WABUNGE wa Mkoa wa Dar es salaam wamenywea kwa Waziri wa Ujenzi, Dk John  Magufuli, huku wakieleza kusubiri majibu ya malalamiko yao kutoka kwa  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Mwenyekiti wa wabunge hao, Abbas Mtemvu,  alisema kinachofanywa na Waziri Magufuli ni maoni yake, lakini wao  wanasubiri majibu ya Pinda.
Mtemvu alisema uwezo wa kumjibu  wanao, lakini kutokana na kuandika malalamiko yao kwa waziri mkuu  watakuwa wanavunja kanuni.Alisema alisikiliza kwa makini hoja za Dk  Magufuli, lakini kutokana na kumwandikia barua Pinda watajibu pindi  watakapopata majibu hayo.
Mbunge huyo alisema Ofisi ya Waziri  Mkuu inatarajia kutoa majibu kuazia kesho, hivyo baada ya kupitia majibu  hayo watatoa msimamo wao. Hata hivyo, wakati wabunge hao wakipinga  kupanda kwa nauli hiyo ya Sh200, kifuko cha Misungwe mkoani Mwanza  kinatoza Sh400.
“Sasa nitazungumza nini maana anachoongea waziri  sijajua, lakini ninachosema hapa hebu tusubiri waziri mkuu ili tuweze  kumjibu maana tuanalo la kujibu,” alisema.Aliwataka wananchi wawe  watulivu maana kuanzia kesho majibu yatatolewa na Pinda kutokana na  malalamiko yao.Dk Ndungulile akata tamaa
Naye, Mbunge wa  Kigamboni, Dk Faustine Ndungulile, alisema Dk Magufuli amebeza wananchi  wa Kigamboni, maana kinacholalamikiwa siyo tangazo la kupandisha nauli,  bali mchakato uliotumika kufikia uamuzi huo.
Dk Ndungulile  kinachosubiriwa hapa na wananchi siyo kushuka kwa nauli, bali  kuangalia  makundi maalumu yanayotumia kivuko hicho jinsi yatakavyosaidiwa.
“Nimemsikiliza  Waziri Magufuli kwa makini sana, lakini ameshindwa kujua watu gani  wanokwenda kufaidika na watu gani watakaoathirika na ongezeko hilo,”  alisema.
No comments:
Post a Comment