Tuesday, March 20, 2012

Wamisri wamuaga papa Shenouda

 Idadi kubwa ya watu wamejumuika mjini Cairo katika mazishi ya Papa Shenouda wa Tatu wa Kanisa la Coptic.
Papa Shenouda alifariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka themanini na minane.
Viongozi wa kijeshi nchini Misri wametangaza siku ya maombolezi ya kitaifa kwa heshima ya papa huyo aliyeongoza waumini wa Copti kwa zaidi ya miongo minne.
Baada ya misa mwili wa papa utasafirishwa na kuzikwa katika makao ya watawa eneo la Nile Delta.
Papa huyo alikuwa kiongozi wa kidini wa waumini hao ambao ni asilimia kumi ya idadi yote ya watu wa Misri na wamelalamika kutengwa sana nchini Misri katika miaka ya hivi karibuni.
Baada ya misa ya wafu , papa Shenouda atazikwa katika nyumba ya watawa ya St Bishoy monastery katika eneo la Nile Delta.
Wa Copti ndio jamii kubwa ya wakristo mashariki ya kati. Hii leo walipewa likizo kuweza kufanya maziko huku siku moja ya maomblozi ya kitaifa ikitangazwa.

No comments:

Post a Comment