KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeiagiza Serikali kutafuta njia ya kushusha bei ya mafuta ya taa na kuhakikisha mafuta yote yanayoingia nchini yana ubora unaotakiwa. Pia Kamati hiyo imeitaka Serikali kutafuta suluhu ya uchakachuaji wa mafuta, kwani uwezo wa kufanya hivyo inao.
Akizungumza na waandishi wa habari , Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyokutana juzi pamoja na kujadili mambo mbalimbali ya chama, haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa. Alisema nishati hiyo ndiyo inayotumiwa na wananchi wengi wa kipato cha chini nchini, na kwamba kupandishwa bei kwa kisingizio cha kupunguza uchakachuaji, si sahihi.
Aliongeza kwamba, kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta hayo Serikali inapaswa kukaa na kutafuta njia zitakazoshusha bei hiyo na kuvitaka vyombo husika kuhakikisha ubora wa mafuta yanayoingia nchini.
“Tunaitaka Serikali itafute njia ya kushusha bei ya matufa ya taa na pia kutafuta suluhisho la uchakachuaji na si kupandisha bei,“ alisema Nape.
Aidha, alisema suala la umeme ni nyeti na kwa hali ilivyo sasa si nzuri na kuishauri Serikali kuja na njia za kunusuru hali hiyo.
“Athari ya kukosekana kwa umeme nchini ni kubwa, hivyo Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, itumie muda iliopewa kurekebisha bajeti yao vizuri na kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hili na pia kuja na majibu ya suluhu ya tatizo hili,” alisema Nape
Aliongeza kwamba madhara yanayoipata nchi na mtu mmoja mmoja ni makubwa na inasikitisha kwa hali ilivyo na kwamba lazima Serikali ije na suluhu ya jambo hilo.
Aidha, Nape alisema Kamati Kuu pia ilijadili masuala yanayogusa wananchi likiwamo la migogoro ya ardhi, madini bei ya pamba na kuagiza Serikali iyashughulikie kabla migogoro hiyo haijawa mikubwa.
Hivi sasa mafuta ya taa yanauzwa bei kubwa kuliko dizeli na petroli ambapo katika baadhi ya vituo bei elekezi ni Sh 1,940 na kikomo ni Sh 2,086 kwa Dar es Salaam wakati kigoma elekezi ni Sh 2,117 na kikomo ni Sh 2,334 kwa lita.
Kwa hali hiyo hiyo, bei elekezi ya dizeli kwa Dar es Salaam ni Sh 1,939 na kikomo ni Sh 2084 huku kwa Kigoma elekezi ni Sh 2170 na kikomo ni Sh 2,333.
Hatua ya kupandishwa kwa bei hiyo ya mafuta ilifikiwa bungeni katika Bajeti ya Mwaka huu wa Fedha, kwa lengo la kuhakikisha kwamba kodi ya mafuta ya taa haizidiani sana na ya dizeli na hivyo kuondokana na uchakachuaji.
Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya uchumi wanadai kwamba wachakachuaji wanafahamika na hivyo ni wajibu wa Serikali kuwabana kuliko kumwumiza Mtanzania masikini anayeishi kwa kutegemea mafuta ya taa.
Lakini pia wanasema tatizo linalosababisha yote haya ni kwamba mafuta yote yanaagizwa kutoka nje ya nchi ambako bei inatoka huko huko lakini pia kodi ya mafuta nchini ni kubwa. Wanatoa mfano kwamba lita moja ya mafuta ya taa huitozwa kodi ya Sh 400.30, ya petrioli ni Sh 534 na dizeli ni Sh 415.
Wachambuzi hao wanasema pia kwamba hata thamani ya sarafu kulinganisha na dola ya Marekani ni tatizo, “angalia Machi kiwango kilikuwa dola moja kwa Sh 1,400 leo ni Sh 1,600,” alisema mchambuzi ambaye hakuta kutajwa jina.
Asilimia 14 tu ya Watanzania ndio wanaotumia umeme huku asilimia iliyosalia ambayo wengi ni wananchi masikini waishio vijijini, wanatumia mafuta ya taa kumulikia na hata kupikia, hivyo bei ya nishati hiyo inapopanda inawaumiza.
Wakati huo huo, habari zilizopatikana jana jioni Dodoma, zilisema leo Serikali inatarajiwa kutangaza bei mpya ya mafuta nchini, baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) kukokotoa kwa kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali
Showing posts with label CCM. Show all posts
Showing posts with label CCM. Show all posts
Tuesday, August 2, 2011
Saturday, July 16, 2011
Lowassa aweka mambo hadharani
MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, amesema atatangaza uamuzi kuhusu nyadhifa zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati muafaka ukifika. Amesema ameshitushwa na kitendo cha aliyekuwa mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, kutangaza kuachia nafasi hiyo na ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.
Lowassa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Serikali ya Muungano, alisema hayo baada ya kutakiwa kutoa maoni kuhusu uamuzi wa Rostam kujiuzulu nyadhifa hizo. "Ninachoweza kusema ni kuwa, Rostam kujiuzulu ni haki yake lakini nimeshituka kuona amejiuzulu na ubunge. Nimeguswa pia na wananchi wake walivyopokea uamuzi huo," alisema. Rostam akitangaza uamuzi wa kuachia ngazi juzi, alisema amefikia uamuzi huo ili kulinda maslahi ya Chama. Kwa upande wake, Lowassa alipoulizwa ana mpango gani wa yeye kujiuzulu alisema: "Nitazungumza wakati muafaka ukifika."
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kwa upande wake alisema kwa kufuata utaratibu wa kawaida ndani ya Chama, hakina taarifa za kujiuzulu Rostam. Hata hivyo, alisema jambo hilo litazungumzwa katika vikao vya juu vya Chama na baadaye taarifa zitatolewa. "Chama hakina taarifa yoyote, tumeona kwenye vyombo vya habari ametangaza kujiuzulu kwake akiwa Igunga," alisema Mukama na kuongeza kuwa, CCM bado inalihitaji jimbo la Igunga.
Naye mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), aliibuka bungeni na kuomba muongozo wa Spika Anne Makinda, akitaka atangaze kuwa jimbo la Igunga lipo wazi. Spika Anne alisema hana taarifa rasmi kuhusu kujiuzulu kwa Rostam, na kama ilivyo kwa wengine ameona habari hizo kwenye mitandao.
"Sisi tuna taratibu zetu, Rostam hajaniandikia barua, tutatoa taarifa wakati muafaka utakapowadia," alisema. Katika hatua nyingine, wanasiasa na wasomi nchini wameendelea kuwa na maoni tofauti kuhusu uamuzi wa Rostam, wengine wakipongeza hatua hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti , walisema uamuzi huo ni mzuri ingawa umechelewa. Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema, alisema Rostam amechukua uamuzi mzuri. “Ni uamuzi mzuri ingawa amechelewa, hasa kutokana na tuhuma zake kuwa za muda mrefu,’’ alisema. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hajji Semboja, alisema Rostam anapaswa kupigiwa mfano na wafanyabiashara wengine.
“Ni sawa tu kuondoka, nina hakika CCM haiwezi kuyumba, ikizingatiwa kuwa wameondoka wakongwe kama hayati Julius Nyerere na Mzee Rashidi Kawawa na CCM bado ipo,’’ alisema. Alisema CCM ni chama chenye wanachama wengi, hivyo kinachopaswa kufanyika ni kwa wafanyabiashara wengine kujitoa na kuwaachia watu wa siasa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mohamed Bakari, alisema CCM inapaswa kuwa makini kutokana na Rostam kushika nafasi kubwa, hivyo ni lazima alikuwa na wafuasi. “Suala hili ni kubwa na lina faida na hasara, hivyo kinachotakiwa ni kujipanga vyema ili kuepusha matatizo yatakayoweza kujitokeza baadaye,’’ alisema.

Wednesday, July 13, 2011
Rostam Aziz ajivua gamba
HUENDA katika siku 90 zijazo, wananchi wa jimbo la Igunga mkoani Tabora , wakaingia kwenye uchaguzi mdogo, baada ya Mbunge wao mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya CCM ukiwamo ubunge. Mbali na ubunge wa Igunga mkoani Tabora alioushikilia kwa miaka
Sitta: Wabunge wa upinzani wanafiki
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema mambo mengi ya wapinzani ni ya kinafiki na wamekuwa wakiibeza Serikali kwa kauli nyepesi nyepesi.
Sitta alitoa kauli hiyo jana bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijaribu kutuliza Bunge lililokuwa limechafuka baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), kudai kuwa Serikali iliyoko madarakani ni legelege na imeshindwa kukusanya kodi.
"Nawasihi wenzangu hasa wa CCM, hawa wapinzani hii (kupinga mambo) ndiyo kazi yao, wanabeza kila tunachofanya kwa lugha nyepesi nyepesi na mambo mengi wanayozungumza ni unafikinafiki hivi, sisi tuwaachie wananchi wawahukumu.
Kauli hiyo ilisababisha baadhi ya wabunge hasa wa upande wa upinzani kusimama na kuomba mwongozo wa Mwenyekiti na wengine wakizomeana, huku Sitta ambaye ni Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, akiwa amesimama akiomba kuendelea.
"Subirini nitoe mfano ... wanazungumza posho za vikaoni ni kuibia wananchi na baadhi yao wamekuwa wabunge kwa miaka mitano iliyopita na walikuwa wakizichukua, kama kweli ndivyo hivyo, basi warudishe," alisema Sitta.
Kauli hiyo ilisababisha wabunge zaidi, karibu 10 wakiwamo wa CCM kusimama kuomba Mwongozo wa Mwenyekiti, lakini Mwenyekiti Jenista Mhagama akaahirisha shughuli za Bunge kwa mapumziko ya mchana, kwa kuwa muda ulikuwa umefika, huku akiwaacha wabunge wakipiga kelele za kuomba Mwongozo.
Kabla ya kuibuka tafrani hiyo, Kafulila aliyekuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, alisema tangu Uhuru moja ya maadui waliopigwa vita ni maradhi; lakini akashangaa bajeti ya Afya ni ndogo na kuongeza kuwa inatokana na Serikali legelege kushindwa kukusanya mapato.
"Miaka 50 ya Uhuru asilimia 90 ya bajeti ya maendeleo ya afya inategemea fedha za nje, tatizo hamkusanyi kodi na Nyerere (Baba wa Taifa) alisema Serikali legelege inashindwa kukusanya kodi," alisema Kafulila.
Kauli hiyo ilipingwa na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangala (CCM) aliyesema Kafulila alitumia neno la kuudhi kwa kuiita Serikali ya CCM legelege.
Dk. Kigwangala alifafanua kuwa Kafulila hakuwa na taarifa sahihi, kwa kuwa katika miaka mitatu iliyopita, Serikali ilikuwa ikikusanya karibu Sh bilioni 200, lakini mpaka mwaka huu, makusanyo yaliongezeka na kufikia karibu Sh bilioni 400.
Baada ya ufafanuzi huo, Mwenyekiti wa Bunge, Mhagama alimtaka Kafulila kufuta usemi, lakini mbunge huyo alipinga akisema ni kauli ya Baba wa Taifa, ambaye kila mtu anamuenzi bila kujali anatoka chama gani.
"Tunapoteza muda kujadili suala ambalo liko wazi, mwaka 2005/06 Serikali ilikuwa ikikusanya wastani wa Sh bilioni 260 lakini dola moja ilikuwa sawa na Sh 1,000.
"Leo mnakusanya karibu Sh bilioni 400 kwa mwezi, dola moja ni Sh 1,600 ni hesabu rahisi, hakuna kilichoongezeka ... sifuti usemi, niko tayari kufia ukweli huu," alisema Kafulila na kusababisha Sitta kuamka na kuwaita wapinzani wanafiki huku akiwataka CCM kuwavumilia.
Hata hivyo, Mwalimu Nyerere alisema chama legelege huzaa Serikali legelege na pia aliwahi kusema "Serikali corrupt (inayokula rushwa) hushindwa kukusanya kodi," na si Serikali legelege hushindwa kukusanya kodi.
Awali, kabla ya tafrani hiyo, Kafulila alimtaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, ikibidi ajiuzulu kuliko kukubali kuwasilisha bajeti ya fedha ndogo bungeni huku ikitegemea fedha nyingi za wahisani.
Alisema hiyo inatokana na wabunge na familia zao kuwa na uwezo wa kutibiwa sehemu yoyote ndani na nje ya nchi, ndiyo maana hawawekezi katika hospitali za vijijini.
Wakati akisema hayo, mmoja wa wabunge ambaye hakufahamika lakini mwanamke, aliwasha kipaza sauti akasema: "Pamoja na wewe (Kafulila) na Mbunge wa Mpanda Mjini Chadema (Said Arfi ambaye alilazwa India hivi karibuni)."
Hata hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, alisimama na kupinga kauli ya Kafulila, akisema: "Hili ni Bunge Tukufu, tuzungumze kwa heshima."
Mbunge mwingine mwanamume akawasha kipaza sauti na kuhoji: "Nani ana heshima?" Nagu akaendelea kufafanua kuwa mwanawe ni daktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ni ya Serikali na hata baba yake mzazi alilazwa katika hospitali ya Katesh ambayo ni ya vijijini.
Hata hivyo, sauti ile ya kiume iliendelea kumkatisha Nagu na safari hii Mbunge huyo alisema, "so what(kwa hiyo?"
Kutokana na kauli hizo za kukatishana, Mhagama alisimama na kusema ameisikiliza sauti ya mmoja wa wabunge wanaotoa kauli hizo za kejeli huku akimkatisha waziri aliyekuwa akizungumza na kubaini kuwa sauti hiyo inafanana na ya Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema).
Alionya kuwa wanachofanya wabunge kuwasha vipaza sauti holela ili kuzuia hoja za wenzao kusikika au kuwakatiza, ni kinyume na Kanuni za Bunge na akifuatilia anaweza kuwabaini na kuwachukulia hatua.

Thursday, June 30, 2011
Ex-spy chief backs Chadema protests
Dar es Salaam. Former Intelligence chief Hassy Kitine yesterday came out in support of the opposition Chadema’s stance on various issues.He told journalists in Dar es Salaam that demonstrations organised by Chadema across the country in protest at the spiralling cost of living and the party’s demand for the scrapping of sitting allowances were pertinent issues which the country’s leadership should take seriously. Dr Kitine is the first prominent CCM cadre to have publicly supported Chadema’s cause, which has in recent months been roundly criticised by the ruling party and some opposition parties. He said it was a fact that the high cost of living was a heavy burden on Tanzanians, adding that something should urgently be done to address the situation. Dr Kitine, a former Cabinet minister and MP, said whatever Chadema was doing to draw attention to such issues deserved support, and added that the opposition party should not be demonised for practising its democratic rights. He made the remarks when journalists sought his comments on various national issues at the end of a meeting organised by Faidika, a microfinance institution in which he is a director. Dr Kitine said he had also been closely following the debate on whether or not MPs and other holders of public office deserved sitting allowances.“What Chadema is doing is healthy for our democracy because everyone is entitled to their own opinion, but the views should be constructive…they should not be aimed at destroying the country.” Dr Kitine warned that the widening gulf between the rich and poor was “very dangerous”, saying it posed a serious threat to peace and stability in Tanzania.He said the country could not expect to remain peaceful forever when a few individuals controlled 99 per cent of the economy. Dr Kitine said he was only trying to speak the “truth”, although he was aware that his comments would not go down well in some quarters.“I, like other Tanzanians, am giving my views on various national issues, but I know that some people are not happy with my comments. But even if I don’t say what I am saying, other people will say it.” On the Chadema demonstrations, Dr Kitine said what the opposition party was doing was a challenge to the government and other political parties. “What we need to look at is what they (Chadema) are advocating in their demonstrations. If you talk of life having become unbearably tough, that’s reality because many people are feeling the pinch...I support the demonstrations although I’m a CCM member,” he said. Comparing the reign of retired President Benjamin Mkapa and President Jakaya Kikwete’s Fourth Phase government, Dr Kitine said he had not noticed any major difference between the two phases.He said, however, that things had gone from bad to worse after principles enshrined in the Arusha Declaration were abandoned, adding that people were now freely buying their way into elective office. “In the past, when I was appointed Director of Intelligence by Mwalimu Nyerere and later a minister before I became an MP, the sole motive for seeking leadership was to serve the people,” he said. Dr Kitine said the political landscape had changed dramatically since the Arusha Declaration was shunted aside. It was very difficult in the past for people who had amassed wealthy and failed to explain its source to be allowed to seek elective office, he said. In a swift response, CCM Publicity Secretary Nape Nnauye told The Citizen that there was nothing wrong with convincing people to fight for their rights, adding that the issue was how this was done. “Even CCM has been doing a lot to raise people’s awareness and sensitise them on their rights. Take for instance the decision to construct a secondary school in every ward across the country…this aims at increasing people’s awareness by giving them education,” he said when he toured Mwananchi Communications Limited head office in Dar es Salaam. “The difference is that while we (CCM) are empowering the people by educating them, Chadema stops people from engaging in economic activities by holding demonstrations daily and deceiving them that this is a shortcut to State House,” he said. |
Wednesday, June 15, 2011
CCM WAFUTA POSHO ZA VIKAO
HOJA ya kutaka kufutwa kwa posho za vikao za wabunge na watumishi wengine wa umma imechukua sura mpya baada ya jana Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba kuliambia Bunge mjini hapa kuwa suala la kufutwa kwa posho ni la kitaifa na ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa na serikali.
Kauli hiyo ya Makamba ambaye pia ni Katibu wa Mambo ya Nje wa Sekretarieti ya CCM imekuja huku kukiwa na malumbano makali baina ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kuhusu suala hilo la posho za vikao vya wabunge.
Juzi, Spika Makinda alisema Zitto ambaye ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, anaweza kufukuzwa ubunge kwa kutosaini karatasi za mahudhurio, hatua ambayo Zitto alisema ataichukua ili asilipwe posho za vikao.
Spika alisema Zitto anaweza kukumbwa na adhabu hiyo iwapo hatasaini karatasi za mahudhurio ambazo ndizo zinathibitsha uwepo wa mbunge katika mikutano na vikao vya bunge na kwamba kanuni zinamwadhibu mbunge kwa kumfukuza asipohudhuria mikutano mitatu. Hata hivyo, Zitto amepuuza kauli hiyo ya Spika kwa kusema kwamba kama ni kwa ajili ya kukataa posho, yuko tayari kufukuzwa bungeni.
"Nitafanya hivyo tuone, Kanuni inasema mikutano mitatu mfululizo na siyo vikao vitatu mfululizo. Nitatumia uzoefu wangu wa siasa za wanafunzi kukwepa mtego wake. Lakini kama anadhani ni sawa kunifukuza ubunge kwa kukataa posho, nipo tayari," alisema.
Kauli ya jana ya Makamba pia inaonekana kutofautina na mawazo ya wabunge wengi wa CCM akiwamo Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ambaye amesema wanashabikia suala hilo wanajitafutia umaarufu.
Akichangia huo wa maendeleo wa miaka mitano jana, Makamba alionekana kupigia chapuo suala la kufutwa au kuangaliwa upya kwa posho za vikao huku akisema kwamba ni la kitaifa na ni sehemu ya mpango huo.
Makamba alisema kuwa suala la nidhamu na usimamizi wa matumizi ya fedha za umma ni muhimu na kwamba mpango huo umeliona katika ukurasa wa 17 wa kitabu kilichochapishwa kwa Kiingereza na kutoa mapendekezo ya kufutwa kwa posho za vikao na zile za usafiri.
"Mpango unabainisha kwamba kuna umuhimu wa kufutwa kwa posho za vikao na usafiri hivyo iwapo wabunge mtalisikia likiwasilishwa hapa kwa mbwembwe kesho (leo), basi msije mkashangaa kwani ni sehemu ya mpango huu," alisema Makamba.
Kujadiliwa bungeni leo
Mjadala kuhusu malipo ya posho ambao umekuwa ukiendelea kwa wiki moja sasa hasa zaidi nje ya Bunge, leo unatarajiwa kuingizwa rasmi bungeni wakati Bajeti ya Serikali iliyowasilishwa na Mkulo Jumatano iliyopita itakapoanza kujadiliwa.
Suala hilo ni dhahiri litajitokeza katika bajeti mbadala itakayowasilishwa na kambi ya Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe ambaye amekuwa katika mvutano usio rasmi na Spika kutokana na kukataa kulipwa posho za kikao.
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema jana kuwa kambi yake inatarajiwa kutoa ushauri mgumu ambao haujazoeleka kwa watendaji wa serikali na kwamba suala la kufutwa kwa posho ni sehemu ya mapendekezo hayo.
Alisema kufutwa kwa posho hizo kunaweza kuokoa zaidi ya Sh900 bilioni ambazo zinaweza kuelekezwa katika maeneo mengine ya huduma kwa wananchi.
Uhalisia posho za wabunge
Mmoja wa wabunge wa CCM ambaye hakutaka kutaandikwa jina lake alisema anasikia kuhukumiwa katika nafsi yake kutokana na kupokea posho za vikao ambazo kimsingi ni sawa na "kuwaibia wananchi".
"Ujue bwana sisi ndani ya CCM mambo hayaendi kama kwa wenzetu (Chadema), wale wanaweza kukaa leo na kuamua, sisi ni tofauti lazima kuwepo na mchakato lakini ukweli ni kwamba hoja yao ni nzuri," alisema mbunge huyo.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa malipo ya wabunge yamegawanyika katika sehemu nne ambazo ni pamoja na mshahara ambao ni Sh2,300,000 kwa mwezi, posho ya ubunge kila mwezi ambayo ni Sh5 milioni, posho ya kujikimu (per-diem) Sh80,000 wawapo nje ya majimbo yao kikazi na posho ya vikao (sitting allowance) ambayo huwa ni Sh70,000 kwa kila mbunge.
Kwa maana hiyo, kwa kawaida mbunge hulipwa Sh7.3 milioni kila mwezi kabla ya kukatwa kodi na wawapo Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya vikao vya kamati na bunge au mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli zilizopo chini ya kamati zao. Hulipwa kiasi cha Sh150,000 kila mmoja kwa siku ambazo ni Sh70,000 kwa ajili ya vikao na Sh80,000 kwa ajili ya kujikimu.
Kwa maana hiyo bunge linatarajiwa kutumia kiasi cha Sh1.788 bilioni kwa ajili ya kugharamia vikao 73 vya Bunge la Bajeti iwapo wabunge wote 350 waliopo watahudhuria vikao hivyo.
Kwa hesabu hizo, kila mbunge katika mkutano wa Bunge la Bajeti anatarajiwa kuondoka na kikita cha Sh5.1 milioni mbali na Sh 5.58 milioni ambazo ni malipo kwa ajili ya kujikimu, fedha ambazo ni mbali na mshahara wake kwa mwezi na posho ya ubunge.
CCM yakataa posho
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza machakato wa kufuta posho hizo ikiwa ni hatua ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Habari kutoka ndani ya CCM, Dodoma na Dar es Salaam zinasema kuwa mkakati wa kufutwa kwa posho ulianzishwa takriban mwezi mmoja uliopita na sekretarieti mpya inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya wajumbe wa sekretarieti walihoji uhalali wa posho wanazolipwa hata pale vikao vinapofanyika katika sehemu ambako ni makazi yao na kwamba hoja hizo ndizo zilizozaa wazo la kufutwa kwa posho katika vikao.
"Hoja ilikuwa kwamba kama chama hakina fedha na tunataka kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, basi posho za vikao zifutwe kwa sababu hakuna ulazima wa posho hizo hasa kwa wajumbe wa sekretarieti ambao kazi zao ni za kila siku," kilieleza chanzo chetu na kuongeza:
"Hivi sasa mpango huo uko kwenye mchakato wa kuwekewa mwongozo na nadhani baada ya kupitia katika vikao vyetu utaanza kutekelezwa. Lakini kimsingi ni kama utekelezaji wake umeshaanza kwa sababu baadhi ya wajunbe wamekataa kabisa kusaini posho hizo."
Habari zaidi zinadai kuwa waraka wa mapendekezo ya kupunguza matumizi ndani ya CCM unakwenda mbali zaidi hadi katika matumizi ya magari na kwamba pale usafiri unapohitaji wa kuelekea kwenye mkutano mmoja, basi viongozi watumie magari machache kwa maana ya usafiri wa pamoja badala ya utaratibu wa sasa ambao unamruhusu kila kiongozi kutumia usafiri wake.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu sekretarieti kufuta posho katika vikao vyake, hakukanusha wala kuthibitisha, badala yake akadai kuwa hayo ni mambo ya ndani ya chama ambayo hayana faida yoyote kwa umma.
"Hivi ninyi waandishi wa habari, haya mambo mnayapata kwa nani! Haya ni mambo ya ndani ya chama sidhani kama yana tija yoyote kwa umma, maana haiwezi kusaidia chochote," alisema Nape kwa kwa simu.
Alipoelezwa kwamba suala hilo lina uhusiano na sakata linaloendelea bungeni, Nape alisema: "Bunge ni bunge na chama ni chama. Kila taasisi inajitegemea na ina uamuzi wake, lakini pia sisi kama chama tulishatoa kauli mara nyingi kwamba suala la posho kwa wabunge na watumishi wengine wa serikali linazungumzika, ni la kisera na wanaohusika wapo waulizeni hao."
Mwishoni mwa wiki iliyopita Nape akizungumzia malumbano miongoni mwa wabunge kuhusu suala la posho alisema suala hilo linajadilika na kwamba si vyema kulipinga kwa sababu tu linatokea kambi ya upinzani.
Kwa upande wake, Makamba alipoulizwa kuhusu kufutwa kwa posho katika vikao vya Sekretarieti ya CCM naye kama ilivyokuwa kwa Nape, hakukanusha wala kuthibitisha.
"Wewe si unamfahamu msemaji wa chama ni nani? Mwulizeni Nape tena nadhani anakuja Dodoma. Akija mwulizeni, mimi siwezi kulizungumzia.... lakini ninyi waandishi haya mambo ya ndani ya chama huwa mnayapata wapi? Anyway, mwulizeni mwenezi atawaambia," alisema Makamba.
Chanzo: Mwananchi 15/6/2011
Monday, June 6, 2011
Hali tete: Chadema, Polisi wakwaruzana
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, jana lililazimika kuimarisha ulinzi katika Kituo chake Kikuu (Central) na baadhi ya maeneo ya jiji kukabiliana na tishio la wanachama wa Chadema kuandamana ili kushinikiza Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe aliyekamatwa juzi aachiwe.Mbowe ambaye alikamatwa juzi ikiwa ni kutekeleza amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyoamuru akamatwe popote alipo na afikishwe hapo kwa kutotii amri ya kufika mahakamani katika kesi inayomkabili, alitarajiwa kupelekwa huko wakati wowote kuanzia jana akiwa chini ya ulinzi.
Jana, vijana wa Chadema walikusanyika katika kituo hicho huku wakilaani kitendo cha kukamatwa kwa mwenyekiti wao huku wengine wakijikusanya katika vikundi vidogovidogo katika maeneo mbalimbali katika Barabara za Morogoro na Nyerere, lengo likiwa kushinikiza kiongozi huyo atolewe rumande na asisafirishwe kupelekwa Arusha.
Taarifa kutoka Arusha ambako kesi ya kiongozi huyo inatarajiwa kuendelea leo asubuhi zinaeleza kuwa polisi jana jioni waliendesha msako wa wanachama wa Chadema waliokuwa wakihamasishana kuhudhuria kwa wingi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha.
Wanachama na mashabiki hao wa Chadema walidai kwamba kitendo cha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni ni mpango uliobuniwa na CCM wa kubinya demokrasia ya vyama vingi nchini.
Mbowe na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Zitto Kabwe walikamatwa katika maeneo tofauti nchini juzi. Wakati Mbowe alidaiwa kutotii amri ya mahakama, Zitto alidaiwa kuzidisha muda wakati wa kuhutubia mkutano wa hadhara mkoani Singida.
“Tumeongea na polisi, bado wanamng'ang'ania Mbowe. Msimamo wao ni kumpeleka Arusha, tuangalie utaratibu utakaotumika katika kumsafirisha,” alisema Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika.
Baada ya kauli hiyo ya Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubunge, vijana wa chama hicho wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Jacob walianza kuimba nyimbo za kulaani kukamatwa kwa mwenyekiti wao huku wakisema muziki wa Chadema polisi hawauwezi.
Ofisa mmoja mwadamizi wa Polisi Ilala ambaye hakujitambulisha jina aliwaambia vijana hao kuwa polisi walishakubaliana na viongozi wa Chadema kuwa mtuhumiwa huyo amepangiwa utaratibu wa kusafirishwa kwenda Arusha kuhudhuria kesi yake.Ofisa huyo aliwataka wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo kuondoka ili kupisha jeshi hilo kuendelea na kazi ya kutoa huduma kwa watu wengine.
“Tumeshaongeza na wakubwa wenu, hiki ni kituo cha polisi watu mbalimbali wanakuja kupata huduma hapa. Mtu haji kuangaliwa kwa aina hii ya hamasa na nyimbo, tunaomba muondoke,” alisema ofisa huyo.Kauli hiyo ilipingwa na vijana hao wakisema ofisa huyo ni mtu wa kawaida hawezi kuwaeleza mambo kama hayo.
“Sisi hapa tuna viongozi wetu mambo kama hayo tungeelezwa na kuelewa kama yangesemwa nao na si mtu wa kawaida kama wewe,”alisikika mmoja wa wanachama hao akisema kwa sauti.
Kauli hiyo ilimshangaza ofisa mwingine wa polisi aliyeibuka na kuhoji: “Mnasema huyu ni mtu wa kawaida? Akajibiwa “ndiyo”, “huyo siyo mtu wa kawaida."Vijana hao waliendelea na msimamo wao: “Sisi tunasema huyo ni mtu wa kawaida kwa sababu siyo kiongozi wetu, ndiyo maana tunasema angekuwa kiongozi wetu tungemwelewa.”
Kauli hiyo ilimlazimisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile kujitokeza na kuwataka watu hao kuondoka katika eneo hilo kwa sababu kulikuwa na shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea.
“Tumeongea na viongozi wenu, tumeshakubaliana tunawaomba mtawanyike na sisi tuendelee na kazi, sitaki mkusanyiko wowote katika kituo cha polisi,” alisema Shilogile. Mara baada ya kauli hiyo gari la maji ya kuwasha lilianza kusogea walipokuwa wafuasi hao wa Chadema likitanguliwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia waliokuwa wakiwafukuza katika eneo hilo.
Kundi hilo liliondoka na kuelekea makao makuu ya Chadema ambako Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alikuwa na mkutano na waandishi wa habari.
Msimamo wa Kamanda Kova
Akizungumzia mvutano huo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jeshi lake haliwezi kumwachia Mbowe kwa sababu wanaheshimu amri ya Mahakama.
Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba jeshi hilo lilipokea amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kumkamata kiongozi huyo wa Chadema na kwamba hawaruhusiwi kuhoji lolote juu ya amri hiyo.
“Sisi kama jeshi la Polisi tumepokea amri ya mahakama ya kumtia hatiani Mheshimiwa Mbowe na hatuna mamlaka ya kumwachia huru hadi mahakama itoe amri ya kumwachia,”alisema.
Alisema sheria hairuhusu kuhoji sababu za amri inayotolewa na mahakama na kufafanua kuwa hizo ni sheria zilizotungwa na wabunge wenyewe. Alisema Mbowe anatarajiwa kusafirishwa chini ya ulinzi wa Polisi kwenda mkoani Arusha kujibu kesi inayomkabili na kwamba taratibu zote za safari tayari zimekamilika.
“Tunachokifanya ni maagizo ambayo yametoka ngazi ya juu kuhusu suala hili kwa hiyo Mbowe atapelekwa Arusha chini ya ulinzi wa polisi muda wowote kuanzia sasa alimradi awahi muda wake wa mahakama,”alisema Kova.
Alisema atapelekwa Arusha chini ya ulinzi wa polisi kwa sababu amekiuka masharti yake ya dhamana na kwamba tayari wamezungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani waliokwenda kumuona kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni jana.
Kova alisema kulingana na taratibu na sheria za Tanzania, mahakama ikitoa amri hakuna mtu anayeweza kuipinga.
Aliwataka wananchi watulie na kuipa fursa mahakama itekeleze sheria zilizotungwa na Bunge. Akizungumzia kukamatwa kwa Mbowe, Mnyika alisema hizo ni njama za kuudhalilisha upinzani na pia mbinu za kumtaka Mbunge huyo wa Hai asihudhurie kwenye Kikao cha Bunge la Bajeti.
“Endapo watashindwa kutumia busara za mazungumzo tuliyoyafanya kumwachia Mbowe, jambo hili tutalirudisha kwa wananchi na nguvu ya umma itatumika kusuluhisha tatizo hilo,” alisema.
Alisema amani ni tunda la haki lakini inaweza kupotea kama haki haitatendeka na kuongeza kuwa kuna watu ambao wanashutuma nzito za ufisadi, lakini hawachukuliwi hatua zozote isipokuwa viongozi wa upinzani.
Tamko la Dk Slaa
Dk Slaa alisema kesi zinazowakabili viongozi wa chama hicho na wabunge wa vyama vya upinzani vinalifedhehesha Bunge la Tanzania kimataifa.
“Ili mtuhumiwa akamatwe sheria iko wazi, notisi zilitakiwa kutolewa kwa mdhamini wake na pia kwa wakili, lakini kwa Mbowe haikuwa hivyo na hiyo inaonyesha ni agizo kutoka mahali Fulani,” alidai.
“Polisi mkoa wa Mwanza wametuma barua kwa Katibu wa Bunge kuomba kibali cha kwenda kumhoji Mbunge wa Jimbo la Busega, Dk Titus Kamani, iweje kwa wabunge wa upinzani kukamatwa bila utaratibu? Alihoji Dk Slaa.
Alisema kutokana na mazingira hayo kama Mbowe hatafikishwa leo mahakamani wabunge wa Chadema hawataingia bungeni.
Kuhusu uwakilishi kwenye kamati ya uongozi alisema hata kama Zitto atakuwa nje ya mahabusu, hataingia kuwakilisha upinzani kwa sababu anayetakiwa kumpa kibali cha kufanya hivyo yupo ndani.
Kuhusu kosa la Zitto kukamatwa na polisi alisema inashangaza kwa sababu alikuwa kwenye mkutano wa hadhara kama mbunge na alizidisha dakika 20 kwenye mkutano huo.
Alisema hiki siyo kipindi cha kampeni na Zitto ni kiongozi mwenye haki ya kufanya hivyo na kusisitiza kilichofanyika kimelenga kufifisha demokrasia nchini.
Friday, May 27, 2011
Tamko la Vijana Arusha lazidi kuivuruga CCM
TAMKO la baadhi ya vijana wa UVCCM, Mkoa wa Arusha kutaka mafisadi wafukuzwe, limezidi kukivuruga chama hicho baada ya Katibu Mkuu, Wilson Mukama kusema hawezi kujiingiza 'kichwa kichwa' kuzungumzia suala hilo, huku baadhi ya watuhumiwa wakikataa kulizungumzia. Mukama alisema CCM inafuatilia kwa karibu mgogoro huo, lakini haiwezi kuuzungumzia sasa kwa kuwa hajapata taarifa rasmi kutoka umoja wa vijana. Kwa mujibu wa Mukama, UVCCM ni jumuiya halali ya chama tawala yenye mamlaka kamili ya kuzungumzia matatizo yake, hivyo yeye kusema chochote itakuwa ni kuingilia kazi za jumuiya hiyo. “Chama chetu kina utaratibu wake, UVCCM ni jumuiya ndani yake, hayo yaliyotokea kule Arusha siwezi kuyazungumzia, ila kesho (leo) tuna kikao, hivyo wao vijana watatupa taarifa zao,” alisema Mukama, huku akisoma ujumbe mfupi wa simu (sms) alioandikiwa na katibu mkuu wa umoja huo, Martin Shigella kuwa watatoa taarifa ya yaliyotokea Arusha. “Suala la Arusha tunalifuatilia kwa ukaribu sana, ila utendaji tunawaachia wao (UV-CCM), nasi tukishapata taarifa zao ndio tutaweza kulizungumzia suala hilo, ila kwa sasa mtafute Shigella,” alielekeza Mukama. Alipotafutwa kwa simu jana kuzungumzia tuhuma hizo, Shigella alisema kuwa hawezi kutolea ufafanuzi kwa kuwa alikuwa nje ya nchi kikazi. “Sikuwapo nchini, kwa hiyo sitaweza kuzungumza lolote, kuna mtu alikuwa akikaimu nafasi yangu, hivyo nikipata maelezo kutoka kwake nitakuwa tayari kuzungumza, nitafute kesho (leo),”alisema Shigella. Naye makamu mwenyekiti wa umoja huo taifa, Benno Malisa alisema wamesikitishwa na kauli zilizotolewa na vijana wenzao wa Arusha, hivyo watatuma kamati ya maadili kwenda kuzungumza na makundi yanayolumbana. “Hivi karibuni Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM itakaa na kutoa uamuzi, lakini ni baada ya Kamati ya Maadili itakayotumwa kuzungumza na wanachama wanaolumbana huko Arusha kuleta ripoti makao makuu ya umoja wetu,”Alisema Malisa. Akizungumzia adhabu wanazoweza kupewa wanachama wa umoja huo, Malisa alisema adhabu hizo zitatokana na aina ya makosa watakayokutwa nayo. “Suala hili liko ndani ya uwezo wetu na tutalifanyia kazi na kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni za UVCCM, kama kutakuwa na makosa makubwa zaidi yatapelekwa ngazi za juu zaidi,”alisema Malisa. Juzi, UVCCM Mkoa wa Arusha waliuomba uongozi wa juu wa chama tawala kuwafukuza uanachama viongozi watatu, wakiwamo Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na mwenzake wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge wanaotuhumiwa kwa ufisadi. Vijana hao pia walikishauri chama hicho kupitia kamati yake ya maadili kuwaita na kuwahoji makada hao maarufu na baadaye kuwachukulia hatua, zikiwamo za kuwafukuza kwa maslahi ya chama na taifa. Tamko hilo lililosomwa na mjumbe wa baraza la umoja huo mkoani Arusha, Ali Babu lilitaka watuhumiwa hao waliowaita mapacha watatu, kuwa ndio chanzo cha kudhoofika kwa chama hicho tawala. "Pia, tunasisitiza Andrew Chenge aondolewe kwenye Kamati ya Maadili ya CCM mara moja na kumtaka mtuhumiwa mwingine (jina tunalo) aondolewe pia kwenye uongozi wa ndani ya umoja wetu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Lakini, alipotafutwa jana kuzungumzia tuhuma hizo, Chenge alijibu kwa ufupi: "Kwa sasa sitaki kuzungumzia masuala hayo. Kila la heri." Naye Lowassa alipotafutwa alisema kwa ufupi: ‘no comment’ akimaanisha kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo. Hata hivyo, wakati makada hao wakigoma kuzungumzia suala hilo, mwenyekiti wa umoja huo Mkoa wa Arusha, James ole Milya anayeshinikizwa kujiuzulu wadhifa huo, jana aliibuka na kudai kuwa tamko hilo lilitolewa na kundi la vijana aliowaita wahuni wa mitaani na wasiokuwa na kazi. “Wale ni wahuni, hawana chochote wala lolote, wanapenda kukaa vijiweni hawana kazi za kufanya, tuna taarifa kwamba walitumwa na baadhi ya viongozi hapa Arusha kupindisha na kuvuruga hoja za umoja wetu mkoani Arusha,” alisema Milya Alisema kuwa vijana hao wakiongozwa na Ali Babu hawatambuliki ndani ya umoja huo, huku akisisitiza kwamba hoja na malalamiko yote hupitishwa katika ngazi husika ili ziweze kufanyiwa kazi na sio kuibuka na kutoa matamshi yasiyo na tija. Millya aliendeleza msimamo wake wa kutaka Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu aondoke madarakani kwa madai ya kusababisha jimbo kwenda upinzani (Chadema), huku akimtaka katibu huyo asikilize kilio chao (UVCCM) cha kumtaka aondoke. Alisema kuwa endapo kiongozi huyo ataendelea kung'ang'ania nafasi yake, basi atang’olewa kwa maandamano ya vijana yasiyokuwa na kikomo ambayo yatafanywa na wanachama wa umoja huo. “Msimamo wetu uko pale pale, Chatanda ni lazima aondoke kwa kuwa amekivuruga chama chetu, ametuchonganisha na viongozi wa dini, lakini pia amesababisha Jimbo la Arusha Mjini liangukie upinzani kwa kukimbilia Tanga kusaka ubunge wa viti maalumu kipindi cha uchaguzi,”alisisitzia Milya. Juzi, katika mkutano wao wenye malengo makuu sita, vijana hao wa Mkoa wa Arusha walisema wanaunga mkono falsafa ya CCM ya kujivua gamba."Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa Watanzania," ilisema taarifa hiyo na kuongeza: "Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa ufisadi (wakiwataja kwa majina) na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania." |
Subscribe to:
Posts (Atom)