Tuesday, June 14, 2011

Majambazi wavamia hospitali ya Muhimbili, wapora mamilioni ya fedha

RPC Suleiman Kova 
Kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni Majambazi wakiwa na Pikipiki wamevamia na kupora Mamilion ya fedha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam. Tukio hilo la ujambazi limefanyika leo asubuhi ambapo inadaiwa kuwa askari Juma Magungu, wa Kampuni ya Full Time Security aliyekuwa analinda katika Idara ya Uhasibu amepigwa risasi Kifuani na majambazi hao na kusababisha kifo chake. 
 
Afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Ndugu Aminiel Aligeisha alisema kuwa tukio hilo limetokea leo saa mbili asubuhi ambapo wahasibu wawili wa Hospitali hiyo walikuwa katika zoezi la kuzipeleka fedha Idara kuu ya Uhasibu wakiwa na gari ndipo kundi hilo la Majambazi likatokea na kuwavamia. 
 
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano huyo, gari hilo lenye namba za usajili SU-36713 aina ya Nisani ikiwa na watumishi Wanne wa Idara ya Uhasibu walivamiwa na kundi hilo la watuhumiwa wa ujambazi wakiwa na Bastola moja.  Zaidi ya shilingi Miloni13 zinadaiwa kuibiwa.

No comments:

Post a Comment