Tuesday, March 29, 2011
20 PERCENT AWAANGUSHA MASHAROBARO - KILI MUSIC AWARDS
Abbas Hamis, marufu kama “20 percent” aliwashangaza masharobaro na kuibuka mfalme pale alipojinyakulia Tuzo tano katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, siku ya jumamosi usiku.
20 percent ambaye hakuwepo ukumbini, alijitwalia tuzo za Mwanamuziki wa mwaka wa kiume, Mwanamuziki bora wa kiume na Mwandishi bora wa Mwaka, ambapo nyimbo zake mbili “Tamaa mbaya” na “Ya nini Malumbano” zilipigiwa kura kwa Wimbo wa mwaka, na Wimbo bora wa Kiafrika. Nyota huyo ni Mwimbaji na mtunzi bora.
Tuzo za 20 percent zilipokelewa na producer wake Man Walter
Monday, March 21, 2011
Una kazi ya sanaa unataka kuitangaza?
Iwapo una kazi ya sanaa unayotaka kuitangaza, kama kwaya, muziki,ngoma, sanaa za maonyesho, n.k. tuma picha ya kazi hiyo pamoja na maelezo mafupi kwenda kwa wangahp@gmail.com. Kazi hiyo itawekwa katika blog bure. Ukiona tangazo hili mtaarifu na mwenzako.
Wednesday, March 2, 2011
Utafiti kwenye sanaa na wasanii
Napenda kufahamu kama kuna mtu aliyefanya utafiti (research) kwenye kuboresha maslahi ya wasanii na ubora wa kazi zao. Pia kama kuna mtu anayefahamu journal yeyote Tanzania, au Afrika inayohusu kazi za wasanii.
Wednesday, February 23, 2011
Wasanii wa kike hutembea na producers
Kumekuwa na fununu kwamba ili msanii wa kike apangwe kucheza filamu au kutoa kazi yake toka studio hana budi kutembea na producer, yani kutoa rushwa ya ngono. Je kuna ukweli wowote kuhusu suala hili? Wanaharakati mmefatilia na kuona kama kuna udhalilishaji wa namna hii? Naomba mchango wenu wadau.
Kwa nini makundi ya wasanii huvunjika?
Tanzania kuna makundi mengi sana ya wasanii, hasa wa filamu, muziki wa kizazi kipya, na ngoma. Makundi haya huwa na malengo ya kuendeleza vipaji vyao na kujipatia ajira. Utakuta kundi limetoa filamu au album yao na kuanza kupata mafanikio. La kushangaza ni pale ambapo baada ya muda mfupi tu wanaanza malumbano, ugomvi na hatimaye kundi kuvunjika. Napenda kufahamu kama kuna mtu ameona au imetokea kwenye kundi lake atuambie sababu ilikuwa nini, na wengine wachangie nini kifanyike ili mambo hayo yasijirudie na hatimaye tuendeleze sanaa na ajira nchini.
Subscribe to:
Posts (Atom)














