Msemaji huyo Meja Jenerali Emmanuel Chirchir, ameiambia BBC kuwa miji hiyo - ni pamoja na Kismayo na Baidoa - ambayo ni ngome ya kundi la al-Shabaab.
Kenya imetuma wanajeshi nchini Somalia mapema mwaka huu, kwa sababu inalaumu kundi la al-Shabaab kwa wimbi la utekaji nyara.
Al-Shabaab, ambayo inadhibiti eneo kubwa la upande wa kusini, inakanusha madai hayo.
"Jeshi la Kenya linatoa wito kwa yeyote anayeishi au mwenye jamaa na marafiki wa miji 10 kuwashauri," Meja Emmanuel Chirchir aliandikwa kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo miji aliyoitaja ni tisa ambayo ni Baidoa, Bardhere, Dinsor, Afgoye, Buale, Barawe, Jilib, Kismayo na Afmadow.
No comments:
Post a Comment