vifo vya watu watano na kuwaacha wengine wengi wakiwa hawana makazi kwa sasa.

Mvua hiyo iliyonyesha kwa zaidi ya saa tatu, mbali na vifo pamoja na majeruhi hao, pia imesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara na madaraja pamoja na mali
yakiwemo magari, ambapo hata hivyo thamani yake haijajulikana.

Hali imeonekana kuwa mbaya zaidi kwa wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni ambao baadhi yao walinusurika kupoteza maisha yao baada ya vikosi vya Uokoaji na Zimamoto vya
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kufika katika maeneo hayo na kutoa msaada wa kuwaokoa.

Mvua hiyo iliyoanza kunyesha kuanzia saa 10 alfajiri, pia imesababisha mamia ya watu kukosa
mahali pa kulala baada ya nyumba zao kujaa maji kutokana na mvua hiyo.

Akizungumza matokeo ya mvua hiyo ambayo pia ilisababisha tatizo kubwa la usafiri jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa, Said Mecky
Sadiki alisema hadi kufikia saa 10 jioni, maiti wanne akiwemo ya mtoto mchanga walipatikana.

Aliwataja waliokufa kuwa ni Ibrahim Tulihama (65), mkazi wa Ubungo Msewe, Maganga Said (10-15) mkazi wa Mbagala aliyekufa baada ya kudondokewa na nguzo ya umeme, Gathi Mseti (39) wa Mburahati pamoja na mtoto mchanga ambaye hata hivyo hajatambulika.

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alimtaja mtu
mwingine aliyekufa kuwa ni Viane Maxmillia (13) ambaye alikutwa chini ya uvungu wa kitanda
katika eneo la Mburahati.

Aidha, Kova alisema mtoto mchanga ambaye jina na umri wake havijafahamika, aliokotwa katika eneo la Mtogole, Tandale akiwa amesombwa na maji.

Mkuu wa Mkoa Sadiki alisema majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilala ya
Amana wakiendelea na matibabu.

Aidha, alisema kutokana na taarifa walizozipata kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), mvua hizo zitaendelea kunyesha na hivyo kuwataka wakazi wa maeneo ya mabondeni kuondoka ili kuepuka madhara zaidi yanayoweza kuendelea kutokea.

Aliyataja maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua hiyo ambayo pia yalishuhudiwa na gazeti hili
kuwa ni Jangwani, Mburahati, Kigogo, Tabata, Buguruni Mnyamani, Tandale, Mtogole, Manzese, Ubungo External, Loyola, Msasani Bonde la Mpunga, Riverside na Magomeni Chini.

Eneo la Jangwani na Kigogo pamoja na Mburahati, ndiyo yaliyoathirika zaidi na mvua hiyo, kwani ilisababisha nyumba za wakazi wa maeneo hayo kuzingirwa na maji yaliyowafanya
baadhi ya wananchi wanaoishi katika makazi hayo kujiokoa kwa kupanda juu ya mapaa ya
nyumba.

Katika eneo la Kigogo, gazeti hili lilivishuhudia vikosi vya Uokoaji na Zimamoto vya Jiji vikinusuru maisha ya mama mmoja na watoto wake sita, waliokuwa wameanza kuzama baada ya nyumba waliyokuwa wamekaa juu ya paa kubomoka.

“Hali ni mbaya sana, hapa tunapozungumza bado kuna watu wapo ndani ya nyumba zao
wamezuiliwa na maji kutoka, wanahitaji msaada ili kuokolewa,” alisema mmoja wa wananchi
aliyekuwepo eneo hilo ambaye hata hivyo hakuwa tayari kujitambulisha jina lake.

Polisi waliokuwa katika magari na helikopta pia waliungana na vikosi vya Uokoaji kufanya
doria katika maeneo yaliyokumbwa na madhara ili kuangalia namna ambavyo wangeweza kutoa msaada katika tukio hilo.

Mkuu wa Mkoa amewataka wakazi waliopo katika maeneo yote ya mabondeni kuondoka
haraka ili kuepuka madhara yanayoweza kuwakuta kabla ya hatua zaidi za kuwahamisha kwa nguvu hazijachukuliwa dhidi yao.

Mkoani Dodoma, Sifa Lubasi anaripoti kuwa mvua kubwa iliyoambatana na upepo imeziacha
kaya zaidi ya 74 zenye watu 269 katika kata za Ntyuka na Iyumbu katika Manispaa ya Dodoma,
zikiwa hazina mahali pa kuishi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma, Nicolaus Buretta mvua hiyo ilinyesha usiku wa kuamkia juzi.

Alisema kutokana na hali hiyo, tayari Kamati ya Maafa ya Halmashauri imejipanga kwa ajili ya
kuwasaidia waliopatwa na maafa hayo kwa kutoa chakula na mahema kwa ajili ya kujihifadhi.

Alibainisha kuwa zaidi ya wakazi 269 kutoka katika vitongoji vitano vya Kata ya Ntyuka
wameachwa katika mazingira magumu baada ya mali zao ikiwemo vyakula kuharibiwa. Pia nyumba ya Mganga wa Zahanati ya Kata ya Ntyuka pamoja na zahanati hiyo zimeezuliwa na upepo.

Wakati huohuo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Fulgence Ngonyani
amesema kutokana na mvua kubwa hiyo kubwa daraja na reli eneo la Gulwe wilayani Mpwapwa limeharibika.

Shirika la reli nchini jana lilitangaza kuahirisha safari ya treni kutokana na uharibifu huo.

Tuesday, December 20, 2011


BEIJING - Chinese police have arrested 52 people for making and selling cooking oil dredged up from restaurant gutters, state media reported on Tuesday, in the latest food safety scandal to hit the country.
Investigators found that a company in the southern province of Jiangxi had made more than 2,000 tonnes of "gutter oil" since 2010, which it sold to a feed-processing firm in the neighbouring province of Guangdong, the official Xinhua news agency said.
The oil was then sold to restaurants around the region after"being mixed with quality cooking oil and labelled with unregistered trademarks", the report added.
Cooking oil safety scandals have surfaced periodically in China in recent years, and pictures of oil being scooped up from drains have circulated widely online to public revulsion, denting government claims to be addressing food safety problems.
China has struggled to rein in the health safety violations in the unruly and vast food sector despite tough penalties and repeated vows to crack down.
Since July, Chinese courts have sentenced at least a dozen people to jail, including one person who received a suspended death sentence, for their roles in producing or selling pork tainted with toxic chemicals.
In 2008, at least six children died and nearly 300,000 fell ill from drinking milk laced with melamine powder, an industrial compound added to milk to give misleadingly high results in protein tests.

NGO wants action over man's same sex marriage: KL

KUALA LUMPUR - A non-governmental organisation has lodged a police report urging investigation into the case of a 28-year-old man who had allegedly gone through a same-sex marriage abroad.
Kepong Islamic Youth Orga­nisation (PBIK) chairman Norizan Ali said the group, which made the report at Sentul police headquarters, wanted a probe over the man whose wedding pictures had been widely circulated online.
"We made the report to pressure the Higher Education Ministry and government-linked companies to check on those whom they sponsor as scholars," he said.
The man was reportedly studying medicine in Dublin but he did not complete the course.
"They may choose students who have excellent academic results but do not check the person's character and religious faith," Norizan said.
He said PBIK would pass a copy of the police report to the Federal Territory Islamic Affairs Depart­ment (Jawi) to urge it to take action against the man if he returned to Malaysia.
"The marriage is a disgrace to our religion, race and country," he added.
Umno Youth Community Com­plaints Bureau chairman Datuk Muhd Khairun Aseh said the man's mother had sent a letter to her son, asking him to not only reunite with the family, but to also settle his RM890,000 (S$365,612) education loan.