Saturday, December 24, 2011

Alia mara mbili baada pesa kwenda na maji

MWANAMKE ambaye ameombwa jina lake lisiandikwe hapa [31] mkazi wa Kigogo, amejikuta akilia mara mbili baada ya kupata hasara ya kuondokewa na fedha zake zaidi ya laki mbili na nusu ambazo aliziweka kwenye boksi maarufu kama “kibubu” zlizoziweka chumbani
  Mwanamke huyo ambaye kwa jana alikuwa na homa kali ya kuwaza kuanza upya maisha yake mbaada ya mali zake kuondokewa na maji vikiwemo samani za ndani na amejikuta akilia kama motto mdogo kwa kufikia kadhia hiyo

MWanamke huyo aliiambia NIFAHAMISHE kuwa, alikuwa akiihsi na waatoto w ake wawili katika chumba alichopanga maeneo ya Kigogo huku akilipa kodin yake shilingi elfu kumi na tano kwa mwezi baada ya kutengana na baba watoto wake aliyezaa nae watoto hao

Amedai siku ya tukio maji yalijaa kuzingira nyumba hiyo na alichofanya ni kuokoa maisha ya watoto wake na yeyey mwenyewe huku akishuhudia mali zake zikielea na maji na kushindwa kuviokoa likiwenmo sanduku hilo alkilohifadhia fedha zake hizo ambazo alisema alitoka kupokea mchezo na alizihifadhi humo

"Hayo ndiyo yaliyonikuta, yaani nikifikiria sina hamu kabisa ya kuishi kwani fedha hizo zingenisaidia kutafuta chumba kingine na wanangu “ alimaliza

No comments:

Post a Comment