Mahakama moja nchini Thailand imemhukumu mzee mwenye umri wa miaka 61 miaka ishirini jela kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu unaokashfu mamlaka ya kifalme.
Mtu huyo, Ampon Tangnoppakul, alipatikana na hatia kwa kutuma ujumbe huo mara nne kwa njia ya simu ya mkononi kwa afisa mmoja wa ofisi ya waziri mkuu wa zamani, Abhisit Vejjajiva, wakati wa maandamano ya kupinga serikali mwaka uliopita.
Mtu huyo amehukumiwa chini ya sheria ya makosa ya matumizi mabaya ya kompyuta, na sheria inayolenga kulinda heshima ya mamlaka ya kifalme nchini humo.
Wakosoaji wanasema sheria zote mbili zimegubikwa na siasa na zinazuia uhuru wa kutoa maoni nchini Thailand.
No comments:
Post a Comment