WANAFUNZI wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuanzisha mijadala ya kina ya namna ya kutanzua tatizo la ajira kwa vijana na sio kukaa na kuanza kulaumu.
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alitoa ushauri huo jana na kuongeza kuwa wakati katika nchi za Kenya na Uganda vijana wameamua kwenda nje kutafuta ajira, sisi tukae chini na kuangalia namna ya kutatua na sio kukimbilia nchi za nje.
Lowassa alitoa kauli hiyo mara baada ya kutembelewa na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kilimanjaro vya Ushirika, Mwenge, Kumbukumbuku ya Mtakatifu Stefano na Chuo Kikuu cha Afya cha KCMC waliokwenda kumpa pole kwa msiba wa mdogo wake.
Lowassa ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu amewataka vijana waliopo vyuoni kuanza kujadili kwa
kina tatizo la ajira kwa vijana nchini.
Alitoa mfano wa vijana wa vyuo vikuu namna ya kujikomboa kwa kujiajiri kwa kukopeshwa matrekta na kulima kilimo cha kisasa na kueleza kuwa hilo linaweza kuwakomboa badala ya kulalalmika.
No comments:
Post a Comment