Monday, January 2, 2012

Tanzania yatukanwa na kudhalilishwa


Huku akitumia, mtindo wa dharau na kebehi kubwa, Ehud Barak, ametolea mfano wa nchi zisizo na maana kuwa ni Tanzania, Mouritania na Tripolitania.
Wakati huo huo msimamizi wa ubalozi mdogo wa Tanzania nchini Israel, Bwana Altzanzy Noraal, kwa niaba ya serikali makini ya Tanzania, amepeleka barua rasmi ya malalamiko dhidi ya kebehi za Ehud Barak. Katika nakala za barua hiyo ambayo NIFAHAMISHE imebahatika kuona nakala yake, Mheshimiwa Altzanzy Noraal ameitaka serikali ya Israel ilaani vikali kauli za waziri Ehud.
Akiendelea kutoa malalamiko yake, Noraal, alimfafanulia waziri wa mambo ya nje wa Israel kuwa, Ehud ameamua kuidhalilisha Tanzania kwa kuifagilia Ulaya kiasi cha kuifanananisha Tanzania na nchi isiyokuwepo duniani, akimaanisha ile Tripolitania.
Noraal aliwahabarisha Waisrael kuwa Tanzania ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika Mashariki ikiwa na idadi ya watu kama milioni 46. Huku akiikumbusha Israel uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Israel kiuchumi na kiusalama. “Tanzania ni nchi muhimu sana wala haipaswi kupuuzwa” amesema Bw. Noraal. “Nitafurahi sana nitakapotembelea Tanzania nikiwa na mwakilishi wa Israel ili aone uzuri wa Tanzania nchi yenye eneo kubwa na mazingira halisia na watu wanaopenda amani” amesisitiza kwa kuwakejeli kisiasa kwa namna wanavyopenda vita na Warabu kila kukicha.

No comments:

Post a Comment