Thursday, February 9, 2012

Serikali kutowalipa fidia wafugaji


WAZIRI wa Maliasili na Utaalii, Ezekiel Maige amesema kuwa Serikali haijui kama askari wa wanyamapori waliuawa ng’ombe 56 katika Wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa.

Alisema kuwa kutokana na kutotambua tukio hilo, Maige alisema hakuna mpango wowote kwa Serikali kulipa fidia kwa wafugaji wa eneo hilo kutokana na hasara hiyo kwa kuwa  hakuna ushahidi kamili.

Katika swali la msingi Anna Mallac (Viti Maalu-Chadema), alitaka kujua Serikali inachukua hatua gani kwa kitendo cha askari wa wanyamapori kuua ng’ombe 56 katika vijiji vya Ikiba, Kishishi na Chamaledi wilayani Mpanda.

Mbunge huyo alitaka Serikali itamke ni lini talipa fidia hiyo kwa wafugaji ambao wamesubiri kwa muda mrefu.

Waziri Maige alisema kuwa Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa) halijawahi kupokea taarifa zozote kutoka Hifadhi ya Taifa ya Katavi, kuhusu madai ya malalamiko yanayohusiana na mauaji ya ng’ombe yaliyofanywa na askari wake.

Alisema tuhuma za mauaji ya mifugo ni moja ya mashauri ya jinai ambapo mlalamikaji anatakiwa kupeleka shtaka polisi, ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika kwa ajili ya kubaini ukweli wa jambo hilo.
 “Hadi sasa shirika haliwezi kulipa fidia yoyote kw ajambo hilo ambalo halijathibitika kisheria kuwa lilifanywa na watumishi wa Tanapa,’’alisisitiza Maige.

Waziri huyo alisema kwamba vitendo vya kuuawa kwa wanyama ikiwemo mifugo mara nyingine umekuwa ukifanywa na majangiri ambao wanakuwa na siraha nzito kuliko za askari.

Alisema kuwa majangili hao kwa kipindi cha miaka mine wameweza kuwaua kwa risasi askari wa wanyamapori wapatao wanane jambo linalothibitisha kuwa kazi hali ni mbaya katika maeneo ya ulinzi ambayo inahitaji nguvu ya Serikali na wananchi katika kulinda hifadhi hizo.

No comments:

Post a Comment