ASHANGAA SMZ KUZIDIWA NGUVU, UAMSHO YAKUBALI KUSHIRIKI MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Ibrahim Yamola
ASKOFU
Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ‘kudhibiti wahuni
wanaotaka kuvuruga amani visiwani humo’.Kauli hiyo ya Pengo ni ya
kwanza tangu kuibuka kwa vurugu visiwani Zanzibar mapema mwezi huu, na
kusababisha uharibifu wa mali, huku makanisa yakilengwa zaidi na kikundi
kinachojiita cha Jumuiya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI).
Pengo
alitoa kauli hiyo wakati wa ibada maalumu iliyofanyika katika Kanisa la
Msalabani Bagamoyo, mkoani Pwani, ikiwa ni maandalizi ya Mkutano Mkuu
wa Shirika la Roho Mtakatifu, utakaofanyika kwa siku 30 kuanzia jana.
Kardinali
Pengo alisema, ‘wahuni hawawezi kuizidi Serikali makini’.“Makanisa yetu
yamecomwa moto na watu wahuni. Kama Serikali ipo na haiwezi kuchukua
hatua dhidi ya wahuni, usalama uko wapi?” alihoji Kardinali Pengo.
“Wahuni
wanaweza kutuunguzia makanisa saba kwa mpigo, lakini mbele ya hapo kuna
makanisa kadhaa ambayo yalikwishaunguzwa na kubomolewa na hao wahuni,”
alisema.Pengo aliendelea kuhoji, “Kama sasa wahuni wameishinda nguvu
Serikali ya watu kwa hiyo tutawaliwe na wahuni na wafanye lile
wanalolitaka, tunajiuliza tunakwenda wapi?
Mara baada ya vurugu
za Zanzibar, jopo la maaskofu kutoka madhehebu mbalimbali, walifanya
mazungumzo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), huku wakiituhumu
kushindwa kudhibiti vitendo vya uchomaji moto makanisa na kuihadharisha
kuchukua hatua za haraka.
Jana, Pengo alilitaka shirika hilo
kumsaidia Askofu Augustine Shayo wa Jimbo Katoliki Zanzibar, kuunganisha
nguvu zao katika harakati za kuimarisha amani.
Pengo alisema
mbali ya vurugu hizo, hivi sasa utumwa bado unandelea kukithiri nchini,
hususan kwa viongozi wa Serikali kuwakandamiza wananchi wa hali ya
chini.
Alisema wapo baadhi ya viongozi wanaotaka utumwa uendelee kuwapo kutokana na matendo yao dhidi ya wananchi.
“Tanzania
ni huru sawa, lakini mimi sitaki kusadiki kuwa ni huru kwa kila mmoja
na kila Mtanzania, wapo watu ambao wangependa wao waneemeke hata kwa
madhara ya wengi bila huruma hadi siku ya leo,” alisema na kuongeza:
“Tangu
Shule ya St. Marian inaanzishwa, kuna baadhi ya viongozi wamekuwa
wakitaka watoto wao wakasome pale na watoto wa maskini wasipate nafasi.”
Alitoboa
siri kuwa ‘kuna barua za maombi zisizo za msingi ambazo amekuwa
akipelekewa Askofu Shayo na kuzikataa, na wakati mwingine amekuwa
akitishiwa maisha, kwani wapo wanaotaka kuwasomesha watoto katika shule
nzuri ili waendele kujineemesha. Sasa huu sio utumwa?’
Kardinali
Pengo alililitaka Shirika la Roho Mtakatifu kutumia mkutano huo
kuendelea kuhimiza amani hapa nchini na kutupia jicho Zanzibar, ambako
amani inavurugika kwa matendo ya watu aliowaita wahuni.
Mkutano wa Shirika
Kwa
mujibu wa Makamu Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu, Padre John Kuff
kutoka Ghana, mkutano huo unafanyika Afrika kwa mara ya kwanza, tangu
kuanzishwa kwa shirika hilo mwaka 1868.
Tanzania ni mwenyeji wa
mkutano huo wa 20 ambao umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka sita, na
mkutano wa mwisho ulifanyika Ureno mwaka 2004.
Baadhi ya nchi zitakazoshiriki mkutano huo ni Canada, Nageria, Ureno, Ufaransa, Ghana, Uingereza, Irand na mwenyeji Tanzania.”
Akizungumzia
shirika hilo, Pengo alisema wakati linaanza kazi nchini walikuta amani
imevurugika, lakini walifanya kazi kubwa amani ikarejea, hivyo alilitaka
kusimamia ukweli hata kama watu wengine watawabeza.
Kipozi aahidi amani
Akitoa
salamu za Serikali kanisani hapo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed
Kipozi alisema washiriki wa mkutano huo wawe na amani kwani ulinzi
utaimarishwa wakati wote.
“Kwa siku zote 30 za mkutano huu ulinzi na usalama utaimarishwa ili kuhakikisha mnafikia malengo yenu,” alisema Kipozi.
No comments:
Post a Comment