MKAZI wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Phillipo Tango (25),
amependekeza Katiba Mpya itoe haki na usawa katika suala la ndoa kwa
wanawake kuruhusiwa kuchumbia, kutoa mahari na kuoa wanaume wanaowapenda
na kukubaliana.
Akitoa maoni yake mbele ya Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Mpya juzi, Tango ambaye ni mkazi wa Kata ya
Olmotonyi, wilayani Arumeru alisema lazima Katiba hiyo mpya ikomeshe
mfumo dume unaotawala suala la ndoa.
“Katiba itoe haki sawa kwa jinsi zote mbili katika
suala la kuoana na haki zote za ndoa tofauti na sasa ambapo wanaume
ndiyo wenye maamuzi makubwa kulinganisha na wanawake,” alisema Tango.
Kwa upande wake, Makamba Meshilieki (32), mkazi wa
kijiji cha Ngaramtoni yeye alipendekeza wabunge na madiwani kuingia
mikataba na wananchi wa maeneo yao kuhusu utendaji na utekelezaji wa
miradi ya maendeleo mara baada ya kushinda uchaguzi.
Alipendekeza pamoja na kuonyesha muda wa
utekelezaji, mkataba baina ya wabunge, madiwani na wananchi kutaja
adhabu atakayostahili kiongozi anayeshindwa kutimiza wajibu wake kwa
jamii.
“Mbunge au diwani atakayeshindwa kutimiza
yaliyoahidi katika mkataba wachapwe viboko 60 hadharani ili kuwa
fundisho kwa wengine wenye tabia ya kutoa ahadi zisizotekelezeka kipindi
cha kampeni za uchaguzi,” alisema Tango.
Emanuel Mollel (44), yeye alitaka Katiba Mpya
kuwazuia viongozi na watendaji Serikalini, mashirika na taasisi za Umma
kufanya biashara wakiwa madarakani ili kudhibiti migongano wa kimaslahi.
Alisema viongozi kuendelea kushiriki shughuli za kibiashara wakiwa madarakani kunachochea vitendo vya ubadhirifu, wizi na matumizi mabaya ya madaraka na ofisi za umma kwa faida na maslahi binafsi.
Alisema viongozi kuendelea kushiriki shughuli za kibiashara wakiwa madarakani kunachochea vitendo vya ubadhirifu, wizi na matumizi mabaya ya madaraka na ofisi za umma kwa faida na maslahi binafsi.
No comments:
Post a Comment