Thursday, November 24, 2011

MAMA SALMA KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUNAWA MIKONO DUNIANI



Baadhi ya watoto pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za mkoa wa Dar es salaam wakipita mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani  leo. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) ndiye aliyekuwa mgeni kwenye sherehe hizo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar leo
  
 Watoto wakicheza ngoma ya msewe ya Zanzibar
 Wasanii wa Kikundi cha Orijino Comedy kikionyesha zoezi la kunawa mikono wakati wa maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani lililofanyika leo  jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete hayupo pichani
 Mama Salma Kikwete akiwaonyesha watoto zoezi la jinsi ya kunawa mikono kwa sabuni wakati wa maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani 
 Sehemu ya tukio lilifanyika sherehe ya maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani 
 Baadhi ya watoto wa shule za msingi jijini Dar es Salaam wakiangalia aina ya kibuyu chirizi ambacho hutumika kuweka maji kwaajili ya kuoshea mikono.
Watoto wakitoa burudani.
Picha na Mwanakombo Jumaa – MAELEZO

No comments:

Post a Comment