Taarifa  hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime na  kusema kuwa watu hao wamekufa maji baada ya kupigwa na wimbi zito na  hadi sasa miili hiyo bado haijaonekana. 
Aliwataja kuwa ni  Emmanuel Mwanyika (23), mkazi wa Kibada ambaye alikufa fukwe  iliyopo  eneo la Sunrise Beach Kigamboni kwa kupigwa na wimbi zito kuzama na  kunywa maji mengi akiwa na wenzake 
Wa pili ni Asha Ibrahim (14),  mkazi wa Kibugumo,  ambaye alizama wakati akiogelea na wenzake katika  eneo la Zabada Beach Kigamboni. 
Kamanda Misime amesema miili hiyo bado haijapatikana na juhudi za kuisaka bado zinaendelea
No comments:
Post a Comment