Friday, September 16, 2011

Wapinzani wa Gaddafi waingia Sirte

Wapiganaji wa utawala mya wa Libya
Wapiganaji wa Baraza la Kitaifa nchini Libya walioingia Sirte

Viongozi wa muda wa Libya wanasema wapiganaji wao wameingia mji wa pwani wa Sirte, moja ya maeneo ya mwisho ambayo bado yalikuwa yanadhibitiwa na wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi.
Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Mpito anasema wapiganaji walikiuka kanuni za ulinzi za Sirte lakini ni kutokana na kuwa walikabiliwa na upinzani mkali.
Mapema, watu waliokuwa mjini Benghazi walimshangilia Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy.

Wako kilometa 8-10 toka kati kati mwa mji wa Sirte

Ni viongozi wa kwanza wa nje kuzuru Libya tangu kuondolewa kwa Kanali Gaddafi.
Msemaji wa Baraza la Mpito la Kitaifa ameambia BBC kuwa wapiganaji wao wamekiuka utaratibu wa mipaka ya kujihami kusini na magharibi mwa mji wa Sirte.
Wapiganaji hao - kutoka mji wa Misrata, kilomita 200 upande wa magharibi - wako umbali wa kilomita 8-10 kufika katikati mwa mji, msemaji amesema.

Wapiganaji wanne wa baraza la mpito waliuawa

Wamekabiliwa na upinzani mkali na mara kadhaa wamelazimika kurudi nyuma kilomita kadhaa ili kuwapa matibabu walojeruhiwa, aliongeza.
Ali Gliwan wa Baraza hilo aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa wapiganaji waliingia katikati ya mji wa Sirte, na walikabiliana na washambuliaji wa kuvizia na kitengo maalum cha vikosi vya Gaddafi.
Wapiganaji wanne wa Baraza la Kitaifa la Mpito wameuawa na wengine saba kujeruhiwa,aliambia shirika la habari la AP.

Msemaji wa Kanali Gaddafi, Moussa Ibrahim, ameambia kituo cha Televisheni cha Syria kuwa "maelfu ya watu wamejitolea" kusaidia "kukomboa Libya" kutoka kwa Baraza la Mpito la Kitaifa.

No comments:

Post a Comment