Mazishi ya Kanali Gaddafi yamesitishwa kutokana na tofauti zilizozuka baina ya maafisa wa Libya kuhusu jinsi ya kufanya maziko hayo.
Haifahamiki kama kiongozi huyo wa zamani atazikwa Sirte, mji aliouawa siku ya Alhamis, au Misrata, mji aliopelekwa baada ya kufa, au mahala pengine.
Wakati huohuo Nato inatarajiwa kutangaza kumaliza shughuli zake nchiniLibya.
rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema kifo cha Muammar Gaddafi kinamaanisha shughuli za Nato nchini Libya zimefikia kikomo.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa mamlaka nchini Libya zinafanya mipango ya kufanya mazishi ya siri kwa kiongozi huyo.
Hata hivyo, inaonekana huenda kukawa na kuchelewa kufanyika kwa mazishi hayo, ambayo chini ya utamaduni wa Kiislam mazishi hufanyika haraka iwezekanavyo.
Waziri wa mafuta Ali Tarhouni aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mwili wa Kanali Gaddafi huenda ukahifhadhiwa "kwa siku kadhaa".
Nato inatarajiwa kutangaza kumaliza shughuli zake nchini Libya katika saa chache zijazo.
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema kifo cha Gaddafi kinamaanisha shughuli za kijeshi za Nato nchini Libwa zimefikia mwisho wake.
"Ni wazi shughuli hiyo imefikia kikomo," amewaambia waandishi wa habari.
Mapema, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe alisema shughuli za Nato zitamalizika "baada ya kuzingatia hatua kadhaa za mpito katika wiki moja ijayo".
No comments:
Post a Comment