Tuesday, November 15, 2011

VURUGU ZA WANANCHI IRINGA, ASKARI NA WAANDISHI WAJERUHIWA VIBAYA

Majeruhi wa mapingano kati ya polisi na wananchi mjini Iringa leo
Mwanahabari wa kituo cha radio Overcomers Fm Devota Romanus akiwa wodi namba 7 katika Hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kujeruhiwa mguu wake wa kushoto kwa mawe
Askari polisi aliyejeruhiwa akipelekwa wodini kulazwa
Nguo za majeruhi ambaye alijeruhiwa kwa risasi baada ya kutaka kuwachoma moto wanahabari na polisi ndani ya nyumba hiyo
Magari ya mfanyabiashara huyo yakiwa yamevunjwa vioo kwa mawe
Mwandishi akisaidiwa kutolewa eneo la mapigano leoNyumba ya mfanyabiashara huyo ikiwa imevunjwa na wananchi
Umati wa wananchi wa mji wa Iringa wakikimbia mabomu ya machozi
wananchi wakiwa nje ya lango la nyumba hiyo wakitaka kuonyeshwa watu wanaodaiwa kufa na kuonekana wakiwa hai (Misukule)Wananchi wakiishambulia nyumba yenye wanahabari na watuhumiwa na polisi kwa mawe.

Zaidi ya watu 10 wakiwemo askari wanne na wanahabari wamejeruhiwa huku baadhi yao wakitibiwa na kuruhusiwa na wengine kulazwa katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kuibuka kwa mapigano hayo kati ya polisi na wananchi ,mapigano ambayo yametokana na imani potofu za wananchi katika kuamini ushirikina.

Wananchi hao zaidi ya 200 walivamia nyumba ya mzee wa kanisa moja la kilokole katika mji wa Iringa eneo la Frelimo jina limehifadhiwa kwa sababu za kimaadili .

Hata hivyo pona ya wanahabari na polisi waliokuwa wamefungiwa ndani ya nyumba hiyo na kushambuliwa kwa mawe na kunusurika kuteketezwa kwa moto wakiwa ndani ya nyumba hiyo ilionekana baada ya askari polisi wa FFU kutumia mbinu kubwa ya kulazimika kutumia risasi ya moto kumshambulia mguuni mmoja kati ya watu wanaodaiwa kutaka kuongoza wengine kuichoma moto nyumba hiyo iliyokuwa na wahahabari ndani, polisi na mchungaji mmoja .

Baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa kuokoa maisha ya wanahabari hao na watu wengine zaidi ya 10 ambao walipaswa kuuwawa na wananchi hao .

Wananchi hao walionekana kuongezeka idadi baada ya FFU kuwatisha kwa mabomu ya machozi huku wakidai kuwa mabomu hayo hayaui na bila polisi kupata mbinu ya haraka ya kutumia risasi ya moto zaidi ya watu hao 10 wakiwemo wanahabari waliokuwa ndani ya nyumba hiyo wangekuwa wameuwawa na wananchi hao ambao waliondoa imani na kikosi hicho kuwa wamehusika kuificha misukule hiyo.

No comments:

Post a Comment