Saturday, December 24, 2011

Msiba Mkubwa Dar es Salaam


NewsImages/6137790.jpg
KUTOKANA na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kuleta mafuriko katika maeneo mengi jijini Dares Salaam kumepelekea wakazi wa jiji hilo kuwa na msiba mkubwa kutokana na kukatika na kuzolewa na maji kwa madaraja mengi yanayounganisha kutoka upande m
Msiba huo unakuja baada ya wakazi hao kukosa mawasiliano kati ya upande mmmoja na mwingine kutokana na madaraja hayo kuzolewa na maji na mengine kukatika na mafuriko yanayosababisha watu kushindwa kuvuka upande mmmoja kwenda mwingine kwenda kwenye shfughuli zao za kila siku

Daraja la Tandale uzuri, Kwa Ali Maua , Mbezi, Kigogo yameripotiwa kuanguka kutokana na mvua kubwa yaliyoathiri madaraja hayo na kupekeka wakazi kushindwa kusafiri na kukosekana wka mawasiliano kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumbwa jiji hilo

Daraja la Msimbazi limefurika maji na kutoonekana kabisa kwa darasa kwa daraja hilo hali iliyopeleka kukosekana kwa usafiri

Daraja la Jangwani lililopo barabara ya Morogoro nalo lilifurika maji na kutoonekana kwa kingo la darja hilo hali iliyopelekea jeshi la polisi kuzuia kwa muda njia hiyo kutokana na mafuriko hayo

Daraja la Salendar lilijaa maji na kupeleka kufungwa kwa njia hiyo

Hivyo kutokana na kuzuiliwa kwa njia hiyo ilifanya magari ya usafiri na binafsi kushindwa kupita njia hiyo na wakazi kukosa usafiri na walikwua wakivunjwa na mitumbiwi kwenda upande mwingine


Mbali na madaraja pia nyumba zimeathiriwa na maji na nyingine kuanguka hasa waliopo maeneo ya mabondeni
na watu waliozunguwka na maji walaiweza kujiokoka kwa kupanda juu ya mapaa ya nyumba kwa kujisalimisha na kuokolwa na wasamaria wema

Hata hivyo utaabiri wa hali hewa unaonyesha mvua hizi kubwa bado zinaendelea

No comments:

Post a Comment