Saturday, July 30, 2011

Mpenzi wangu hataki kuvaa kondomu

Watu wengine hawapendi kutumia kondom, lakini ukweli ni kuwa – watu wakichagizwa kati ya kufanya mapenzi kwa kutumia kondom na kutofanya mapenzi kabisa, wengi huchagua kondom!
Basi tafakari - na ukichagua kutumia kondom jadili swala hili na mpenzi wako na muafikiane mapema, hata kabla hamjaanza kwani huenda kajisahau mkiwa katika lindi la nyege!
Halafu linabaki kuwa wazo tu kichwani je tutumie kondom, je ipo? na mambo kama hayo. Kama hamuwezi kujadili swala la kondom na yule unaemwita mpenzio, je huyo ni mpenzi wa kweli?
Kuwa mwazi - toa sababu zako za kutaka kutumia kondom, mfano wa sababu mwafaka nikama
  • Kutumia kondom kutaniondolea wasiwasi.
  • Nitaweza kufurahia mapenzi zaidi nikitumia kondom kwani ntakuwa sina hofu ya kupata mimba au magonjwa ya zinaa.
Kama atakuwa bado hajashawishika kutumia kondom au hata anajaribu kukushawishi msiiitumie, ni haki yako kukataa kufanya mapenzi nae. Jiheshimu, na kama mpenzio hajali maoni yako basi mpenzi huyo hakufai, kwa hivyo hustahili kamwe kufanya mapenzi nae. Kumbuka hatua yoyote utakayochukua ni uamuzi wako. Sije ukajikuta unajuta baada ya kukubali matakwa ya mpenzio.
Wanaume wengine hutoa kila kisingizio na kisababu cha kutotaka kutumia kondom … Huenda akakwambia:
"Ninataka kuwa karibu nawe zaidi mpenzi! Nakupenda sana! kwani wewe hunipendi?" ...
"kufanya mapenzi na kondom ni kama kula peremende na karatasi yake!"...
"Kwa mara moja tu, basi tufanye leo kesho tutatafuta hizo kondom" ...na kadhalika
Hapo una mawili ya kuchagua.
1. Unaweza kuendelea kucheza mchezo wa mapenzi bila kuingiliana.
2. Unaweza kufunga virago na kujiendea zako!

Kamanda wa waasi auawa Libya

Abdel Fattah Younes alimuasi Gaddafi na kujiunga na waasi

Kiongozi wa kijeshi wa waasi nchini Libya wanaokabiliana wakitaka kumpindua Kanali Muammar Gaddafi ameuawa, baraza la mpito la Libya limesema.

Kiongozi wa baraza hilo Mustafa Abdul-Jalil amesema Jenerali Abdel Fattah Younes ameuawa na watu wanaomuunga mkono Gaddafi, na kiongozi wa watu hao tayari amekamatwa. Amesema Jenerali Younes aliitwa kwenye mkutano ambapo alitakiwa aeleze kuhusu harakati za kijeshi, lakini aliuawa kabla ya kufika kwenye kikao hicho. Taarifa zinasema kuwa Jenerali Younes alishukiwa kuwa na uhusiano na majeshi yanayomuunga mkono Gaddafi.

Jenerali Younes ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani ambaye alikimbia na kujiunga na upande wa upinzani mwezi Februari. Wasaidizi wawili wa Jenerali Younes, Kanali Muhammad Khamis na Nasir al-Madhkur, pia waliuawa kwenye shambulio hilo, Bwana Jalil alisema.

Taarifa ambazo hazikuweza kuthibitishwa zilisema kuwa Jenerali Younes na wasaidizi wake wawili walikamatwa mapema siku ya Alhamisi katika eneo la kaskazini mwa Libya. Mapema siku ya Alhamisi, waasi walisema kuwa wameteka mji muhimu wa Ghazaya karibu na mpaka wa Tunisia, baada ya makabiliano makali na vikosi vya Kanali Gaddafi.

Thursday, July 28, 2011

Mapigano makali Somalia

Mapigano Somalia
Mapigano Somalia

Mapigano makali yamezuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, siku moja baada ya shirika la Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa(WFP) kupeleka kwa ndege ya msaada wake wa kwanza wa dharura kwa watu walioathiriwa na ukame.

Inaarifiwa takriban watu wanne wameuawa baada ya vikosi vya serikali vikisaidiwa na askari wa Muungano wa Afrika kuwashambulia wapiganaji wa harakati za kiislamu. Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu Mohamed Dhore anasema mapigano hayo yametokea katika maeneo ya kaskazini na hayataathiri shughuli za kupeleka misaada.

Maelfu ya watu wamewasili katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali wakitafuta chakula.
Waandishi wa habari wanasema ikiwa vikosi vya serikali vitaweza kuyateka maeneo zaidi, basi mashirika ya misaada yataweza kuyafikia maeneo mengi zaidi yalikumbwa na njaa. Shehena hizi za WFP ndio sehemu ya kwanza ya kupeleka chakula tangu Umoja wa Mataifa uyanadi maeneo mawili ya kusini mwa Somalia kwamba yanakabiliwa na janga la njaa.

Kundi la Al-Shabab, lenye fungamano na al-Qaeda ambalo linadhibiti sehemu nyingi za Somalia, limelipiga marufuku shirika la WFP katika maeneo yake.

Hali ya ukame katika Pembe ya Afrika imesababisha janga la ukosefu wa chakula katika nchi za Kenya, Ethiopia, Djobouti na Somalia. Hali ya hewa katika bahari ya Pacific imesababisha ukosefu mkubwa wa mvua kwa misimu miwili mfululizo na hakuna matumaini ya kunyesha mpaka mwezi wa September.

Takriban watu millioni kumi wameathiriwa na ukame mbaya ambao haujapata kutokea katika kipindi cha miaka 60. Na hali imezidi kuwa mbaya kwa sababu ya mapigano yanayoendelea katika eneo hilo.

New Scholarships and Financial Aid Updates from Scholarship-Positions.com


New Scholarships and Financial Aid Updates from Scholarship-Positions.com

Dear Student,

Please find recently updated scholarships on Scholarship-Positions.com. Help Others: Please forward this email to your friends if they are also interested in scholarships.


Netherlands Govt Fellowship for International Students on Broadcast Management, 2012, Netherlands 
Dutch Government Diploma Fellowship for International Students in the field of Broadcast Management at RNTC in Netherlands-2012 Study Subject(s):Broadcast management Course Level:Diploma.. [Read Full Scholarship Detail]

International PhD Program Molecular Biology, Germany
International PhD Program Molecular Neurobiology : Berlin, Germany, Max Delbrueck Center for Molecular Medicine The Helmholtz International Research School Molecular.. [Read Full Scholarship Detail]
PhD Scholarship in Computer Science at Saarland University, Germany 
Scholarship  opportunities for international students at University of Saarland in Germany. Study Subject(s):Computer Science Course Level:PhD Scholarship Provider: German Excellence.. [Read Full Scholarship Detail]

Call for Doctoral Scholarships in “Materials for Engineering ” at University of Brescia, Italy 
Scholarships for international students in the field of engineering at University of Brescia, Italy Study Subject(s):Chemical Basis of Technologies, Physics,.. [Read Full Scholarship Detail]
SAB Bursaries for Undergraduate Degree Program, South Africa 
SAB Ltd is the South African beverage arm of SABMiller plc calls  South African students for scholarship applications for Undergraduate.. [Read Full Scholarship Detail]



2011 Short-term Grants for PhD Students in Information Structure at University of Potsdam and Humboldt University Berlin, Germany 
6 Short-term Grants for PhD students in the Integrated Graduate School of the Collaborative Research Centre in Information Structure at.. [Read Full Scholarship Detail]


OTSS Graduate Studies Bursary Program at OCAD University, Canada 2011/2012 
Graduate Bursary for Canadian Citizen in the field of Contemporary Art History, Art,  Media & Design, Strategic Foresight, Criticism & Curatorial.. [Read Full Scholarship Detail]


Call for Indo-Danish Proposals for Strategic Research Collaborations within Health Science Biotechnology, India 
Research Proposals in the field of health science biotechnology funded by Department of Biotechnology (DBT) ,and the Programme Commission on.. [Read Full Scholarship Detail]




2012 IEDC Executive MBA Scholarships, Slovenia 
IEDC-Bled School of Management announced scholarship for Master’s student, Slovenia -2012 Study Subject(s): Management Course Level: Master’s Scholarship Provider: IEDC-Bled.. [Read Full Scholarship Detail]

Scholarships for College Sophomores in USA - 2011 
Are you already attending the college?  Do you know that even though you have been attending college for a year,.. [Read Full Scholarship Detail]


Read more: International PhD : College Scholarships, PhD Scholarships, Postdoctoral, Graduate International Scholarships Fellowships 
http://scholarship-positions.com 

Research Studentship at University of Oslo/Institute of Cancer Research the Norwegian Radium Hospital, Norway
Center for Breast Cancer Research at University of Oslo/Institute of Cancer Research The Norwegian Radium Hospital and partners at NTNU.. [Read Full Scholarship Detail]


Postdoctoral Position in Nanomedicine at University of Copenhagen, Denmark
University of Copenhagen offers Postdoctoral Position in the field of molecular pharmacology, molecular biology and protein biochemistry, Denmark Study Subject(s):Nanomedicine.. [Read Full Scholarship Detail]

Wabunge wataka ukweli kuhusu samaki wa Japan

SAKATA la samaki wanaodaiwa kuwa na sumu kutoka Japan walioingizwa nchini, limefikishwa bungeni na wabunge wameitaka Serikali ifafanue ukweli wa jambo hilo ikiwa ni pamoja na kueleza ni namna gani waliingizwa.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kambi ya Upinzani pamoja na wabunge waliochangia jana bungeni kwa nyakati tofauti, walieleza kushitushwa na taarifa hizo na wakataka Serikali itoe tamko bungeni.

“Kuna taarifa kwamba samaki wenye sumu wameingizwa nchini, pamoja na uzito wa jambo hili, Serikali haijatoa tamko. Kwa mamlaka niliyo nayo, naitaka Serikali itoe tamko ieleze ukweli wa suala hili na hatua zinazochukuliwa,” alisema Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba (CCM) kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati, Profesa David Mwakyusa.

Mbunge huyo alikuwa akisoma taarifa ya Kamati ya Bunge kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Makadirio ya Matumizi ya mwaka 2011/12.

Kambi ya upinzani kupitia kwa Msemaji wake Mkuu kwa Wizara ya Maendeleo na Mifugo, Silvester Kasulumbayi, ikitumia taarifa za vyombo vya habari vya Julai 26, ilihoji ni namna gani kampuni ya Alphakrust Limited ya Dar es Salaam, iliruhusiwa kuingiza samaki hao.

“Kama TDFA ndiyo waliotoa kibali cha kuingizwa kwa samaki hao baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha kuwa hawana madhara, ni nani na wa mamlaka gani aliyegundua kuwa wana madhara? Ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya maofisa waliohusika kutoa kibali husika?” alihoji Kasulumbayi.

Wabunge hao wa upinzani walihoji sababu ya Tanzania yenye maziwa na bahari kuagiza samaki kutoka nje ya nchi. “Kwa rasilimali hii yote tuliyopewa na Mwenyezi Mungu iliyojaa samaki wengi wa kila aina, kama Taifa tuna haja kweli ya kuagiza samaki kutoka nje ya nchi?
“Kwa nini fedha zetu za kigeni zisitumike kununua mahitaji mengine ambayo hayapatikani nchini?” aliendelea kuhoji.

Naye Amir Mhando, anaripoti kwamba Mbunge wa Nyamagana Ezekia Wenje na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, wote wa Chadema jana ‘walichafua hewa’ kwa muda kwenye ukumbi wa Bunge kutokana na hoja zao tofauti.

Hatua hiyo ilisababisha Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Dole, Sylivester Mabumba (CCM), kumtoa nje ya ukumbi Wenje na pia kumtaka Lissu athibitishe kauli yake, kwamba Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa, amesema uongo bungeni.

Zogo lilianza muda mfupi baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu saa nne asubuhi, wakati Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), aliposimama na kuomba kutoa taarifa kuhusu tukio lililotokea mapema wakati wa kipindi cha maswali na majibu likimhusisha Lissu.

Machali alisema isingekuwa busara kwa Lissu kuambiwa apeleke uthibitisho wake kwa Mwenyekiti kuhusu kauli kwamba Naibu Waziri kasema uongo.

Alisema badala yake Lissu alitakiwa afanye hivyo saa tano asubuhi, wakati muda huo ilikuwa saa nne, huku shughuli zikiendelea, hivyo angepewa nafasi mpaka saa saba mchana wakati shughuli za Bunge zinapokuwa zimesitishwa kwa muda.

Lakini akizungumzia jambo hilo, Mwenyekiti Mabumba alisema kwa vile Lissu wakati anatoa kauli hiyo alisema ana ushahidi ambao angeweza kuuwasilisha hata wakati anazungumza, hilo si tatizo na kuongeza kuwa wakati anatoa kauli yake pia alishaanza kugusia uthibitisho wake.

Kutokana na majibizano hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisimama na kusema hakuna haja ya wabunge kuvimbiana na kwa vile Lissu aliahidi mwenyewe apeleke na kama ataona muda hautoshi amwambie Mwenyekiti amwongeze muda.

Baada ya kauli ya Lukuvi, Wenje alisimama na kuomba Mwongozo wa Mwenyekiti, lakini hakuruhusiwa na kusikika akiita mara kadhaa: “Mwenyekiti hoja ya dharura… hoja ya dharura Mheshimiwa Mwenyekiti ”.

Mwenyekiti alijibu kuwa hakuna haja ya hoja ya dharura, kwani hoja hiyo inawasilishwa kama kuna vita na nchi sasa haina vita, hivyo kumtaka Katibu aendelee na ratiba nyingine, ambayo ilikuwa ni hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Lakini Wenje aliendelea kumwita Mwenyekiti na kutaka Mwongozo, huku Mwenyekiti naye akimtaka akae chini, lakini waliendelea kubishana kwa dakika kadhaa na Mwenyekiti kutishia kumtoa nje ya kikao.

Hata hivyo bado Wenje hakutii agizo la Mwenyekiti, ndipo alipoagiza askari wamtoe ukumbini na hatua hiyo kutekelezwa mara moja, huku baadhi ya wabunge wakilalamika chini chini hasa wa upinzani, wakati wa CCM wakipiga meza zao kuunga mkono.

Akizungumza nje, Wenje alisema Mwenyekiti hakumtendea haki kwani hoja yake ya dharura aliyokuwa anataka izungumzwe ni kuhusu taarifa ya kuingizwa nchini kwa samaki wenye sumu kutoka Japan.

Alisema taarifa alizonazo ni kuwa kuna tani 1,600 za samaki hao mitaani hazijakamatwa na Polisi na wananchi wanawatumia na hali hiyo ni hatari na jambo linalohitaji udharura.

Wabunge waghushi saini ya Pinda

BUNGE la Tanzania linakoelekea sasa si kuzuri. Pengine ndivyo inavyoweza kuzungumzwa kuhusu mambo yanavyokwenda ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali. Hali hiyo inatokana na tukio la juzi usiku baada ya wabunge au Mbunge asiyefahamika, kughushi saini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati kikao kikiendelea.

Aliyeweka wazi aibu hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, muda mfupi baada ya Bunge kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka 2011/12 yaliyowasilishwa Jumatatu na Waziri Profesa Jumanne Maghembe, ambapo Sh. bilioni 258.3 ziliidhinishwa.

Baada ya Mwenyekiti wa Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (CCM) kuzungumzia kupitishwa kwa bajeti hiyo na kumpongeza Waziri na wabunge, huku akijiandaa kusitisha shughuli za Bunge ikiwa ni karibu saa 2:15 usiku, alisimama Waziri Lukuvi na kuomba Mwongozo wa Mwenyekiti.

Katika maelezo yake ya kuomba Mwongozo, Lukuvi alisema kumeibuka tabia ndani ya Bunge ambayo si ya kistarabu, kwani baadhi ya wabunge wamekuwa wakiandika ujumbe kwenye vikaratasi kuonesha mhusika fulani anaitwa wakati hakuna jambo kama hilo.

“Kwa leo (juzi) hapa yametokea matukio mawili ya wabunge Joseph Selasini (Rombo-Chadema) na Leticia Nyerere (Viti Maalumu-Chadema) kupelekewa ujumbe kwa nyakati tofauti ukionesha umesainiwa na Waziri Mkuu akiwaita.

“Lakini jambo la ajabu Waziri Mkuu mwenyewe hajui lolote na anashangaa jambo hili maana hakuandika ujumbe kuwaita,” alisema Waziri Lukuvi na kusababisha mshangao kwa baadhi ya wabunge.  Kutokana na mazingira hayo, aliomba suala hilo liachwe na kwamba si tabia nzuri ambayo imeanza kujitokeza.

Akizungumzia suala hilo, Simbachawene naye alilaani jambo hilo na kusema kwa vile karatasi iliyoandikwa alikuwa nayo, itakuwa rahisi kumbaini mhusika na kumshughulikia.

“Karatasi yenyewe imeandikwa hivi: Mheshimiwa Joseph Selasini, naomba uje kuna jambo tujadili, nahitaji ufafanuzi kutoka kwako - Mizengo Pinda,” alisema Simbachawene na kuongeza kuwa karatasi hiyo imesainiwa kuonesha aliyesaini ni Waziri Mkuu.

“Ndiyo maana nilimwona Mheshimiwa Selasini amekwenda kwa Waziri Mkuu akiwa amejikunyata kistaarabu kuona ameitiwa kitu gani, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu wala alikuwa hamfuatilii, alikuwa ameelekeza mawazo yake katika majibu ya Waziri,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alieleza kuwa jambo hilo ni la aibu kubwa kwa wabunge, kufikia hatua ya kughushi saini ya Waziri Mkuu na kusisitiza lazima ichukuliwe uzito unaostahili.

Tangu Bunge la 10 lianze, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba limepoteza heshima kutokana na baadhi ya wabunge kufanya mambo ambayo hayaendani na chombo hicho – ya kitoto.

Masuala ya kuzomeana, kupigana vijembe na wakati mwingine kuzungumza bila mpangilio, ni baadhi ya mambo yanayopigiwa kelele na wadau kwamba yanakivunjia heshima chombo hicho, ambacho ni moja ya mihimili mikuu mitatu ya Dola.

Libya yashtumu Uingereza kwa kutambua waasi

Kanali Muammar Gaddafi

Serikali ya Libya imeshtumu uamuzi wa Uingereza kuwatambua waasi wa Libya kama "serikali yenye mamlaka" baada ya Ufaransa na Marekani kufanya hivyo pia.Khaled Kaim, naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni katika serikali ya Muammar Gaddafi,ameambia waandishi wa habari kwamba uamuzi huo si wa busara na ni wa kupotosha.Libya itaomba mahakama ibatilishe uamuzi huo, alisema.

Uingereza imeamrisha kufukuzwa kwa wanadiplomasia wanane wa Gaddafi nchini humo. Uongozi wa waasi, Baraza la utawala wa mpito (NTC), limempendekeza Mahmud Al-Naku, mwandishi wa habari, kama balozi mpya wa Libya mjini London.

Akizungumza na BBC alisema amekuwa uhamishoni kwa miaka 33 kwa sababu ya kupinga utawala wa Gaddafi.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza William Hague amesema baraza hilo la mpito limeonyesha nia yake ya "kuwa na Libya yenye uwazi na demokrasia... tofauti na Gaddafi ambaye udhalimu wake dhidi ya watu wa Libya umemuondolea uhalali wa kutawala nchi".

Bendera ya kijani ya serikali ya Gaddafi bado ilikuwa inapepea nje ya ubalozi wa Libya eneo la Knightsbridge mchana wa Jumatano huku waandamanaji waliobeba bendera zenye rangi nyekundu, kijani na nyeusi za waasi wakikusanyika nje ya ubalozi huo.

Kufwatia uamuzi wa Marekani wa kutambua baraza la mpito wiki mbili zilizopita, BBC imefahamishwa kuwa Marekani imepata ''ombi rasmi'' kutoka kwa waasi kufungua tena ubalozi wa Libya mjini Washington.
bendera ya waasi nchini Libya

Maafisa wa Marekani wanasema "wanatafakari" ombi hilo.
Waasi wa Libya na vikosi vinavyomuunga mkono Gaddafi bado wanapigana, miezi mitano tangu kuanza upinzani dhidi ya utawala wa miaka 42 wa Muammar Gaddafi, huku shirika la Nato likiendelea kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la kutoruhusu ndege kupaa juu ya anga ya Libya.

Watendaji wa Kata sasa kuwa na shahada

SERIKALI imesema itahakikisha kuwa watendaji wa Kata wanaoajiriwa ni waliohitimu chuo kikuu na si wenye elimu ya msingi.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) aliliambia Bunge jana kwamba itahakikisha watendaji hao wanapatiwa pia elimu ya uongozi kabla ya kupelekwa kuongoza kata yoyote.

Mwanri aliwataka wabunge wenye kata zisizo na watendaji wapeleke orodha kwake ili pengo hilo lizibwe kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu kuhakikisha kwamba tatizo la ukosefu wa watendaji katika kata linatatuliwa.

Naibu Waziri huyo alikuwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali akiwemo Mbunge wa Longido, Michael Laizer (CCM) ambaye katika swali la nyongeza alisema baadhi ya kata na vijiji jimboni mwake havina watendaji. “Je Serikali haioni lengo la kupeleka madaraka na huduma vijijini halijatimia,” alihoji Laizer.

“Tumejaribu kuzibaziba. Kama kuna kata ambazo hazina watendaji wa Kata, hatupeleki waliomaliza darasa la saba, bali wahitimu wa chuo kikuu, kama kuna wabunge wenye kati zisizo na watendaji, walete orodha, tayari tuna maelekezo kutoka kwa Waziri Mkuu tuhakikishe tatizo linamalizwa," alisema na kuongeza kuwa watahakikisha wanapelekwa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, wanolewe kabla ya kuajiriwa.

Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akunaay (CHADEMA) alishutumu kuwa uundaji wa vijiji unafanywa kienyeji na wakati huo huo akasema wakati wa uchaguzi vijiji vimekuwa vikiundwa na kutengeneza kata kisiasa.

Akijibu hoja hiyo, “kusema kuunda uunda ni kufanya kienyeji. Hakuna kijiji kimeundwa kienyeji. Habari kwamba tunaundaunda hapa hakuna.”

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Biharamulo, Dk. Anthony Mbassa (CHADEMA) alitaka aelezwe ni lini Serikali itatenga tarafa mbili zilizokuwepo na kuwa angalau nne ili kufanikisha suala zima la kiutawala na kiutendaji katika Wilaya ya Biharamulo.

Alitaka pia kufahamu ni lini Serikali itatoa miliki za vijiji hivyo. Mwanri alisema Serikali imegawa maeneo mapya ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi na kuharakisha maendeleo ya nchi ambapo kupitia tangazo la Serikali Namba 173 la Mei 7, 2010, Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo ilipatiwa maeneo mapya kutoka kata saba na kuwa kata 15.

Vijiji viliongezwa kutoka 25 hadi 74, vitongoji vipya vikaongezwa kutoka 85 hadi 384. Hata hivyo alisema halmashauri imeendelea kuwa na tarafa mbili za Nyarubungo na Lusahunga.

Wednesday, July 27, 2011

Mapenzi Salama

Vijana wanaohisika kimapenzi

Kama unahisi uko tayari kufanya mapenzi, au tayari unashiriki katika ngono, ni vyema kuchukua tahadhari. Hakikisha katika harakati zako za kufanya mapenzi, unajali afya yako kwa kufanya ngono iliyo salama.
Inaweza kuwa vigumu, na jambo unalolionea haya kujadiliana na mpenzi wako, swala la uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa, na kutumia njia za kuzuia mimba. Lakini kulikwepa swala hilo kwaweza kumaanisha kuhatarisha afya na maisha yako kwa jumla. Kufanya mapenzi salama , maana yake ni kutafakhari maswala hayo na kisha kuchukua hatua zifaazo.
... bofya link ufahamu hatua zifaazo...


Punyeto Ni nini?

Kufanya au kupiga punyeto, ni tendo la kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi.
Kwa hivyo katika kupiga punyeto hamna hofu ya kuambukizwa magonjwa yanayosambazwa kupitia ngono, kwani haimshirikishi mtu mwengine.

Punyeto ni toshelezo kamili la kimapenzi kama utatumia njia mbali mbali za kujitomosa na kujipa papasa ya kujistarehesha.

Hakuna mtu anayezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inakubidi kujifunza kwa majaribio salama.

Na, kwa vile kila mtu yuko tofauti, njia nyengine ya kujua jinsi unavyoweza kumstarehesha mpenzi wako, ni kujifunza kutoka kwako mwenyewe. Shughulika zaidi na sehemu ambazo zinasisimka kwa urahisi.

Unaweza kufikia kilele cha starehe yako kwa kuitomasa tomasa mboo au kisimi, lakini kutakupa hamu kubwa na ashiki, na kufikia kutoshelezwa vya kutosha, kama utapapasa pia sehemu nyenginezo za mwili wako.

Kwa nini punyeto huonekana kuwa makosa?

Msimamo wa dini nyingi na watu wengi ni kuwa punyeto ni dhambi, mwiko, jambo lililokatazwa, jambo lisilokubalika kabisa. Lakini wanasanyansi wanasema ni jambo salama kiafya na dhana zilizopo kulihusu, ni imani za kibinafsi na chaguo la mtu.

Wanaume wengi na wanawake hupiga punyeto maishani mwao, kwa sababu huwafanya wakajisikia vizuri na huondoa dhiki za mihemko ya kimapenzi bila kujiingiza katika ngono na mtu mwengine. Pia hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya HIV ni kichocheo tosha kinachopelekea baadhi ya watu kupiga punyeto.


Njia za kuzuia mimba

Dawa au vifaa vya uzazi ni baadhi ya taratibu zinazotumiwa kuzuia mimba kutungwa. Ikiwa msichana au wanamke atafanya mapenzi pasi na kutumia mojawapo ya mbinu hizo basi, kuna uwezekano wa theluthi moja kwamba atapata mimba. Hata hivyo aina yoyote ya kuzuia mimba utakayoichagua ni lazima itumiwe kama ilivyoagizwa, ili kuleta matokeo ya hakika.

Baadhi ya njia hizo kama vile kutumia kondom wakati wa ngono, pia kwa kiasi fulani humpa mtu kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya HIV, na magonjwa mengine yanayoathiri afya ya uzazi. Kwa vile mbinu za kuzuia uzazi ni za aina tofauti tofauti, ni muhimu basi uchague kwa makini ile inayokufaa. Utapata usaidizi wa kitaalam kama utashauriana na daktari wako, au pata usaidizi katika kituo cha kwenu cha upangaji uzazi, au kituo cha vijana.

Mbinu za kuzuia mimba (Contraception)

Hivi ni vifaa au dawa zinazotumiwa kwa minajili ya kuzuia mimba kutungwa wakati wa kufanya ngono.
Kuna zile zinazotumiwa kwa mda mfupi na nyengine kwa mda mrefu. Nyengine hufanya kazi papo hapo na nyengine huitaji maandalizi ya mda.

Kondom au tembe maalum ndizo njia bora zinazojulikana zaidi za kuzuia mimba. Pia kondom zina manufaa bora zaidi zinapotumuwa kwani mbali na kuzuia mimba zinapotumika kama inavyopaswa zinaweza pia kumkinga mtu asiambukizwe vurusi vya HIV, na magonjwa mengine ya zinaa.

Vifaa vya kuzuia mimba.

Moja ya mbinu bora na rahisi za kuzuia mimba, ni kuweka kizuizi, kwa lengo kuwa mbegu ya mwanaume na ile ya mwanamke zisikutane. Kwa maana hiyo kifaa maalum kinaweza kuwekwa katika njia inayotumiwa na mbegu ya kiume ndio isilifikie yai la mwanamke.

Baadhi ya vifaa hivi (hasa kondom) pia vinaweza kukinga kuambukizwa virusi vya Ukimwi, na magonjwa mengine ya kuambukizana kupitia ngono.

Kuna aina kadhaa za vifaa vya kuzuia mimba. Kondom za wanaume na zile za wanawake ndio vifaa vinavyofahamika zaidi, hata hivyo kuna pia vifaa vyenginevyo viitwavyo diaphragm na caps kwa kimombo ambavyo vinaweza kutumiwa na wanawake.
kondomu
kondomu

Kondom za wanaume: Hivi hutengenezwa kutokana na aina maalum ya mpira uitwao latex, au plastiki nyembamba. Kondom ya mwanaume huvaliwa kwenye uume iliyosimama, tena kabla ya uume kuingizwa ukeni. Ikitumiwa kama inavyotakikana inakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98.

Kwa kawaida kondomu hupatikana kwenye vituo au kliniki za upangaji uzazi, kwenye maduka ya madawa au hata maduka ya kawaida.

kondomu
Kondomu za wanawake

Kondomu za wanawake: Halkadhalika hutengenezwa kwa mipira laini ya latex au plastiki nyembamba maalum. Huvaliwa ndani ya uke, huku sehemu iliyowazi ikichomoza nje kidogo. Kwa kawaida kondom za wanawake ni ghali, na pia utendaji kazi wake unakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 95.


Aina nyenginezo na vifaa vya kuzuia mimba huwa hazipendekezwi kwa vijana lakini ni vyema kuvijua.
Kuna aina nyenginezo za vifaa vya kuzuia mimba viitwavyo diaphragms na caps. (tazama michoro) Hivi hutengenezwa kutokana na kitu kiitwacho silicone au mpira laini maalum. Vikiwekwa ukeni hutumika kama vizibo vya kuzuia mbegu za mwanaume kupenya hivyo basi haiwezi kukutana na yai la mwanamke.

Kwa kawaida caps ni ndogo kuliko diaphragms lakini kwa vile wanawake pia wana maumbo tofauti, ni sharti upate saizi utakayokutosha. Hapa ni sharti upate usaidizi wa daktari wako, au muuguzi, kuiweka.

Inapowekwa mahali pake ndani ya uke, iwe diaphragm au cap, huziba kilango cha mfuko wa uzazi hivyo basi mbegu ya mwanaume haitapatanafasi ya kupita. Ukishaonyeshwa na daktari jinsi ya kuipachika, baadae unaweza kuipachika mwenyewe kabla ya kufanya mapenzi.

Kwa matokeo bora zaidi, diaphragms na caps hutumiwa pamoja na dawa iitwayo (spermicide) ambayo huuwa mbegu za uzazi za mwanaume. Hapo diaphragms au caps humpa mwanamke kinga dhidi ya mimba kwa asilimia kati ya 92 na 98.

Hata hivyo itachukua mazoezi ya muda ili kuvitumia itakikanavyo. Wakati mwengine pia hutumiwa na gel yake maalum lakini bado havina hakikisho la asilimia mia moja kuzuia mimba. Faida yake nyengine ni kuwa, kwa kiasi fulani, vinaweza kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na saratani ya (cervix) lango la nyumba ya uzazi.
Ikiwa wewe hutumia vifaa kama diaphragms au caps, au hata kondom, ni vyema kujipangia mapema ndio usikose akiba, ndio haitakuwa karaha kuvitafuta pale unapovihitaji.

Mbinu nyingine za kuzuia mimba

Kuna chembe chembe za kimaumbile, zinazojulikana vyema kama homornes ambazo hutumiwa kutengeneza tembe au chanzo ya kuzuia mimba. Chembe chembe hizi kwa jina maalum progestogen yaani mchanganyiko wa oestrogen na progestogen, huingizwa mwilini mwa mwanamke kwa mpangilio na kiwango maalum ili kuzuia mimba kutungwa.

Hufanya kazi kwa namna hii:
* Kwa kuzuia ovari kuangua mayai
* Kwa kuzuia mbegu za mwanamme kulifikia yai (kwa kufanya majimaji ua ukeni kuwa mazito na kunata hivyo kuzuia mbegu ya mwanamme kupenya)
* Kwa kulizuia yai kujipachika kwenye kiota cha nyumba ya uzazi.

Chembe
Chembe za kimaumbile

Tembe mchanganyiko - huwa ni kidonge cha dawa kilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa chembe chembe za oestrogen na progestogen. Hii huzuia mimba kwa njia zote tatu tulizozitaja hapo juu na ikitumiwa itakikanavyo, vinategemewa kuzuia mimba kwa asilimia 99.

Tembe ni rahisi kutumia - Mradi tu unakumbuka kumeza vidonge kulingana na maagizo. Wakati mwengine pia huifanya hedhi, kupungua na kupunguza pia maumivu wakati wa hedhi.

Lakini athari zinazoandamana na utumiaji wa vidonge hivyo ni pamoja na kuchafukwa na moyo, kuongezeka unzani, na athari mbaya zaidi ni iwapo itatokea hali ya kuganda kwa damu kwenye mishipa ya kupitisha damu.

Vidonge vya Progestogen pekee (POP) - Aina hii ya Tembe huitwa pia “mini pill” na huwa ina chembe chembe za progestogen pekee. Huzuia mimba kwa njia kama zile zile zinazozuia tembe za mchanganyiko, na ina utendaji kazi wa kati ya asilimia 96 na 99. Hata hivyo kama una uzani wa zaidi ya kilo 70 uwezo wake wa kuzuia mimba hupungua

Faida kuu ya kutumia vidonge hivi ni kwamba vina athari ndogo za kiafya. Lakini tatizo ni kuwa ni sharti tembe imezwe wakati ule ule kila siku , kama umechelewa basi isipitishe zaidi ya masaa matatu.

Sindano - Hii ni chanjo ya kuzuia mimba inayotengenezwa na chembe chembe hizo hizo za homoni ya progestogen. Tofauti na tembe, ambazo ni sharti kumeza moja kila siku, sindano pindi inapodungwa inakupa kinga dhidi ya mimba, kwa mda wa kati ya wiki nane hadi 12 kuambatana na aina inayotumiwa. Hudungwa takoni, na dawa kuingizwa ndani ya mishipa ya damu na ina uwezo wa kuzuia mimba kwa asilimia 99.

Faida kuu ya njia hii ya sindano, ni kwamba hutakuwa na wasiwasi wa kupata mimba unapofanya ngono, kwa mda wa angalau wiki nane au 12.

Lakini pia ina athari zake - ni kwamba huenda dawa hii ikavuruga mpangilio wako wa kawaida wa kupata hedhi, au ukatoka hedhi kiwango kisicho cha kawaida cha damu, au kwa mda mrefu, au hedhi ikapotea kabisa. Pia inaweza kusababisha kuongezeka uzani.

Homoni au Vidonge vya kupachika chini ya ngozi - Hapa dawa kama ile ile ya tembe au chanjo, hutengenezwa na kuwekwa kwenye kifaa cha plastic mfano wa kijiti cha kiberiti. Hupachikwa ndani ya ngozi chini ya kwapa kwa kufanyiwa upasuaji mdogo.

Hii ni njia ya mda mrefu ya kuzuia mimba. Inaaminika kuzuia mimba kwa aslimia 99 na inaweza kufanya kazi kwa mda wa hadi miaka mitatu. Kuna aina nyenginezo za upangaji uzazi ambazo, ingawa kwa hali ya kawaida hazipendekezwi kwa vijana, si vibaya kuzijua.

Kitanzi au koili, ambacho kwa lugha ya kitaalam kinajulikana kama Intra-uterine device au IUD hutengenezwa kwa plastiki na shaba, na hupachikwa kwenye mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.
Vitanzi huanza kufanya kazi pindi kinapopachikwa. Hufanya kazi kwa njia mbili kuu. Kwanza, kwa kuzuia mbegu za kiume kutangamana na yai, na pili kuzuia yai kukubaliwa kujipachika ndani ya mfuko wa uzazi.

Kitanzi au koili kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98 na 99. Na pindi kikitolewa asili ya uwezo wa wanamke wa kushika mimba anapofanya ngono, unarudi vilevile.

Hata hivyo moja ya matatizo ya kitanzi ni kwamba vinaweza kuifanya hedhi yako kuwa nzito (damu kutoka nyingi) na pia huenda ukapatwa na maumivu, mara nyengine inaweza kutoka mahali kilipowekwa na kusukumwa nje ya mfuko wa uzazi. Hivyo ni vyema kumuona daktari mara kwa mara ili kama imechomoka, ipachikwe tena vyema.


Njia asilia ya mpango wa uzazi.

Njia hii inahitaji makini sana kuitumia. Kwani inafanya kazi tu ikiwa wanamke anafanya mapenzi tu wakati ule ambao kiasilia hawezi kushika mimba. Hii inawezekana kwa kutayarisha tarakimu za siku za hedhi, na kupima hali ya joto la mwili. Njia hii inahitaji uangalifu na uzoefu mkubwa – Kwa vile ni ya kubahatisha haipendekezwi kwa vijana ambao hawako tayari kupata mtoto.

Kwa bahati mbaya watu wengi hudhani kwamba kutoa uume kutoka ukeni, pindi tu kabla ya kufikia kilele cha kumwaga manii, ni moja ya njia za kuzuia mimba. La sivyo kwani mara nyingi mbegu za kiume hutangulia kutoka hata kabla kufikia kilele katika hali ya kufanya mapenzi. Hivyo basi hata ukitoa uume huenda umeshachelewa!

Vasectomy au Tubuligation - Hii ndiyo njia pekee ya kudumu ya kuzuia mimba.
Vasectomy ni njia ya kumfanya mwanamme asiwe na uwezo wa kutunga mimba ilhali Tubuligation ni njia ya kumfanya mwanamke asiwe na uwezo wa kushika mimba. Hii inafanyika kwa njia ya upasuaji mdogo. Mwanamme anafanyiwa upasuaji kwa kukata vibomba vinavyopitisha mbegu za kiume kutoka kwenye makende hadi kwenye uume. Upasuaji huu kwa mwanamke unahusisha kukatwa au kuzibwa kwa vibomba vinavyopitisha mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi.

Baada ya upasuaji huu, ni vigumu mwanamke au mwanamme kurudishwa tena katika hali ya mwanzo ya kuweza kuzaa, kwa hivyo njia hii inatumiwa tu kwa sababu za kimatibabu au ikiwa mhusika amefikia uamuzi wa hakika kwamba hataki tena kupata watoto (zaidi).

Kitanzi cha Intra uterine system au IUS - Hiki nacho kimetengezwa kwa plastiki, yenye muundo wa T kikiwa na chechembe za homoni ya progestogen ndani. Kinaweza kupachikwa ndani ya mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.

Kitakapopachikwa, progestogen pole pole huingia ndani ya mwili, na kuzuia mimba katika njia ile ile kama vinavyozuia tembe. Kinaweza kutumika kwa mda wa miaka 5, na kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 99.

Kitanzi cha IUS ni kizuri kwa wale walio na matatizo ya maumivu wakati wa hedhi, kwa sababu kinapopachikwa (ingawa wakati wa kupachikwa huenda ukapata maumivu kidogo) baadaye husaidia kupunguza hedhi au hata kuisitisha kabisa, kutokana na homoni hizo za progestogen.

Madhara ya njia hii nayo ni kama, kuongeza uzani, kuumwa na kichwa, kutokwa na damu kusiko na mpango, na mabadiliko ya majira ya hedhi. Pia inaweza kuchopoka, hivyo itabidi kumwona muuguzi au daktari kila mwezi kuhakikisha kiko sawa.

Ni vyema kujadili juu ya aina mbalimbali za mpango wa uzazi ili kuchagua vyema. Daktari wako au muuguzi atakushauri ipasavyo.

Hata hivo kumbuka njia hizi za kuzuia mimba hutumiwa zaidi kwa minajili ya mpango wa uzazi, hivyo basi haziwezi kukukinga dhidi ya maambukiko ya virusi vya Ukimwi, au magonjwa mengine yayayosambazwa kupitia ngono.

Ni busara kutumia kondom kila unapofanya mapenzi na mtu ambaye afya yake ya uzazi huifahamu - Hakikisha pia unaufahamu vizuri jinsi ya kutumia kondom na unajua jinsi ya kufanya ngono salama kwa jumla.

Condom zawa adimu Kenya

Huku Serikali ya Kenya ikiimarisha kampeni dhidi ya UKIMWI, mbinu moja imekuwa kuhamasisha jamii kuhusu kinga kwa kutumia mipira ya kufanyia mapenzi, CONDOM. Kinga hii imefanikiwa katika maeneo ya mijini. Hata hivyo hali ni tofauti vijijini. Miongoni mwa jamii ya wafugaji, Condom imekuwa ni bidhaa nadra sana kupatikana, hali inayowafanya kutumia njia mbadala, baadhi zikiwa hatari, wafugaji watumia plastiki.

Kenya: Wabunge walipe kodi au wasilipe?

Idara ya forodha nchini Kenya inawataka wabunge wawe wakilipa kodi za mishahara yao kikamilifu, ikiwalaumu kuwa wamekiuka katiba kwa kukosa kulipa. Idara hiyo pia inataka wabunge walipe kodi za tangu mwezi Agosti mwaka 2010 wakati katiba mpya ya nchi ilipozinduliwa. Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge wanaopokea mishahara mikubwa zaidi duniani, kila mmoja akipokea $ 9,300 kwa mwezi .

Tuesday, July 26, 2011

Umoja wa Mataifa kupeleka misaada Mogadishu

Mtoto amekaa anasubiri chakula

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP litaanza kupeleka chakula kwa ndege nchini Somalia siku ya Jumanne,mkuu wa WFP Josette Sheeran amesema wakati wa mazungumzo ya kujadili suala la ukame Afrika Mashariki.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa chakula kufikishwa huko tangu Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa kuna ukame katika maeneo mawili ya Somalia wiki iliopita.

Katika mkutano wa dharura mjini Roma, Italia waziri mambo ya nje wa Somalia Mohamed Ibrahim ameonya kuwa watu zaidi ya milioni 3.5 "huenda wakafariki dunia kutokana na njaa" katika nchi yake.
Makundi ya kiislamu, ambayo yanadhibiti sehemu kubwa ya Somalia, yamepiga marufuku shirika la WFP katika maeneo wanayoyasimamia.

Kundi la Al-Shabab, lenye uhusiano na kundi la al-Qaeda, limeshtumu mashirika waliyoyapiga marufuku kwa kujihusisha na siasa zaidi.

Bi Sheeran amesema msaada utapelekwa kwa ndege hadi katika mji mkuu, Mogadishu, serikali ya muda - inayosaidiwa na vikosi vya kuweka amani vya Muungano wa Afrika - inadhibiti sehemu tu ya mji mkuu.
Maelfu ya raia wa Somalia wamekuwa wakikimbia kutoka maeneo ya al-Shabab na kuelekea Mogadishu na nchi jirani za Kenya na Ethiopia kutafuta chakula.
mtoto aliyedhoofishwa na njaa

Bi Sheeran alihudhuria mkutano wa Roma - baada ya kutembelea Mogadishu na kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya.
"Tulichoona sisi watoto wanawasili wakiwa wamedhoofika kabisa wakiwa katika hali mbaya ya utapia mlo na wana nafasi ndogo - chini ya asilimia 40% - ya kuishi," alisema.

"Muhimu ni kuokoa maisha ya watu sasa. Si suala la kisiasa, hakuna nia nyingine isipokuwa kuja pamoja na kuokoa maisha."

Bwana Ibrahim alisema kuwa msaada wa chakula unahitajika zaidi katika maeneo yanayodhibitiwa na al-Shabab.

Kilo 1000 za samaki wa sumu zasambazwa Dar, Morogoro


Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Blandina Nyoni
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imetahadharisha kuhusu kusambazwa kwa zaidi ya kilo 1,000 za samaki wenye sumu sehemu mbalimbali za nchi na kuwataka wananchi washiriki msako iliouanzisha kuwatafuta.

Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa samaki hao ni sehemu ya kilo 124,992 zilizoingizwa nchini kutoka Japan.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tayari Serikali imeanza msako mkali kuwatafuta samaki hao, lakini ikaonyesha wasiwasi kwamba juhudi hizo huenda zisizae matunda kwa kuwa sehemu ya shehena hiyo imeshaingia sokoni.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa samaki hao tayari wameingizwa katika masoko ya Dar es Salaam na Morogoro.

“Wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Idara za Afya za Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro na Jeshi la Polisi, ili samaki waliobaki wapatikane,” alisema Nyoni.

Nyoni aliutahadharisha umma kuwa athari za sumu inayohofiwa kuwapo kwenye samaki hao ni ya mionzi ya nyuklia ambayo kimsingi hujitokeza taratibu katika mwili wa binadamu.“Samaki wenye uzito wa tani 1.319 wanafuatiliwa na kumbukumbu zinaonesha kuwa wamesambazwa kupitia soko la Feri, Dar es Salaam, Morogoro Mjini na Kilombero,”alisema

Katika kuhaha ili kuokoa maisha ya Watanzania, Nyoni anasema: “Wizara inaviomba vyombo vya habari, viiarifu na kuielimisha jamii juu ya kuwepo kwa samaki hao wanaochunguzwa kwa kuhisiwa kuwa na madhara.”

Pamoja na juhudi hizo, alifafanua “kazi hii ya ufuatiliaji na uchunguzi, inaendelea usiku na mchana hadi samaki hao watakapopatikana.”

Samaki hao wametoka wapi?
Nyoni alisema samaki hao aina ya “Mackerel” waliingizwa nchini na kampuni ya Alphakrust Ltd ya Dar es Salaam kutoka kampuni ya Kaneyama Corporation ya Chiba, Japan. “Samaki hao walisafirishwa kupitia Bandari ya Yokohama, Japan na kuingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Nyoni akidai kuwa taarifa zinaonyesha waliingizwa baada ya kukidhi masharti ya kisheria na taratibu zilizowekwa

“Kwa mujibu wa nyaraka za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mzigo huo ulifika Bandari ya Dar es Salaam tarehe 18 Julai, 2011,” alisema Nyoni na kuongeza:

“Wizara ilipata taarifa siku ya Jumamosi kwamba samaki hao wanahisiwa kuchafuliwa na mionzi ya nyuklia iliyotokea huko Japan, mwezi Machi, 2011.”

Nyoni alisema hadi kufikia juzi asubuhi, kiasi cha samaki wenye uzito wa tani 123.673, kati ya tani 124.992 walioingizwa nchini, walipatikana na kuzuiliwa katika maghala ya kampuni ya Alphakrust Ltd.Kufuatia taarifa hiyo, Nyoni alisema wizara yake  iliiagiza TFDA kuchukua hatua za haraka za kuzuia usambazaji wa samaki hao hadi uchunguzi utakapokamilika.

Alisema samaki hao walisindikwa tangu Desemba mwaka jana na muda wake wa mwisho kutumika ni Juni, 2012.Alisema samaki hao waliruhusiwa kuingizwa nchini kwa kibali cha TFDA namba TFDA11/F/IPER/0896, cha Julai 11 2011.


Wauzaji wanasemaje?
Baadhi ya wauzaji wa samaki wa Soko Kuu la Feri, walisema hatua ya Serikali ya kusitisha usambazaji wa samaki hao, imechelewa kwani tayari sehemu kubwa ya mzigo ilishauzwa.

“Hawa Kamongo ni Samaki adimu sana, Ijumaa tulipopata taarifa kuwa mzigo umeshuka, haraka tulifika kule Jet ambapo ndiyo kuna hilo ghala la Wajapani kwa ajili ya kununua,” alisema Juma Rashid kuongeza:

“Tulifika pale na watu wa vipimo wakaingia na DFP yao  (namba za ushajili za gari), wakafungua kontena wakapima halafu wakatuambia mzigo uko safi. Tukachukua kila mtu kwa kiasi alichotaka, mpaka Jumapili wanakuja kukamata mimi nilishamaliza mzigo wangu wa boksi tano wote.”

Kwa mujibu wa wachuzi hao, boksi moja la samaki hao ambalo lina uzito wa kilo15, linauzwa Sh51,000 kwa bei ya jumla.Juma Amiri (45), alisema shughuli ya kukamata samaki hao ikifanyika Jumapili, alikuwa amebaki na boksi moja tu.Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Samaki sokoni hapo, Abdala Mjanga, alisema hana taarifa rasmi za suala hilo, lakini alishuhudia kamata kamata hiyo iliyokuwa ikiendeshwa sokoni hapo.


Kauli ya TFDA

Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Hiiti Silo alisema taarifa hiyo ya wizara ni msimamo wa Serikali na idara zake zote ikiwamo TFDA

"...Lakini TFDA tunafanya uchunguzi kwa kasi ili tuimalize kazi hiyo mapema kuokoa maisha ya watu," alisema.

Kisa na mkasa na Salim Kikeke

Kumpata mke balaa

Bwana mmoja nchini Marekani hatimaye amefunga ndoa kwa mara ya kwanza, baada ya kusaka mchumba kwa zaidi ya miaka sabini.

Bwana huyo Gilbert Harrick mwenye umri wa miaka tisini na tisa sasa ambaye alipigana katika vita vya pili vya dunia amesema hakuwahi kukutana na msichana aliyempenda kwa miaka yote hiyo.
Bwana Gilbert amefunga ndoa na Bi Virginia Hartman mwenye umri wa miaka themanini na sita.
Gazeti la Rochester Cronicle limesema wawili hao kwa sasa wanaishi katika nyumba ya kutunza wazee, mjini New York.

"Tulitaka tuishi pamoja katika chumba kimoja, lakini walitukatalia hadi tufunge ndoa" amesema bwana Gilbert, "Kwa hiyo nikamuomba tuoane na yeye akakubali" ameongeza mzee huyo.
Kabla ya kuoana na kuishi katika chumba kimoja, wapenzi hao walikuwa wakiandikiana barua za mapenzi kila mara.

"Ni wazimu, lakini ndio raha yenyewe" amesema Bi Virginia, ambaye ana watoto watano katika ndoa yake ya awali.

Chupi si lazima

Mamlaka za magereza katika jimbo la Florida zimeamua kubana matumizi kwa kuacha kutoa bure nguo za ndani kwa wafungwa.

Badala yake, mkuu wa gereza la Polk amesema kuanzia sasa wafungwa watalazimika kununua chupi ambazo awali zilikuwa zikitolewa bure.
"Hakuna sheria inayotulazimisha kuwapa wafungwa vazi hilo" amesema Liwali Grad Judd, ambaye pia ndio mkuu wa gereza hilo.

Gazeti la Telegraph limesema vivazi hivyo vya ndani vitawagharimu wafungwa hao dola mbili na nusu hadi dola nne na nusu kutegemea aina na mtindo.

Hata hivyo utawala wa gereza umesema si lazima wazinunue, wasiotaka kuvaa, wataachiwa wafanye hivyo.
Chupi hizi pia zitapatikana katika rangi moja tu, nyeupe.
"Wanaotaka watanunua, wasiotaka, basi waache upepo uingilie mguu mmoja na utokee mguu mwingine wa suruali" amesema Mkuu wa gereza.

Pombe ikizidi...

Walevi wawili nchini Marekani waliingia matatani baada ya kuingia ndani ya karandinga la polisi ili wajipige picha kama vile wamekamatwa.

Wawili hao Ryan Letchford na Jeffrey Olsen waliingia katika gari la polisi lililokuwa limeegeshwa barabarani, na kuanza kupeana zamu kujipiga picha.

Hata hivyo shughuli hiyo iliingia doa wakati vitasa vya mlango wa gari vilipojifunga, wakati wawili hao wakiwa bado ndani ya karandinga.

Rafiki wa tatu wa jamaa hao alikuja kujaribu kuwatoa, lakini akashindwa na kulazimika kupiga simu polisi kuomba msaada.

Constable wa polisi Mike Connor ameliambia gazeti la kila siku la Philadelphia kuwa alifika na kuwafungulia walevi hao.
"Walikuwa wakiona aibu sana" amesema polisi huyo.
Hata hivyo wawili hao hawakuwa huru kwa muda mrefu, kwani walikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kutaka kuiba gari la polisi, ukorofi wa kihalifu na ulevi hadharani.

Makahaba kuchumbiwa

Kituo kimoja cha televisheni nchini zambia kimeanzisha kipindi kinachosaidia wasichana waliokuwa makahaba zamani, kutafuta wachumba.

Wasichana hao wapatao kumi na wanane mbali na kusaidiwa kutafutiwa wachumba, watapatiwa zawadi ya dola elfu tisa kila mmoja na pia kulipiwa gharama zote za harusi.

Kituo hicho kiitwacho Muvi TV, kimesema kinataka kuwapa wasichana hao nafasi ya kuanza maisha mapya.
Kipindi hicho kinaitwa "tayari kwa ndoa".

Mhubiri mmoja Mchungaji Jeff Musonda ametoa baraka zake kwa makahaba hao wa zamani.
Kituo hicho cha TV kimesema kiliwatafuta wasichana hao kutoka mitaa mbalimbali ya nchi hiyo.
Baadhi ya washiriki wamesema walikuwa wakiuza miili yao ili kuwahudumia watoto wao.

Hata hivyo watu wamepokea kwa hisia tofauti kipindi hicho, wengine wakisema mtu akishakuwa kahaba ni vigumu kubadilika kwa muda mfupi, huku wengine wakisema, hakuna haja ya kuwahukumu kwa mambo waliyoyafanya siku za nyuma.

Kulipa kulala jela

Gereza moja nchini marekani mwishoni mwa wiki liliwatoza fedha watu kwa kulala ndani ya gereza.
Hiyo ilikuwa kwa watu waliokuwa wakitaka kuhisi maisha ya gerezani.
Gereza hilo Cole County, liliwatoza watu dola thelathini kwa usiku mmoja kwa watu waliotaka kuonja maisha ya jela siku ya Ijumaa na Jumamosi.

Maafisa wamesema nafasi hiyo imetolewa kwa wananchi ili kulijaribu gereza hilo jipya kabla halijaanza kazi rasmi ya kuwafungia wahalifu.

Shirika la habari la reuters limesema watu wapatao mia moja na sabini walifurika katika gereza hilo wakitaka kuona usingizi wa jela ukoje.

Baadhi ya watu waliofika kulala gerezani ni pamoja na mawakili na wanandoa waliokuwa wakiadhimisha miaka yao ya ndoa.

Watu hao walipitia misingi ya kuswekwa gerezani, ikiwa ni pamoja na kukaguliwa, kunyanganywa simu za mkononi, mikanda pamoja na vito walivyokuwa wamevaa.

Pia walipigwa picha kama wafungwa."Ingawa hakikuwa kifongo cha ukweli, lakini nilihisi kukosa uhuru" amesema Bob watson, mmoja wa watu waliolipa kulala jela.

Kila chumba kidogo ndani ya gereza hilo kina kitanda cha chuma na godoro jembamba, huku balbu yenye mwanga mdogo ikiwaka usiku kucha.

Hata hivyo kuna TV yenye channel moja ambayo haisikiki kutokana na kelele ndani ya gereza.
Na kwa Taarifa yako... Konokono anaweza kupita kwenye ncha ya wembe bila kujikata.

LIPUMBA, SLAA WATAMBA KULINYAKUA JIMBO LA IGUNGA CCM BADO KIMYA


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga Mr Rostam Azizi
SIKU chache baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kutangaza kuwa kiti cha Jimbo la Igunga liko wazi kufuatia kujiuzulu kwa Rostam Aziz, vyama vya siasa vimeanza mbio za kuwania jimbo hilo.Rostam alijiuzulu ubunge wa Igunga Julai 13 mwaka huu, kutokana na kile alichokiita siasa uchwara ndani ya CCM, na wiki iliyopita Spika Makinda, alitangaza kuindikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuieleza kuwa kiti hicho cha ubunge, sasa kiko wazi.

Hatua ya Spika Makinda kuijulisha Nec kuhusu kujiuzulu kwa Rostam, ni mwanzo wa mchakato wa kukijaza kiti hicho cha ubunge kilichokuwa kikikaliwa na kada huyo wa CCM kwa miaka 18 iliyopita. Baada ya taarifa hiyo ya Spika Makinda, Nec sasa itatakiwa kutangaza uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo ndani ya siku 90 kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Lakini katika kile kinachoonekana harakati za kukitwaa kiti hicho, vyama vya CUF, Chadema, NCCR Mageuzi, TLP, UDP,  CCM na SAU, jana vililithibitishia gazeti hili kwamba vitasimamisha wagombea wao wa ubunge katika uchaguzi mdogo utakaotangazwa na Nec hivi karibuni.

CUF yataja wagombea wao
CUF kimetoa onyo kwa vyama vya upinzani kuwa ni bora vingeacha kugombea jimbo hilo kwa kuwa tayari chenyewe kimelitwaa.

Katika kuonyesha majigambo, chama hicho kilisema kina nafasi kubwa ya kuchukua ushindi katika jimbo hilo kutokana na mgombea wao, Leopard Mahana, kuombwa na wananchi kugombea tena ubunge baada ya kubwagwa na Rostam kwenye uchaguzi wa mwaka jana. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, CUF haitafanya kosa la kuliacha jimbo hilo tena.

Alisema hayo muda mfupi baada ya kutoa rambirambi kwa Ubalozi wa Norway nchini kutokana tukio la vifo vya watu 93 vilivyotokana na milipuko ya mabomu nchini humo. “Vyama vya upinzani wasijidanganye kusimamisha mbunge katika jimbo hilo kutokana na chama chetu kuwa na nafasi kubwa ya kushinda kutokana na wananchi wa eneo hilo kumchagua kijana wetu kugombea jimbo hilo,” alitamba Lipumba na kuongeza:

“Katika uchaguzi wa mwaka jana chama chetu ndio pekee kilichosimamisha mgombea kati ya vyama vya upinzani kushindana na Rostam, hivyo vyama vya upinzani kwa sasa vinapaswa kuachia nafasi kama vilivyofanya kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana,”alisema Lipumba.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, Jimbo la Igunga lillikuwa na wagombea wawili ambao ni Rostam  kupitia CCM pamoja na   Mahana kupitia CUF.

Chadema waja na Opesheni Chukua Igunga
Kwa upande wake,Chadema kimesema kitaweka mipango yake hadharani hivi karibuni ya namna kilivyojipanga kuingia kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.

Katibu Mkuu wa Chadema hicho, Dk Willibrod Slaa alisema jana kuwa chama kimedhamiria kuweka mgombea katika jimbo hilo na hata sasa vijana wako jimboni.“Mikakati ipo,na tutaiweka hadharani baadaye kwa sasa ni mapema mno, lakini  vijana wetu wapo kule,”alisema Dk Slaa.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, John Heche aliliambia Mwananchi juzi kuwa wanakwenda Igunga kuzindua Opresheni ya Chukua Igunga.“Kama tulivyo na utaratibu wa kuwa na operesheni za kujenga chama ambazo mara nyingi zimejulikana kwa jina la Operesheni Sangara, safari hii katika moja ya mikakati ya kulichukua Jimbo la Igunga, Chadema imeandaa Operesheni Chukua Igunga,”alisema Heche.

Oparesheni hiyo ya siku ilianza juzi Jumapili na inaongozwa na vijana ambapo Mwenyekiti huyo alisema kazi ya kuchukua jimbo imekabidhiwa kwao.

NCCR-Mageuzi yapeleka ujumbe Igunga
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema chama hicho kitasimamisha mgombea katika Jimbo la Igunga na kusisitiza kuwa kwasasa kimetuma timu ya watu sita kwa ajili ya kutizama hali ya kisiasa ilivyo.

“Timu tuliyoituma itakapolejesha majibu ndio tutaweza kutangaza watakaochuana kuwania nafasi ya kugombea katika jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR,” alisema Ruhuza,

Hata hivyo, Ruhuza alisema kuna dalili za wazi kwamba  idadi kubwa ya vyama vya upinzani vitasimamishwa wagombea katika jimbo hilo, huku akionyesha wasiwasi hali hiyo inaweza kuipa CCM mwanya wa kushinda.

“Kuna dalili za wazi kila chama cha upinzani kitataka kuweka mgombea katika jimbo la Igunga. Ni vyema vyama vya upinzani kukubaliana na kusimamisha mgombea anayekubalika ili iwe rahisi kushinda, lakini waking’ang’ania wataishia kugawana kura tu,” alisema Ruhuza.

Sau nao wamo
Mwenyekiti wa Sau, Paul Kyara alithibitisha kuwa chama hicho pia kitaweka mgombea katika jimbo hilo huku akisisitiza kuwa katika uchaguzi huo mdogo jimbo hilo litachukuliwa na wapinzani.

“Tumetuma timu ya wajumbe watatu kwa ajili ya kutizama hali ya kisiasa wilayani Igunga, timu hiyo itarudi wiki hii na majibu kamili, pamoja na hayo mchakato wa kupata mgombea tayari umeshaanza kufanyika,” alisema Kyara.

UDP yavuta pumzi

Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo alisita kuzungumzia uchaguzi huo huku akifafanua kwamba ni mapema mno.“Ndio kwanza imetangazwa kuwa jimbo liko wazi…, sasa ndio kila mtu aseme kuwa atasimamisha mgombea, ni mapema sana kuzungumzia suala hilo,” alisema Cheyo kwa ufupi.


CCM bado inavuta pumzi

Kwa upande wake, CCM kimesema bado hakijakaa kujadili namna kitakavyoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga.Akizungumza jana Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CCM bado haijakaa vikao kujadili suala hilo.

“Chama chetu hufanya uamuzi wake kwa kupitia katika vikao, hadi sasa sisi hatujakutana kujadili suala hilo, ”alisema Nnauye.Jimbo la Igunga limeachwa wazi kufuatia aliyekuwa Rostam kujuuzulu nyazifa zake zote ndani ya CCM kwa kile kilichodaiwa ni kujivua gamba, ingawa mwenyewe alikataa.


Nec yapokea barua ya Spika
Kwa upande wa  NEC, imekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa Rostam baada ya Spika Makinda kuiandikia.Kaimu Mkurugenzi wa Tume hiyo, Sisti  Cariah, alisema barua hiyo imewasilishwa jana kutoka bungeni.“Ni kweli leo (jana) tumepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhusu kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga, Rostam Aziz,” alisema Cariah
Kwa mujibu wa Cariah, uteuzi unafanyika kuanzia  siku ya 20 hadi 50 tangu Spika wa Bunge kupokea barua na kuiarifu Nec.

Monday, July 25, 2011

Hereni, rasta ruksa mahakamani Kenya



WANASHERIA na mawakili Kenya, wanaume kwa wanawake, kuanzia sasa wanaruhusiwa kuingia katika Mahakama ya Rufani nchini humo wakiwa wamevaa hereni pamoja na kufuga nywele za rasta bila kipingamizi.

Uamuzi huo, ambao umetangazwa na Jaji Mkuu, Dk. Willy Mutunga, umefikiwa kwa pamoja katika kikao cha pamoja cha majaji kilichoketi kuangalia iwapo mavazi na mwonekano huo unakiuka sheria za nchi hiyo au la.

Majaji hao wa Mahakama ya Rufani pia hawatakuwa wakivaa majoho pamoja na kofia maalum walizokuwa wakivaa siku za nyuma na sasa wananchi wa Kenya watapewa fursa ya kuamua ni nguo za aina gani zitakazowafaa majaji wa mahakama hiyo.

Dk. Mutunga, ambaye ameanza kazi kwa staili mpya ya kuuzika utamaduni uliozoeleka katika viunga vya Idara ya Mahakama tangu enzi za mkoloni, aliamua kutangaza uamuzi huo kupitia mtandao wa kijamii wa facebook, mtandao ambao pia haujawahi kutumiwa na watangulizi wake tangu uhuru.
Jaji Mkuu huyo mpya alikuwa akijibu maswali ya mawakili vijana waliomuuliza iwapo wanaruhusiwa kuvaa hereni wakiwa mahakamani pamoja na nguo ambazo wakili anatakiwa kuzivaa anaposimamia kesi mahakamani.

Jaji Mutunga pia amekuwa akivaa hereni katika sikio lake la kushoto, suala ambalo limesababisha mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi wa Kenya, huku wahafidhina wakipinga kwa nguvu zao zote, wakisema hizo ni dalili za uhuni na kwamba Jaji Mkuu hatakiwi kuvaa kitu kama hicho.

Hata hivyo, wananchi wengi, ambao wamekuwa wakiichukia Idara ya Mahakama kutokana na kuzingirwa na rushwa, wanasema ni bora kuwa na Jaji Mkuu mvaa hereni anayesimamia haki, kuliko majaji wakuu wahafidhina waliopita, ambao ndiyo wameiharibu idara hiyo kutoakana na kuabudu rushwa.

“Ninachoweza kusema ni kwamba majaji wa Mahakama ya Rufani tumekubaliana kwamba hatuna matatizo na mtu yeyote atakayesimama mbele ya mahakama akiwa amevaa hereni. Msimamo wetu ni kwamba maofisa wa Mahakama, wawe mawakili au majaji, wanaweza kuvaa nguo za heshima, bila kujali kama wamesuka rasta au wamevaa hereni, kwa kuwa hilo halizuii utawala wa sheria,” anasema Dk. Mutunga katika taarifa yake,” anasema Jaji Mutunga na kuongeza:
“Sisi majaji wa mahakama hii hatutavaa majoho na kofia tulizorithi kutoka kwa wakoloni, tutazishauri mahakama nyingine za chini kuchagua mavazi mazuri zaidi na tunaratajia wananchi wa Kenya watashirikishwa katika hili.”

Sunday, July 24, 2011

Mwanamke aolewa na wanaume wawili


MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, zilifanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji ya iitwayo kayoga.

Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi. Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.

“Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sauti pale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anaweza kuongeza mwanamume mwingine,” anasema mmoja wa majirani hao.

Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa na amani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.

Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mume mkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliweka pingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’ wa mtoto huyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sita iliyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye baba mzazi wa mtoto.

“Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandalizi yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huo ilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia pale Padri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.

“Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado bali wake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena na majibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana,” alisema Katekista Abel.

Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wake ni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapo na baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidia mkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogo wake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.

Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.

"Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugia mpangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa hao yanawahusu nini watu hao?” alihoji.

“Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumba nitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?” alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwamba wataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akina mama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaume wawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufunga ndoa na mume mmoja.

Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili na kuwa na mamlaka juu yao.

Ndugu wa Arcado wao wanalaani kitendo cha ndugu yao kuolewa na mama huyo, wakidai kuwa walishamshauri na kumuahidi kuwa endapo ataachana na mama huyo watamwozesha mwanamke mwingine, lakini yeye Arcado, amedai kuwa yuko tayari kufa, lakini si kuachana na mama huyo, kwani ndiye ubavu wake wa maisha.

“Sasa tumebaki tunamwangalia tu huyu ndugu yetu Arcado, tumemshauri, lakini mkaidi, hatusikilizi. Basi nasi hatuna la kufanya zaidi ya kumwangalia,“ alisema mmoja wa ndugu wa karibu wa Arcado. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Florence Katobasho, alikiri kuwa mwanamke huyo anaishi kinyumba na wanaume wawili na wanaishi kwa amani kwani hajawahi kufikishiwa malalamiko yoyote kuhusu wanandoa hao.

“Ni ukweli usiopingika, kwamba Mama Kaela anaishi na wanaume hao wawili … lakini kwa kuwa sijafikishiwa malalamiko yoyote kuhusu maisha ya wanandoa hao, mimi kama kiongozi hapa sina la kufanya na siwezi kuwafukuza, kwa kweli wanaishi kwa amani, mengine ni yao,” alisema Mwenyekiti wa Kijiji.

Saturday, July 23, 2011

Jairo awekwa benchi


SERIKALI imemsimamisha kazi Katibu Mkuu  wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo.  Hatua hiyo inalenga kutoa nafasi ya   ufanyika uchunguzi dhidi ya tuhuma  zinazomkabili zilizoibuliwa bungeni. Jairo anadaiwa kuziandikia barua idara na  taasisi zilizo chini ya wizara ili kila moja itoe  sh. milioni 50 kwa ajili ya kufanikisha  uwasilishaji wa makadirio ya matumizi ya  wizara kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012. Anadaiwa pia kuwalipa posho za safari  watumishi wa wizara waliofuatana na  viongozi wa juu licha ya kuwa walishalipwa  na idara na taasisi zao. 
Wabunge Beatrice Shellukindo (Kilindi-CCM)  na Christopher Ole Sendeka (Simanjiro  -CCM), ndio walioibua tuhuma hizo  walipojadili makadirio ya wizara, kabla ya  serikali kuyaondoa bungeni.  Serikali iliyaondoa makadirio hayo bungeni  kutokana na hoja za wabunge kuwa  haijajipanga kukabiliana na tatizo la umeme.  Bunge limetoa wiki tatu kwa serikali  kujipanga na kuyarejesha. 
Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo,  akizungumza na waandishi wa habari jana  mjini hapa, alisema amemwagiza Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG), kufanya uchunguzi wa kina, ambao  anatakiwa kuukamilisha ndani ya siku 10  kuanzia alipopewa kazi hiyo. "Wakati uchunguzi ukiendelea, Jairo   amesimamishwa kazi.
Hatua nyingine  zitafanyika baadaye kulingana na matokeo  ya uchunguzi," alisema. Luhanjo alisema anatarajia kufanya uteuzi  wa mtu atakayekaimu nafasi hiyo katika  kipindi kisichozidi siku tatu. Luhanjo alisema baada ya uchunguzi  kukamilika na endapo tuhuma dhidi ya Jairo  zitathibitika, uamuzi dhidi yake utachukuliwa  na rais kwa kuwa ndiye mamlaka yake ya  uteuzi.

Alisema amechukua uamuzi huo dhidi ya  Jairo kwa kuwa sheria ya  utumishi wa  umma inampa uwezo wa kushughulikia  nidhamu serikalini. "Kwa sababu suala hili ni zito nimeamua  aende likizo, lakini baada ya uchunguzi na  nikipata matokeo ya uchunguzi huo nitampa  taarifa itakayoambatana na hati ya  mashitaka," alisema.
Akizungumzia utaratibu alisema baada ya  matokeo ya uchunguzi kupatikana, Jairo  atapatiwa taarifa itakayoambatana na hati  ya mashitaka, itakayoeleza kwa kifupi kosa  alilotenda na namna alivyolitenda ili atoe  majibu.  Luhanjo alisema katika kipindi hicho,  atakuwa amesimamishwa kazi na kuanza  kulipwa nusu mshahara.  Kwa mujibu wa Luhanjo, katika majibu,  anaweza kukubali au kukana tuhuma dhidi  yake, ambapo mamlaka ya nidhamu  itaendelea kutoa adhabu kulingana na uzito  na kwamba, kwa kuwa Jairo ni mteule wa  rais, ndiye atakayeamua hatima dhidi yake.

Awali, kabla Luhanjo hajatangaza uamuzi  huo, wabunge waliibua hoja hiyo wakitaka  kufahamu hatua zilizochukuliwa dhidi ya  Jairo. Hoja hiyo iliibuliwa wakati wa kipindi cha   maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu  bungeni, ambapo Rashid Ali Abdalah  (Tumbe -CUF), alihoji hatua ya Waziri Mkuu  Mizengo Pinda, kudai hana mamlaka ya  kumwadhibu Jairo. Katika swali la msingi Rashid alitaka  kufahamu ni kwa nini waziri mkuu alitoa  kauli kuwa hawezi kumwajibisha Jairo hadi  Rais Jakaya Kikwete atakaporudi wakati  makamu wake na yeye wapo.
Akiwasilisha hoja ya kuondoa bungeni  makadirio ya Wizara ya Nishati na Madini,  Waziri Mkuu Pinda alisema Rais Kikwete  ndiye atakayeamua kuhusu hatima ya Jairo  kwa kuwa ndiye aliyemteua. Waziri Mkuu Pinda akijibu swali la Rashid,  alisema makamu wa rais au waziri mkuu  hawana mamlaka kikatiba ya kumwajibisha  Jairo, kwani mwenye uamuzi wa mwisho ni  rais wa nchi.
"Naomba niwaambie waheshimiwa wabunge  kwamba, si kila jambo linalotokea wakati  rais anapokuwa hayupo au yupo nje ya nchi  linaweza kutolewa uamuzi na makamu wa  rais au waziri mkuu," alisema. Alisema ni kweli kwa mujibu wa Katiba ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kifungu  cha 47 (1) (c), rais anapokuwa nje ya nchi  makamu wake ndiye anayeshika madaraka  ya kuongoza taifa. Pinda alisema kuna wakati hata waziri mkuu  hupewa nafasi hiyo, kama na makamu wa  rais hayupo, lakini wote wawili wana ukomo  katika utekelezaji wa majukumu yao,  ikiwemo kuamua mambo ambayo ni rais  pekee anayepasa kuyaamua.

Watu 91 wameuawa Norway; mwananchi Sven Olsen azungumza na Ayisha Yahya

Polisi nchini Norway sasa wanasema kuwa mtu aliyekuwa na bunduki aliyefyatua risasi katika mkusanyiko wa vijana katika kisiwa chenye kambi ya vijana nje ya mji mkuu, Oslo, Ijumaa jioni, alisababisha vifo vya watu 84. Awali mlipuko wa bomu ulikuwa umesababisha vifo vya watu saba.
Majeruhi walioogeleea kutoka kisiwa cha Utoeya, kinachonekana kwa mbali

Polisi wamemfungulia mashtaka raia mmoja wa Norway, mwenye umri wa miaka 32, kwa kutekeleza mashambulio yote mawili.

Mtu huyo aliyekuwa amevaa mavazi ya afisa wa polisi wakati wa kufanya mashambulio hayo, alikamatwa katika kisiwa kidogo cha Utoeya, baada ya kufyatua risasi ovyo kwa kipindi cha saa nzima. Waziri mkuu Jens Stoltenberg amesema watu wengi bado wanaendelea kuwatafuta watoto wao kufuatia mashambulio hayo.
Waziri mkuu alisema hayo kufuatia kuwatembelea walioathiriwa na vile vile jamaa zao.

Kiongozi huyo alikuwa ameandamana na Mfalme wa Norway, Harald na Malkia Sonja, na vile vile mwanamfalme Haakon, walipoutembelea mji wa Sundvollen, karibu na kisiwa cha Utoeya.
Mtu aliyekamatwa amehusishwa na makundi yenye itikadi za siasa kali.

Anders Behring Breivik

Anders katika Facebook anasema yeye ni Mkristo. Jina lake ni Anders Behring Breivik.
Polisi usiku mzima wamekuwa wakiikagua nyumba anayoishi mjini Oslo, na bado wanaendelea kumhoji.

Mwandishi wa BBC Richard Galpin, anasema Norway imekuwa na matatizo ya kisasa yanayotokana na makundi yanayounga mkono siasa za ki-Nazi, lakini raia wengi wamekuwa wakiamini kwamba makundi mengi ya aina hiyo yamekomeshwa.

Polisi wanaendelea kuchunguza iwapo alitekeleza mashambulio hayo kama mtu binafsi, au alisaidiwa na makundi fulani.

Amuua mkewe kwa kupunjwa kitoweo

MKAZI wa Isalalo wilayani Mbozi mkoani Mbeya, Amina Tulianje (18) ameuawa na mumewe kwa kukatwa shoka kichwani.

Sababu ya kifo hicho ndiyo inayoonekana kushangaza, kwani inadaiwa kuwa mumewe Nemes Muyombe, alifikia hatua hiyo, baada ya kukasirishwa na kitendo cha kumpunja kitoweo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Advocate Nyombi, jana alithibitisha kutokea tukio hilo akisisitiza kuwa chanzo cha ugomvi ni kitoweo.

Ilielezwa kwamba, katika tukio hilo, mume alitumia shoka kumkata mkewe na kukimbia huku akiliacha kichwani kwa mkewe.

Kamanda Nyombi alieleza kuwa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi iliyoko Vwawa wakati uchunguzi na juhudi za kumsaka mtuhumiwa vikiendelea.

Katika tukio lingine, Kamanda Nyombi alisema mkazi wa Kijiji cha Igogwe, Rungwe, Alex Hezron (22) amekutwa amekufa huku amekatwa koromeo na kutobolewa macho na kutupwa kwenye Mto Igogwe na watu wasiofahamika.

Thursday, July 21, 2011

Kikwete atoa ufafanuzi wa umeme


Katika mahojiano maalum na Rais Kikwete, mwandishi wa BBC, Omar Mutasa, kwanza alitaka kujua, pamoja na kutafuta wawekezaji ambao kimsingi watahitaji nishati ya umeme ya uhakika, kwa nini tatizo la umeme halijapatiwa ufumbuzi.

"Serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe", alisema Rais Kikwete.

Habari zaidi
http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2011...

Kikwete amweka kiporo Jairo

RAIS Jakaya Kikwete amemweka kiporo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo akisema ataona cha kufanya baada ya ziara yake ya Afrika Kusini.

Akizungumza jana nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu uvumi wa kujiuzulu kwa Jairo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema hakuwa amepata taarifa rasmi ya kujiuzulu kwake.

Lakini alisema kilichopo ni kuwa alimjulisha Rais Kikwete mambo yaliyotokea Jumatatu bungeni kuhusu mjadala wa Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo baadhi ya wabunge walitaka Jairo aondolewe.

“Amenijibu kuwa ‘sawa, nisubiri nitakaporudi Afrika Kusini tuone tunafanyaje’,” alisema Pinda akimnukuu Rais Kikwete.

Jumatatu wakati wa mjadala wa makadirio hayo, wabunge waliibua kashfa wakituhumu wizara hiyo kuchangisha Sh bilioni moja kutoka idara na taasisi zake kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa makadirio hayo.

Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), ndiye aliyeibua sakata hilo wakati akichangia hotuba ya Makadirio hayo kabla hayajaondolewa bungeni.

Katika kuthibitisha kashfa hiyo, Shelukindo aliwasilisha barua bungeni iliyoandikwa na Jairo ikizitaka idara na taasisi zote za wizara hiyo, kila moja ichangie Sh milioni 50 kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya uwasilishaji wa hotuba ya bajeti.

Mbunge huyo wa Kilindi pamoja na wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM) kwa nyakati tofauti, walihoji bungeni mantiki ya fedha hizo, takribani Sh bilioni moja na wakataka wizara ifafanue zimekusanywa kwa ajili gani.

Pinda katika hoja yake bungeni, alikiri kwamba Jairo aliudhi na kutibua wabunge na akaahidi kuwasilisha suala hilo kwa Rais Kikwete aliyemteua ili achukuliwe hatua.

“Lazima nikiri hata mimi nilishtuka sana tena si kidogo, kwani suala hili limegubikwa na maswali mengi hakuna namna ya kutetea,” alisema Pinda siku hiyo.

Wednesday, July 20, 2011

Ngeleja, Malima watakiwa kujiuzulu

MBUNGE wa Arusha, Godbless Lema (CHADEMA) jana aliomba Mwongozo wa Spika akitaka Waziri na Naibu Waziri wa Nishati na Madini wawajibike katika sakata la wizara hiyo kuchangisha Sh bilioni moja kutoka idara na taasisi zake kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa Bajeti.

Lema aliomba Mwongozo wa Spika kwa kutumia kanuni ya 68(7) kwa kusema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, David Jairo, asingeweza kuwa na ujasiri wa kuchangisha fedha hizo bila mawaziri husika kuwa na taarifa.

Mbunge huyo ambaye alitaja moja kwa moja bungeni kwamba Katibu Mkuu huyo alijihusisha katika vitendo vya rushwa kutokana na fedha hizo, alihoji kama kweli ndiye anapaswa kuwajibika pekee na si pamoja na Waziri mwenye dhamana, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima.

Spika Anne Makinda hakukubaliana na hoja ya Lema kutokana na kile alichosema kwamba mjadala wa suala hilo umewekwa pembeni kutokana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuliomba Bunge juzi kwamba anakwenda kulifanyia kazi. “Naomba waendelee kufanya inavyostahili kiutawala,” alisema Makinda.

Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), ndiye aliyeibua hilo sakata wakati akichangia hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kabla haijaondolewa bungeni juzi.

Shelukindo aliwasilisha barua bungeni iliyoandikwa na Katibu Mkuu Jairo ikizitaka idara na taasisi zote za wizara hiyo kila moja ichangie Sh milioni 50 kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya uwasilishaji wa hotuba ya bajeti.

Mbunge huyo wa Kilindi pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM) kwa nyakati tofauti, walihoji bungeni mantiki ya fedha hizo takribani Sh bilioni moja na wakataka wizara ifafanue zimekusanywa kwa ajili gani.

Pinda katika hoja yake bungeni alikiri kwamba Jairo kawaudhi na kuwatibua wabunge na akaahidi kuwasilisha suala hilo kwa Rais Jakaya Kikwete aliyemteua ili achukuliwe hatua.

“Lazima nikiri hata mimi nilishtuka kweli sana tena si kidogo, kwani suala hili limegubikwa na maswali mengi hakuna namna ya kutetea,” alisema Pinda.

Wakati huo huo, baadhi ya wadau wa umeme nchini wamewatupia lawama watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwa ndiyo chanzo cha matatizo ya umeme kutokana na kutotekeleza kivitendo, mipango ambayo ingesaidia kuondokana na tatizo hilo.

Watendaji hao pia wameshutumiwa kuwa mabingwa wa kupiga maneno na kufanya ujanjaujanja katika kushughulikia tatizo la umeme.

Pia wameshutumiwa kuwa wanapuuzia mchango wa sekta binafsi wakati ndio watumiaji wakubwa wa umeme.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Haji Semboja, alisema kinachokosekana kwa watendaji hao ni akili na ubunifu, badala yake alisema wanatanguliza ujanjaujanja na ni werevu wa kupiga maneno.

“Tatizo letu tunakwepa kuwatumia wataalamu katika masuala haya; badala yake tunawatanguliza wachekeshaji na wapiga porojo … katika hali ya namna hii, kamwe hatuwezi kuondokana na tatizo la umeme,” alisema Dk Semboja. Alisema kwa sasa suala si fedha bali ni akili ya kubuni mikakati ya kuondokana na tatizo hilo kama walivyofanya Kenya na Ethiopia.

“Kama suala ni fedha, Tanesco wanahitaji bajeti ya miaka 20 ijayo, kumaliza tatizo la umeme, lakini sasa tunahitaji ubunifu na akili.” Alitoa mfano kuwa ndani ya Tanesco na Serikali kuna wataalamu ambao wameshirikishwa katika mipango inayohusisha ushiriki wa jumuiya za kanda kama ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) na ile ya Bonde la Mto Nile, lakini utekelezaji wake kwa Tanzania hautiliwi maanani.

“Mimi nimekuwa nashiriki miradi yote hiyo, lakini ushiriki wa Serikali yetu ni mbovu, ndiyo maana nasema tuna watu wenye uwezo, watafutwe tuachane na hawa wachekeshaji na wapiga maneno,” alisema Dk Semboja. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Felix Mosha, alisema Tanzania itaondokana na tatizo la umeme iwapo wataishirikisha sekta binafsi katika mipango yake.

Mosha alisema asilimia 85 ya watumiaji wakubwa wa umeme wa Tanesco ni wenye viwanda, hivyo alishauri Serikali kuwa inapaswa kuwahusisha katika mipango yote kuanzia ya muda mfupi, kati na mrefu ili nao watoe maoni yao ya namna ya kuondokana na tatizo hili. Alisema matatizo haya yanayoendelea ya mgawo wa umeme ni matokeo ya Serikali kuidharau sekta binafsi hasa kwenye suala la umeme.

“Hata pale jambo linalogusa sekta binafsi, Serikali haitaki majadiliano nasi na badala yake wamekuwa wanajadiliana wenyewe na kuamua mambo yao.” Mosha alisema: “Naamini kukwama kwa bajeti hii sasa itatoa fursa ya kutushirikisha, na sisi tuko tayari, kwani tuna mapendekezo yetu ambayo tutawapatia watu wa Serikali.”

Alisema, kama Serikali itaendelea kuwapuuza, ustawi wa viwanda nchini uko katika hatihati, kwani vingi vinategemea jenereta ambazo zilikuwa maalumu kutatua tatizo la muda mfupi na si ilivyo sasa kutokana na gharama zake kuwa juu kuliko umeme.

Mwenyekiti huyo pia alisema katika hali ya sasa, viwanda vya Tanzania havina ubavu wa kushindana na vya nchi zingine za nchi wanachama wa EAC kutokana na kutokuwa na nishati ya uhakika.

Alionya pia kuwa watu wengi watapoteza ajira, kwani viwanda vingi vinafanya kazi kwa siku mbili kwa wiki jambo ambalo linamwia vigumu mwajiri.