Saturday, May 28, 2011

Basi la Sumry laua 15 Mbeya

Wimbi la ajali za barabarani limeendelea kuikumba nchi ambapo jana usiku majira ya saa nne usiku basi linalomilikiwa na kampuni ya Sumry lilipata ajali na kuua 15 papo hapo na kujeruhi wengine 20. Basi hilo lililokuwa linatoka Arusha kuelekea Mbeya lilipata ajali eneo la Igawa, Mbarari, Mbeya. Maiti na majeruhi waliwahishwa katika hospitali za Ilembula na Mbarari.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alisema chanzo cha ajali ni kupasuka kwa gurudumu la basi hilo. Dereva wa basi ni kati ya watu waliokufa katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment