Saturday, November 19, 2011

Papa Benedict awasili Benin

 Papa Benedict amewasili nchini Benin kwa ziara ya siku tatu katika Taifa hilo la Afrika ya magharibi.Katika ziara yake ya pili barani Afrika ambako kuna ongezeko kubwa la waumini wa dini katolika kuliko sehemu nyingine duniani.
Ingawa kuna ongezeko la waumini wa dini hiyo nchini Benin, wakaazi wengi wa nchi hio hufuata imani ya kale ya 'vodoo' inayotambuliwa kama dini rasmi ya Benin. Wadadisi wanasema kua hata Wafuasi wa hizo dini nyingine nao huchanganya imani za kale na imani zao kama Waislamu au Wakatoliki.
Siku ya leo imetangazwa kua siku ya mapumziko nchini humo na mitaa ya mji mkuu Cotonou imepambwa kwa mabiramu yanayomkaribisha Papa Benedict.
Akizungumza na wandishiw a habari kwenye ndege aliyosafiria kutoka Roma kwa ziara hii, Papa alisema lazima dunia ijiulize sababu kuu ambapo baada ya juhudi kubwa na mara nyingi zimeshindwa kuiopoa Afrika kutoka janga la ufukara.
Mikutano mingi imefanywa: maneno matamu kutamkwa. Lakini kawaida maneno na dhamira ni muhimu kuliko mafanikio na ndio sababu tuulize sababu.
Papa amesema alichagua kuitembelea nchi ya Benin kuwasilisha hati muhimu ya kanisa kuhusu Afrika itakayochapishwa jumamosi kwa sababu hati hio ni tofauti.
Benin ni nchi inayofuata demokrasi ambako wafuasi wa dini za Kikristu, waislamu na wafuasi wa dini za kale wanaishi kwa amani, alisema Papa.
Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Cotonou alilakiwa na Kiongozi wa nchi ya Benin ambapo Papa alizungumza kuhusu umuhimu wa Afrika kuleta mageuzi, ingawa aliongezea kua mageuzi hayo yasifanywe kwa hasara.
Miongoni mwa masuala ambayo Papa alishauri yazingatiwe ni kutosalimu amri sheria zinazotawala masoko ya bidhaa zao pamoja na hazina.

No comments:

Post a Comment