Friday, September 9, 2011

Obama ahaidi kubuni nafasi zaidi za kazi

Rais wa Marekani Barack Obama amtangaza mpango wa kubuni kazi utakao gharimu dola bilioni 450.
Rais wa Marekani
Rais wa Marekani

Katika hotuba ya kipekee mbele ya bunge la Congress, rais Obama amesema mpango huo utasaidia kuuchepua uchumi wa nchi hiyo.

Amewataka wabunge wa chama cha Republican kuidhinisha sheria ya utekelezwaji wa mpango huo haraka iwezekanavyo na waache sarakasi za kisiasa.

''Watu wa taifa hili hufanya kazi kwa bidii, ili kutosheleza wajibu wao, suala lililoko kwa sasa ni ikiwa sisi wanasiasa tutatekeleza wajibu wetu na ikiwa tutakomesha sarakasi za kisiaisa na kufanya kitendo kitakachosaidia kufufua uchumi wa taifa letu'' alisema Obama.

John Boehner
John Boehner

Rais Obama ameahidi kubuni nafasi zaidi za kazi katika sekta ya ujenzi, elimu na pia kwa wanajeshi wastaafu na wale ambao hawana kazi, na pia kupunguza kodi.

Spika wa bunge la waakilishi ambaye ni mwanachama wa Republican, John Boehner, amesema mapendekezo ya Obama yatachunguzwa kwa kina na wabunge wa chama chake.

No comments:

Post a Comment