Harakati za wanajeshi kujaribu kuwaokoa
raia wa kigeni waliozuiliwa mateka na wapiganaji katika kiwanda kimoja
cha kutengeneza Gesi nchini Algeria zimesababisha vifo vya wapiganaji
kadhaa huku mateka wao wakiwa hawajulikani waliko.
Idhaa ya Serikali imesema kikosi maalum cha
wanajeshi bado kimezingira sehemu ya kiwanda hicho ambako wapiganaji hao
bado wanawazuilia mateka kadhaa.Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa wanamgambo wanne wameuawa. Walikuwa wanadai kuwazuilia mateka 41.
Baadhi ya mateka hao waliachiliwa lakini idadi ya walionusurika ilithibitishwa na maafisa wa serikali ya Uingereza ikisema kuwa inajiandaa kwa taarifa za majeruhi wengi wa Uingereza.
Wapiganaji hao wenye uhusianao na kundi la Al-Qaeda, walivamia kituo cha Amenas siku ya Jumatano.
Wakati wa harakati zilizofanywa siku ya Alhamisi, waalgeria wengi pamoja na mateka wanne wa kigeni, wawili kutoka Scotland, mmoja mfaransa na mwingine mkenya waliachiliwa.
Japan nayo ilisema kuwa raia wake watatu waliachiliwa wakati wa harakati za jeshi lakini wengine 14 hawajulikani waliko.
Mapema wanamgambo walisema kuwa mateka 34 na wapiganaji 14 waliuawa huku saba wakinusurika.
Duru zinaarifu kuwa jeshi la Algeria halijaweza kudhibiti eneo hilo lote na kwamba msako ungali unaendelea.
Wanamgambo walisema kuwa walifanya shambulizi hilo kama kulipiza kisasi hatua ya Ufaransa kuingilia hali ya Mali.
No comments:
Post a Comment