Thursday, November 3, 2011

Binti ajifungua njiani- amtumbukiza kitoto kwenye mfuko wa rambo

Na Benjamin Masese

KATIKA hali isiyo ya kawaida msichana aliyefahamika kwa jina la Ndeku Augostino (22) akiwa njiani anatoka kupata matibabu katika hospitali ya Mwananyamala, ghafla alijikuta akijifungua mtoto wa kiume  bila kujifahamu ambapo aliamua kununua mfuko wa rambo na kumtumbukiza humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi jana na Kamanda wa wilaya ya Kinondoni Bw. Charles Kenyela alisema kuwa tukio hilo lilimtokea msichana huyo juzi eneo la Luhanga wakati akirejea nyumbani kwao.

Bw. Kenyela alisema kwa wakati msichana huyo akipatwa na tukio hilo njiano hapo baadhi ya wananchi walimuona akiweka mtoto huyo kwenya mfuko na rambo huku akihangaika kuangalia sehemu ya kuutelekeza ndipo walipomkamata na kumfikisha kituo cha polisi.

Alisema kuwa mtoto huyo alifariki muda mchache baada ya kuzaliwa na  mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala. Hata hivyo alisema mahojiano yanaendelea na msichana huyo ili kubaini chanzo cha kujifungulia njiani ni kukosa huduma hospitalini au alikusudia kufanyia hivyo.

Wakati huo huo mwanaume aliyefahamika kwa jina la Shaban Ramadhani (40-45)mkazi wa Temeke ghafla  alianguka chini na kufariki papo hapo wakati akiosha gari eneo la Urafiki Kilimani wilaya ya Kinondoni.

Bw. Kenyela alisema kuwa tukio lilitokea saa tatu asubuhi eneo hilo wakati akiwa na wenzake wakiendelea na shughuli yao ya kila siku.Chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi na hakuna aliyekamatwa kuhusu tukio hilo.

No comments:

Post a Comment