Wednesday, August 10, 2011

Amuua mke kwa wivu wa mapenzi

MUME anadaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga na nyundo kichwani kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Anthony Ruta alimtaja Said Mrisho (68) kuwa anatuhumiwa kumuua Zaituni Ramadhan (40) .

Ruta alisema tukio hilo ni la mwishoni mwa wiki katika Mtaa wa Sikanda, katika Manispaa ya Tabora.

Alisema, chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi kutokana na mwanamume kumtuhumu mkewe kutembea na wanaume wengine nje ya ndoa yao.

Kamanda alisema, tangu Aprili mwaka huu, mke na mume huyo walikuwa hawajapeana unyumba jambo lililomfanya mwanamume ahisi mkewe ana wanaume wengine nje ya ndoa yao.

Alisema, kwamba Polisi inamshikilia mtuhumiwa kwa mauaji ya mkewe na ambaye atafikishwa mahakamani muda wowote upelelezi utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment