Friday, December 30, 2011

Kunyongwa au kupigwa mawe?


NewsImages/6143574.jpg
Picha ya mwanamke mtuhumiwa wa uzinzi na mauaji
Sakineh Mohammadi Ashtiani, mwanamke wa Kiirani anayetuhumiwa kwa makosa ya kumuua mumewe na kufanya uzinzi akiwa anatambukuwa kuwa ana mume, Huenda akaepuka adhabu ya kupigwa mawe hadi afe na badala yake anakabiliwa na adhabu ya kunyongwa.
Vyanzo vya Nifahamishe, vimearifiwa kuwa, mwanamama huyo aliyekuwaanakabiliwa na adhabu ya kurembewa mawe hadi anakata roho kwa mujibu wa sheria za Kiisalam kwa mtu mzinzi ambaye ameshaoa au kuolewa, huenda akapewa adhabu ya kunyongwa kwa kosa la kupanga njama na kutekeleza mauaji ya mumewe ili apate nafasi ya kustarehe na mwanamume mwingine. Hili linatokana na namna kesi ilivyoendeshwa na kutopatikana uthibitisho wa uzinifu wake, kwani kwa mujibu wa sheria za Kiislam, lazima pawepo na wanaume wanne walioshuhudia tukio la uzinifu kwa kuona kwa macho! Au muhusika wa uzinifu akiri mwenyewe kuwa amezini na anataka apewe adhabu ya kumtakasa na dhambi ya zinaa.

Kwa upande wake bibi Sakineh Mohammadi Ashtiani, amekana madai ya kuzini na kwa hiyo hakuna ushahidi wa kumtia hatiana kwa kosa la zinaa, na kilichobaki ni kesi ya mauaji inayomkabili na kwa mujibu wa sheria za Kiislam zinazofuatwa na serikali ya Iran, adhabu ya muuaji ni kulipiziwa kisasa kwa kuuliwa au ndugu wa marehemu wamsamehe.

No comments:

Post a Comment