Wednesday, September 14, 2011

Washukiwa Wawili wakiri kushambulia Uganda

Washukiwa wa ugaidi Uganda
Wanaume wawili ambao walishtakiwa kwa kuhusika na ulipuaji wa mabomu mjini Kampala mwaka uliopita wamekiri makosa hayo.Wawili hao ni miongoni mwa washukiwa 14 ambao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo mauaji ya watu 70 katika mashambulio hayo.
Washukiwa wa mashambulizi hayo walikuwa 19 lakini watano wakaachiliwa huru jana na mahakama kuu mjini Kampala. Wengine miongoni mwao raia wawili wa Tanzania walikanuha mashtaka dhidi yao
Mbele ya hakimu Alfonse Owiny dollo walikuwa Edris Nsubuga a na Mohammoud Mugisha mbao walikiri kuhusika na mashambulizi ya mabomu mjini Kampala mwaka jana wakati wa fainali za kombe la dunia.
Nsubuga amekiri makosa matatu ikiwemo kutekeleza vitendo vya kigaidi kusafirisha na pia na kusambaza vilipuzi.Mwenzake Mugisha amekiri kosa la njama za kufanya vitendo vya kigaidi.
Baada ya kufikishwa mahakamani mshukiwa Nsubuga alinyoosha mkono wake na kumuomba jaji amukubalie kukiri makosa japo jana alikuwa amekana makosa. Mshukiwa huyo aliambia mahakama kuwa jana alitishiwa na wenzake ambao walikuwa wamekana mashtaka na akaamua kukiri mashtaka.
Hapo jana mahakama kuu ya Uganda ilimuondolea Muhamoud Mugisha makosa 76 ya mauaji na ila kosa la njama za kutenda visa vya ugaidi.
Alenyo George William ni wakili anaeleza maana ya watu hawa wawili kukiri makosa yao.
Kesi hii ya shambulio la bomu mjini Kampala mwaka jana inaendelea ambapo washukiwa wengine wakiwemo raia sita wa Uganda Watanzania wawili na Wakenya Sita.

No comments:

Post a Comment